Yound Dee:Amber Lulu Hana Hadhi Ya Kutembea Na Mimi

Wasanii Amber Lulu na David Genzi maarufu kama Young Dee wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu huku ikisemekana kuwa wawili hao inawezekana bado wanapendana au wamekuwa wakioneana wivu tena hasa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu na kisha kuachana na wote kuendelea na maisha yao ya kawaida. Lakini swala linakuja palepale  ni aidha wawili hao watakuwa bado wanapendana lakini hakuna anaeweza kumuanza mwenzake ndio maana inakuwa ni vita kila siku katika mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Amber Lulu aliwaonya mashabiki katika mitandao kuacha  kumfananisha Young Dee ambae alikuwa mpenzi wake wa zamani na mpenzi wake wa sasa ambae ni Prezzo mwanamuziki kutoka Kenya na kusema kuwa Young Dee hana kiwango chochote cha kulinganishwa na Prezzo katika mambo yote.

Msanii Young Dee ameamua kumjibu na kuwajibu waandishi kuwa amekuwa anachoshwa sana na tabia ya waandishi wa habari kuwa na maswali yanayomuhusu Amber Lulu kwake, na amesema kuwa  Amber Lulu hana hadhi ya kuwa na yeye ana swala la kuwa wanamuuliza maswali ya Amber Lulu mara kwa mara yamekuwa yakisumbua uhusiano wake mpya.

Nimechoka kuulizwa maswali kuhusu mimi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Amber Lulu,hana hadhi ya kuwa na mimi na ninaomba nisiulizwe kwa sababu mnaniharibia sana mahusiano mapya na mpenzi wangu wa sasa.

Amber lulu ambae amejiingiza katika mahusiano na prezzo maekuwa akichukizwa na baadhi ya watu katika mitandao ambao wamekuwa wakimfananisha msanii huyona mpenzi wake huyo mpya .

Amber Lulu aeleza sababu hawezi toka kimapenzi na wanamuziki wa Bongo

Amber Lulu anaonekana kuwa anazifuata nyayo za Gigy Money kwani pia yeye anajitambulisha kama muimbaji. Video vixen huyo kutoka Tanzania hata hivyo amefunguka kueleza sababu yeye Kama mwanamke hawezi taka kutoka kimapenzi na wasanii wa Bongo.

Amber Lulu alibainisha haya alipokuwa akizungumza na Bongo Dot Home ya Time Fm akisema kuwa wasanii wengi wa Bongo hues hawana msimamo na kwa sababu ya jambo Kama hilo, yeye hatamani kupata mpenzi anayefanya mziki wala mtu maarufu. Amber Lulu alisema,

” Mastaa wengi bongo ni wasumbufu sana, mimi huko nyuma niliwahi kuwa katika mahusianio na hao mastaa nikaona aah basi bora niachane nao, naona walivyo kwa sasa na najua wanavyoishi ndio mana sina mpango nao.”

Aliendelea kwa kusema,

“Wastaa wengi hawako serious sana na hata kwenye maisha yao hawako serious, mie naona mastaa naoshindanao naona kabisa hata akiwa na mpenzi kuna kitu kinamiss , unakuta mtu anakaa na watu hata watano yani.”

 

Amber Lulu ataja sababu amazomtamani Diamond Platnumz

Amber Lulu ambaye anatamba sasa kwa kutokea kwenye video za mziki za Bongo ni mrembo ambaye anatisha.

Kwa hivi sasa anafanya vyema kwenye career yake na ingawa bado yeye ni mdogo. Hata hivyo, hivi karibuni alifunguka kumuongelea Diamond Platnumz huku akisema kuwa ni mmoja wa wasanii ambao anatamaniwa na warembo wengi.

Lulu alisema kuwa Diamond Platnumz anaonekana Kama mwanaume kwenye bidii na ikiwa hangekuwa na familia pia yeye angejaribu bahati yake, akiongea na Times FM, Lulu alisema…

 

“Kibongo Bongo sijaona mwanaume zaidi ya Diamond kwanza ana ni inspire na maisha yake yaani anajiweka kazi na kila kitu na sio kwamba na wish ku’date nae tuu bali kufanya nae kazi pia,”

Aliendelea kwa kusema,

“Kama ikitokea kutembea nae is ok….sio mimi peke yangu kila mwanamke anawish kuwa nae…kila mtu mimi naamini wachache sana ambao hawamuhitaji.”