Mabango ya Wana BUKOBA kwa Diamond ni Kizungumkuti

Mwili wa aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi vya Clouds radio na Clouds fm Bwana Ruge Mutahaba uliwasili siku ya jumapili katika kijiji chao huko Bukoba ambapo kabla ya kufika huko ulitembezwa katika baadhi ya mitaa ili kugawa na watu wa Bukoba.

watu wengi walijitokeza kwa ajili ya kuupokea mwili huo kutoa uwanja wa ndege mpaka kuusindikiza kufika nyumbani kwao Kisiru -Kabale ambapo ndipo atakapopumzishwa hapo.

Hata hivyo , mabango mengi yaliandikwa kuonyesha wasifu na mengi aliyokuwa akiyafanya Ruge lakini yapo pia yaliyokuwa yakitoa lawama kwa msanii Diamond .

Hali ya mtandaoni na akili mwa watu ni tete kwa sababu hakuna swala la wazi kwa nini watu wamekuwa wakimshambulia msanii Diamond  kuhusu kuudhuria katika msiba wa Ruge tangu siku ya kwanza.

Hakuna anaejua sababu iliyomfanya diamond kufanya hivyo , inawa hisia za watu wengi mitandaoni zinaonyesha kuwa Bifu lilokuwepo kati ya Ruge na Diamond ndilo lilimfanya Diamond kufanya hivi , lakini ni kitu mabacho hata yeye hajaonyesha kutaka kuzngumzia hilo.

Katika moja ya mabongo yaliyopigwa picha na kusambaa sana ni hili lilokuwa likisema “DIAMOND MUOGOPE MUNGU NA WEWE UTAKUFA TU, R.I.P RUGE”

Matukio ya Kupokea na Kuaga Mwili wa Marehemu Ruge jijini Dar Es Salam

Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba Uliwasili siku ya Ijumaa na kupita maeneno mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na baade kupelekwa katika hospitali ya Lugalo.

Siku ya jumamosi , ulipelkwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuagwa na watu mbalimbali na kuupatia heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa na kupelekwa kijijini kwao BUKOBA  ambapo ndipo mwili huo utazikwa katika nyumba yake ya milele.

Ruge ameliza wengi na wengi wameumia na msiba huo , huku kila mmoja aamini kwa jinsi watu walivyojitokeza kwa ajili ya kuupokea na kuupoa heshima zake za mwisho kwa DAR  na hata ulipofika kwao BUKOBA.

Mwili wa Ruge ukiwasili na kushushwa Uwanja wa Taifa.

Mwili wa marehemu ukipita katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar.

jeneza la marehemu likiwa limewasili viwanja vya karimjee tayari kwa kuagwa.

Familia ya marehemu (watoto wake na wazazi wenzake na Ruge) wakiwa katika ukumbi wa Karimjee.

Mh Magufuli akitoa mkoo wa pole kwa wazazi wa marehemu.

Baadhi ya wasanii wa THT wakiwa katika majonzi wakiimba Nyimbo za kuombeleza.

Nandy ni moja ya wasanii waliopata fursa ya kuimba wimbo aliokuwa akiupenda marehemu lakini alishindwa kuendelea na mtoto wa marehemu alimsaidia kushuka jukwaani.

Barnaba alipokuwa akiongea machache kuhusu  baba yake Ruge na baada ya hapo alishindwa kuendelea na kuzimia.

Zamaradi mketema ambae ni mzazi mwenza na Ruge akiingia uwanjani hapo.

Baadhi ya wasanii wakiwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu.

Baadhi ya watu siku ya jumapili wakisubiri mwili wa marehemu Ruge kuwasili katika viwanja vya ndege  BUKOBA.

 

 

Mrisho Mpoto Amshukuru Diamond Kufika Msibani.

Msanii Mrisho Mpoto ambae alituma salamu kwa msanii Diamond platinumz kuwa anatakiwa kufika katika msiba wa ruge mutahaba na baada ya salamu hizo Diamond platinumz alifika kweli katika msiba huo katika uwanja wa Karimjee mabapo ndipo alipokuwa akiagwa Ruge.

Hata hivyo kutokufika kwa Diamond kwa muda mrefu msibani tangu msiba huo ulipotokea kumezua gumzo kwa watu kwamba kwanini hakutokea tangu siku ya kwanza ya msiba na hata kufika siku ya kuaga na bado hakufika katika muda unatakiwa.

Hata hivyo msanii huyo alifika na familia yake na kukaa nje na hata hakuruhuiswa kukaa ndani  kwa sababu ya kuchelewa kwake.

katika ukurasa wake wa instagram, Mrisho Mpoto alisema “NIMETUKWANA SANA KWA SABABU YA KUKUOMBA KUJA KUMZIKA RUGE ,ASANTE KWA KUNIHSHIMU NA KUNISIKILIZA, KWA KILA ALIENITUKANA NAOMBA ALALE NA HILI NENO HILI “nyumba ya mzaramo haikosi kuwa na mbilimbi”

 

Baada ya Kushambuliwa na mashabiki, Diamond Afika Msibani

Baada ya msanii Daimond kushambuliwa kwa muda mrefu na hata wasanii wenzake kutuma salamu kumuomba kufika katika msiba wa mkurugenzi wa Clouds media Group bwana Ruge mutahaba , hatimaye msanii huyo alifanikiwa kufika msibani.

Ingawa hakuruhuiswa kuingia mpaka ndani ambapo walikuwa wamekaa wasanii wengine na wageni wa VIP kutokana na kuchelewa kwake na umati wa watu wengi kumfuata kwa nyuma.

Hata hivyo msanii huyo alifika msibani akiwa na  walinzi wengi na kufuatwa  na watu wengi  akiwa ameongozana na familia yake ambayo ni dada yake ESMA na mama yake Mama Dangote.

Hata hivyo msanii huyo hakukaa muda mrefu msibani hapo aliamua kuondoka na group lake la wasanii aliokuja nao katika msiba huo.

 

 

Nay wa mitego ;-Natamani kumuona Diamond Msibani.

Msanii Nay wa Mitego ambae pia alikuwa moja ya watu waliofika katika msiba wa Ruge amefunguka na kusema kuwa amekuwa akitamani sana kumuona Diamond Platinmz katika msiba wa bwana Ruge mutahaba lakini anashangaa kwanini msanii huyo hatokei.

Akiongea na waandishi wa habari, Nay wa mitego  anasem “Duniani Tunapita tu, leo hatunaye Bosi Ruge , kiukweli natamani sana kumuona Diamond hapa msibani, muda bado lakini tusubiri labda tutamuona”

Diamond amekuwa moja ya wasanii walioshangaza watu wengi hasa kutokana na ukweli kuwa hakuna alieyetegemea kutokumuona msibani ukizingatia kuwa hata yeye alipita mikononi mwa Ruge hata kama wawili hao wanasemwa kuwa na mfarakano hapo nyuma.

 

Niliwahi Kushika Pesa Kuliko Msanii Yoyote , Ruge Hakuwahi Nidhurumu :-Chid

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini mabae kwa sasa amekuwa chini kutokana na hali yake ya kiafya kidogo kudhoofu CHID BENZ amefunguka na kusema kuwa tangu amekuwa msanii kwa zaidi ya miaka 10 sasa yeye no moja ya wasanii wenye historia ya kuwa na pesa nyingi kuliko msanii yoyote lakini hakuwahi kufanyiwa dhuruma na Ruge.

Chid benz ambae anasema kuwa yeye ni msanii aliyewahi kushika pesa sana kipindi cha nyuma kuliko msanii yoyote na alikuwa akisaidwa sana na bwana Ruhe lakini hakuwahi kufanyiwa yale ambayo baadhi ya wasanii wamekuwa wakizusha katika mitandao ya kijamii.

hata hivyo moja ya wasnaii DUDUBAYA amezua kashfa mbaya sana kwa marehemu Ruge mutahaba kwa kusema kuwa amekuwa akidhurumu sana wasanii hasa waliopitia mikononi mwake ilhali wasanii waliolelewa hapo wanasema hakukuwa na kitu kama icho.

Mh Rais Atoa Ndege Kusafirsha Mwili wa Marehemu Ruge na Waombelezaji

Mh rais John Pombe magufuli ametoa ruhusa ya kutumika kwa ndege kubwa moja ya AirTanzania kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu kutoka jijini Dar es salaam mpaka Bukoba ambako ndipo mwili huo unakwenda kuzika.

Hata hivyo mwili wa marehemu unatarajiwa kufika siku ya ijumaa saa 10 jioni katika uwanja wa mwl Nyerere na kutembezwa baadhi ya maeneo ya jiji na kisha kwenda kuwekwa hospitali ya Lugalo kwa ajili ya siku ya ijumaa ambapo utaagwa katika viwanja vya Karimjee na kwusafishwa mpaka Nyumbani kwao Bukoba.

Mh rais magufuli aliweza kuwa mstari wa mbele katika mapito yote ya Ruge tangu akiwa mgonjwa kwa kutoa pesa ya matibabu na hata sasa amekuwa mstari wa mbele kuwa karibu na familia katika kipindi hiki kigumu.

 

Ruge Mutahaba Afariki Dunia

Mkurugenzi wa vipindi clouds tv na clouds radio Bwana Ruge mutahaba aliekuwa akipigania maisha yake huko nchini Afrika ya Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu afariki Dunia jioni ya February 26.

Ruge ambae alikuwa akipigania sana maisha yake na hata kulikuwa kunaendelea kwa kampeni za kupata pesa kwa ajili ya matibabu yake , ameshindwa kuendelea kupigania maisha yake baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya .

Habari kamili kutoka kwa wanafamilia na watu wake zitatolewa hivi punde.

 

Kufuatia Kifo Cha Mkurugenzi wa Clouds Media,Mh Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi.

Hawezi kusahaulika na wanafamilia na wapenzi wa Clouds na wapenzi wa bwana Ruge Mutahaba kwa sababu sio yeye ni  kiongozi lakini pia kutokana na moyo wake wa kuwa mwenye huruma hasa pale anapoguswa na familia zenye matatizo.

Akiwa kama mmoja waliosaidia sana katika kupigania maisha ya bwana Ruge Mutahaba, Mh rais   aliwahi kutoa pesa nyingi kwa ajili ya kusaidia matibabu yake lakini juhudi hizo zimegongwa mwamba.

Akituma salamu za rambi rambi kwa  familia  ya marehemu, Mh Rais amesema ameguswa sana na msiba wa bwana Ruge na kusema kuwa katika maisha yake atakuwa akimkumbuka kama kijana muhimu sana aliyeweka nguvu zake nyingi katika tasnia ya burudani  na kujenga fikra pevu kwa vijana.

 

Wewe Ulinibadilisha na Kunifanya Niache Kupiga Picha za Nusu Uchi -Maneno ya Gigy kwa Ruge

Moja ya wasanii ambao kwa sasa wamepata majina makubwa bongo kutokana na kazi zao, Gigy money amefunguka na kutoa maneno yake ya huzuni hasa baada ya kusikia kifo cha mkurugenzi wa Clouds media groud bwana Ruge Mutahaba.

Gigy money ameandika ujumbe mrefu na wenye kuhuzunisha akijitahidi kuonyesha mchango wa mkurugenzi huyo katika maisha yake huku akimwita kuwa yeye ndio mzazi wake baada ya mama yake aliemlea.

Gigy money anasema kuwa Ruge ndie aliemfungulia maisha kwa kumpa nafasi hata katika kituo chake kama mfanya kazi hapo huku akijitahidi kil siku kumyoosha katika njia mbaya alizokuwa akipita.

Gigy anasema kuwa hata ile tabia yake ya kupiga picha za uchi , ni Ruge ndie alimfanya kuachana na swala hilo kutokana na kuwa kila mara alikuwa akimjali na kuongea nae ili kujaribu kumbadilisha.

https://www.instagram.com/p/BuWuw-MntWs/