“Diamond Anapendeza na Tanasha Zaidi”- Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwamwagia sifa kibao staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi wake Tanasha Donna.

Siku za nyuma Shilole hakuficha hisia zake za Jinsi gani alikuwa anamkubali Mama Watoto wa Diamond, Zari na hata kumuomba Diamond arudiane naye Baada ya kuachana.

Lakini Hivi sasa Zari anaoenekana kumsahau Zari na kuhamisha majeshi yake kwa wifi yake Mpya Tanasha kwani ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa kibao mrembo huyo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Shilole ameweka wazi kuwa Tanasha anapendezana na Diamond na hata kudai tangu amekuwa naye amekuwa akipendeza zaidi hasa Baada ya kunyoa.

Diamond na Tanasha wanapendezana sana, siku hizi naona hata Diamond ananyoa vizuri kusema Ukweli wapo kizazi sana”.

Stori za chini chini zinadai kuwa Shilole alikoromewa na Diamond Baada ya kumtaka arudiane na Zari kwenye mkutano na waandishi wa habari Wiki chache zilizopita.

Shilole Awataka Wasanii Waache Unafiki Wa Kusapotiana Baada Ya Kifo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwajia juu wasanii ambao wameonekana kusapoti na kulilia wasanii wenzao Baada ya kifo.

Siku ya jana Msanii wa muziki wa hip hop nchini Godzillah alifariki dunia Baada ya kuugua ghafla nyumbani kwake Salasala. Wasanii mbali mbali walijitokeza kutoa pole na hata kumposti katika kurasa zao ya Mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Shilole amewajia juu baadhi ya wasanii ambao amediriki kuwaita wanafki na kudai wamejitokeza Baada ya kifo chake na kuanza kumposti na kudai wameguswa wakati kwenye uhai wake hakuna hata mmoja aliyeposti kazi zake.

Mimi naona ni vizuri mtu akapewa heshima yake wakati yuko hai ili aone kama kuna watu wanampenda na kumjali sasa Leo hii amekufa ndio anapewa hio sapoti anajuaje sasa? 

Wakati yupo hai anatoa nyimbo hamposti wengine Mpaka wanatumia ngoma zake kama cover lakini bado hawamposti wala kumpa heshima yake kama legendari Ndio maana  mimi kila siku nasema wasanii tuache unafiki wengi watu ni wanafiki sana”.

 

Shilole Awatolea Uvivu Wasanii Ambao Hawamuungi Mkono Raisi

Mwanamuziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amewajia Juu wasanii wenzake ambao hawakujitokeza kumuunga mkono Raisi katika uzinduzi wa treni mpya leo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na waandishi wa habari siku ya jana kwenye tukio la wasanii kutembelea mradi wa SGR, amesema kuwa wasanii wawe kitu kimoja kwa kumsapoti Rais Magufuli kwa vitu anavyovifanya.

Unajua unavyojichanganya na wenzio ndio unavyopata connections. Mtu ambaye anaitwa na kiongozi wako halafu hautii, hiyo sio heshima, it means huwezi kuheshimu wazazi wako. Unajua unavyoitwa na Rais huwezi jua anakuitia nini?je, akikuteua kuwa mkuu wa mkoa, au mkuu wa Wilaya utakataa”.

Lakini pia Shilole amemtumia maombi Raisi ili aweze kumpa tenda ya kwenda kuuza chakula:

Kwanza nataka nimuombe ombi Mhe. Rais Magufuli, nataka aniruhusu niuze chakula kwenye Treni itakapoanza kazi, mimi sitaki hela nataka tu anipe nafasi hiyo basi“.

Shilole Awachana Watu Wanao ‘Fake’ Maisha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema kuwa hakuna kitu kinamchukiza kama watu wanaopenda kudanganya kuhusu maisha yao.

Shilole amefunguka hayo kwenye mahojiano na kipindi cha ‘Uhondo’ cha EFM ambapo amewataka watu kuwa wakweli kuhusu maisha yao na sio kudanganya wengine kama wana maisha mazuri wakati ni uongo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/Btin7GvB5ie/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=x6kg9xerd025

Shilole Amtema Zari na Kumkubali Tanasha

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amedaiwa kumsaliti na kumwaga Zari na kumkubali zaidi Mpenzi Mpya wa Diamond Tanasha.

Kama utakumbuka siku mbili zilizopita Shilole alisimama mbele ya waandishi wa habari na kumuomba Diamond aachane na Tanasha na kumuoa mama Watoto Wake Zari.

Lakini sasa Shilole ameonekana kukubaliana na hali halisi na kumkubali Tanasha kama wifi yake mpya na kusema wazi kuwa anapopenda Diamond basi na yeye hana budi kufuata.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole ameandika maneno haya:

ANAPOPENDA KAKA YANGU SINA JINSI! HI TANASHA, DIAMOND PLATNUMZ WIFI YETU KARIBU DADA HII NDO TANZANIA NITAFANYAJE SASA JAMANI”.

Ni takribani mwaka mmoja tangu Diamond kuachana na Zari na kuanzisha mahusiano mapya na mrembo Natasha kutoka nchini Kenya. Hivi karibuni Diamond Platnumz alikaririwa na kituo hicho cha runinga akieleza kuwa ndoa yake aliyopanga kuifunga mwezi wa pili mwaka huu ameisogeza mbele.

Shilole Amlilia Diamond Amuoe Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na mapya Baada ya kumuomba Diamond amuoe Zari.

Tukio hilo lilitokea siku ya Leo katika viwanja vya Leaders Club ambapo RC Makonda alikuwa anaongea na wasanii ndipo Shilole alipoibuka na ombi lake hilo.

Shilole alimuomba Diamond arudiane na mama Watoto Wake Zarinah Hassan ambaye waliachana mwaka jana na kumtaka amuoe kabisa kwani Ndiye mwanamke anayefaa kuwa mke wake .

Tazama Video hii kwa taarifa zaidi:

 

Shilole- Sijapendezwa na Kitendo Cha Uwoya na Dogo Janja Kuachana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefungukia taarufa za Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja na mke Wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya kuachana.

Baada ya Uwoya na Dogo Janja kufunga ndoa iliyozungukwa na utata mwaka juzi na kuachana mwaka jana mwishoni hatimaye wawili hao walithibitisha kuachana siku chache zilizopita Baada ya kurushiana maneno ya kejeli kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Shilole amefunguka na kuweka wazi masikitiko yake Baada ya kusikia wanandoa hao wameachana ambao pia walihudhuria harusi yake na Uchebe:

Mimi kusema ukweli sijisikii vizuri kabisa kusikia kuwa wameachana hasa kwa sababu haya dini hairuhusu kuachana labda pale inapobidi sanaa Lakini pia huwezi kuingilia maamuzi ya watu.

Unajua kwenye ndoa kuna mengi Mimi na wewe hatuji Lakini wao waliopo humo ndani ndio wanajua nini kinaendelea kwaiyo ni vyema mara nyingi kuwaacha wao wenyewe wanandoa waamue wanachoamua”.

 

 

Idris Sultan Amwagia Misifa Kibao Shilole

Mchekeshaji na msanii wa Bongo movie Idris Sultan ameibuka na kumwagia sifa kibao Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole.

Siku ya jana ilikuwa ni siku ambayo Shilole alikuwa a ashehereka siku yake ya kuzaliwa na mastaa mbali mbali walimposti katika kurasa zao kwenye mitandao ya kijamii.

Mmoja wapo ni Idris Sultan ambaye alimposti na kumuandikia ujumbe mzito ambapo ndani ya ujumbe huo alindika ni Jinsi gani msanii huyo ni mchapakazi na anajituma tofauti na mastaa wengine.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris Sultan aliweka picha ya Shilole na kuandika ujumbe huu kumlenga Shilole:

Ana Nyumba, ana biashara zaidi ya tatu, ana watoto, ameolewa na ni maarufu na bado ana baby face, Mimi Nina kingereza tu. Tuendelee kuendekeza ujinga tutajua nani anamcheka mwenzake”.

Mbali tu kuwa msanii wa Bongo fleva na Bongo movie, Shilole pia ni mjasiriamali ambaye ni ana mgahawa wake anapouzia chakula pia anamiliki bidhaa zake mwenyewe kama vile Chili na nyinginezo.

Shilole Athibitisha Kuhamia Kwenye Mjengo Wake Wa Thamani

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa amehamia kwenye mjengo wake mpya uliopo Majohe jijini Dar-Es-Salaam.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Shilole alisema kuwa anashukuru Mungu kuona baadhi ya mipango yake kwa mwaka huu ikitimia ikiwa ni pamoja na kuhamia kwenye nyumba hiyo ya kisasa.

Katika interview hiyo Shilole alitakiwa kumtaka thamani ya Nyumba lakini alishikwa na kigugumizi na kusema hapendi kuweka wazi hilo.

Kikubwa ni kwamba nakaa kwenye nyumba yangu, hilo ndilo la kumshukuru Mungu, ukiniuliza nimetumia kiasi gani siwezi kukujibu kwa haraka kwa kuwa kama unavyojua pesa zetu za mawazo na nilikuwa nahanga ikanikipata kidogo naweka mpaka nilivyofika hapa“.

 

Shilole Afungukia Mipango Ya Kuzaa na Uchebe

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuwajibu watu ambao wamekuwa wakimteta kwa kuchelewa kwake kumzalia mtoto mumewe Uchebe waliyefunga ndoa mwaka jana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Shilole amefunguka kuwa kushika ujauzito na kujifungua salama ni mipango ya Mwenyezi Mungu, hivyo hana haraka na hilo, kwani anaamini ni muda tu haujafika. ya Mwenyezi Mungu, hivyo hana haraka na hilo, kwani anaamini ni muda tu haujafika.

Nadhani kila kitu ni mipango ya Mungu, wakati ukifika kila kitu kitakuwa hadharani, kwani mimba ni pembe la ng’ombe halifichiki, alisema, Shilole“.

Shilole ameweka wazi kuwa kwa Hivi sasa yuko bize na shughuli zake za ujasiriamali, lakini wakati huo huo akiwa anaihudumia familia yake kama ilivyo kwa wanawake wengine.

Shilole Aweka Wazi Siri Ya Mafanikio Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi Siri iliyompa mafanikio makubwa.

Mbali tu ya kuwa msanii wa Bongo fleva na kutoa nyimbo kali kama Chuna Buzi, Nyang’anyang’a, Kigori, Hatutoi Kiki, Malele, Nakomaa na Jiji, Say My Name, Paka la Baa na nyinginezo Lakini pia Shilole ni mjasiriamali.

Shilole ambaye alianza safari yake ya Sanaa kwenye kuigiza filamu za Kibongo na kutoa kazi kali kama vile Fair Decision’, ‘Crazy Of Love’, ‘Pigo’, ‘Bed Rest’, ‘Cut Off’ na nyinginezo Lakini pia Shilole anamiliki mgahawa unaoitwa Shishifood.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shilole amefunguka kuhusu kufungua kampuni yake ya Shilole Entertainment:

Nilianza biashara zangu na mtaji wa shilingi 50,000 tu mpaka hapa mnaponiona nimefikia kwa sasa, japo haikuwa rahisi kama mnavyodhani kwa sababu walikuwepo walionisema vibaya kwamba sitafika popote, wakunikatisha tamaa walikuwa wengi lakini namshukuru Mungu kwa kuwa maneno yao hayakufanikiwa.

Nilihakikisha napambana kadri niwezavyo ili nifikie malengo yangu, nashukuru leo hii wote waliokuwa wananisema vibaya wanayaona mafanikio”.

Lakini pia Shilole alizidi kufunguka zaidi na kuanika Siri ya mafanikio yake:

Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na biashara zangu, nikiendesha maisha yangu bila kumtegemea mtu yeyote, hivyo nawashauri na wengine ambao wana ndoto yakuja kuwa wajasiriamli wakubwa, kwanza kabisa wasikate tamaa waamini katika malengo yao na pia waanze biashara na kidogo walichonacho siyo mpaka wawe na mtaji mkubwa mwisho wa siku watayaona mafanikio”.

 

Shilole Awatahadharisha Watu Wanaomuiga Biashara Zake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwataka somo kali mastaa wenzake ambao wamekuwa wakijiingiza katika biashara za kupika.

Shilole ni mmoja kati ya wasanii ambaye pamoja kuimba Lakini pia ni mjasiriamali kwani anamiliki mgahawa unaojulikana kama Shishi Food ambao unafanya vizuri sana hapa mjini.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Amani, Shilole alisema anafurahi kuona kile alichoanzisha kinaigwa na wasanii wenzake wengi ila tahadhari ni kwamba wanatakiwa kukomaa sana kwani vitu vya kuiga bila kuwa na misingi imara watashindwa.

Ni sawa wameniiga wengi lakini wanatakiwa kuwa na misingi imara vinginevyo wataanguka, nimekuwa mfano wa kuigwa kwa sababu mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuanzisha mama lishe kwa kufungua mgahawa ndiyo wengine wakafuata hivyo watambue kuwa aliyeanza kaanza tu, niko kwenye biashara hii kwa miaka mitatu sasa hivyo naamini hakuna wa kunishinda“.

Mastaa wambao pia wanatajwa kuanzisha biashara ya mgahawa Baada ya Shilole ni pamoja na msanii wa Bongo movie Esha Buheti.

Povu la Shilole Kwa Media Zinazompa Kiki Lynn

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ametoa Povu zito kwa media ambazo amedai zimekuwa zikitoa Kiki za bure kwa watu ambao hawana vipaji na sio wasanii.

Watu wengi wamekuwa wakihoji kuhusiana na mafanikio ya ghafla na umaarufu wa video vixen Irene Hillary maarufu kama Lynn huku wengi wakitaka kujua ni kazi gani hasa anazifanya na kumpatia pesa alizonazo pamoja na mali.

Shilole ameamua kufunguka kuhusiana na media zinazompa air time officiallynn na kuuliza wadau ni kitu gani hasa amekifanya kwenye jamii mpaka kinawafanya wampe nafasi sana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Shilole alimwaga Povu hilo na kuandika:

Tuseme ukweli huyu dada anafanya kitu gani mpaka mwandishi aseme anatreand je anafanya movie ni mwanamuzik na amefanya nini ktk jamii ? Jamani waandishi wa habari kuweni makini ndio maana mnatuletea mambo ya akina Amber Rutty”.

Watakuja kuchafua sanaa yetu tuonekane wote wapumbavu kwa ajili ya mtu mmoja anapewa promo ya kijinga ili wapate habari Alafu wanaweka YouTube bila kujali mnazalilisha tasnia yetu wandishi wengine shame on you”.

Lynn alijizolea umaarufu Baada ya mahusiano na Diamond Platnumz ambapo miezi michache iliyopita Msanii huyo alimnunulia mrembo huyo gari kwenye birthday yake.

 

Shilole Afungukia Mkosi Wa Nyumba Yake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kuweka wazi kuwa baada ya kuhamia kwenye mjengo wake mpya lakini amekiri kukaribishwa na mkosi.

Global Publishers wanaripoti kuwa Shilole alitokelezea kwenye uzinduzi wa Albamu ya Nandy lakini Ghafla aliibua minong’ono Baada ya kuonekana na nundu usoni hali iiyopelekea watu kudhani huenda Mumewe Uchebe amemtembezea kichapo.

Katika mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda Shilole alifunguka na kusema:

Aaa…Unajua juzijuzi ndiyo nimehamia nyumbani kwangu Majohe, sasa nyumba yenyewe bado sijaizoea na bado sijaweka umeme, sasa niliporudi usiku nikiwa nimechoka ndiyo nikajikuta napiga mwereka na kuumia hivi.

Si unajua nyumba usiyoizoea? Hayo ndiyo yaliyonikuta na hii pati kwa kuwa nilishaalikwa na kumhakikishia Nandy kuwa nitakuwepo, nimeona nijikongoje nifike haina jinsi”.

Miezi michache iliyopita Shilole alianika mjengo Wake mpya alioujenga kwa kutumia pesa aliyopata kupitia Sanaa na biashara zake.

 

Gigy Money Amuomba Msamaha Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameibuka na kumuomba msamaha Msanii mwenzake Shilole baada ya bifu la muda mrefu.

Bifu la Shilole na Gigy Money liliwahi kutawala vichwa vya habari siku za nyuma ambapo Gigy Money alimtolea povu Shilole na kuponda muziki wake na kudai hajui kuimba Lakini pia aliponda kingereza chake anachoongea.

Lakini baada ya miaka kadhaa kupita tangu sakata hilo hatimaye Gigy Money amemuomba radhi Shilole Kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo amemshukuru kwa mchango wake na kumpa ushauri wa kumlea mtoto wake kama mama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy Money ameandika:

Miaka michache nyuma mimi nilikuwa namuongelea vibaya shishi bila kujali ni mama au ana mawazo gani kwa wakati ule basi leo nachukua nafasi hii kumwambia samahani Dada Shilole kwani sikua najua kama na mimi ntakuwa mama au nilikuwa najiona keki kumbe maandazi”.

Hivi sasa Gigy Money ni mama wa mtoto mmoja wa kike anayeitwa Mayra aliyezaa na aliyekuwa mpenzi wake Mo J.

Shilole Alamba Dili Nono CRDB

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amelamba Shavu jingine nono Kwenye Kampuni ya CRDB.

Shilole amelamba Dili la ubalozi wa bidhaa mpya kutoka CRDB iitwayo, Sim Account. Kwa sasa watumiaji mbalimbali wa huduma hiyo ya ‘Sim Account’ ya wanajishindia mamilioni ya pesa kupitia promotion mpya ya ‘Shinda na Sim Account’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 mara baada ya kutangazwa balozi Shilole amefunguka haya:

Nimefurahi sana kuwa balozi wa Sim Account kwa sababu ni huduma ambayo anaona kabisa inaenda kurahisisha maisha wa watu wa chini, wanavikoba wenzangu, ukitaka kulipa kitu ni rahisi sana na ni huduma ambayo hata mimi mwenyewe nikikaa mbele ya watu wanaweza kujivunia nayo. Kwahiyo nimeaambie tu Watanzania wenzangu na mashabiki wa Shishi, huu ni muda wa kuanza kwenda kidigitali zaidi.

Kwenye biashara yangu ya Shishi Trump Food wateja hawatapata tabu kabisa, ishu za chenji zilikuwa zinasumbua sana lakini sasa hivi kwa Sim Account unaweza kulipa kile unachodaiwa bila usumbufu wa chenji. Pia Sim Account inahuduma mbalimbali ndani yake kama zakulipa bili, wale wenzangu wa vikoba, yaani ni kitu ambacho ukiwa nacho hautapata tabu kabisa kwenye ishu za manunuzi”.

Mwaka huu umezidi kuwa mzuri kwake kwani ameongeza ubalozi mwingine wa CRDB kwani tayari ni Balozi wa kampuni ya simu ya TTCL na British council.