Aunty Ezekiel na Tunda Ndani ya Bifu Kali Warushiana Matusi ya Nguoni

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amejikuta katika vita kali ya maneno na mrembo Tunda baada ya kupishana kuhusu malipo ya pesa ya pombe ambayo Tunda alikopa.

Siku ya Jana Warembo hawa waaili waliingia kwenye mabishano makali kwenye mtandao wa Instagram baada ya Aunty Ezekiel kwenda kwenye ukurasa wa Tunda na kumdai pesa yake kiasi cha laki moja alichochukua pombe ya Belaire.

Ambapo kwenye ukurasa wa Tunda Aunty Ezekiel aliandika maneno haya:

Baada ya Aunty kumuandikia vile inaelekea Tunda hakupenda kabisa kwani mara moja alianza kutokwa na povu kueleza kuwa alimpa pesa Mose Iyobo huku akimuita kiben-10 na kumtuhumu kwa kuitumia pesa ile. Hili ndio lilikuwa povu la Tunda:

 Uzee unakujia vibaya we we Bibi Mdashi na Una lako jingine nje ya pombe jibu ni lile lile ongea na Ben-ten wako akueleze pesa alipopeleka”.

 

 

Lakini habari chini ya kapeti zinafai kuwa kilichotokea ni kwamba Aunty Ezekiel anafanya biashara ya kuuza hizo pombe za Belaire sasa Funds alimpa ofa Diamond ya hiyo chupa moja ambayo ni laki moja kwa kipindi hiko Diamond na Tunda walikuwa wapenzi sasa baada ya Tunda kumuona juzi Diamond yuko na Wema na kusikia wamerudiana alikasirika na kugoma kumlipia tena ile pombe aliyompa ofa na hapohapo ndipo kizazaa zaa kilipoanza rasmi na wao kuja kurushiana maneno mtandaoni.

Aunty Ezekiel Kuhusu Ugomvi Wake na Iyobo “Hata Vikombe Vinagongana”

Muigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amefunguka kuhusu ishu ya ugomvi wake na mpenzi wake pia baba watoto wake mcheza shoo kutoka WCB, Mose Iyobo.

Aunty Ezekiel na Iyobo wamekuwa kwenye mahusiano sasa kwa muda wa miaka minne name kwa pamoja wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Cookie, lakini couple hii sio zile za kupenda kiki mitandaoni kwaiyo ilivotokea Aunty kurusha dongo mtandaoni wengi walishtuka.

Wiki iliyopita Aunty Ezekiel alizua gumzo mtandaoni baada ya kuweka posting yenye utata mtandaoni iliyoashiria kuwa yeye na mpenzi wake Mose Iyobo wapo kwenye migogoro fulani hivi.

Baada ya posti hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii tetesi zilisambaa labda huenda Aunty na Iyobo tayari wameachana kutokana na michepuko.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo TV Aunty alifunguka na kudai kuwa kwenye mahusiano kugombana ni kawaida kwa sababu wote ni binadamu:

Unajua waswahili wanasema hata vikombe vinagongana kabatini kwaiyo mimi na Mose pia ni binadamu tuko pamoja kwa miaka minne sasa sidhani kama ni kitu kidogo ambacho kitaweza kupita bila kukwazana kwaiyo ndio kama binadamu ni jambo la kawaida kuna muda ananikwaza lakini na uhakika na mimi pia huwa namkwaza kama binadamu lakini mimi ni mtu ambaye sipendi kuweka mambo yangu mtandaoni lakini hiyo siku nilikuwa nimekwazika sana mpaka nikafika mwisho lakini tulishasemehana na tumeyamaliza”.

Aunty Ezekiel amesisitiza kuwa  hapendelei kuanika mambo yake mtandaoni lakini pia hata kwa marafiki kwani hana kawaida ya kuwaambia hata marafiki zake wa karibu mambo yake binafsi.

 

Mose Iyobo Akanusha Kuwa na Mgogoro na Mama Cookie

Dancer maarfu wa msanii mkubwa nchini Diamond Platinumz kutokea wasafi anaejulikana kama Moze Iyobo aMefungukia ishu inayoendelea mitandaoni kuwa yeye na mzazi mwenzie mama cookie maarufu kama Aunty Ezekiel kuwa wapo katika mgogoro wa kutaka kuachana kuwa sio kweli hata kidogo.Mose Iyobo amesema kuwa watu wamekuwa wakitasfiri vibaya baadhi ya meseji na vitu wanavyoviona katika mitandao ya kijamii bila kujua kwanini mtu ameamua kuweka post flani katika ukurasa wake.

Hivi karibuni Aunty Ezekiel aliwka post ilikuwa ikiashiria kuwa ana matatizo katika mahusiano yake,ambapo hii iliibua hisia tofauti kwa mashabiki wake na kusema kuwa inawezekana msanii huyo kwa sasa amambo yake yameenda kombo kati yake na mpenzi wake.

Hata hivyo hayo yote yalikuja kujiweka wazi pale  moze alipoamua kuweka maoni yake katika moja ya videoa alizochapisha mama cookie tena katika ukirasa wake wa instagram ambapo moze iyobo aliandiaka “umeninyima mapenzi alafu  upost, freshi?” kitu kilichowafanya mashabiki kupigia mstari na kupata jawabu kuwa wawili hao wako katika mgogoro.

Akiongea na gazeti la Ijumaa Mose Iyobo aliamua kuliongelea hilo na kusema kuwa wao wameishi kwa muda mrefu na kwa sasa wamekuwa watani sana kiasi kwamba wanaweza kutaniana hata katika mitandoa ya kijamii,

unajua watu wanashndwa kuelewa kuwa  mimi na mama cookie tunataniana sana,kwiao hata mimi kuandika vile katika instagram  ilikuwa ni kumtania tu lakini watu wamekuja wametokwa na mapovu.-Alisema Mose Iyobo.

Mahusiano kati ya mose na aunty yameanza miaka kama minne aliyopita na ni moja ya couple ambayo imekuwa na heshima bila kuwa na skendo za hapa na pale tangu ianze, ingawa wasanii wa watu wengi maarufu wamekuwa wakiingia katika mahusiano na kuachana kwa muda mfupi hii imekuwa ni tofauti na kwao.

Penzi la Aunty Ezekiel na Mose Iyobo Ladaiwa Kuwa Matatani

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Aunty Ezekiel amesemekana kuwa matatizoni na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni mcheza shoo/ dancer wa Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Aunty Ezekiel na Mose Iyobo wamezaa pamoja mtoto mmoja wa like anayeitwa Cookie, mwanzoni wakati mahusiano yao yanaanza wapo watu wengi sana ambao waliponda kwa kudai kuwa Aunty hana hadhi ya kuwa na mtu kama Iyobo ambaye ni mcheza shoo lakini wenyewe walipendana na walilidhihirisha hilo. 

Aunty na Iyobo ni moja kati ya couple chache Bongo za mastaa ambazo hawana sana skendo mtandaoni au hawana sana kiki lakini kuna mara chache ambazo Aunty alitumia mitandao ya kijamii kulalama kuhusiana na uhusiano wake na Iyobo.

Miezi michache iliyopita Aunty Ezekiel alitumia ukurasa wake wa Instagram kumlalamikia mwanamke amnaye alikuwa anajigonga kwa Mose Iyobo na alifunguka nakudai kuwa mwanamke huyo alikuwa amedhamiria kumharibia familia yake.

Tangu hapo kumekuwa na tetesi kuwa penzi la Aunty na Iyobo limekuwa likilega lega ingawa hakuna hata mmoj kati yao aliyethibitisha tuhuma hizo.

Siku ya Jana Aunty aliandika maneno yaliyowapelekea watu wengi kudhani kuwa labda ni kweli penzi lake na baba watoto wake Moses Iyobo liko matatani. Kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha inayomuonesha akiwa na mawazo makali alafu akaisindikiza kwa maneno yafuatayo:

Sina kawaida ya kuweka maisha yangu kwenye mitandao ya kijamii ila huku tunakoenda dah! Wanaume?”.

Maneno hayo ndio yalizidi kuzua tetesi kuwa labda penzi la Aunty na Iyobo limekufa kwa maana ni juzi tu Iyobo aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kungekuwa sehemu ya wakina baba kudai haki zao wakinyimwa unyumba maana amenyimwa unyumba na Aunty!.

Aunty Ezekiel Awatolea Povu Wanawake Wanaojigonga Kwa Iyobo

Mwigizaji wa Bongo movie Aunty Ezekiel amewatolea povu wanawake wote wanaojigonga kwa mpenzi wake na baba wa mtoto wake Moses Iyobo.

Kupitia ukurasa wake Instagram Aunty amefunguka kuwa kuna wanawake wamekuwa wakimtumia meseji za kimapenzi Iyobo wakati wakijua wazi yupo kwenye uhusiano na ana familia tayari.

Aunty Ezekiel aliandika haya kwenye ukurasa wake wa Instagram;

“Naomba nisema maana nimekaa nalo rohoni naona nashindwa siwezi kuvumilia kidudu mtu kuja kuharibu familia yangu kirahisi kama ulivyodhani mala** wa mji wewe koma uliza kabla hujavamia wanaume wengine hutokaa ujisamehe, kwa uhandsome gani alionao huyu sahivi mkajifanya kutwa kumtongoza kama sio tu ilimradi umeshare na fulani sasa mimi sio mzungu ndugu yangu ntakukanyaga hutaamini kamuulize yule mwanamke wa China akupe habari yangu. Watu gani hamjui kusafisha wako ukatulia mbona hamkumfata alipokuwa mabonde kuinama na tulivyoanza wote mlijifanya kushangaa sahivi kutwa mnapishana inbox kumtongoza”.

Aunty Ezekiel alimuacha mume wake aliyeenda jela na kuzaa na Moses Iyobo ambaye ni mmoja Wa mcheza shoo wa Diamond.