“Diamond Anapendeza na Tanasha Zaidi”- Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwamwagia sifa kibao staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi wake Tanasha Donna.

Siku za nyuma Shilole hakuficha hisia zake za Jinsi gani alikuwa anamkubali Mama Watoto wa Diamond, Zari na hata kumuomba Diamond arudiane naye Baada ya kuachana.

Lakini Hivi sasa Zari anaoenekana kumsahau Zari na kuhamisha majeshi yake kwa wifi yake Mpya Tanasha kwani ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa kibao mrembo huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Shilole ameweka wazi kuwa Tanasha anapendezana na Diamond na hata kudai tangu amekuwa naye amekuwa akipendeza zaidi hasa Baada ya kunyoa.

Diamond na Tanasha wanapendezana sana, siku hizi naona hata Diamond ananyoa vizuri kusema Ukweli wapo kizazi sana”.

Stori za chini chini zinadai kuwa Shilole alikoromewa na Diamond Baada ya kumtaka arudiane na Zari kwenye mkutano na waandishi wa habari Wiki chache zilizopita.

Fahyma Adaiwa Kumsaliti Zari na Kujipendekeza Kwa Tanasha

Mzazi mwenzake na staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny, Fahyma amefungukia tetesi za uyuda  baada  ya kudaiwa kumsaliti Zari na kujiweka kwa Tanasha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Risasi Jumamosi, Fahyma amesema kuwa anashangaa kwa nini watu wanamuita Yuda wakati hayupo hivyo na hajawahi kugombana na mtu yeyote aliyeachana na Diamond.

Hivi watu wakoje jamani sasa u-Yuda huo vipi? Kwa hiyo walitaka Diamond akibadilisha msichana mwingine basi huyu wa sasa mimi nisiwe na urafiki naye kwa sababu nilikuwa na urafiki na X wake?.

Hivi watu wana akili kweli? Mimi uhusiano wa Diamond unanihusu nini mimi? Sina mamlaka ya kumchagulia mchumba Diamond hata akimuacha Tanasha akawa na mwingine pia tukikutana kwenye sherehe nitaongea naye vizuri na kupiga naye picha kama kawaida kwa sababu mimi mwenyewe ni mpenzi mtazamaji tu.

Halafu kwanza huwa tunakutana kwenye event (hafla) tu, sijawahi kuwa na urafiki wa hivyo kama watu wanavyosema kwa hiyo waniache kabisa sitaki maneno jamani na mimi sio Yuda”.

Kama utakumbuka wakati Diamond yupo na Zari, Fahyma alionekana kuwa karibu na Zari na hata kuwepo pamoja katika mitoko mbali mbali walikuwa wote.

Familia Ya Tanasha Yaingilia Kati Penzi Lake na Diamond

Familia ya mrembo Tanasha Donna Oketh imedaiwa kuingilia Penzi lake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya tetesi za mrembo huyo kuwa mjamzito kusambaa Mitandaoni.

Global Publishers wanaripoti kuwa familia ya Tanasha imekaa kikao kizito na kuweka maazimio muhimu kuhusu binti yao huyo huku kubwa likiwa ni kumtaka mrembo huyo asizae na Diamond, ndugu wa karibuni wa Tanasha amefunguka na kusema:

Yapo mengi, lakini familia kwa sasa imesisitiza Tanasha asizae na Mondi. Tumejadiliana mengi kama familia…hadi tumefikia uamuzi huo, ni kwamba tumechambua mengi. Kwanza lazima ujue kuwa Tanasha anatoka familia ya watu walioshika dini sana. Wazazi wake ni waumini wazuri wa Dini ya Kikristo na hawapendi mambo yasiyofuata utaratibu”.

Baada ya tetesi hizo mama mzazi wa Diamond, Bi. Sandra amefunguka kuhusu tetesi hizo na kusema:

Hayo mambo unayosema umeyapata kutoka Mombasa hatuyajui, lakini sisi kama familia tumekaa na Nasibu (Mondi) na tumemshauri kwa sasa atulie kwanza, aache mambo ya kuzaa. Lakini zaidi ongea na Esma (Khan) atakuambia zaidI”.

Gazeti la Ijumaa lilizungumza na Esma ambaye ni dada wa msanii huyo. Kitu cha kwanza Ijumaa lilimhoji kuhusu tetesi za Tanasha kuwa na mimba ambapo Esma alisema:

Weee! Weee! Weee! Mimba? Hakuna kitu kama hicho, Tanasha hana mimba, Hayo ya Mombasa sijayasikia kwa kweli, lakini sisi tumemketisha Mondi na kuzungumza naye. Kwamba kwa sasa atulie kwanza, afanye muziki na kula bata na mchumba’ke Tanasha. Kama ni watoto anao, tena wa jinsia zote, hana haja ya kuwa na haraka. Ana watoto wawili wa kiume na wa kike mmoja”.

 

 

Tanasha Azidi Kujiamini na Penzi la Diamond

Mpenzi wa staa wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh ameonekana kuweka maneno ya watu pembeni za kuzidi kukolea Kwenye Penzi na Diamond.

Tangu Diamond aweke hadharani kuwa yupo kwenye mahusiano na Tanasha mwaka jana mwishoni ni wazi kuwa hawajapita njia nyepesi kwani Penzi Lao linapingwa sana hasa kwenye Mitandao ya kijamii.

Lakini Diamond na Tanasha wameonekana kupuuzia maneno ya watu na kufanya mambo yao na inaonekana wazi kuwa Tanasha amekolea kwenye Penzi na Mbongo fleva huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha ujumbe ambao ni mfupi Lakini unabeba maneno mazito kuhusiana Penzi lake na Diamond:

Kujiamini ya kweli huwa haina chumba cha chuki, ni pindi unapofahamu kitu kizuri hauna sababu ya kuchukia”.

 

Shilole Amtema Zari na Kumkubali Tanasha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amedaiwa kumsaliti na kumwaga Zari na kumkubali zaidi Mpenzi Mpya wa Diamond Tanasha.

Kama utakumbuka siku mbili zilizopita Shilole alisimama mbele ya waandishi wa habari na kumuomba Diamond aachane na Tanasha na kumuoa mama Watoto Wake Zari.

Lakini sasa Shilole ameonekana kukubaliana na hali halisi na kumkubali Tanasha kama wifi yake mpya na kusema wazi kuwa anapopenda Diamond basi na yeye hana budi kufuata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameandika maneno haya:

ANAPOPENDA KAKA YANGU SINA JINSI! HI TANASHA, DIAMOND PLATNUMZ WIFI YETU KARIBU DADA HII NDO TANZANIA NITAFANYAJE SASA JAMANI”.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Diamond kuachana na Zari na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo Natasha kutoka nchini Kenya. Hivi karibuni Diamond Platnumz alikaririwa na kituo hicho cha runinga akieleza kuwa ndoa yake aliyopanga kuifunga mwezi wa pili mwaka huu ameisogeza mbele.

Shekhe Amjia Juu Diamond Kwa Mavazi Ya Tanasha

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Amemjia juu  mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa mavazi ya mpenzi wake Tanasha.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa Tanasha alizua gumzo wiki iliyopita Baada ya kuonekana akiwa amevaa gauni ambalo liliweka sehemu kubwa ya maungo yake nje jambo ambalo pia limeonekana kumkereketa Shehe mkuu.

Jamani…jamani…ndiyo nguo gani ile mbele ya kiongozi wa dini? Kiukweli si sawa na ndiyo maana hata Shehe Alhad alikataa kumpa mkono Tanasha na kuishia kumpungia. “Kwani Tanasha hakujua au hakuambiwa anakwenda kwenye mkusanyiko wa watu wengi wa kada mbalimbali ili ajisitiri? Ona sasa anavyoaibika hata anashindwa kutazama watu kutokana na aibu.

Lakini yote kwa yote, wa kulaumiwa hapa ni Diamond kwani ndiye aliyetakiwa kumpanga mtu wake juu ya namna ya kuvaa kwenye shughuli kama hii. Kiukweli atakuwa amemtibua mno Shehe Alhad”.

alisema mmoja wa wahudhuriaji waliokuwa wamedamshi ile mbaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko juu ya kitendo hicho na kwamba alikichukuliaje, Shehe Alhad alitema nyongo kwa kumvaa Mondi mzimamzima.

Diamond hakufanya kitu kizuri, lakini alitekeleza amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar (Paul Makonda) kujitokeza pale mbele na mwenzake (Tanasha).

Lakini hata mimi nilivyokwenda pale mbele sikupendezwa kumuona huyo mwanamke na ndiyo maana hata hukuniona nikimpa mkono wangu. “Ila niliheshimu kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kumpa mkono Diamond, lakini yeye (Tanasha) sikumpa mkono kwa kuwa nilimuona yupo vile.

Lakini pia Diamond naye anaonesha udhaifu kwa mwanamke kwa kumuacha namna ile kwa sababu mali zako lazima uzione wewe mwenyewe, mwanaume lazima uwe na wivu, haiwezekani unayetarajia kumuoa mwili wake unakuwa wazi ina maana hana thamani. “Diamond anatakiwa kumuongoza yule binti (Tanasha), hakutakiwa kumuacha vile.

 

Dini Yatajwa Kama Kikwazo Cha Ndoa Ya Diamond na Tanasha

Msanii wa Bongo fleva na Mkurugenzi wa WCB Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameshaweka wazi kuwa anataka kumuoa Mpenzi Wake Tanasha Donna Oketh Lakini inadaiwa kikwazo ni tofauti za kidini.

Gazeti la Risasi Jumamosi linaripoti kuwa Diamond  ni Muislam huku Tanasha akiwa ni Mkristo ambapo inaaminika kuwa  lazima mmoja abadili dini kumfuata mwenzake.

Tanasha, akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa mashabiki kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram, alisema kuwa kutokana na mipango ya ndoa inayofuata hawezi kukataa kuhamia Tanzania kwa sababu kwake kwa sasa ni nyumbani kwa pili.

Tanasha alisema kuwa, kuhamia kwake Tanzania haiwezi kuwa shida, lakini kwa suala la dini, hawezi kubadili dini. Tanasha alisema kuwa kila dini imekuwa ikimuamini Mungu mmoja hivyo hakuna sababu ya yeye kubadili dini zaidi ya kila mmoja kuheshimu dini ya mwingine.

Akizungumza na Risasi Jumamosi, mmoja wa wanafamilia ya Mondi aliyefuatilia mjadala huo alisema kuwa, jambo hilo ni kikwazo kikubwa kwani wao kama familia walitarajia Tanasha angebadili dini ili kuungana na Mondi ambaye ni Muislam safi.

Tayari hapo naona kuna shida kubwa. Sisi tulitarajia Tanasha atabadili dini, lakini naona ameanza vikwazo kwa ndugu yetu (Diamond). “Tunachojua ni kwamba, Diamond hawezi kuoa mwanamke ambaye hawatakuwa dini moja”.

Diamond alitangaza kumuoa Tanasha siku ya wapendanao tarehe 14 February Lakini alihairisha harusi hiyo na Mpaka sasa hawajatangaza tarehe mpya ya harusi.

Tanasha Awajibu Wanamkosoa Kisa Gauni Lake

Mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Tanasha Donna Oketh ameibuka na kuwajia juu watu ambao wamekuwa wakimkosoa kisa gauni lake alilovaa siku chache zilizopita.

Wikiendi iliyopita Diamond na Mpenzi Wake Tanasha walihudhuria Hafla ya Haji Manara ambapo alikuwa anazindua foundation yake na kwenye hafla hiyo Tanasha alivaa gauni la Blue ambalo lilimuonyesha sehemu yake ya kifua.

Katika picha ambazo Tanasha alipigwa anaonekana akiwa amevaa nguo iliyomuacha kifua wazi na kupelekea kukosolewa sana jambo ambalo Tanasha ameshindwa kulikalia kimya.

Kupitia Instastory yake Tanasha amewajia juu wanakosoa gauni lake na kusema kuwa lilishonwa dakika za mwisho na pia wanaonekana maziwa yake yamelala Ndiyo hayo hayo ambayo Diamond ameyapenda na yanamdatisha.

 

Diamond Platnumz na Tanasha Wapigana Mabusu Hadharani (video)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna wanaonekana wapo katika mahaba mazito na wanayaonyesha Hadharani.

Tukio hilo limetokea siku chache zilizopita baada ya Diamond na Tanasha kuhudhuria hafla ya Haji Manara ambapo alikuwa anafungua foundation yake na kutambulisha perfume yake rasmi.

Diamond na Tanasha walikuwa miongoni mwa wageni katika Shughuli hiyo ambapo walionekana karibu wakati wote na zaidi walikuwa katika mag a mazito kwani walikuwa wanapeana mabusu hatari.

Hii ni video inayowaonyesha Diamond na Tanasha wakiwa katika mahaba mazito:

 

Tanasha Ana Kila Sifa Ya Kuwa Mke Wangu- Diamond Platnumz

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kumwagia sifa kibao Mpenzi wake ambaye ni mrembo kutoka Mombasa Kenya Tanasha Donna Oketh.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online Diamond amemwagia sifa mke Wake mtarajiwa na kusema mbali na mambo mengine Lakini mrembo huyo anajua sana kupika.

 Ni mwanamke pekee aliyenionesha yupo makini na ana sifa zote za kuingia naye kwenye ndoa na sasa ni rasmi ninatangaza kwamba ninamuoa…

Ana sifa zote ambazo mwanaume yeyote aliyekamilika angetamani awe mkewe. Sisi wanaume tulio wengi huwa tunaangalia shepu, maumbile, mvuto wa nje na mengineyo ambayo yote anayo. Lakini kikubwa zaidi kuliko vyote ni TABIA! Ana tabia nzuri”.

Diamond alitangaza kufunga ndoa na Tanasha muda mfupi tu Baada ya Kukutana ambapo mara ya kwanza ndoa ilitakiwa ifungwe mwezi wa pili katika siku ya wapendanao Lakini imesogezwa mbele.

Queen Darleen Adaiwa Kuchomoa Kwa Tanasha

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’ amedaiwa kuwa hana shobo na Mpenzi mpya wa kaka yake Tanasha Donna.

Wiki iliyopita Diamond alimtambulisha Mpenzi Wake Tanasha kwa Familia yake nzima ambapo alikuwepo Mama Yake, Dada yake Esma na Ndugu wengine Lakini Queen Darleen hakuwepo katika tukio hilo.

Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Queen hakuwepo kwenye ‘mnuso’ huo kwa sababu ‘haziivi’ kivile na Tanasha. “Unajua Queen yeye katika wanawake wote wa Diamond, hakuna mwanamke ambaye anamkubali zaidi kama anavyomkubali Zari.

Yeye chaguo lake ni Zari na si mwanamke mwingine. Ndio maana unaona hana taimu na Tanasha, Esma na mama yake wao hawana shida, wanaunga mkono mwanamke yeyote ambaye Mondi atawatambulisha”.

Baada ya tetesi hizo, Gazeti hilo lilimtafuta Queen Darleen ambaye aliulizwa sababu za kutoonekana na wifi yake kama wanafamilia wengine alijibu:

Queen alianza kwa kuhoji kuna ulazima gani kuwepo

Kwani Tanasha ni mtu wa kawaida tu. “.

 

 

Nampenda Sana Tanasha – Esma Platnumz

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka na kudai kuwa anamkubali sana wifi yake mpya Tanasha kwa muda mfupi ambao amemjua.

Esma ambaye amekutana rasmi na Tanasha siku chache zilizopita amedai kuwa ameshaanza kumpenda ‘kumoyo’ wifi yake mpya Tanasha Donna kiasi cha kujiuliza kwamba, mwana­dada huyo alikuwa wapi siku zote hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Esma alisema amekuwa na ukaribu kwa muda mfupi na wifi yake huyo lakini ametokea kumkubali na sasa ame­kaa kwenye moyo wake tofauti na alivyotarajia mwanzo kwani mtu akiwa mpya kumzoea inahitaji moyo kuridhia.

Huwezi amini Tanasha tayari ameshakaa ndani ya moyo wangu, nampenda sana na kuna muda najiuliza alikuwa wapi muda wote? Kwa nini hakutokea mapema kwenye familia yetu? Hayo mambo ya kuniita Yuda hata siyajali kabisa, wata­jua wenyewe kwani mimi maisha yanasonga”.

Diamond alimtambulisha Tanasha kwa Familia yake aliweka mama yake mzazi Mama Dangote siku chache zilizopita.

 

“Nilikutana na Diamond Club Miaka Miwili Iliyopita”- Tanasha

Mtangazaji na video vixen maarufu kutoka nchini Kenya Tanasha Donna Oketh ambaye pia ni Mpenzi wa  staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amefunguka na kuweka wazi Jinsi walivyokutana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tanasha aliwapa mashabiki zake uhuru wa kumuuliza maswali ambapo alifunguka kwa Kuwapa majibu.

Tanasha aliulizwa ni Jinsi gani alikutana na Mpenzi Wake Diamond na aliweka wazi kuwa walikutana miaka miwili iliyopita walipokuwa Club Lakini hawakuwahi kuongea Mpaka mwaka jana mwishoni.

Nilikutana naye miaka miwili iliyopita klabu Lakini hatukuwahi kuongea mpaka mwaka jana mwishoni”.

Lakini pia Tanasha alianika mapenzi yake kwa Diamond na kusema wazi wazi kuwa anampenda sana Diamond na pia kusema ana sifa zote za mwanaume ambaye angependa kuwa naye yaani ni muaminifu, mchapakazi, ana Upendo na sifa nyingine kedekede.

Diamond Amtambulisha Tanasha Kwa Mama Yake Mzazi

Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha kuwa Penzi lake na Tanasha ni la kweli Baada ya kumtambulisha rasmi kwa Familia yake.

Kwenye utambulisho huo, Diamond aliwaalika pia ndugu, jamaa na marafiki zake. tukio lilifanyika nyumbani kwake Madale.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameweka video hizi zinazoonyesha tukio zima:

https://www.instagram.com/p/BslCce6FkDy/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=uhtfhnvhmvrk

 

https://www.instagram.com/p/BslGUDJhTCk/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=uucpxgp4ofnr

Kim Nana Amwaga Povu Kisa Penzi la Diamond na Tanasha

Video vixen na mwanamitindo Lilian Kessy  maarufu kama Kim Nana amejikuta akimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu Ex Wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi Wake Mpya Tanasha Donna Oketh.

Kim Nana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Diamond kwa muda kabla ya kumwagwa chini miezi michache iliyopita na Diamond kuanza mahusiano na Tanasha.

Kim Nana ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la Diamond na Tanasha baada ya Gazeti la Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha.

Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.

 Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?”.

Diamond Abadili Tarehe Ya Ndoa Yake na Tanasha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amesogeza mbele tarehe ya ndoa yake na Mpenzi Wake Mkenya Tanasha Donna.

Siku chache Baada ya kuweka hadharani mapenzi yake Man mrembo Tanasha Diamond alitangaza nia yake ya kumuoa binti huyo na kusema ndoa yao ingekuwa tarehe 14 mwezi wa pili siku ya Wapendanao duniani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Wasafi Tv, Diamond amesema kuwa tarehe waliyopanga awali kwa ajili ya ndoa wameisogeza mbele kutokana anataka harusi yake iwe nzuri na kuhudhuriwa na watu wengi.

Ndoa yangu ilitakiwa iwe siku ya Valentine tarehe 14 lakini tumeipeleka mbele. Watu wengi wanatakiwa kuja kuhudhuria kwa sababu ndoa yangu watakuja kina Rick Ross”.

Mara ya kwanza Diamond alipotangaza kumuoa Tanasha Siku ya wapendanao mwaka huu ilivutia watu wengi kwani siku ya wapendanao mwaka jana Diamond aliingia kwenye headlines baada ya aliyekuwa Mpenzi Wake Zari kumtosa kwa ya Jeusi Kupitia ukurasa wake wa Instagram.