Ujumbe Wa Diamond Kwa Nillan Siku Ya Birthday Yake

Msanii wa Bongo fleva nchini Diamond Platnumz ameandika ujumbe mzito kwa Mtoto Wake aliyezaa na Zari The Bosslady Prince Nillan ikiwa ni siku yake ya kusheherekea birthday yake.

Siku ya Leo Nillan anafikisha umri wa miaka mieili pamoja na kuwepo maneno Mengi kwenye mitandao ya kijamii tangu anazaliwa kuwa sio Mtoto wa Diamond lakini Diamond amesema siku zote ni Mtoto Wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amemuandikia ujumbe mzito mtoto wake huyo na kusema:

Miaka miwili iliyopita Mungu alinibariki na Mtoto wangu wa kwanza wa kiume naye nilimuita jina la Nillan linalomaanisha Mwezi/ Asili/ Umaarufu/ Handsome na ni handsome kweli anayeng’aa zaidi ya nyota Happy Birthday Nillan Baba anakupenda”.

https://www.instagram.com/p/BrBZIwGl_mW/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=3ugwerk3u8km

Zari Adaiwa Kumfanyia Zengwe Diamond

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mzazi mwenzake Zarinah Hassan wamerudi Tena Kwenye headlines ambapo sasa inadaiwa Zari Kamfanyia Zengwe Diamond mpaka kuharibu Birthday ya Tiffah.

Global Publishers wanaripoti kuwa Diamond alitangaza  kuangusha bonge la sherehe nchini humo, Lakini sasa inadaiwa Zari amemfanyia zengwe Diamond kiasi cha kumfanya jamaa huyo anyooshe mikono na kuahirisha sherehe hiyo bila kupenda.

Unajua ile bethide Diamond alikuwa anaiandaa kwa ushirikiano na kampuni (anaitaja jina) na kampuni hii ndiyo ambayo inawadhamini Diamond na Zari katika mambo mbalimbali kwani kampuni hiyo nayo inanufaika pia kwa jinsi wawili hao wanavyoitangaza kupitia matangazo mbalimbali wanayoyaandaa. Sasa kulikuwepo makubaliano kwamba ili wadhamini hao waendelee kutoa fedha, Diamond na Zari wanapaswa kuposti sherehe hiyo katika akaunti zao za Instagram, sasa mwanzoni bidada Zari anaonekana alikubali, lakini kadiri siku zilivyokuwa zinaenda akapiga kimya tu”.

GPL wanazidi kuripoti kuwa kutokana na matukio yaliyokuwa yanaendelea kutokea Zari aligoma kabisa kushiriki kuiposti sherehe ile na badala yake alikuwa bize na mambo yake binafsi ikiwemo Shindano la Miss Uganda.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilimsaka Diamond bila mafanikio lakini Meneja wake Babu Tale alifunguka haya kuhusu sherehe ile:

Unajua hii ni pati, bethidei ya Tiffah ilishapita lakini nikwambie tu itafanyika na kutakuwa na sapraizi mtaona”.

 

 

“Mimi ni Bilionea” Zari Amwagia Povu Mange Kimambi

Zarinah Hassan au maarufu kama Zari The Bosslady ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, amemwagia povu zito Mange Kimambi.

Mange na Zari wamerudi tena vitani huku safari hii Zari akiweka wazi kuwa yeye ni bilionea hivyo asimchukulie Poa.

Sakata hilo lilianza siku ya jana baada ya Zari kumwagia sifa marehemu Ivan za kuwa baba bora na sio mzazi mwenzake Diamond ambapo Mange alimjia juu na kumtaka amshukuru Diamond kwa sababu yeye na watoto wake wanaishi kwenye nyumba ya Diamond.

Baada ya Kuambiwa hivyo Zari alimwaga povu zito na kudai Mange ndio anaishi Kwenye makazi yasiyoeleweka nchini Marekani lakini yeye anaishi Kwenye nyumba ya Diamond kwa sababu ameamu.

Zari aliendelea kumwaga povu na kudai kuwa akiamia kuhaama anaweza kwa sababu Ivan ameacha nyumba tatu na yeye pia anamiliki nyumba moja na kusisitiza kuwa yeye ni bilionea.

Kama utakumbuka Mwanzoni mwa mapenzi yao Diamond alimnunulia Zari bonge la mjumba Nchini South Africa ambapo ndipo anaishi na Watoto wake.

Zari Amwaga Povu Kuhusu Suala la Umri Kwenye Mapenzi

Mfanyabiashara maarufu na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Zari The Bosslady amemwaga povu kwa watu walio na mtazamo hadi juu ya Mahusiano kati ya mwanamke mkubwa na kijana mdogo.

Zari amefunguka na kuonyeshwa kushangwa na jinsi ambavyo jamii ilivyokuwa na haraka ya kumuhukumu mwanamke mwenye umri mkubwa kutoka kimapenzi na mwanaume mdogo kuliko kiumri.

Zari amemwaga povu hilo kupitia ukurasa wake wa Snapchat ambapo amesema lakini anashangazwa na Utayari wa jamii kuona msichana mdogo akiwa Kwenye Mahusiano na mwanaume mkubwa kiumri tena vibabu kabisa.

Sitting here and thinking. Society is so quick to judge an older woman dating a young guy, but not a 40+ guy dating a 19 yr old. so typical! Watu na vibabu vyenu”.

Zari amewahi kuwa Kwenye uhusiano wa Kimapenzi na Diamond ambaye inasemekana kuwa amemzidi zaidi ya miaka kumi.

Zari na Diamond Waibua Tetesi za Kurudisha Penzi Lao

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na mama watoto wake Zarinah Hassan wamerudi tena Kwenye headlines za kurudiana.

Zari na Diamond waliachana mapema mwaka huu baada ya Zari kumwaga Diamond Kupitia post yake ya Instagram katika siku ya wapendanao.

Tangu waachane Zari amekuwa muwazi kuhusu Mahusiano hayo huku akiweka wazi kuwa aliumizwa na vitendo vya kudhalilishwa na Diamond baada ya kutuhumiwa kuwa Kwenye Mahusiano na warembo kibao huku Diamond amekuwa mgumu kuongelea uhusiano huo.

Lakini sasa kuna Tetesi zinazoendelea kuvuma Kwenye mitandao ya kijamii kuwa Zari ameamua Kurudisha majeshi kwa Baby dady wake baada ya Meneja wa Diamond Babu Tale kusafiri kwenda South Africa kwa ajili ya kuwapatanisha.

Siku ya jana kuna clip ilisambaa Kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha Diamond akitua nchini South Africa lakini haijajulikana kama alifikia nyumbani kwa Zari au hotelini lakini Zari aliposti picha ya zawadi alinunuliwa na ‘Baba Nee’ ambaye anaweza kuwa Baba Nillan (Diamond).

Ingawa wawili hao hawajathibitisha taarifa za kurudiana lakini Dada wa Diamond Esma amedokeza hilo na kumposti Zari huku akidai yule ndio wifi yake wa ukweli.