Martin Kadinda Amkana Wema Sepetu

Mbunifu wa mavazi Tanzania na aliyekuwa meneja wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amedaiwa kumkana Wema baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wao wa kibiashara.

Martin Kadinda  amesema kuwa kwasasa yeye sio Meneja wa msanii wa Filamu, Wema Sepetu anafanya kazi na msanii huyo kama kaka yake Lakini sio Kama zamani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Martin Kadinda  amesema kuwa popote Wema Sepetu atakapo muhitaji kwa msaada au ushauri nini afanye huwa ana mshauri.

Mimi sasa hivi nafanya kazi na Wema kama kaka ake, i do everything popote anapohitaji msaada kuanzia ushauri what to do huwa namshauri lakini mambo mengine binafsi anafanya yeye mwenyewe, mimi kwasasa hivi ni ndugu yake sio Manager”.

Mwezi uliopita Wema Sepetu alikumbwa na skendo ya kusambaza picha zake za faragha akiwa na mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.

Martin Kadinda Abeba Tuzo Ya Ubunifu Wa Mavazi

Mbunifu wa mavazi na aliyekuwa meneja wa muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amenyakua tuzo Kama mbunifu bora wa mavazi wa mwaka 2018.

Katika Usiku wa Maonyesho ya Mavazi ya Kiume yaliyofanyika Lagos nchini Nigeria siku ya Novemba 16, 2018, mbunifu wa mavazi maarufu Bongo, Martin Kadinda alijinyakulia tuzo hiyo kubwa na ya heshima.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Martin Kadinda aliandika:

To the World., Designer of The Year Africa?@themanawardsAfrica’s Designer of The Year 2018…!! ??Am Humbled. The World Is ReadY?

Shukurani Za dhati kwa mwenyezi Mungu kwa Afya, akili na ubunifu…Shukrani kwa Wizara Ya Habari, michezo na Utamaduni Kupitia Basata.Shukurani za Dhati kwa Familia, mama Yangu, dada na kaka zangu.. wadogo zangu na ndugu zangu wote…@wemasepetu and Ur Amaizing Team wema and die Hard fans??????..MK empire with All the Love and Support always??My friends mnajijua.. cant mention all of you.. ila asante sana.

Las Vegas nawasahauje sasa????. Majirani zangu vipenzi sijawasahau.Nitamaliza wote ? My fans in Belgium, south africa, Holland, china, states and All of the World ?.

Martini alianza kujizolea umaarufu kwenye ulimwengu wa fashion miaka kadhaa iliyopita Baada ya kutoka na staili ya makoti ya single button ambayo ilivaliwa na mastaa wakubwa Kama Diamond Platnumz na Hemed PHD.

Sijaangalia Video Naogopa, Nitaangalia Nikitulia:-Martin

Aliyewahi kuwa meneja wa mwanadada wema sepetu martin kadinda amefunguka na kusema kuwa kwa kitendo cha wema kuomba msamaha kinaweza kuwa ni jambo kubwa ambalo wema amejifunza na kujutia kile alichokifanya.

Martin anasema kuwa kuna mambo mengi ya wema machafu yamewahi kutokea lakini hajawahi kuita waandishi kwaio kwa hili linaweza kuwa kubwa litakalo weza kumrekebisha sana na kuanzi sasa anaamini kuwa  ataanza kubadilika.

ninaamin kuwa kila mtu ana makosa hata wewe  uliyepo nje ya kamera pia una makosa, na ili uweze kujifunza na kukua lazima kuna mahali unaweza kukosea na kuweza kurekebishwa.kwaio  kitendo cha kuita waandishi ni kitendo cha kuonyesha kuwa kweli amekosea na anataka kujifunza, aliniambia kuwa anahitaji press nyumbani kwa mama yangu nikajua ni muda muafaka wa yeye kuongea na watu wake.

kwa sababu sasa hivi ameweza mpaka kuita press basi ni kweli atakuwa amejifunza, video sijaina ingawa ipo kwenye simu yangu lakini sijataka kuifungua kwa sababu ujumbe tu unaogopesha.nina shughuli kubwa ya kufanya ijumaa nikitulia na kumaliza shughuli zangu nitaiangalia.

Martin Kadinda Ajikanyaga Kuhusu Penzi La Wema na Diamond

Mbunifu wa mavazi na mwanamitindo maarufu nchini Martin Kadinda ambaye pia anajulikana hasa kwa kuwa Meneja wa Muigiaji wa Bongo movie Wema Sepetu, amejikuta katika wakati mgumu na kujikanyaga alipoulizwa kuhusu hali ya penzi la Wema Sepetu na Diamond Platnumz.

Wiki iliyopita aliyekuwa Staa Diamond Platnumz aliachana rasmi na mpenzi wake Zari na hivyo kuacha nafasi ya watu kujaza nani atakuwa na Diamond kwa hivi sasa na moja kwa moja kila mmoja alielekeza macho yake kwa Wema.

Wema na Diamond wamekuwa wakitawala headlines mbalimbali kwenye social media wakidaiwa kuwa wamerudiana huku kitu kikubwa kilichosababisha hiyo yote ni baada ya Wema kuonekana akikumbatiana na Diamond hadharani.

 

Diamond na Wema wiki chache zilizopita

Martin sio tu alikuwa meneja wa Wema bali pia ni rafiki wa karibu kwaiyo kutokana na ukaribu alionao na Wema gazeti la Amani lilimtafuta na kumuuliza endapo hizi tetesi zinasombaa kuwa Diamond na Wema kurudiana zina ukweli wowote m? Cha ajabu Martin alijikanyaga sana kujibu swali hili mwishowe alisema;

Jamani mimi siwezi kuzungumzia lolote kuhusu hilo na hata sijui nianzie wapi kuzungumza lakini kama ishu nyingine yoyote nitazungumza kwa mapana yote lakini sio suala hilo hata kidogo kwa kweli”.

Martin aliulizwa swali hilo kwa sababu siku ya tukio la Diamond na Wema kukumbatiana na kupeana busu wiki chache zilizopita Martin naye alikuwepo na alionekana kuongea na Diamond Pamoja na Wema.

Wema Ni Mkorofi Kutoka Ndani -Martin Kadinda

Mwanamitindo maarufu nchi Martin Kadinda ambae pia ni mtu wa karibu wa Wema Sepetu, amefunguka na kusema tabia za Wema ambazo inawezekana mashabiki wake  wamekuwa hawajui kuhusu yeye.Martin Kadinda anaasema kuwa kwa watu wasiomjua wanaweza kusema Wema ni mpole lakini ukweli ni kuwa Wema ni mkorofi sana kuliko vile watu wengi wanavyoweza kuamini.

Akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, mwanamitindo huyo amesema kuwa  Wema Sepetu yupo tofauti sana na vile watu wanavyomfikiria na kumuona kwenye mitandao ya kijamii, kwa sababu yeye anamjua Wema vizuri kuliko mtu yoyote na hivyo huwa anajua kabisa pale anapogombana na mtu kuwa Wema ameguswa wapi mpaka amefikia hatua ya kuongea maneno hayo.

wema ni mkorofi kutoka ndani kabisa,lakini huwa anajitahidi kadri ya uwezo wake na nguvu zake zote ili ukorofi ule usionekane,lakini pia akiamua kukorofisha anakorofisha kwelikweli,kuna matukio mimi nakisikia anafanya tu najua kabisa hapa wema ameguswa wapi” Alisema Martin

Hata hivyo Martin anaendelea kusema kuwa Wema Sepetu ni mwanadada ambae ana moyo wa huruma sana na anapenda sana kuongeza marafiki kiasi kwamba huweza kumuamini mtu yeyote hata kama bado hajamjua vizuri  “lakini pia kitu kingine ambacho Wema anacho ni open door,milango ya moyo wake iko wazi sana, na yuko wazi kiasi kwamba anaweza kumuamini mtu yeyote,mtu yeyote anaweza kuaj kwake na akwa rafiki yake na akalala hata kwake” aliongea Martin Kadinda

Martin ambae amekuwani mtu  karibu zaidi na Wema kuliko mtu yeyote yule, amekuwa ni moja ya watu wanaojitahidi kumuongelea sana Wema hasa pale watu wanaongea maneno tofauti na vile alivyo,kuna kipindi Martin alishawahi kusikika akisema kuwa  ni vigumu kufanya kazi na Wema kwa sababu Wema ni mtu asiyekuwa kiakili, amekuwa ni mtu wa kupaniki sana anapokutana na jambo.

Ukiachana na kuwa mwanamitindo na Designer wa Wema kwa kipindi cha nyuma, Martin pia alishawai kuwa meneja wa Wema Sepetu lakini baadae walisitisha kazi hizo na sasa wamebaki kuwa marafiki tu.

 

Martin Kadinda Afunguka Kuhusu Ugumu Anaopata Kufanya Kazi na Wema Sepetu

Mbunifu wa mavazi Martin Kadinda ambaye pia ni meneja wa Msanii wa Filamu na Mwanamitindo Wema Sepetu amefunguka kuhusu changamoto anazopata kufanya kazi na mtu maarufu kama Wema Sepetu.

Katika mahojiano aliyoyafanya na kituo cha redio cha East Africa Martin aliweka wazi kuwa anapata wakati mgumu sana kufanya kazi na Wema kwasababu hakui kimawazo kutokana na wakati unavyozidi kwenda. Amesema licha ya kuwa anampenda sana Wema na kuwa ni mtu muhimu kwenye maisha yake iwe kwa sababu ya kazi au bila kazi bado ataendelea kumheshimu   kwani tayari wana uhusiano mzuri sana.

Martin aliendelea kusema;

“Changamoto kubwa kwangu unajua Wema ni mtoto hakui, yaani miaka inakwenda bado yupo vile vile kikubwa ni kuweza kumtengenezea  mazingira ili kesho na kesho kutwa aweze kuheshimika. Unajua Wema ana maisha yake binafsi na vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.

Wema ni moja kati ya msanii anayependwa sana na Watanzania kutokana na Urembo wake lakini pia  ana kundi kubwa la mashabiki wanaojiita #teamwema. Hivi sasa Wema amejiingiza kwenye biashara zaidi ambapo anauza pia bidhaa mbalimbali za urembo pia hivi karibuni amefanya filamu yake mpya inayoitwa ‘Heaven sent’ ambayo inafanya vizuri sana sokoni

 

 

Wema Sepetu amsifu Martin Kadinda katika ujumbe alioamwandikia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa

Aliyekuwa manager wa Wema Sepetu, Martin Kadinda hivi leo amesherekea siku yake ya kuzaliwa na kama kawaida marafiki wake wa dhati wamekuwa wakimpost kwenye Instagram huku wakimsherekea leo.

Wema Sepetu ni mmoja wa marafiki waliompost Martin Kadinda. Katika ujumbe wake, Wema Sepetu alimsifu Martin na kumfungulia roho katika ujumbe wake uliowaacha mashabiki na tabasamu. Aliandika kusema,

Wema sepetu akiwa na Martin Kadinda

The World Knows How I feel about You… I have nothing more to add to dat… I love you more everyday than yesterday… (Mi nakupenda Leo kuliko Jana, ?) Happy Birthday wa kwangu mimi apa…. Wa Sunny, Wa Sunshine, Kaka manager wa kwanza kabisa duniani… Yaani hapa natafuta maneno mapya mapya ambayo sijawahi kukwambia ila najikuta nakosa maana yote nishamalizaga… Basi wacha niache kutype….

Wawili hawa wamekuwa marafiki kwa miaka mingi na ata baada ya Martin kuanza biashara zake, bado wako pamoja kama ndugu na dada.