Ebitoke: Sijampenda Ben Pol kisa nimpe ubikira yangu

Mchekeshaji wa kike Ebitoke aligonga vichwa vya habari kwa kusema kuwa anampenda sana Ben Pol na anataka mwimbaji huyo amoe.

Ebitoke alifungua roho katika mahojiano na Sasa TV na kueleza jinsi anavyompenda Ben Pol, machozi yalimchuruzika usoni mchekeshaji huyo akieleza jinsi anavyompenda Ben Pol.

Soma Pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ebitoke

Katika mahojiano na Juma3tata, Ebitoke alifunguka kuhusu kumpea Ben Pol ubikira wake. Alisema kuwa lazima mwimbaji huyo amoe kwanza ndo ampe ubikira wake.

“Napenda watu waelewe kitu kimoja, mimi sijampenda Ben Pol kisa nimpe bikira yangu, kwa mfano akikataa kunioa basi nitamwacha aendelee na familia yake, kwa sababu watu wanaongea kinoma, lakini kuhusu hilo nitaendelea kujituza mpaka mwanaume wa kweli atokee kwenye maisha yangu ndiyo nitampa bikira yangu,” Ebitoke alisema.

“Tulimpunguza Baraka” Ben Pol aeleza chanzo cha bifu yake na Baraka The Prince

Baraka the Prince ana bifu kubwa na Ben Pol na Jux. Ben Pol ameeleza chanzo cha kilochosababisha wao kutoelewana na walikua marafiki awali.

Ben Pol and Baraka wamewai kushirikiana kuachia wimbo unaoitwa ‘Mwambie’. Hata hivyo wiki mbili zilizopita Baraka alimkashifu Ben Pol alipowachia wimbo wake mpya ‘Tatu’.

Soma pia: “Ni upumbavu tu!” Baraka Da Prince atoa kauli yake kuhusu wimbo mpya ya Ben Pol

Baraka the Prince na Ben Pol

Ben Pol sasa ameeleza nini ilitokea kati yake na Baraka the Prince; katika mahojiano na Ayo TV, Ben Pol alisema Baraka alianza kuwa na chuki nay eye na Jux baada ya wao kumpuguza kimuziki kwa kushirikiana kufanya shows pamoja na tours.

“Mimi napenda sana kukoselewa, napenda kupokea maoni lakini ina matter sana maoni yanatoka kwa mtu gani au wewe na huyu mtu mko kwenye situation gani. Baraka maoni yake yanaweza yakawa mazuri, yanaweza yakawa ni ya kuboresha, yanaweza yakawa ya kujenga, kukosoa. Lakini mimi nawaza status yangu na Baraka ilivyo sasa sahi alafu nahusianisha na yale maoni yake, naona kuna msuguano. Baraka ana hali ya chuki na mimi, especially mimi na Jux, wote wawili sisi ana matatizo na sisi, ana chuki. Ata last time tulikutana naye alikua hataki kutusalamia akageuza mgongo kabisa…muda mrefu kama wiki tatu…Hataki kutusalamia ameweka mgongo hivi. Tumeenda kumsalamia Baraka, ‘Baraka tumekuona, umependeza na tumekumiss’, lakini alikua hataki kuongea na sisi, alikua na chuki.

“Sasa mtu ambaye ana chuki, ana tatizo na wewe akitoa maoni kuhusu kitu chako unakua na mashaka kidogo kwamba ni honest opinion au kwasababu ya misunderstanding ambayo munayo. Na Baraka hii source ya kutuchukia mimi na Jux sababu tulimpunguza kwenye umoja ambayo tulikua tumeuanzisha kufanya shows, kufanya tours…tulimpunguza. Hatukuwai kusema, hatukuwai kumuaibisha kwenye media kusema kwamba tumempunguza au nini… Ni mdogo wetu tumesema tumlindie heshima, tumempunguza lakini hatutasema hivyo kwenye redio au kwenye mtendao…kwenye sehemu yoyote. Lakini kumbe yeye alikua na kinyongo, kwanzia hapo ukimtumia post, ukimwambia kitu akusaidie kushare anakuwekea hivi ‘hapana, no’, si support’. Kwa hivyo twasema kwamba ana chuki. Na kumpunguza ilikua lazima tumpunguze kwasababu ya discipline, kukosa nidhamu. Ilikua lazima tumpunguze.” Ben Pol alisema.

Tazama mahojiano hayo kwenye video hapo chini:

 

Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Mchekeshaji wa kike Ebitoke anampenda Pel Pol kwa dhati, alilia akifanya mahojiano huku akimwomba Ben Pol amuoe.

Ebitoke alifungua roho katika mahojiano na Sasa TV na kueleza jinsi anavyompenda Ben Pol, alisema ishu ya Ben Pol kuwa na mtoto ilimuuma sana kwasababu alikua anadhani ako na bibi.

https://www.youtube.com/watch?v=h_cKUc2TVgQ

Ben Pol amemjibu Ebitoke, anataka kukutane naye uso kwa uso ili kudhibitisha kama mchekeshaji huyo anamaanisha anachosema ama ni utani tu.

“Kwanza niseme tuu naheshimu hisia za kila mtu yeye ni binadamu na ameonesha hisia zake soo naziheshimu sana. Kweli nimeziona habari mitandaoni tuu tangia jana watu wakiposti lakini sikuamini siunajua habari za mitandao bro! ila leo pia nimeona video yake akisisitiza ombi lake lakini bado siamini na nitaamini na nitafurahi kama tukionana uso kwa uso,” alisema Ben Pol.

 

Ben Pol apata dili kubwa baada ya picha zake za Uchi

Msanii wa Tanzania Ben Pol aliwaacha wengi kama wameduwaa baada ya kuachia picha zake huku akionekana uchi. Kama kawaida mashabiki walimponda na wengi kumkashif kwa kuachia picha kama zile mitandaoni ya kijamii.

Hata hivyo msanii huyo sasa hivi amepata dili na kampuni ya mafuta ambayo imempa jukumu la balozi. Ben Pol alifunguka kuhusu dili hiyo alisema,

“Hapa sasa hivi tunaongea kuhusu majukumu yangu kama balozi, nione nina show ngapi katika hiyo event na mambo ya maslai inakuaje, anione matangazo ya runinga na mabango na nijue amount ya kazi yote ilivyo ni kiasi gani ninaweza kunufaika.Tukifikia muhafaka watu wataniona kwenye mabango, nimekoleza mafuta nimeweka na logo za hiyo kampuni,” 

“Ni upumbavu tu!” Baraka Da Prince atoa kauli yake kuhusu wimbo mpya ya Ben Pol

Baraka Da Prince amekashifu wimbo mpya ya Ben Pol unaoitwa ‘Tatu’. Msanii huyo alisema alikuwa anategea wimbo kali sana kwasababu Ben Pol alitengeneza kiki kubwa mitandaoni na picha zake za utupu kabla ya kuachia wimbo wake mpya.

Da Prince alisema ‘Tatu’ ni upumbavu tu na kuongezea kusema kwamba hakufurahiswa kabisa  na wimbo huo.

“Nimekuwa ‘disappointed’ sana huu wimbo…Kwa jamaa alivyojitoa nilidhani ni kitu kikubwa kumbe upumbavu..’Save our music”. Da Prince aliaandika kwa Instagram.

Skiza ‘Tatu’ hapo chini:

 

Baraza la Sanaa Tanzania yatoa kauli yake kuhusu picha za utupu za Ben Pol

Ben Pol alizua uzushi katika jukwaa zote baada ya picha zake za utupu kuibuka katika mitendao za kijamii siku chache zilizopita.

Msanii huyo alionekana akiwa uchi wa mnyama katika picha za kitaalamu alizopiga. Watu wengi walikerwa na picha hizo licha ya sehemu yake nyeti kutoonekana.

Moja ya picha ambazo Ben Pol aliweka kwenye mtendao wa kijamii

Baraza la Sanaa Tanzania – BASATA limetoa kauli yake kuhusu picha za Ben Pol. Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza alilaani kitendo cha Ben Pol na kusema kwamba sanaa ya Tanzania bado haijafikia zama za kufanyika kitendo kama hicho.

“Kwa tamaduni zetu bado hatujafikia hapo ni wengine huko ambao wanaruhusu. Hiyo ni moja, pili ni kitendo ambacho baraza inakilaani lakini kwa utaratibu wa baraza kama baraza tutamtafuta Ben Pol tuweze kumsikia mwenyewe kwamba zile picha kweli amepost yeye au kuna kitu kingine kwa sababu teknolojia imekwenda mbali sana siku hizi kwahiyo tutamsikiliza anahusika vipi moja kwa moja. Lakini kimsingi kwa ujumla wake baraza inakilaani na tutaendelea kumtafuta Ben Pol kuzungumza naye kwa sababu ni haki yake kusikilizwa katika hilo.

“Pia naungana na wasanii waliolaani kitendo hiko ambacho ni cha ajabu sana na baraza kwa mamlaka yake kama mzazi haiwezi kukaa kimya lazima tujue kama ana tatizo la akili au maadili limemkumba Ben Pol,”alisema Godfrey Mngereza.

 

Ben Pol aweka picha akiwa nusu uchi, mashabiki nao wamponda

Ben Pol hataki mchezo na iwapo haujaziona picha zake mpya basi hautaelewa ninacho sema. Kwa Mara ya kwanza msanii huyu wa nyimbo za RnB ameachia picha zake akiwa uchi lakini anaonekana kama ameketi huku akificha sehemu zake za nyeti.

Picha hizi aliziweka kwenye mtandao wake wa Instagram na mashabiki wake ambao hakuwa wanatarajia jambo kama hili walimshambulia kwa meneno ya kumtusi na wengine wakimueleza kuwa amepoteza muelekeo wake ikiwa hii ndio ndio njia ameamua kuichukua.

Yeye ndiye msanii wa kwanza wa kiume Bongo kuachia picha kama hizi. Hapo mbeleni wengi walikuwa wamemzoea kuweka picha kama amejivalia nguo zake za designer lakini kwa sasa inaonekana kuwa ameamua kufanya mambo mapya.

Mtindo huu sana sana hutumiwa na wanawake lakini Ben Pol ameamua kuonesha kuwa pia wanaume Wanaweza pia. Iwapo haujaiona picha hiyo basi itazame hapa.

Ben Pol amsifia mwanawe mali mitandaoni…hili ndilo jambo alilolisema

Mtoto wa kiume wa Ben Pol, Mali ametimiza mwaka mmoja mwezi huu na tayari ameanza kuonesha makucha yake.

Ben ameiambia Bongo5 kuwa licha ya kuwa bado anawachanganya yeye na mama yake nini kinaweza kuwa kipaji chake, kuimba na kikapu ni vitu vinavyoelekea kuja kuwa passion ya mtoto wao.

“Ukimpa mpira anapenda kucheza sana kwa mikono, anapenda kudundadunda sana mpira,” amesema Ben Pol.

“Lakini vile vile pia mama yake anaimbaga naye mara nyingi sana, nyimbo za kitoto. Mama yake akiwa anaimba anamfuatisha sijui sauti ya pili, sijui anaimba sauti ya ngapi. Kwahiyo anaonekana anapenda kuimba, anapenda mpira, kwahiyo sijui itakuwaje, sijui atakuwa mcheza mpira sijui atakuwa muimbaji, lakini all in all nashukuru Mungu anakua vizuri,” ameongeza.

“Ila kiukweli kwenye kipaji hapo bado tunaendelea kuangalia sababu kiukweli anatuchanganya, atakuwa Shaquille O’Neal au atakuwa R.Kelly, hapo ndio au atakuwa Ben Pol au atakuwa Hasheem Thabeet.”