Diamond Azidi Kuzua Gumzo Baada Ya Kuishia Nje Kwenye Kuaga Mwili Wa Ruge

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amezidi kukamata headlines kwa matukio ambayo amekuwa akiyafanya ikiwemo Sakata la kuishia nje ya ukumbi wa Karimjee siku ya kuaga mwili.

Maulidi Kitenge mtangazaji wa EFM, leo amezua gumzo mitandaoni kwa kudai kwamba muimbaji huyo alizuiliwa kuingia ndani kwa madai kwamba alichelewa pamoja na kuwa na kundi kubwa la watu.

https://www.instagram.com/p/BukuRa2hmYS/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1gcr1w2aypwa1

Ujumbe huyo wa mtangazaji huyo hodari wa michezo kutoka EFM, umezua gumzo mitandaoni huku kila mmoja akiwa na maoni yake kuhusiana na sakata hilo la aina yake.

Mengi yalizungumzwa kuhusu uhusiano wa Diamond na Marehemu ikiwemo Bifu lao enzi za uhai Wake ambapo ilisemekana Msanii huyo asingeweza kuhudhuria msiba huo.

Babu Tale Amjia Juu Mrisho Mpoto Kisa Diamond

Meneja wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amejikuta akimtolea Povu zito Msanii wa muziki Mrisho Mpoto Baada ya Msanii huyo kuhudhuria msiba wa Ruge Mutahaba.

Siku chache zilizopita Mrisho Mpoto alimtaka Diamond aweke tofauti zake pembeni na Marehemu Ruge na ahudhurie msiba Wake na Kupitia ukurasa wake wa Instagram, alimuandikia ujumbe mzito.

Siku ya jumamosi Ruge aliagwa na wasanii Mbali Mbali na viongozi wa serikali katika viwanja vya Karimjee Hall na Diamond na timu yake ya WCB walihudhuria hafla hiyo.

Baada ya Diamond kuhudhuria hafla hiyo Mrisho Mpoto alitumia ukurasa wake wa Instagram kumshukuru Diamond kwa kuenda kauli iliyomkera Babu Tale ambapo alimjia juu Diamond na kusema kuwa hakuenda kwenye msiba kwa sababu yeye alimwambia.

Harmonize Adai Kuwa Yeye na Diamond Wanamiliki Hisa Sawa Sawa

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Harmonize amefunguka na kuweka wazi yeye na Bosi wake  Diamond Platnumz wanamiliki hisa pasu kwa pasu kwenye kampuni ya Zoom Production.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha redio cha A FM cha jijini Dodoma, Harmonize ameanika ukweli ambapo amesema kuwa wote wawili wamegawana hisa sawa kwa sawa.

Wazo la kuanzisha Production company ni langu na nilipolipata nilienda Africa ya kusini na Marekani kununua kamera na baadae nikaja kusambaa Diamond, Bro! mimi naona tunapoteza hela nyingi sana kwenye video, mimi nimepata wazo la kuanzisha kampuni ya Video Productions wewe unaonaje?“

Harmonize amesema Diamond akakubali wazo hilo na kwa kuwa alikuwa ameshanunua kila kitu alivyorudi Bongo alimrudishia nusu ya manunuzi na kwa muda huo anasema kuwa alikuwa ameshmtafuta Director Kenny.

Zoom Production ni moja ya kampuni zinazofanya vyema kwenye ulimwengu wa Burudani na haimilikiwi na Diamond pekee ilivyoaminika hapo awali bali na Harmonize pia ana mkono mule.

Baba Diamond Kukatwa Miguu Kutokana na Kansa Ya Ngozi

Baba mzazi wa staa wa Bongo fleva Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amedaiwa kuwa katika hai mbaya itakayompelekea kukatwa miguu katika siku za usoni.

Baada ya kujionea baba Dia­mond akiwa anasumbuliwa na tatizo la kansa ya ngozi, Gazeti la Ijumaa Wikienda lilimpigia simu dak­tari Godfrey Charle wa jijini Dar alipoelezwa kuhusu tatizo hilo, alisema kuna mambo ya kufanya ili kumnusuru kwani tofauti na hapo basi huenda akalazimika kukatwa miguu.

Kwa baba Diamond sambam­ba na kutibiwa kansa anatakiwa atibiwe pia maambukizi mbalim­bali yanayojitokeza kwani hayo ndiyo yanasababisha mgonjwa kukatwa mguu au kiungo chochote kilichoathirika na siyo kansa.

Kwa kweli kwa hatua ile aliy­ofikia kupona kwake ni asilimia 50 tena kwa msaada wa ndugu yaani kama ndugu zake watam­saidia katika matibabu hivyo inategemea na msaada ataka­opata lakini vinginevyo asipopata msaada wa matibabu tena kwa haraka anaweza kukatwa miguu“.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Baba Diamond alisema amepitia changamoto za muda mrefu kwa kusumbuliwa na miguu hiyo bila kupata matibabu hivyo ilifika wakati alikata tamaa ya maisha kabisa.

Kwa kweli miguu hii imen­isumbua kwa muda mrefu sana. Nimehangaika katika hospitali nyingi tu lakini kwa kweli nimeshindwa kujitibia kutokana na gharama kuwa kubwa”.

Baba Diamond alipoulizwa kama ame­shamwambia mwanaye amsai­die, baba Diamond hakutaka kumzungumzia lakini akasema anaamini kama ni tatizo hilo, Diamond atakuwa analifahamu vizuri maana lina muda mrefu.

Siwezi kumzungumzia sana lakini kikubwa mimi kwa sasa namshukuru Mungu kanikutani­sha na dada kutoka Uingereza anaitwa Zubeda Humphries ambaye amekuja na kuahidi kunisaidia ili niweze kutibiwa”.

 

 

Harmonize Kuja na ‘EP’ Aliyowashirikisha Diamond na BurnaBoy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema chini ya Label ya WCB Harmonize ameweka wazi ujio wa ‘EP’ yake ambayo itakwenda kwa jina la ‘Afro Bongo’.

EP (Extended Playlist) inategemewa Kubeba jumla ya nyimbo 4 na nyimbo hizo nne zitatolewa kwa Mpigo na itawashurikisha wasanii Kama Diamond Platnumz na BurnBoy wa nchini Nigeria.

https://www.instagram.com/p/BuDqYQ-nYJT/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1b911qv81c77n

Lakini pia Harmonize ameweka wazi kuw wasanii ambao watasikika katika EP hiyo ni pamoja na Mr. Eazi, Yemi Alade na Mpenzi Wake Sarah.

https://www.instagram.com/p/Bt_nrHcnuHw/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=ok4sqy5qjy8y

 

Lemutuz Aingilia Kati Sakata la Diamond na Baba yake

Moja ya watu maarufu katika mitandao ya kijamii Lemutuz amefunguka na kuingilia kati sakata la Diamond na baba yake ambalo linandelea katika mitandao ya kijamii , huku watu wengi wakimshambulia msanii huyo kwanini hataki kumsaidia baba yae ambae ni mgonjwa .

Lemutuz anasema kuwa watu wanatakiwa kujua kuwa Diamond ni mtu mzima hivyo anajua kile anachokifanya kwa sasa na kikubwa zaidi kutoa msamaha ni uamuzi wa mtu sio kulazimishwa.

Lemutuz anasema kuwa pamoja na yote , alichokosea baba wa diamond ni kuleta maswala ya kifamilia katika mitandao ya kijamii kwa sababu walitakiwa kukaa chini kama familia na sio kwenda katika mitandao.

Ikumbukwe kuwa baba huyo kwa sasa ni mgonjwa kitandani akisumbuliwa na vidonda miguuni,lakini pia wiki iliyopita dada mkubwa wa msanii Diamond alikuja akitokea nje ya nchi kwa ajili ya kumsaidia baba yake lakini pia kufanya usuluhisho wa matatizo yake.

 

Mange Kimambi Amlilia Diamond Amsamehe Baba Yake

Mange Kimambi amemuandikia ujumbe wa wazi staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuhusu kumsaidia baba yake mzazi Mzee Abdul Juma ambaye anatajwa kuwa mgonjwa.

Kwa muda mrefu kumekuwa na Ugomvi wa kifamilia kati ya Diamond na baba yake ambapo amewahi kuweka wazi kuwa hajalelewa na baba yake bali na Mama yake ambaye ndiye anayemjali.

Wiki iliyopita Baba yake na Diamond aliweka wazi kuwa anaumwa na anasumbuliwa na maradhi mbali mbali ikiwemo miguu ambayo ipo katika hali mbaya na kumlilia mwanaye amsaidie japo akapate matibabu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuomba Diamond aweke tofauti zao pembeni na amsaidie baba yake ambaye yupo katika hali mbaya:

https://www.instagram.com/p/Bt-nyKVBEgD/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=tevtyrdp2c9w

Dada wa Diamond Amtaka Diamond Amsaidie Baba Yao Maana Ana Hali Mbaya

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kama Dada yake na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, anayejulikana kwa jina la Zubeda amempigia magoti Diamond amsaidie baba yake ambaye anaumwa hoi.

Dada huyo ambaye wakati akiwasili nchini alipokelewa na Baba mzazi wa Diamond, mzee Abdul Juma, amesema hajui kipi kibaya ambacho baba alimkosea Diamond hadi kufika hatua ya kuwa mbali naye na kutomsaidia ilihali ni mgonjwa sana akisumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba kwa muda mrefu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Zubeda amemtaka Diamond akubali kuonana naye ili waongee na amwambie kwanini amemtelekeza baba yake kwani ni mgonjwa sana na anahitaji msaada wa hali na Mali.

Nimetoka London nimekuja Tanzania kuonana na Diamond na kumuuliza Mzee Abdul amemfanya nini Mpaka hutaki kumuona wala kumsaidia Baba yake kwani kiukweli Baba yake anaumwa sana anahitaji msaada”.

Lakini pia Mwanamama huyo amesema kuwa yupo tayari kusaidia kumaliza tofauti zilizopo kati ya Diamond na Baba yake.

Kevin Gates Awakubali Diamond Platnumz na Rayvanny

Msanii wa muziki wa Hip hop kutoka pande za Marekani Kevin Gates ameonekana kuikubali nyimbo mpya ya Rayvanny na Diamond Platnumz Baada ya kuonekana akiwa anaisikiliza.

Kevin Gates ambaye alishawahi kutamba na ngoma kibao ikiwemo ‘Out The Mud’ ameposti kipande cha video kwenye ukurasa wake wa Instagram, akisikiliza ngoma ya Tetema.

Tetema imeendelea kuvunja rekodi kuanzia kuwa nyimbo ya kwanza Tanzania kutazamwa mara milioni moja ndani ya mastaa 17 Mpaka kufikisha watazamaji milioni 3 ndani ya siku tatu.

 

Tetema Ya Diamond na Rayvanny Yavunja Rekodi

Wimbo mpya unaofanya vizuri Hivi sasa ‘Tetema’ ulioimbwa na wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny umevunja rekodi Mpya Baada ya kufikisha watazamaji milioni moja ndani ya mastaa 17.

Wanamuziki Diamond Platnumz na  Alikiba ni baadhi ya waliofanikiwa nyimbo zao kutazamwa mara milioni moja kwa muda wa masaa 24.  Mpaka wakati huu wimbo huo umetazamwa mara milioni 1.2.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond ameshukuru mashabiki zake kwa kuangalia wimbo huo mara milioni moja:

“Siwezi Kutoka WCB, Diamond Ni Mtu Mmoja Poa Sana”-Mose Iyobo

Dansa maarufu kutoka WCB ambaye anafanya kazi kwa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa muda mrefu, Mose Iyobo ameibuka na kudai kuwa bosi wake  huyo ni mtu poa sana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Mose Iyobo amefunguka na kusema Bosi Wake Diamond ni mtu poa sana na ni bosi mzuri kufanya naye kazi.

Diamond ni mtu fulani ambaye yupo poa sana yaani Siwezi kusema nitoke pale (WCB) eti niende sehemu nyingine! Labda nikafungue kitu changu mwenyewe”.

Lakini pia Mose Iyobo ametupilia mbali Tetesi Za kuwa analelewa na mzazi mwenzake Aunty Ezekiel na kudai anatengeneza hela nzuri tu kama Dansa wa Diamond hivyo hahitaji kulelewa.

Nalelewaje wakati nafanya kazi kwa Diamond? Nikimwambia Diamond nataka gari Fulani yaani inachukua dakika chache tu”.

 

 

Mume Wa Mama Diamond Afunguka Mazito

Mume wa mama Mzazi wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Mama Dangote amefunguka mazito kuhusu mke Wake na kuamua kuyaanika hadharani kabisa.

Mume wa Mama Diamond anayejulikana Kama Maisara Shamte ameibuka na kumfungukia mazito mke Wake Mama Diamond.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shamte amefunguka na kueleza Jinsi gani anavyompenda bibi huyo wa wajukuu watano na kusema amemchaganya Mpaka anataka kulipa tena mahari:

Yaani kuna wakati nakuangalia Mama Dangote halafu nasema mbona mahari nimelipa kidogo halafu nimeishia kupata kitu kikubwa sana basi naishia tu kusema Asante Mungu, Yaani Ikifika asubuhi natamani kukuamsha uende shule kwa Jinsi ulivyofanana na vitoto vya shule “.

 

Shilole Amlilia Diamond Amuoe Zari

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na mapya Baada ya kumuomba Diamond amuoe Zari.

Tukio hilo lilitokea siku ya Leo katika viwanja vya Leaders Club ambapo RC Makonda alikuwa anaongea na wasanii ndipo Shilole alipoibuka na ombi lake hilo.

Shilole alimuomba Diamond arudiane na mama Watoto Wake Zarinah Hassan ambaye waliachana mwaka jana na kumtaka amuoe kabisa kwani Ndiye mwanamke anayefaa kuwa mke wake .

Tazama Video hii kwa taarifa zaidi:

 

Shekhe Amjia Juu Diamond Kwa Mavazi Ya Tanasha

Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Amemjia juu  mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa mavazi ya mpenzi wake Tanasha.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa Tanasha alizua gumzo wiki iliyopita Baada ya kuonekana akiwa amevaa gauni ambalo liliweka sehemu kubwa ya maungo yake nje jambo ambalo pia limeonekana kumkereketa Shehe mkuu.

Jamani…jamani…ndiyo nguo gani ile mbele ya kiongozi wa dini? Kiukweli si sawa na ndiyo maana hata Shehe Alhad alikataa kumpa mkono Tanasha na kuishia kumpungia. “Kwani Tanasha hakujua au hakuambiwa anakwenda kwenye mkusanyiko wa watu wengi wa kada mbalimbali ili ajisitiri? Ona sasa anavyoaibika hata anashindwa kutazama watu kutokana na aibu.

Lakini yote kwa yote, wa kulaumiwa hapa ni Diamond kwani ndiye aliyetakiwa kumpanga mtu wake juu ya namna ya kuvaa kwenye shughuli kama hii. Kiukweli atakuwa amemtibua mno Shehe Alhad”.

alisema mmoja wa wahudhuriaji waliokuwa wamedamshi ile mbaya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko juu ya kitendo hicho na kwamba alikichukuliaje, Shehe Alhad alitema nyongo kwa kumvaa Mondi mzimamzima.

Diamond hakufanya kitu kizuri, lakini alitekeleza amri ya Mkuu wa Mkoa wa Dar (Paul Makonda) kujitokeza pale mbele na mwenzake (Tanasha).

Lakini hata mimi nilivyokwenda pale mbele sikupendezwa kumuona huyo mwanamke na ndiyo maana hata hukuniona nikimpa mkono wangu. “Ila niliheshimu kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa kumpa mkono Diamond, lakini yeye (Tanasha) sikumpa mkono kwa kuwa nilimuona yupo vile.

Lakini pia Diamond naye anaonesha udhaifu kwa mwanamke kwa kumuacha namna ile kwa sababu mali zako lazima uzione wewe mwenyewe, mwanaume lazima uwe na wivu, haiwezekani unayetarajia kumuoa mwili wake unakuwa wazi ina maana hana thamani. “Diamond anatakiwa kumuongoza yule binti (Tanasha), hakutakiwa kumuacha vile.

 

Wema na Diamond Uso Kwa Uso Waishia Kukumbatiana (video)

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amekutana uso kwa uso na aliyekuwa Mpenzi Wake Wema Sepetu katika mkutano siku ya jana.

Diamond alikutana na Wema uso kwa uso katika mkutano uliofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda wakati anaongea na wasanii Mbali Mbali.

Diamond alionekana akisalimiana na Wema kwa Kumkumbatia kamaalivyo wakumbatia wasanii wengine mbali mbali waliokuwa katika ukumbi huo.

Kama utakumbuka mara ya mwisho Wema na Diamond walipoonekana wanakumbatiana mbele ya hadhara Zari alithibitisha kuwa Wema bado alikuwa anatembea na Mondi na hata kumtuhumu kwa kuvunja mahusiano yake na Diamond.

Hii ni video ambayo inawaonyesha Wema Diamond wakiwa wanakumbatiana:

Tumekoma Hatuwezi Kurudia Tena Makosa-Babu Tale

Meneja wa Kampuni ya Wasafi (WCB) Babu Tale amekiri kuwa adhabu waliyopewa wasanii wake Diamond na Raymond Mwakyusa’ Rayvanny kufungiwa miezi miwili, imewafundisha na hawatarudia tena.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la mwananchi, Babu Tale ameweka wazi kuwa adhabu waliyopata Diamond na Rayvanny imekuwa somo kwao wote na hawatorudia tena makosa.

Kwa kweli kwa muda wote ambao wasanii wetu walikuwa wamefungiwa pamoja na kusitishwa kwa tamasha letu la Wasafi, tumejifunza mengi, hatuna budi kuishukuru BASATA na serikali kwa ujumla tunachowahaidi ni kwamba tumrjifunza mengi na hatutarudia tena”.

Diamond na Rayvanny walifungiwa mwaka jana Desemba 15 na kuzuiwa kufanya maonyesho ya nje na ya ndani hata hivyo Wiki chache zilizopita BASATA Ilitangaza kuwafungulia rasmi.