Wema Sepetu Afungukia Furaha Anayopata Kufanya Biashara Anayofanya

Msanii wa filamu wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kazi anafurahia kama kuzaa nguo kwenye duka lake jipya.

Baada ya Kupitia kipindi kigumu mwishoni mwa mwaka huu hatimaye Wema ameweza kupata tena Furaha Baada ya kufungua biashara yake mpya na kuelekeza nguvu zake kwenye kazi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa Wikienda, Wema Sepetu alisema kuwa Hivi sasa anaanza kuona utamu wa biashara hiyo ndiyo maana sasa hivi hapati usingizi kama zamani.

Biashara ni tamu kinoma ukiweza kuipatia. Kufanya biashara ambayo unaipenda ni jambo la msingi sana. Nafurahia kazi yangu hii, kuna vitu nimejifunza pia,”

Wema ambaye anamiliki duka hilo la nguo alilolipa jina la Little Sweetheart lililopo Mwananyamala, Koma-Koma jijini Dar.

Masharti ya Wema Aliyopewa na Familia Baada ya Kuanza Biashara.

Mwanadada Wema sepetu  ametakiwa kufuata masharti ya familia yake ili kufankisha  biashara yake ambayo  ili pia kuepuka masswala  ya aibu hasa baada ya yale yaliwahi kumtokea hivi karibuni kabla ya kufungua baishara hiyo.

Wema Sepetu ambae amefungua duka la watoto  hivi karibuni baada ya kwenda china kufuata mzigo, anatakuwa kufuata mashart yafuatayo :-

1.Biashara anayoiendesha itakuwa chini ya dada yake Nuru ambae ndio atakuwa akimuongoza kwa kila kitu hata kama biashara hiyo ni ya kwake.familia imefanya hivyo il kuweka limits ya mambo mengi ambayo anayo mwanadada huyo.

2.Kujilinda na kuacha kabisa skendo za mara kwa mara kwa sababu licha ya kufubaza jina na brand yake lakini inaua biashara pia.

3.kuepukana na vyombo vya habari hasa mahojiano ya mara kwa mata yasiyokuwa na umuhimu owowte kwa ajili ya kutafuta kiki au umaarufu wowote.Atakae kuwa msemaji mkuu wa mwanadada WEMA ni dada yake anaejulikana kwa jina la NURU.

4.Kuepukana sana  marafiki anao wengi wamekuwa wanafiki kwake , wamekuwa wakionekana kuwa wanampenda lakini linapotokea baya lolote wamekuwa wakimkimbia na bila kumsaidia.

5.Kuepuka kufanya starehe za mara kwa mara na watu wanaojifanya marafiki kumbe nia kubwa ni kutaka kufanya starehe bila kuwa na msaada owowte kwa mwanadada huyo.

 

 

 

Gigy Money Afungukia Uwamuzi Wake Wa Kumuachia Mtoto Wema Sepetu

Video vixen na msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefungukia uamuzi Wake wa kumuacha Mtoto Wake na Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

Wiki iliyopita Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gigy Money aliweka wazi kuwa kabla ya kusafiri kwenda kufanya shoo mkoani Mwanza ameamua kumuacha binti yake na Wema kwani anaamini ni mama mzuri na anapenda sana watoto.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Gigy Money aliyekuwa safarini jijini Mwanza huku akimwacha mwanaye kwa Wema jijini Dar, Gigy alisema amemuona Wema ana upendo na pia anapenda watoto hivyo akaamua kumuachia na kwenda kutafuta maisha akijua yupo mikono salama.

Namuomba Mungu amjalie Wema apate mtoto maana ni mama mwenye upendo ndiyo maana nimemuachia Maira amlee na ninajua atakuwa kwenye mikono salama“.

Wema ameshaweka wazi mapenzi yake kwa watoto licha ya kushindwa kupata Mtoto Wake wa kumtaka mwenyewe.

Mwili Mpya wa Wema Sepetu Wazua Gumzo

Mwili wa mwanadada Wema Sepetu umezua mjadala mkubwa katika mitandao ya instagram baada ya mwanadada huyo kuanza kuonyesha picha zake za mwili wake kwa jinsi livyopungua kwa sasa.

Mwanadada huyo ambae alisemwa sana kipndi fulani baada ya habari kusambaa kwamba mwanadada huto amekwenda kukata utumbo ili aweze kupunguza mwili wake na kuumwa sana hata afya yake kulegalega.

Wema sepetu kwa sasa anazidi kurudi katika  mwili wake wa zamani kipindi alipokuwa miss na umbo hilo limewafanya watu wengi kumtamani sana kuwa kama yeye.

“Marafiki Wabaya Walitaka Kumpoteza Wema”-Mama Wema

Mama mzazi wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Bi. Mariam Sepetu ‘Mama Wema’ amefunguka na kuwataja marafiki kama watu waliokuwa wanampoteza Wema.

 

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Mama Wema Mama Wema alimuongelea binti yake Wema  ambaye kwa sasa amekuwa kimya huku akionekana kufanya mambo ya maendeleo ikiwemo kufungua duka lake la nguo lililopo maeneo ya Kinondoni jijini Dar.

Wale watu waliomzunguka hawakuwa sahihi, alikuwa na msururu wa watu wakufuata tu mkumbo, wanafuata tu kama mkia vile.

Wema anapendwa, hata hawa unaowaona kila siku wanampinga kwenye mitandao ya kijamii sio kwamba wanampinga, wanampenda sema Wema anakuwa hajui tu“

Lakini pia Mama Wema alifunguka mapenzi aliyonayo kwa binti yake na kumpongeza kwa kufungua duka lake jipya:

Walimpinga hata katika suala hili la duka lakini namshuru Mungu amefanikiwa, amelifungua tayari na leo (juzi) amenialika niende kuona.

Mimi huyu ni mwanangu, nampenda sana na ndio maana hata afanye nini bado nitaendelea kuwa naye bega kwa bega, naamini kabisa sasa hivi ameachana na marafiki wasiofaa na amebadilika”.

Wema amekuwa kimya sana tangu skendo yake ya kusambaza picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii ambapo kesi yake bado inaendelea kusikilizwa mahakamani.

Wema Sepetu Atinga Bodi Ya Filamu Kuomba Kufutiwa Adhabu

Staa wa filamu za Bongo movie Wema Abraham Sepetu siku ya jana ametangaza katika Otis I ya bodi za filamu Tanzania kwa ajili ya kuomba kupunguziwa adhabu aliyopewa Baada skendo yake.

Wiki chache zilizopita Wema Sepetu alifungiwa kujihusisha na filamu katika kipindi kisichojulikana baada ya kuposti video zake za faragha za chumbani kwenye mitandao ya kijamii.

Siku ya jana Wema aliwasili katika Ofisi za bodi ya filamu kwa lengo la kuangalia Kama anaweza kupunguziwa adhabu yake ambapo alijitetea kuwa amekuwa na mwenendo mzuri na kusema:

Filamu ndio kitu ninacho kitegemea kwenye maisha yangu na tangu nimefungiwa nimekosa fursa nyingi za kazi ambazo zingetutangaza kimataifa, hivyo naahidi kuendelea kuwa na mwenendo chanya katika jamii pasipo kuharibu maelekezo niliyopewa na Bodi ya Filamu katika kuisafisha taswira yangu ambayo imechafuka”.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo Alieleza kuridhishwa na mwenendo wa Wema Sepetu  kufuatia utiifu wake wa adhabu aliyopewa na kusema Tasnia ya Filamu bado inamuhitaji na kama akiendelea na mwenendo mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa.

Tunamuhitaji sana Wema Sepetu katika Tasnia ya Filamu kutokana na umahiri wake katika kazi lakini tunachukia maadili mabovu aliyoyaonesha katika jamii na sisi kama Bodi ya Filamu hatutasita kumfungia moja kwa moja kama akiendelea na matendo yauvunjifu wa maadili yetu kama Watanzania”.

Bodi ya Filamu Tanzania (TFB) inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa Wema Sepetu kuhakikisha anarudisha Taswira yake chanya iliyopotea na kuwa mfano wa kuigwa katika jamii na ikiwa mwenendo wake utazidi kuwa mzuri basi atafunguliwa kutoka kwenye adhabu aliyopewa.

 

Calisah Aanika Mastaa Aliobanjuka Nao

Mwanamitindo maarufu wa kiume Bongo ambaye pia hivi sasa ni Mr. Africa Calisah Abdul ameanika Listi nzima ya mastaa wa kike ambao amewahi kuwa nao kwenye mahusiano.

Calisah amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na Kipindi cha Ala Za Roho ya Clouds Fm ambapo alimsanua Diva The Bawse kuwa ameshakuwa kwenye mahusiano wasanii Kama Wema Sepetu, Irene Uwoya, na Jacqueline Wolper.

.

Calisah ameweka wazi kuwa alianza mahusiano ya kimapenzi na Wema wakati bado akiwa kwenye mahusiano na Idris Sultan bila Idris mwenyewe kujua.

Lakini pia Calisah ameweka wazi kuwa ameshawahi kuwa kwenye mahusiano na wasanii wa Bongo movie Kama vile Irene Uwoya na Staa mwingine Jacqueline Wolper.

Kwenye mahojiano hayo Calisah amekana  kuwa kwenye mahusiano na Hamisa Mobetto na Socialite maarufu kutoka Kenya Vera Sidika na kukiri iliyotrend kwenye mitandao ni Kiki.

Kesi ya Wema , Bado Ngoma Nzito.

Kesi ya mwanadada Wema Sepetu ya kurekosi na kujipiga picha akiwa faragha na mpenzi wake bado inaonekana kuwa nzito hasa baada ya kesi hiyo kushindwa kuendelea kusomwa mahakamani kwa madai kuwa uchunguzi wa kesi iyo bado haujakamilika.

Wema ambae anakabiliwa na kesi hiyo amekuwa akitakiwa kwenda katika mahakama ya Kisutu kila mara kesi yake inaposomwa.

Akiongea mbele ya mahakama, wakili wa kesi hiyo anasema kuwa kesi hiyo ilipangwa kusoma lakini haitawezekana kwa sababu upepelezi haujakamilika.

Wema amekuwa na mwaka mbya mwaka huu hasabaada ya kukumbwa na kesi moja baada ya nyingie, kama itakumbukuwa mwanadada huyo aliweza kusota na kesi ya madawa ya kulevya kwa mwaka mzima na hata baada ya hukumu kutoka alitakiwa kulipa faini ili asiweze kwenda jela.

Lakini hata baada ya kupambana na kesi ya madawa ya kulevya sasa limekuja lingine la kumfanya asote tena mahakamani ambalo ni kosa la kimtandao.

Kesi iyo inatarajiwa kutajwa tena January  28, 2019.

 

Hatimaye Wema Sepetu Akamilisha Ndoto Yake

Mwanadada Wema Sepetu hatimaye amekamilisha ndoto yake ya siku nyingi aliyotaka kuitiiza baada ya kufanikiwa kufungua duka lake la nguo kwa ajili ya watoto lililopo jijin dar es  salaa.

kwa ara ya kwanza akitoa tamko hilo, mwanadada Wema Sepetu aliweka post katika ukurasa wake wa insta na kusema kuwa  duka hilo litaanza kufanya kazi wiki hii siku ya Jumatano na lengo kuwa ni kufanikisha fuyraha ya wazazi kwa watoto wao.

duka hilo limefunguliwa wakati ambao wanadada huyo trayari ameshapitia miskosuko mingi ikiweo pamoja na ile kudaiwa kuwa moja ya sababu ya lukwama  nibaada ya kutapeliwa kimapenzi na CK na kumuibia pesa zote.

hongera nyingi kwake wema sepetu na mashabiki wanakaribishwa kumfanikisha katika hilo.

 

Diana Kimary Agoma Kumuacha Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie Diana Kimary ameibuka na kudai kamwe hawezi kuacha kuwa na ukaribu na na staa wa Bongo movie Wema Sepetu kwa sababu tu watu wanataka iwe hivyo.

Kutokana na skendo iliyompata Wema siku za Hivi karibuni Baada ya kuachia video za utupu kwenye ukurasa wake wa Instagram, wadau kadhaa walimtaka Wema kubadilika na hata kubadili aina ya marafiki aliokuwa nao ikiwemo Diana.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Diana amesema hawezi kupelekeshwa na maneno ya watu wanaomtaka asiwe na ukaribu na Wema.

Wanaodhani na mimi nimewekwa mbali na Wema na ndiyo maana simposti kwenye ukurasa wangu wa Insta kama ilivyokuwa huko nyuma, wanachekesha.

Niwafahamishe tu kwamba hakuna wa kunitenganisha na Wema, yule ni rafiki, ni kama dada yangu, tumegandana, manenomaneno sitaki, waniache na maisha yangu”.

Tangu sakata lake la kuvujisha picha za faragha Wema amekuwa kimya na kuonekana mahakamani ambapo amekuwa akifuatilia kesi yake hiyo.

Kazi Yoyote Mpya ya Wema Sepetu kufungiwa.

Katibu Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fissoo ,  Bi. Joyce Fisso amesema kama kuna kazi mpya ya Wema Sepetu inayotangazwa baada ya kufungiwa kujihusisha na kazi za filamu iripotiwe.

Fisoo ameiambia E- News  msanii huyo wamemfungia na bado wanaendelea kumfungia na wakitaka kumfungulia watafanya Press na waandishi wa habari kama walivyofanya awali.

“Wema tumemfungia na bado tunaendelea kumfungia, tutamfungulia kwa kutoa press kama tulivyofanya, kama nilivyosema tulisema tunafuatilia mwenendo wake na kweli tunafuatilia na kuna task ambapo tumempa tunazipima tukijiridhisha kuwa amerejea kwenye nidhamu na amejitambua tutakaa na kuona cha kufanya,” amesema Bi Joyce.

“Kama kuna kazi mpya mmeiona baada ya kufungiwa umeiona naomba iwasilishwe na utaona kitakachofuatwa.”

Maneno ya katibu huyu yanakuja baada ya kutolewa kwa uamuzi huo katika bodi hiyo kutokana na kosa la wema la kuvujisha picha za uchi.

Martin Kadinda Amkana Wema Sepetu

Mbunifu wa mavazi Tanzania na aliyekuwa meneja wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amedaiwa kumkana Wema baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wao wa kibiashara.

Martin Kadinda  amesema kuwa kwasasa yeye sio Meneja wa msanii wa Filamu, Wema Sepetu anafanya kazi na msanii huyo kama kaka yake Lakini sio Kama zamani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Martin Kadinda  amesema kuwa popote Wema Sepetu atakapo muhitaji kwa msaada au ushauri nini afanye huwa ana mshauri.

Mimi sasa hivi nafanya kazi na Wema kama kaka ake, i do everything popote anapohitaji msaada kuanzia ushauri what to do huwa namshauri lakini mambo mengine binafsi anafanya yeye mwenyewe, mimi kwasasa hivi ni ndugu yake sio Manager”.

Mwezi uliopita Wema Sepetu alikumbwa na skendo ya kusambaza picha zake za faragha akiwa na mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.

Wema Sepetu Afunguka Baada Ya Skendo Yake Nzito

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuelezeawmaisha yake yanavyoenda tangu akumbwe na ile fedheha ya mwaka Baada ya picha na video zake chafu kuvuja mtandaoni.

Wiki chache zilizopita Wema aliwadhangaza watu wengi Baada ya kuamua kuwanika video na picha zake kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa anakumbatiana kubusiana na aliyekuwa Mpenzi Wake kwa kipindi hiko PCK.

Baada ya sakata hilo Wema amefunguka na kusema kuwa maisha yake ya sasa  anapenda yawe ya siri zaidi na kama ana shida ya kuzungumza vitu ambavyo vinamsibu ni vyema amtafute mtu sahihi ambaye anamuamini kwa asilimia zote.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa, kwa sasa amekuwa makini kwa kila kitu anachofanya ili kumuweka salama tofauti na zamani ambapo mambo yake mengi yalikuwa yakivuja hovyo.

Kwa kweli sasa hivi niko makini sana na kila jambo hivyo nimepitia kipindi kigumu sana mpaka sasa hivi nimeamua kujituliza kufanya vitu vyangu kiakili“.

Baada ya kusambaza picha hizo Wema alifunguliwa kesi mahakamani ambayo inaendelea kusikilizwa.

“Wema ni Zaidi Ya Dada Kwangu, Nampenda Sana”-Diamond Platnumz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini na CEO wa WCB Diamond Platnumz amevunja ukimya juu ya sakata la picha chafu za Msanii wa Bongo movie Wema Sepetu.

Mwezi uliopita Staa Wema Sepetu alipatwa na Janga la mwaka Baada ya kuvujisha picha zake za utupu kwenye mitandao ya kijamii na kuishia kuburuzwa Mahakamani ambako kesi yake inaendelea kuunguruma.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online, Kwa Mara ya kwanza Diamond amefunguka kuhusu sakata hilo la Wema na kuweka wazi kuwa anamheshimu na kuwa alifanya makosa Kama binadamu yoyote.

Wema ni zaidi ya Dada yangu namheshimu na kumpenda sana tulipotokaga Mimi na Wema ni mbali sana na hata Kama hatuna mahusiano lakini urafiki wetu upo na ninaami kila mwanadamu kuna vitu vinatokea ambavyo hatukupangaa vitokee kwaiyo inawezekana walikuwa wamekaa sehemu na hawakupenda vitokee lakini kwa bahati mbaya ikawa hivyo”.

Lakini pia Diamond amemshauri Wema kuwa makini na mambo Kama hayo yasijeyakatokea tena kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anawaangusha mashabiki zake wanaompenda Lakini pia anaiangusha serikali inayomtegemea yeye kuwa kioo cha jamii.

Tumfanyie Wema Maombi kwa Ajili ya Toba :-Mchungaji Mashimo

Mchungaji aliyejulikana kwa jina la  mshimo mkoani Dar Es Salaam amefunguka na kusema kuwa kwa sasa wanahitaji kumfanyia Wema Sepetu moambi kwa ajili ya kuapta msamaha na toba ya mambo yake na dhambi zake zote lakini wanaotaka kumuombea zaidi inabidi wafunge na kusali.

Wamekuwa wakijitokeza wachungaji mbalimbali kwa hizi siku za hapa karibuni hasa baada ya mwanadad wema sepetu kuingia majaribuni katika swala zima  la maisha yake na kutaka kumsaidia kwa kufaya nae maombi lakini mwanadada huyo amekuwa akikataa .

Tumemfanyia maombi Wema kwa sababu ya toba, lakini haya ya pli ni kwa ajili ya kufunga na kuomba  lakini haya ya pili ni kwa ajili ya kufunga na kuomba kwa ajili ya kuchafuliwa jina lake.

Ikumbukwe kuwa kuna kipindi yaliandaliwa maombi kwa ajili ya Wema sepetu katika moja ya makanisa ya kilokole huko jijini Dar lakini ilishindikana kwa sababu Wema hakutaka kuonekana katika maombi hayo akidai kuwa hakuwa na taarifa za maombi hayo.