Mashabiki wa King Kiba wamtolea Barakah the Prince hasira baada ya kumpost Chibu

Ingawa Baraka the Prince alifanya wimbo na King Kiba Nisamehe haamanishi kuwa hawezi msupport Diamond Platnumz. Hata hivyo hivi sivyo mashabiki wa Kiba wanavyofikiria. Hivi Karibuni muimbaji huyu wa Bongo, Baraka the Prince aliupost wimbo mpya wa Diamond Platnumz na kilichofuatia ni matusi kutoka team Kiba.

Soma: Baada ya kufanya collabo na King Kiba, Barakah The Prince aeleza changamoto alizopitia

Barakah The Prince
Barakah The Prince

Mashabiki wengi ambao wamekuwa wakicomment kwa picha hii wanashangazwa na Baraka kupost wimbo huu kwa sababu wengi wanajua Baraka yuko kwenye lebel moja na Alikiba.

Kama mnavyoelewa Kiba na Diamond wamekuwa na beef kwa muda sasa kwa hivyo Baraka asingeweza kupost chochote kuhusu Diamond Platnumz, wengine wamecomment kwa kutopendezwa na post hiyo wengine wamepost kumpongeza.

Kupitia Instagram Barakah the prince aliandika kusema…

Chanzo cha kutengenezewa maden na makaka poa..ila mama alinifunza kukaa kimya..eeehh mungu niokoe vita

Baada ya kufanya collabo na King Kiba, Barakah The Prince aeleza changamoto alizopitia

Mwimbaji wa Tanzania Barakah the Prince ameeleza baadhi ya changamoto alizopitia baada ya kutoa colabo ya wimbo wake Nisamehe aliyomshirikisha King kiba. Hii ni kufuatia tofauti zilizopo kati ya team Kiba na team Diamond Platnumz.

Akizungumza katika interview na kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir, Barakah alisema kuwa ilikuwa vigumu kupata support kutoka team Diamond ambao hawampi support Kiba.

Ujue Alikiba ni brand kubwa na ni brand ambayo ina mvutano na vitu vingi, kwahiyo unavyofavya collabo na Alikiba kuna mawili hapo, kuna nyimbo kufanya vizuri na kuna nyimbo kufanya vizuri wastani, wa kawaida kwasababu ya ule mvutano wa kibiashara ambao upo kati yake na timu nyingine

Ingawa halalamika kuwa jambo hili liliadhiri wimbo wake, muimbaji huyu amekiri kuwa timu hizi mbili zinangumvu ya kuaffect career ya muimbaji bongo. Kwa hivi sasa anaendelea kuzipush nyimbu zake kabla atoe project nyingine mwaka huu.