Alikiba anayetamba na kibao chake cha Mvumo wa Radi ameyasema hayo katika mahojiano na Azam Tv mwezi huu wa Agosti kupitia kipindi cha Nyundo ya Baruan.

”Mwendo wa muziki wa Bongo Flava unakwenda vizuri ijapokuwa kuna watu wanachanganya tu muziki na wengine wanaaribu muziki na wengine wanakwenda nao vizuri lakini hiyo pia siwezi kuichambua kwa sababu kila mtu anakipaji chake,” amesema Alikiba

Alikiba ameongeza ”Wengine wanafanya kwa kujifurahisha na wengine wanafanya kwaajili ya maisha yao lakini muziki kidogo umepungua nguvu.”

”Ninaimani kwa sababu ya tuzo za Tanzania zilikuwa zinawahamasisha sana watu, wasanii walikuwa wakifanya kazi vizuri na kwa bidii anaamini kwamba siku moja ataitwa na atapewa heshima unajua tuzo ni heshima tu.”

”Kwa hivyo changamoto kidogo imepungua, kasi imepungua ni kutokana na tuzo kwa vijana maana mtu anaweza kujitungia nyimbo yoyote ambayo haina kichwa wala miguu sababu hategemei chochote lakini pia kampuni yangu ya Mo Faya inamipango hiyo ya kuwahamasisha vijana kufanya tuzo baadae Insha allah.”

Mwanamuziki huyo anayefanya vizuri barani Afrika amesema kuwa wasanii anao wakubali kutoka katika bara hili ni Oliver Mtukudzi kutoka Zimbabwe na mama Yvonne Chaka Chaka wa Afrika Kusini.