Wakazi Akiri Hakuna Msanii Kama Davido

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi Music amefunguka na kumnyanyulia mikono msanii kutoka Nigeia David Adeleke maarufu kama Davido baadae ya ushindi wake wa tuzo ya BET.

Davido aliibuka mshindi wa tuzo ya BET 2018 katika kipengele cha ‘Best International Act’, tuzo zilizofanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater huko mjini Los Angeles, jimboni California, Marekani.

Baada ya ushindi huo Davido alitoa hotuba ambayo ilikuwa imejikita katika kutangaza soko la Muziki wa Africa na kuwataka wasanii wa Marekani kufika Africa Kutembea:

Hotuba hiyo Ikiwa huwa watu wengi na mmoja wao ni Msanii Wakazi ambaye alishindwa kujizuia na kumwagia sifa lukuki Davido kwa hotuba hiyo ambapo kipitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Hongera nyingi zimwendee Davido kwa ushindi wa “Best International Act” kwenye @betawards huko Marekani. Mwaka huu hakukuwa na mtanzania Ila pia Category ya International iliunganiswa Africa na Europe, so angechukua mwafrika yeyote tungehesabu Ushindi. Ila kikubwa ni kwamba mwaka huu ndio mara ya kwanza Tuzo za International kupokelewa on the Main Stage. Na niseme ukweli Davido hajatuangusha kwenye Speech yake. Ilikuwa Fupi and I understand maana sio mchezo (kutembea tu kwenda pale mbele unamuona kila Star, hatari) lazima utetemeke. Ila Davido alimshukuru D’banj kama Msanii aliyeanza kutufungulia milango african artists upande wa marekani (Collabo na Snoop Dogg, Signed by Kanye West) na pia alichukua Fursa kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya D’Banj Maana amefiwa na mwanae (R.I.P Daniel III). Kisha akashukuru Fans, Familia yake, Management yake. Mwisho akawasihi wanyamwezi kuja africa wajionee hali, chakula na kufanya Collabo na Wasanii wetu, pia akasema Album yake inakuja soon. Kiukweli I don’t see any other artist kufanya a better job of representing zaidi ya alivyofanya OBO.
Ila sasa hii iwe changamoto na chachu ya sisi huku kupigania muziki wetu na sisi maybe tuje kushinda na kupata fursa ya kuinadi Tanzania kikamilifu. I know I’m inspired and I’m going to the studio leo. Ikiwezekana tuongeze support ya wenyewe kwa wenyewe kama itasaidia. Tuache UMBEA na kuongelea yasiyotuhusu, Tuache Uvivu… tupige Kazi, uwe underground uwe Legend!! Wote tuna nafasi… peace #AfricaPride

Davido kusherekea Eid Tanzania.

Msanii mkubwa na mshindi wa tuzo nyingi Duniani, Davido anatarajiwa kutumbuiza siku ya sikukuu ya Eid itakayofanyika Duniani kote ikiwa ni mwisho wa mfungo wa Ramadhani ulioanza mwezi uliopita.Mwanamuziki huyo ambae atatumbuiza katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar Es Salaam.

Akiongea katika uzinduzi wa Sheba wa The Mafik uliofanyika katika ukumbi wa the next door jijini Dar , bosi wa kundi hilo aliwaambia mashabiki wake kwamba wakae mkaa wa kula kwa sababu anampango wa kumleta Davido katika sikukuu hiyo.

Hata hivyo bosi huyo hakuweka wazi show hiyo itafanyika  vipi lakini aliwatia hamasa watu na mashabiki wake na wamekaa mkao wa kula kusbiria show hiyo kubwa , ukizingatia na ukubwa wa msanii huyo wa  Afrika.

 

Dogo Janja: Davido ako na pesa lakini hajui kuvaa

Rapper Dogo Janja amemshambulia Davido kwa kile alichodai kuwa msanii huyo kutoka Nigeria hajui kuvaa licha ya kuwa na utajiri mkubwa.

Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii wanaong’ara sana nchini Tanzania, hivi karibuni alipigiwa upata kuwa anang’ara sana kushinda Diamond Platnumz.

Davido

Soma pia: Picha 10 za Dogo Janja ambazo ni dhibitisho kuwa anang’ara kimavazi kushinda Diamond Platnumz

Akiongea akiwa Sibuka FM, Dogo Janja alisema Davido ako na pesa nyingi lakini hajui kupendeza kimavazi, alieleza kuwa mara nyingi nguo anazovaa Davido ni kama huwa zimetundikwa tu mwilini mwake.

Janja pia alisisitiza kuwa yeye ndiye anayeng’ara zaidi kushinda wasanii wote nchini Tanzania. Aliwataja G Nako, Jux kwa mbali na Joh Makini kama wapinzani wake kwa uvaaji.

Dogo Janja

 

Joh Makini: Davido alinifwata kutafuta collabo na mimi

Joh Makini aliwaahidi mashabiki wake kufanya collabo kubwa na Davido – msanii anayetajika sana nchini Nigeria na barani Afrika.

Davido alidhibitisha collabo yake na Joh Makini kupitia mitendao ya kijamii. Kwenye Instagram yake, Davido alipost  picha akiwa pamoja na Joh Makini na kuandika maneno yalisomeka “Back to work On set shoot @johmakinitz ft Davido ….. TZ  x NAIJA”

Joh Makini amefunguka na kueleza kuwa Davido ndiye aliyemfwata na kupendekeza wafanye collabo – wengi walikua wanadhani Makini ndiye aliyemwomba Davido kushirikiana naye kimuziki.

“Mimi naona ni kwasasabu alikuwa excited sana kufanya kazi na mimi, halafu wakati wa kufanya hii ngoma yeye ndiye aliyekuwa wakwanza kuniapproach mimi. Kwa hiyo nafikiri ni mtu ambaye alinifuatilia na akaupenda muziki wangu ndiyo maana hata chemistry imekuwa nzuri na tumefanya kitu kikubwa,” Joh Makini alisema.