Nina Ukubwa Gani Hata Nisolewe Tena :-Khadija kopa

Mwanamama khadija kopa amefunguka na kusema kuwa kuna watu wamekuwa wakimuandama sana kuhusu swala la yeye kutka kuolewa tena huku wakiwa kama hawawaoni wale ambao wamekuwa wakitembea na vijana wdogo chini ya umri wao.

khadija kopa anasema kuwa anachoamini yeye ni kuwa kama umri wake bado unaruhusu anachosubiri ni bahati yake kutoka kwa Mungu kumleta mwanaume anaeona yeye kuwa anamfaaa lakini swala la kuolewa halina maajabu tena hasa kwa umri wake.

akijibu tuhuma hizo kwa bashasha Khadija kopa anasema “mimi nia ukubwa gani hata nisiolewe tena, hao wa bibi wanaohangaika na watoto wadogo  hamuwaoni ndo mseme mimi  siweiz olewa tena.mimi nipo tayari kuolewa nasubiri riziki yangu  Mungu akiniletea.

Khadija Kopa Afungukia Skendo Ya Kifumaniwa

Mwanamuziki wa Taaprabu nchini Khadija Kopa au Malkia wa Mipasho amefungukia skendo iliyowahi kumtafuna miaka ya nyuma kwamba moja kati ya ndoa zake nne ilivunjika baada ya fumanizi.

Katika mahojiano yake na kipindi cha Planet Bongo ya EA radio, Khadija amesema pamoja na kwamba miaka hiyo hakukuwa na mitandao ya kijamii lakini vyombo vya habari vilitengeneza stori kama hizo ili viweze kuuza gazeti:

Skendo ambayo niliwahi kuwa nayo kubwa miaka hiyo ni kutangazwa kuwa nimeachwa kwa kile walichodai kuwa nilifumaniwa. Ila kiukweli sijawahi kufumaniwa ila ni watu walizusha ili kusudi ya kwao yawaendee vizuri si unajua miaka hiyo hakukuwa mitandao ya kijamii kama ilivyo hivi sasa”.

Khadija ameweka wazi siri yake ya kuendelea katika tasnia ya Muziki wa taarabu ni kubadilika kutokana na mazingira na mashabiki ili kuendelea kuwapa ladha tofauti tofauti.

khadija Kopa Afunguka Skendo ya Kufumaniwa.

Mwanamuziki bora kabisa katika miondoko ya taarabu Khadija Kopa amfunguka na kutoa dukuduku lake kuwa katika vitu ambavyo aliwahi kuumizwa navyo sana katika maisha yake ni pale aliposingiziwa kuwa ameachwa na mwanaume wake kwa kupewa talaka kwa sababu alifumaniwa na mwanaume mwingine.

Akizungumza katika planet bongo ya EATV khadija ansema kuwa kipindi hicho waandishi wa habari walikuwa wakiandika mambo bila kuwa na ukwei wowote ili kupata habari lakini alimua sana kwa sababu haikuwa kweli hata kidogo.

skendo niliyokuwa nayo kubwa ni kipindi kile nilichotngazwa kuwa niliachwa kwa kupewa talak kisa tu nimefumaniwa, ila kiukweli sijawahi kufumaniwa ila watu tu waliamua kunizushia ili kusudi kwao yaende na kipindi hicho kulikuwa hakuna hata mitandao ya kijamii.

Mimi huwa istafuti kiki ila kiki zinakuja znyewe, nilikuwa sipiti siku bila kuweka front page za magazeti , waandishi walikuwa wanafanya tu vile walikuwa wanataka kuandika.

Hata hivyo khadija kopa anasema kuwa kitu kikubwa kilichomfanya mpaka sasa aweze kudumu katika game ni kwa sababu amekuwa akibadilika kulingana na mazingira ya muziki.

Mimi Bado Kijana Nina Hamu Ya Kuolewa Tena- Khadija Kopa

Malkia wa Taarabu na mipango nchini Bibie Khadija Omary Kopa ameibuka na kudai ana mpango wa Kuolewa Tena kwani yeye bado ni kijana na anapenda kuwa ndani ya ndoa.

Khadija Kopa ambaye tayari amekwisha olewa kwa mara tatu miaka ya nyuma ameweka wazi kuwa ana nia ya Shari kabisa ya Kuolewa ndoa yake ya nne siku za mbeleni.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Khadija Kopa ameweka wazi kuwa ingawa yeye ni kiana na anataka kuolewa Tena lakini hana papara kwa sasa.

Mimi nimeshaolewa ndoa nne na mume wangu wa mwisho aliyekufa alikuwa wa nne kwaiyo endapo Mwenyezi Mungu akileta mwenye heri lazima nitaolewa Lakini pia kama sitapata wa kunioa tena basi naendelea na Maisha Yangu na kazi zangu.

Halafu isitoshe Kuolewa hakunaga umri utakuta kibibi cha miaka sitini kinaolewa itakuwa mimi ambaye najiona kijana wa jana halafu pia sitaki kuzini ikitokea nafasi ya kuolewa lazima”.

 

Sina Muda Mrefu Nitaacha Muziki na Sitatangaza kwa Mtu;-Khadija Kopa

Msanii mkongwe wa taaarabu nchini khadija kopa amefunguka na kuzungumzia hali ya taarabu ilivyo sasa nchin na kusema kuwa wasanii wengi wamekuwa wajeuri na kwamba hawajitunzi kama zamani hivyio wanajishusha thamani wao wenyewe na wala sio kitu kingine.

Akiongea na wandish wa habari, khadija kopa anasema kuwa wasanii wa taarabu wamekuwa wakiimba katika mabar kwa kiinglio cha bia wakati hiyo haikuwa kama zamani na ili kukomesha hilo waimbaji hao wanatakiwa wakifuata wasikubali kufanya hivyo  na kujiona wa thamani ili kupanda hadhi yao.

Hata hivo akizungumzia swala la yeye kustaafu kama alivyofanya gwiji wa taarabu nchini, mzee yusup.malkia hiyo amesema kuwa alichokifanya mzee ni kutokana na imani yake ilivyomtuma na ni jambo zuri , hata yeye siku yoyote atastaafu na sio muda mrefu kutoka sasa kwa sababu anahitaji kutenga muda mwingi pia kwa ajili yake , dini na mungu wake kwa sababu hajuai siku wala saa ya kufa kwake.

Hata hivyo Khadija Kopa ansema kuwa kama ataamua kufanya hivyo atafanya kimya kimya bila kumwamba wala kutangaza kwa watu, bali watashangaatu haingii tena studio wala haonekani tena katika maswala ya burudani.

sina muda mrefu sana, muda mrefu sana kupita kiasi nitaacha huu muziki na nitaapo acha waa sina haja ya kutangaza eti eeh ninaacha muziki, hapana  nitaacha tu na watu wataona kimya tu sitoi nyimbo.

Mimi Sipendi Viben Ten:-khadija kopa

Msanii wa muziki wa taarabu nchini, Khadija Kopa amefunguka na kuongelea swala lake la yeye kutembea na watoto wadogo ambao anawazidi umri na kusema kuwa kwa upande wake hapendi kabisa kutembea na viben ten na hatokaa afanye hivyo hata kama dini inaruhusu.

Khadija Kopa amesema kuwa licha ya kuwa yeye hapendi wanaume wa dizaini hiyo lakini hiyo isiwe sababu ya kuwasema wanawake ambao wamejiingza katika mahusiano na watu hao.

Mbona nyie wazee mnaoa wanawake wadogo na wala sisi hatusemi,sisi kila siku viben ten viben ten weee, mimi sipendi viben tena mimi  nilikuwa na mume wangu kabisa na hata katika dini yetu inaruhusu maana mtume alitufungulia njia.

Hata hivyo Khadija Kopa aliweka wazi na kusema kuwa baada ya mume wake kufariki kwa sasa yupo tayari kuolewa na mwanaume yoyote ila awe ameanzia miaka 40 na kwenda juu.

Khadijah Kopa: Najutia Maamuzi Yangu Ya Kutoa Mimba Ujanani

Mwanamuziki wa taarabu nchini au wengi wanamjua kama Malkia wa muziki wa taarabu Khadijah Kopa amefunguka na kusema moja kati ya vitu anajutia maishani mwake ni kutoa mimba.

Kwenye mahojiano aliyokuwa anafanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Khadija Kopa amekiri ameshawahi kutoa mimba kadhaa na hata mimba nyingine kuharibika.

Ukishafanya kitu kama hicho lazima ujute, mambo hayo mambo makubwa hata Mwenyezi Mungu hayataki lakini ujana unakuwa unakutia wehu unashindwa kujua unakuja kujutia wakati huu.

Mimi najutia kutoa mimba ila nakumbuka wakati huo ndio nimesimama jina ndio limepemba moto halafu na ujauzito wapi na wapi lakini kila siku namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa sababu pengine huyo mwanangu angekuwa raisi? Lakini ni ujana maji ya moto na ninawambia vijana waliokuwepo wasifanye vitu hivyo”.

Lakini pia Khadija ameweka wazi kuwa anashukuru Mungu pamoja na mimba alizotoa alijaaliwa kupata watoto wengine wanne, ingawa alikataa kutaja idadi ya mimba alizotoa na aliweka wazi mimba zake nyingine mbili zilihariibika kwa bahati mbaya.

Nataka Mume Sipendi dhambi-Khadija Kopa

Mwanamama Khadija kopa amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anaona bora atafute mume wa kumuoa na kwamba anataka mwanaume awe kuanzia miaka 40 kwenda juu kwa sababu hataki vijana maana hana muda wa kufundisha tuition.

Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume awe kuanzia miaka 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua nataka nini.atakae weza kujali familia yangu na watoto wangu , awe mnene kidogo  sio mwembamba awe na rangi yoyote na awe wa kabila lolote mimi sio mbaguzi hata kidogo.

Khadija Kopa pia amesema kuwa anataka mwanaume ambae ni mfanya kazi maana hataki mwanaume wa kukaa nyumbani tuanamsubiri yeye ndo amltee chakula na kila kitu.maana maisha ya sasa ni magumu sio ya kutegemea upande mmoja tu.

Hata hivyo akitoa sababu ya kutokuolewa mpaka sasa tangu mume wake amefariki ni kwa sababu anaogopa na ana wasiwasi sana na wanaume wa sasa.

Nina wasiwasi sana na wanaume wa sasa kwa sababu huwa nawaza je atakuwa na huba kama mwanaume wangu wa kwanza ambae sasa hivi ni marehemu.na ndio maana nimekuwa nikifiria sana kwa sababu mume wangu alikuwa na huba sana, na mwenye kunijali sana , nimekaa nae miaka yote  hatujawahi kugombana nae.Nilikuwa natamani sana kumuona akinuna lakini ananuna vipi?

Khadija Kopa Atoa Siri ya Kuwa Kijana Kila Siku.

Mwanamama ambae anafanya vizuri katika muziki wa taarabu tangu enzi za nyuma mpaka sasa bado anafanya vizuri ,Khadija Kopa amefung na kutoa siri ya yeye kuendelea kuwa kijana kila siku na kuonekana mrembo kimuonekana na hata kumuonekano.khadija anasema kuwa hajawahi kutumia vipodozi vyenye kemikali  katika maisha yake kwa sababu anaamini kuwa hiyo ndio inaharibu sana ngozi.

siri ni kujitunza tu , mimi sipaki malotion wala sipaki majitu ya kujichubua na hata kama napaka lotion sio ile ya kuchubua ngozi yangu,sibadilishi ngozi yangu , ngozi inabaki vile vile tu.na pia ninamshukuru mungu ninapata ridhki ya kula maana ukiwa na njaa pia nozi iakunyaa.

lakini pia mimi siitumii mwili wangu vibaya, mwanamke ukitumia mwili vibaya mara umemparamia huyu na mara huyu vilevile unazeeka na ile nuru ya afya yako inapotea pia.

lakini pia matumiz ya masigara, mapombe, mirumbi,mashisha vilevile yanazeesha, unakuta unakunywa pombe makali vile unavyokunywa  unakunja uso yale makunyanzi yanafata uso wako mama, upoooeeh…… mimi sivuti sigara wala situmii pombe nakunwa maji na nikinywa sana ntakunywa soda.

Akiongelea muziki wake kwa sasa, Khadija kopa anasema kuwa tangu alipofiwa na mume wake alikuwa amekuwa mweupe kabisa kwa sababu alikuwa amekaa ndani muda mrefu na hakuwa na sehemu ya kuingiza kipato zaidi ya kutoa tu alkini anamalizia kukamilisha nyimbo yake mpa ambayo itaanza kufanya vizuri kwa sababu amepanga kutoa audio na video kabisa tofauti na ilivyokuwa mwanzo ambapo alikuwa anatoa nyimbo bila kutoa video.

Khadija Kopa: Wasanii wa Taarab Wananiogopa

Msanii wa mziki wa miondoka ya taarabu ambaye anajulikana kama mslkia wa Taarabu nchini ameibuka na kudai kuwa wasanii wenzake wanamuogopa.

Mkongwe wa muziki huo wa taarabu amewachana wasanii wenzake wa taarabu na kudai kuwa wanamuogopa ndio maana hawawezi kutunga nyimbo zenye vijembe vinavyojibu nyimbo zake kama ilivyokuwa zamani, hivyo kawataka waache uoga wafanye wafanye ushindani ili taarabu iweze kufika mbali.

Khadija Kopa alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa ambapo alizidi kufunguka:

Mi naona kama wasanii waliopo wa taarabu ni kama wananiogopa wanaona mimi kama mama yao lakini vile vile hata kwa wao wenyewe wanatupiana madongo kuna nyimbo wanaimbiana lakini hawaendelezi alafu isitoshe sisi watu wa taarab wenyewe kwa wenyewe hatuna umoja yaani hatupendani kabisa yaani anaona nimuimbe fulani ili azidi kuwa staa sijui nsogopa kumpa kiki wakati mimi ni staa zaidi yake hivyo kunakuwa kuna kama wivu Fulani wakati mkifanya mashindano kama hayo ndo mnavutia mashabiki na wote mnajikuta mnapanda”.

Pia Khadija amesisitiza kuwa sio lazima kutafuta kiki kwa nguvu na zisizo za maana kama wasanii wengine wengi kama Bongo fleva bali ni kutumia ushindani wa kawaida wa kuimba ili kuzidi kukuza mziki huh wa taarab.

Hivi karibuni mziki wa Taarab umeonekana kupoteza ladha yake iliyokuwepo kama zamani na hata kupungua kwa mashabiki huku mashabiki wengi kudai taarab ilipoa baada ya Mzee Yusuphu kustaafu kufanya mziki huo.

Hivi Ndivyo Khadija Kopa Alivyowachamba Wasanii Wapenda Kiki

Malkia wa muziki wa Taarabu nchini Bibie Khadija Kopa amewajia juu na Kuwachamba wasanii wenzake wote wale wapenda kiki na kudai kama umaimba mziki mzuri na kuwafurahisha mashabiki wako hutahitaji kutumia kiki.

Wasanii wengi nchini sahivi wameingiwa na hiki kitu kinaitwa ‘kiki’ ambapo wanatengeneza bifu au skendo za uongo kwa maksudi kabisa ilimradi tu wapate attention ya mashabiki ili wakitoa kazi zao zipate airtime ya kutosha kwani watapata interview nyingi kutoka kwa waandishi wa habari.

Khadija Kopa amefunguka kwa kichambo hiko alipofanya mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa kupitia kipindi cha Enews ambapo amefunguka yafuatayo:

Hili suala la kiki linatokana na msanii mwenyewe anavyohisi labda wanahisi wakipata kiki zile za kuwa dhalilisha ndio watapanda zaidi kimuziki labda lakini mimi kitu sina na wala sipendi kwanza mimi mambo yangu binafsi napenda yawe ya siri na mambo yangi ya kifamilia napenda yawe ya siri na pia mambo yangu ya mahusiano au mume napenda iwe siri mimi mwenyewe, hasa nikiwa na bwana tuseme sio mums wa ndoa hiyo ndio kabisa napenda iwe siri zaidi kwa sababu sipendi kwani kitu cha zinaa sio kitu cha kujitangaza wala kujifaraghisha lakini kama mume unaweza lakini sasa sio ndio nipate kiki eti nimepigana na mume wangu watu wote wajue hapana huo sio umaarufu wala usanii wa maana”.

Lakini pia Khadija Kopa amewaasa wasanii wenzake kuwa Usanii wa kweli ni pale ambapo mwenyewe utajiamini unaweza ukafanya kazi watu wakaipokea na kukubali basi hauhitaji vitu vya ziada.

Malkia wa Taarab Khadija Kopa amwomba Diamond kusign mwanawe katika WCB

Diamond alishirikiana na Khadija Kopa kutoa ngoma kali sana unaoitwa ‘Nasema Nawe’. Wimbo huo ulipendwa sana na mashabiki kwasabubu ya wanawake wanaotingiza makalio zako kwenye video.

Akizungumza na Ayo TV, Khadija alisema Diamond atatambulisha mwanawe kama msanii wa Wasafi Classic Baby (WBC) wakati wowote.

Khadija Kopa akitumbuiza

Malkia huyo wa Taarab aliambia Ayo TV kuwa alimwomba Diamond kusign mwanawe na bado anangoja jibu kutoka kwake.

“Nilikwenda kwa Diamond Platnumz nikamwambia amsikilize mwanangu akamsikiliza na anasema amemuelewa yuko anasubiria kwani subira yavuta heri ndio riziki yake mwanangu kuimba kama isingekuwa riziki yake basi angepata label nyingine kwahiyo tutegemee muda wowote mwanangu kusainiwa WCB,” Khadija Kopa alisema.