Ali kiba sio Staa, ni Maarufu Tu :-Pretty Kindy

Mwanadada prety kindy ambae ni msanii wa bongo fleva amefunguka na kusema kuwa kwa anavyoona yeye , Alikiba sio staa wala msanii kama diamond lakini ni umaarufu tu ndio unamsaidia kuuza kazi zake za muziki.

Pretty kindy ameyasema hayo huko akitoa sababu kuwa hata huko nje ya ncini, wasanii kama diamond wamekuwa wakipendwa na kujulikana sana kiasi kwamba mt anaweza kusikia nyimbo yake moja na akaamua kwenda you tube kutafuta nyingine kutokana na ufundi aliousikia katika nyimbo moja kama kwa msanii Diamond lakini sio Alikiba,.

Pretty kindy anasema kuwa uwezi kumfananisha Alikiba na Diamond kwa kujulikana  na kupendwa duniania , alkini pia anasema kuwa alikiba ujikuta anaweza kila kitu na kuvimba ndio maana watu hawamjui.

Alikiba ni msanii maarufu wala sio staa, mimi nimekaa nje kwaio nimekuwa nikiona watu wanavyomfatilia diamond na kufatilia nyimbo zake lakini watu hawamjui kiba.wakati mwingine huwezi kujua ni wapi mtu anakosea lakini kwa Alikiba naona kama anatabia ya kuvimba na kujiona amemaliza kila kitu.

Emoji ya Alikiba Yazua Matusi Mtandaoni.

Ikiwa zimepita siku kadhaaa tabfu msanii wa muziki wa kizazi kipya alikiba kusema kuwa hawezi kuweka picha ya marehemu katika ukurasa wake wa Instagram kwa sababu dini yake hairuhusu na watu kum-judge sana kuwa hakuna dini inayokataza kitu kama hicho .

Baada ya kutokea kwa msiba wa mtoto wa Muna, watu wengi waliweka icha za kijana huyo katika ukurasa zao za instagram lakini Alikiba nae alikuwa mmoja kati ya walioguswa na msiba ingawa kwake imekuwa tofauti kidogo kutokana na picha aliyoitumia kufikisha ujumbe wake wa huzuni katika ukurasa wake.

Baada ya kuweka emoji hiyo  nasio picha ya patrick watu walianza kumshushia matusi msanii huyo huku wakisema kuwa hakukuwa na haja ya yye kuweka emoji wakati picha za mtoto huyo zipo na pia hakuna haja ya kwa sababu kuweka emoji hakumaanishi chochote.

baadhi ya maoni ya mashabiki zake wakimponda kwa kufanya hivyo inasema ‘Ali ulikosea sana uliposema dini yako inakataza kupost marehemu wakati kuna mengi dini yako inakataza lakini bado unayafanya.”

wewe Alikiba una dharau sana na ndio mana sikupendi sasa hilo limdoli linamaanisha nini sasa mfyuuu, R.I.P

Laizer Aliwahi Kufanya Kazi na Alikiba Kabla ya WCB

Mtayarishaji wa nyimbo kutoka wcb amefunguka  na kutoa orodha ya wasanii aliowahi kufanya nao kazi hapo awali kabla ya kuingia na  kufanya kazi na WCB , laizer amewataja watu hao kama Ommy Dimpozi, Alikiba, Sharo Milionea .

Kabla ya kuja WCB niliwahi kufanya kazi na wasanii wakubwa sana m nakumbuka nilisahwahi kufanya kazi na ice prince zaman wa nigeria, nakumbuka nilishawahi kufanya kazi na  Ommy Dimpozi niliwahi kufanya kazi na Alikiba pamoja na marehemu Sharo Milionea.

Pamoja na kufanya kazi na wasanii mbalimbali lakini kwa sasa,Laizer ame-settle na kufanya ngoma nyingi na kazi nyingi za WCB na ngoma hzo zimekuwa gumzo katika kazi za wasanii wa WCB

Kocha Julio Ataka Kumsajili Alikiba Katika Timu Zake.

Baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya timu ya Alikiba na timu ya Mbwana Samatha ailiyofanyika uwanja wa taifa jumamozi iliyopita. kuekuwa na maoni mengi sana kuhusu mechi hiyo huku wakifurahi na kuwashukuru watu wote waliojitokeza kuangalia mechi hiyo iliyokuwa na lengo la kutumia pesa zilizopatikana kwa ajili ya kusaidia elimu katika shule zenye mazingira magumu.

Katika moja ya maoni yaliyojitokeza ni kuhusu  alikia kutoka kwa kocha  Jamhuri Kiwhelu maarufu kama Julio aliyekuwa kocha kutoka upande wa Alikiba huku akisema kuwa msanii huyo ana uwezo mkubwa sana wa kucheza mpira laki i amekuwa akimshawishi kufanya mpira na amekuwa akimkatalia kila mara.

mara nyingi nimekuwa nikimwambia alikiba aje nimsajili katika timu ninazofudisha  ila hatokuwa akicheza mikoani mpaka timu itakapokuwa ikicheza dar es salaam ndio aje kucheza.ninachoweza kusema ni kwamba alikiba ni mchezaji ambae akipata mwalimu anaejua kufundisha kama mimi  anaweza kuwa mchezji mzuri sana .

Nyimbo Moja ya Diamond ni Nyimbo 4 za Alikiba ;-Ripoti ya Youtube

Miaka kadhaa nyuma iliyopita mwanamuziki Diamond Platinumz aliwahi kutoa nyimba na msani kutoka Nigeria Mr. Flavour, wimbo ambao ulimpatia Diamond viewers wengi sana kiasi cha kufikia milion 4o views katika wimbo wake mmoja tu katika mtandao wa you tube.

kwa jinsi idadi hiyo ya views inavyotolewa na youtube kwa upand wa msanii diamond na alikia unakuja kuoa kuwa katika viewers wa alikiba wa nyimbo zake nne za hivi karibuni ikiwepo Seduce me,Aje , Nagharamia na Mwana Dar Es Salaam  kwa ujumla wake zinaleta viewers milioni 40 ambayo ni sawa na wimbo mmoja wa msanii diamond aliwai kufikisha katika wimbo wake huo wa nana.

wawili hawa pamoja na kwamba wamekuwa mahasimu wakubwa lakini wamekuwa wakifanya kazi kwa malengo hasa ya kuwakosha mashabiki zao katika tasnia hii ya muziki.swala sio kuleta ushindani wa kugombana lakini kubwa ni kuangalia jinsi gani wasanii hawa wawili waliweza kufanya ngoma zao na mafanikio yao yalikuwaje kwa hivi karibuni.

Alikiba Aweka Wazi Kikosi Chake , Mpoki Yumo Ndani.

Kuelekea siku ya kuchangia vifaa vya elimu Tanzania huku watu maarufu kama Alikiba na Mbwana Samatha wakiwa katika mechi zitakazochauana uwanja wa taifa kwa ajili ya kuhamasisha kampeni hiyo kutokea na kufanikiwa, mdanii alikiba amweka wazi kikosi chake siku hiyo.

Alikiba ambae atakuwa team pinzani na mbwan samatha ameweka wazi kikosi chake na kuwachukua watu kama Emmanuel Okwi,John Boko, Msuva  Erasto Nyoni na pia amemuweka mdogo wake Abdul Kiba.

kikosi cha alikiba

Hata hivyo jambo kubwa na zuri la kufurahisha siku hiyo ni kwamba abdul kiba amemchagua mpoki kutoka katika uchkeshaji kuwa ndio msemaji mkuu wa timu yao , ambae ndio atakuwa akiongea kila kitu kuhusu team yake.

Msanii wa vichekesho , Mpoki

Alikiba na samatha watakutana uwanja wa taifa june 6 mwaka huu kwa ajili ya kuhamasisha kuchangia elimu kwa watoto wanaosoma katika mazingira magumu.

 

Man Waletr Aelezea Sababu ya Alikiba Kutofanya Collabo na NE-YO

Mtayarishaji wa nyimbo nyigi za msanialikiba , man walter amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa ya msanii alikiba kushindwa kufanya collbao na msanii mkubwa duniani NE-YO katika wimbo wake wa seduce me kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

man walter  anasema kuwa pamoja na kwamba maandalizi yalikuwa yamekamilika na kila kitu lakini walikuja kugundua kuwa msanii huyo alikuwa anakuja afrika na alikuwa na collabo na wwasanii wengi sana frika hivyo wakaona kuwa itachukua muda sana kuwasubirisha masgabiki .

nilipigiwa simu kuwa kiba nakuja kufanyakazi na ne-yo na kweli nikatafuta biti ikawa kidogo inafanana na ile ya miss independence , nikaitoboa kidogo na nikapata kitu nilikuwa nataka yenye maazi ya kiafrika zaidi na hata kiba alifurahi sana.

tukatuma pia kwa neyo zile biti na zote alizipokea lakini baada ya hapo sijui kwa nini kiba aliamua kubadilisha maamuzi yake , labda pengine aliona kuwa ne-yo alikuwa na collabo na wasanii wengi sana afrika , watu wasije wakaona kama vile tumedandia kolabo ya bure tukaona bora tuachane nayo.

Tetesi za alikiba kufanya kolabo na ne-yo zilikuwa sana kipindi cha nyuma na baada ya muda ndipo pia hata diamond alipota kolabo na msani huyo.Hivi karibuni kulikuwa na habari kwamba msanii alikiba anatarajia kufanya kazi na fally ippupa kutoka congo.

Baada ya Kupelekwa Mahakamani, Alikiba Kupima DNA

Msanii alikiba ambae siku kadhaa zilizopita alipelekwa mahakamani kwa ajili ya madai ya kushndwa kumhudumia mtoto wake wa kike aliyezaa na mwanadada sabby angel ametakiwa kwenda kupima DNA kwa sababu msanii huyo aamini kama mtoto huyo ni wa kwake.

Akiongea  na moja ya radio  jijini Dar , mama wa mtoto huyo amsema kuwa msanii huyo aamini kama mtoto ni wa kwake kwaio mahakama imetoa barua ili wakafanye vipimo vya DNA kuthibitisha hilo.

Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa anajiamini na anaamini kuwa mtoto huyo ni wa kwake na alikiba na sio vinginenvyo.

Ninatamani sana yaishe n niliamini kuwa nikimpeleka mahakamani basi tutaongea na yataisha lakini tulipoenda mahakamani , mahakamni ikatoa amrikuwa tukachukue barau na kwenda kwa mkemia mkuu kupima DNA kwa sababu yeye anasema aaamini kama mtoto ni wa kwake na mimi ninajiami sana kwaio ndo maana ninahangaika.

Mama wa mtoto wa alikiba akiongea kwa uchungu.

Sitakuwa na chakumuelezea huyo mtoto kwa sababu anaona kila kitu na kama atajiridhisha basi hakutakuwa na kitu kingine tena, na ninauhakika  kuwa huyo mtoto ni wa kwake na ndio maana nahangaika , na nimeenda leo barua ziko tayari lakini yeye hayatokea.

Alikiba Ajitolea Kuwa Balozi wa Elimu Tanzania.

Msanii Alikiba ametangaza rasmi kujitolea kuwa balozi wa elimu tanzania na kuwatangazia mashabiki wake wote kujitokeza siku ya June 6  katika kufanya harambee ya kuchangia upatikana wa vitabu na vifaa mbalimbali vya mashuleni.

Akiamua kurudisha fadjila kwa jamii yake laikini pia kuamua ku-bond na kuwa  karibu na mshabiki zake , alikiba atakuwepo kama moja ya wachezahji wa mpira wa miguu siku ya tarehe hiyo katika  uwanja wa taifa jijini Dar Es Salaam katika mechi ya kirafiki na mashabiki wake huku lengo kuu ikiwa ni kuhamasisha uchangiaji wa vifaa vya elimu.

mimi Ally Saleh Kiba  kwa kutambua umhimu wa elimu nchini ninaamua kujitolea  kuwa balozi siku ya june 6 nitacheza mchezo wa kirafiki uwanja wa taifa  khamasisha uchangiaji wa vifaa vya elimu  na miundombinu mashuleni

Alikiba nawaalika mashabiki wake na mashabiki wa mpira wote kujitokeza siku hiyo pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ili kufanikisha lengo la kuinua elimu na musaidia kuondoa changamoto mbalimbali zinazopatikana mashuleni.

Hii haitakuwa mara ya kwanza Alikiba kujitokeza hasa katika mpira akiwa na lengo la kufanya bonding na kurudisha mapezni yake kwa mashabiki zake pia.

Mimi ni Supa Staa Nitaishi Maisha Niliyoyachagua ila Nitaendelea Kuwa Humble kwa watu:-Alikiba

Msanii wa bongo fleva Alikiba anefanya vizuri na wimbo wake wa mvumo wa radi amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba yeye ni staa lakini amekuja akijali sana mashabiki zake kwa sababu ndio wanaomfanya yeye kuwa staa kila siku.

Alikiba nasema kuwa alichagua kuwa staa lakini hawezi kuishi maisha ya kuigiza kwa sabbau ya ustaa alionao na hii haitamfanya kuishi na watu vizuri kwa sababu eti yeye ni staa hata siku moja.

Alikiba ambae kila siku amekuwa akitaka kujishusha na amekuwa sio mtu wa kuongea kitu chochcote kuhusu mafanikio yake zaidi ya kuwashukuru mashabiki, anasema kuwa unapofanya kitu kizuri kitajitangaza chenyewe wala hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi kutengeneza kiki ili ujulikana na jamii.

kuna maisha ya ustaa na kuna maisha ya kawaida kabisa, na kuna  maisha ya kuigiza kuwa staa,mimi ni staa na mimi ni supa staa na nitaishi maisha niliyoyachagua  lakini bado nitaendelea kuwa humble kwa watu.

 

Ali Kiba Ataja Jina Lake Halisi, Kumbe Kiba Sio Lake.

Watu wengi wamekuwa wakijua kuwa jina la kiba ni jina la ukoo la familia hiyo na hii yote ni kutokana na kwamba ndio  ilivyozoeleka kwa sababu familia yote na ndugu wa karibu wa ali wamekuwa wakitumia jina hilo kama ndio jina la ukoo na kumbe sio kweli kuhusu hilo.

Kwa mara ya kwanza msanii ali kiba amefunguka asili ya jina lake hilo lakini pia amesema kwa nini na wapi lilitokea jina la alikiba kama watu walivyozea kumuita,Alikiba nasema kuwa jina lake halisi kabisa ni Ali Saleh Gentamilan lakini jina la kiba lilitokea kutokana na utani waliokuwa wakimtania mama yake kipindi cha ujauzito wake.

Alikiba anaelezea kuwa kipindi mama yake mzazi akiwa na mimba alikuwa akipenda kubana nguo zake na  vibanio na ndipo walipoanza kumwita mama vibania na alipozaliwa yeye akapewa jina la kibanioa na ndipo lilipotokea jina la kina ikiwa ni kifupi cha kibanio.

Hata hivyo jina hilo lilizoeleka kutoka utoto kwake na wadogoza ke na ndio aliona liwe jina lake la usanii kitu mbacho limechukua familia yote na kuwa kama jinala ukoo.

Afr_connect Yawakutanisha Vyonne Chakachaka na Mrs. Alikiba.(+picha)

Mke wa msanii Alikiba Bi .Amina amefanikiwa kukutana na msanii mkubwa kutoka afrika ya kusini  vyonne chakachaka  katika kongamano  la Afr_Connect .kongamano ilo ambalo ambalo lima lengo la kuzungumzia maswala ya wanawake ambapo katia kongamamno ilo alikiba alipata bahati ya kuimba kwa mara ya kwanza wimbo wake aliomshirikisha Vyonne Chakachaka unaomzungumzia mwanamke wa kiafrika unaojulikana kama Akili ya mama.

Alikiba na mke wake akiwa na waziri Ummy Mwalimu.

Alikiba akiwa na mama vyonne chakachaka wakiimba wimbo wao mpya.

Alikiba akiwa na vyonne pamoja na mkewe.

wadau na watu mbalimbali wakiwa katika kongamano la Afr_Connect.

Mo Faya ya Alikiba Kudhamini Matangazo ya Kombe la Dunia.

Msanii wa bongo fleva Alikiba siku ya jana aliungana na mashabiki na watu wengine katika uzinduzi wa matangazo ya kombe la Dunia mwaka huu kupitai DSTV ambapo akiwa kama  bosi wa Mofaya Alikiba na kampuni yake pia watahusika katika kudhamini matangazo ya mpira kupitia channel mbalimbali za kombe la Dunia.

Akiongea na waandishi wa habari wa clouds E , Alikba ansema kuwa pamoja na kwamba ndio anaanza lakini haoni kukatishwa tamaa na uamuzi huokwa sababu kwake ni swala la kujivunia kuwa moja ya wadhamini katika matangazo hayo.

Nikiwa kama msanii najivunia sana na mo faya kuwa mdhamini wa matangazo haya ya kombe la dunia katika channel za dstv, tunachotakiwa sio kuvunjika moyo lakini kujaribu kufanya kitu kwa ajili ya kuendeleza na kuwafikia mashabiki wetu.

 

 

Mimi ni Mswahili, Ninajivua Uswahili:Alikiba

Msanii Alikiba anwataka watanzania kutumia lugha ya kiswahili na kujivumia kuitumia lugha hiyo kwa sababu ni lugha adimu nawatu wengi wamekuwa wakiatamani sana kujifunza kutokana na uadimu wake , hivyo watanzania wakitumie kwa kujidai.

Alikiba anasema kuwa hata wasanii wanapaswa kutumia sana kiswahili katika nyimbo zao kwa sababu hiyo ndio njia kubwa ya kukikuza na kukitangaza kwa watu wengine wa nje bila kuona aibu kukitumia kwa watu hata wa nje.

Lugha yetu ni nzuri na tunapaswa tujivunie sana,najivunia sana kuongea kiswahili na nitaongea kiswahili,kwaio kila mtanzania ni lazima ajivunie kukijua kiswahili.asikwambie mtu kuachwa uswahili, aana hiyo siyo sifa mbaya.

Alikiba ansema kuwa watu wengi wamekuwa wakitamani sana kujua kiswahili kwa sababu amekuwa akiona katika matamasha makubwa huko nje ya nchi wanavyopata usumbufu kutaka kufundishwa kiswahili.

 

Mkali Wenu Aongelea Wimbo wa Alikiba Kubuma

Mchekeshaji wa maigizo ya timamu tv Mkali Wenu amefunguka na kuongelea swala la wimbo wa Alikiba mpya uliotoka hivi karibuni jinsi ulivyotoka lakini hakuna attention yoyote katika mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa katika wimbo wa Seduce me.

Mkali wenu anasema kuwa wimbo wa Seduce me ulikuja na kukatokea vitu vingi sana katika mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na bifu zito kuendelea kati ya Kiba na Diamond lakini huu wa sasa haukuwa na vitu hivyo.

kwakweli kuna tofauti katika alivyotoa wimbo wa seduce me  na wimbo wake huu  mpya , wakati wa seduce me kulikuwa na vitu vingi sana mara diamond kamwita Ali Kipusa  mara vitu vilikuwa vingi sana viliwafanya watu wengine wapate attention ya kusubiri wimbo mpya.baada ya kutoa tu watu wakaona kuwa kidume katoa kitu lakini sasa hivi katoa hakuna skendo yoyote , mange hajaposti kama ilivyokuwa kwa seduce me, imeenda lakini sio kama mzuka wa mwanzoni.

Alikiba Apokea Tuzo ya Nyota wa Michezo.

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii Alikiba kutoa wimbo wake mpya wa mvumo wa radi, siku ya jana msanii huyo amepewa tuzo ya heshima kama nyota wa michezo kutoka katika kipindi cha The Playlist cha radio moja nchi ya   Times fm.

Tuzo hitoaliokabithiwa Alikiba amepewa kama kuonyesha jinsi gani amekuwa akitambulika kwa mchango wake mkubwa wa kuipeperusha bendera ya taifa na pia jitihada zake alizokuwa akifanya mpaka sasa tangu alipoanza kwa kuwafanya wasanii wengine kutokata tamaa na kujituma ili kufanikiwa katika muziki huku yeye akiwa kama moja  ya wasanii wanaoangaliwa kama mfano.

Times Fm walishawahi kutoa tuzo hiyo kwa wasanii wawili kabla ambao ni Vannesa Mdee pamoja na Diamond Platinmuz na sasa ni Alikiba.