Mashabiki Wakiendela Kunisumbua Nitakata Kichwa.:-Ben Pol

Msanii ben pola amekuwa akiwashangaza mashabiki wake kila siku kutokana na tabia yake ya kubuni vitu vipya kila siku kuhusu muonekano wake kila kukicha.Akitambulisha wimbo wake mpya wa zai ambao ameimba na Kriss Danuel, Ben Pol alitokea studio akiwa na nguo nyeusi iliyochanika chanika huku kichwani akiwa amenyoa kipara.

Muonekano wa Ben Pol umekuwa wa tofauti kila kukicha tangu alipoanza na kuweka nywele za rangi ya kijani ambapo alipoulizwa alisema ni kutokana na kazi aliyokuwa nayo kipindi hicho ya kuwa balozi wa mazingira.

Hata hivyo alipokuwa akifanya mahojiano na mwanahabari wa Clouds tv, Ben Pol alisema kuwa  ameamua kufaya hivyo ili kuwa na muonekano wa tofauti kila siku kulinagana na kazi anazokuwa akifanya.

Hata hivyo Ben Pol anasema kuwa pamoja na kwamba mashabiki wake wamekuwa mara nyingi wakimshambuklia kwa maneno na kama sasa hivi watamshambulia tena basi atakata kichwa chake kwa sababu kila anachofanya wanakuwa wanamsema.

Nilinyoa kwa sababu nilimaua tukose wote, wengine walikuwa wakisema kuwa nywele zako za kijani nzuri wangeni wanasema nywele zako mbaya nikaona bora tu ninyoe tukose wota lakinipia kama kipara tena wananisema basi nitakata kichwa tu ili tukose wote maana hakuna kitu utafanya wataacha kusema.

Ben Pol- Nilikuwa Chawa wa Barnaba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefunguka na kukiri kuwa siku za nyuma alishawahi kuwa chawa wa msanii mwenzake Barnaba Boy Classic.

Ben Pol amewataka mashabiki kuacha kushangaa urafiki wake na Barnaba umeanzia wapi kwani ukifatilia historia ya muziki wake alishawahi kuwa chawa wa Barnaba.

Ben Pol amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv:

Kwanza watu wengi watakuwa hawafahamu urafiki wetu na Barnaba umeanza siku nyingi sana nilikuwa najiweka kwake kwa sababu nilikuwa naona anaimba vizuri na pia nakumbuka nilikuwa hata namsindikiza studio kwa Allan Mapigo.

Siku hizi hao watu wanawaita hao watu chawa kwaiyo mimi ndio nilikuwa chawa wake yaani namsindikiza lakini uchawa unasaidia hasa uchawa wenye malengo ambao hata mimi ni nao sahivi nina chawa wangu ambao wananifuata kila sehemu”.

Ben Pol amekiri kuwa kupitia kuwa chawa wa Barnaba alijifunza vitu vingi anavyojua leo hii kuhusu mziki kwaiyo uchawa wake ulikuwa wa faida.

Ben Pol Atangaza Kolabo Yake na Kiss Daniel Wa Nigeria

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ben Pol anayetamba kwa muziki wake wa miondoko ya RnB amefungukia mipango yake ya kufanya kazi na wasanii wa kimataifa zaidi.

Ben Pol ameweka wazi kuwa  Kolabo yake ya kwanza itakuwa na staa kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye itatoka hivi karibuni na it aende kwa jina la Zai.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Showbiz Xtra, Ben Pol alisema kwamba mwaka huu amejipanga kwa makubwa na kolabo yake hiyo ni mwanzo wa hayo makubwa ambayo anatarajia kuyatoa kwani anazaidi ya kolabo tatu za kimataifa mwaka huu ambazo zitampeleka ‘level’ nyingine.

Mwaka huu ninatarajia kutoka na kazi zaidi ya tatu za kimataifa na ujio wangu na Kiss Daniel ni mwanzo wa kazi hizo, mashabiki wangu wakae mkao wa kula”.

Lakini pia Ben Pol ametangaza ujio wa wimbo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ben Pol ameachia ngoma yake na Ebitoke inayokwenda kwa jina la natuliza boli ambayo inafanya vizuri bado.

Ben Pol Ajutia Uamuzi Wake Wa Kutoa Albamu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol amefungukia na kudai anajutia uamuzi wake wa kutoa Albamu.

Siku za hivi karibuni wasanii wengi wamerudi kwenye trend ya kutoa Albamu baada ya kukomea kwenye kutoa single kwa muda mrefu hatimaye Siku za hivi karibuni wasanii kadhaa wamejaribu kuingia kwenye upande wa kutoa albamu.

Baadhi ya wasanii ambao wametoa albamu ni pamoja na Diamond Platnumz, Chinbees, Vanessa Mdee, Ben Pol lakini tofauti na wasanii wengine ambao wametoa Albamu, Ben Pol amejutia uamuzi huo wa kutoa Albamu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv, Ben Pol amefunguka na kusema amejuta kufika albamu yake ya The Best Of Ben Pol kwani faida aliyopata Kwenye mauzo ya albamu nzima ni sawa na shoo moja ambayo huwa anafanya:

Bado ni changamoto kusema kweli kwa sababu tukiongelea albamu yangu ya zamani ya 2011 mauzo yake yaliyonifikia mimi ni sawa na mauzo ya shoo yangu moja kwaiyo unaweza ukaona tatizo Lakini pia zamani tatizo lilikuwa kwetu wasanii tulikuwa hatutoi albamu lakini sahivi albamu tunatoa mashabiki hawanunui albamu zetu”.

Lakini pia Ben Pol amewataka mashabiki waache kuongea kuhusu wasanii kutoa Albamu badala yake waanze kununua kazi za wasanii ili wawape sapoti ili wao kuepuka kukata tamaa.

Ben Pol Amenifundisha Muziki:-Paul Clement

Msanii wa muziki wa injili Paul Clement amefunguka na kusema kuwa hakuwahi kujua kama angeweza kufanya vizuri katika muziki ila kwa msaada wa msani wa bongo  fleva Ben Pol aliweza kufanikiwa katika muziki kwa sababu aliweza kumsaidia na kumfunidsha kuimba.

Paul Clement hakuona aibu alipokuwa akiongea na kipindi cha Pambio Live cha Kenya kuhusu kukua kwake kimuziki tangu anaanza kufanya muziki.

Ben Pol alinifundisha muziki,yeye ndio alinifundisha kuimba.Nilikuwa nikienda katika mashindano fulani kuimba nikawa nafukuzwa stageni na ninaambiwa kabisa toka haujui kuimba nenda kajifunze kuimba.Lakini Ben Pol alinifundisha kuimba na nilirudi palepale waliponiambia sijui kuimba nikaenda kuwaonyesha kwa sasa najua kuimba , nilitaka kuwaonyesha kuwa najua.Baada ya hapo nikaanza kuimba katika kundi moja la muziki wa injili la Glorious Celebration.

Sio kila msanii anaweza kuweka wazi kuhusu swala la yeye kufundishwa katika muziki tena hasa pale unapoiona kuwa status yako ni kubwa kwa mashabiki, wasaniiwengi wamekuwa waoga kukiri kuwa pale walipo kuna watu waliwahi kuwashika mkono nyuma yao.

Paul clement ni moja ya wasanii wakubwa wa injili wanaoimba kwa kutoa ujumbekatika jamii yake lakini pia amefanya muziki wake kuweza kupendwa  hata na nchi za jirani.

Ben Pol Kufanya Remix na Tanzania All Stars

 

    

                                                     Willy Paul akiwa studio na Ben Pol

Msanii anaefanya vizuri katika kazi za muziki kutoka kenya willy paul hivi karibuni alikuwa tanzania na alibahatika kufanya mahojiano katika vituo mbalimbali vya habari na katika moja ya mahojiano yake willy aliweka wazi kuwa ameshirikishwa wimbo na ben pol , wimbo ambao ni remix ya moja ya nyimbo zake lakini jambo la kufurahisha zaidi ni kwamba ben pol ameamua kuwaweka mastaa kibao katika wimbo huo.

Willy Paul alisema kuwa katika wimbo huo ben pol alimwambia kuwa nataka kufanya kazi na wasanii wakubwa wa bongo lakini aliamua kumpa nafasi na yeye hivyo kwake ni jambo la kumshukuru Mungu.

Juzi nilikuwa na Ben Pol na amenishirikisha katika wimbo wake fulani na ameniambiani all stars,anafanya remix ya one of hus songs na pale nimemuona kuna vannesa mdee. joh makini, Nandy , joh makini na mimi pia. Siwajui wote lakini kuna Barnabas na Ben pol mwenyewe.

Akizungumzia jinsi alivyofurahi kujiona katika wasanii watakaofanya kazi na wasanii wengine wakubwa wa bongo Willy Paul anasema “nashukuru mwenyezi mungu kwa kila kitu ananipatia kiwe kikubwa au nikidogo ninashukuru kwa sababu ananipatia baada ya kuona kuwa nimekuwa nikimtumikia kwa muda mrefu.”

Willy Paul anasema kuwa yeye ni mwanamuziki ambae anaimba nyimbo za injili lakini pia za mapezni lakini hajwahi kuimba nyimbo zinazoonyesha uchafu wowote kwa sababu yeye anamtumikia mungu na nyimbo anazoimba anataka myu aweze kusikiliza na mpezni wake au mzazi wake , kwaio yeye ni muimbaji mzuri wa nyimbo za mapenzi.

Style ya Nywele ya Vannesa Ilivyompa Faraja Ben Pol

Wakati anaweka style ya nyweel kwa kupaka rangi ya kijani katika nywele zake , watu wengi walikuja juu na kuanza kumkashifu na kumpondea kuwa hajapendeza kabisa ikiwezekana aende akabadilishe kabisa.Lakini  siku zinavosonga style ya kuweka rangi kichwani inazidi kupendwa na wasanii wengine kitu ambacho kinamfanya Ben Pol aone kama vile na yeye sasa amepata wa kumsapoti.

Akionyeshwa kufurahia uamuzi aliouchukua Vannesa Mdee, Ben Pol aliweka picha ya Vannesa katika ukurasa wake wa instagram na kuandika kuwa anazidi kupata faraja akimaanisha kuwa ameshaanza kupata wafuasi wa kumsapoti katika style hiyo mpya ya muonekano wake.

                                                 

.

Uamuzi wa vannesa unakuja siku mbili baada ya msanii Alikiba pamoja na Ommy Dimpozi pia kuambua kuwek style hiyo ya nywele kwa kuamuz kuzipaka rangi, ambapo hapo pia ben pola hakusita kuonyesha furaha yake kuwaona wasanii hao wanafata nyayo zake za fashion.

                                                            

Alichokiandika Ben pol kuhusu muonekano mpya wa alikiba na Ommy Dimpozi

Style hii ya kuweka nywele rangi imezidi kubamba kwa wasanii kwa sababu wasanii wengine walioweka hivi ni pamoja na Harmonize,Lavalava na keysha.

 

Ben Pol Anamtamani Sana Papii Kocha.

Msanii wa muziki nchini Ben Pol ambae kwa sasa anafanya vizuri katika soko la muziki nchini amefunguka na kusema kuwa  kiu yake kubwa sasa hivi ni kufanya  kazi na Papii Kocha na akipatiwa nafasi hyi hawezi kuichezea kwa sababu anamuna ni msanii anayeweza sana kimuziki.

Ben Pol ansema kama endapo atapata bahati ya kufanya kazi na papii kocha hatokaa aichezee nafasi hiyo kwa sababu ni mtu mwenye kipaji na ataacha kila kitu alichokuwa anakifanya na kwenda kufanya nae kazi.

kitokea nimepata nafasi ya kufanya kazi na papii kocha yaani hapo hapo naacha kila kitu nilichokuwa nakifanya naenda  kukesha studio kuhakikisha  nafanya kitu bora, kwa sababu papii ni mtu mwenye kipaji cha kipekee sana

Papii Kocha ambae hivi sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya cha waambie amepokelewa vizuri na mashabiki wake baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu katika muziki kwa sababu ya kutumikia kifungo cha muda mrefu walichohukumiwa kwa kosa la kulawiti yeye na baba yake.

Hata hivyo wawili hao walipata msahama wa Raisi na kurudi uraiani ambapo serikali pia imejitahidi kuingiza mkono wao ili kuweza kuwasaidia kuinuka kimuziki.

Ben pol ambae sasa hivi amekuja na muonekano mpya wa kuweka nywele rangi ya kijanii amekuwa akifanya vizuri na kukubalika sana katika list ya wasanii wa bongo walikuja na kuweka mapinduzi makubwa ya muziki na kuwateka mashabiki zake.

Ben Pol Arudisha Mapigo Kwa TID na Kudai Amemkosea Heshima

Wasanii wa mziki wa Bongo fleva TID mnyama na Ben Pol wamejikuta kwenye bifu zito baada ya TID kumtolea povu zito Ben Pol baada ya kuimba nyimbo yake kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika wikiend iliyopita.

TID alimjia juu Ben Pol baada ya kuimba kiitikio cha wimbo wake wa ‘Nyota yangu’ katika tamasha la Fiesta bila ruhusa yake ambapo TID alikiambia kituoa cha redio cha East Africa kuwa ana mpango wa kuzungumza na wakubwa wake pamoja na wanasheria ili kumchukulia Ben Pol hatua za kisheria kwa kuiba nyimbo yake.

Kwenye mahohiano aliyofanya na Bongo 5, Ben Pol amemtaka msanii huyo mkongwe kumuomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa:

Unajua kilichotokea ni kwamba wimbo wangu wa moyo mashine unaendana na nyota yangu kwa sababu zote zina miondoko ya Zhouk kwaiyo yaani pale nilikuwa kama nampa heshima fulani hivi yeye na mziki wake. Kwanza kiukweli kabisa TID ni msanii aliyeni-insipire mimi mpaka nikaanza kuimba mimi nipo shule ya msingi nasikiliza albamu ya sauti ya dhahabu naiimba yote yaani pale ndipo Ben Pol alipozaliwa kwaiyo nilishangaa yeye kuwaka mimi kuimba kionjo cha nyimbo yake wakati yeye ni staa na ni msomi kama nsanii anaelewa hizo mambo zipo lakini sikutegemea msanii mwenye heshima yake Kama yete anaweza kufanya kitu kama mile kusema kweli I am very confused”.

Lakini pia Ben Pol amekiri kuwa hawezi kumlaumu sana TID kwani hawezi jua wakati anafanyaile interview alikuwa katika hali gani na anaamini akikaa akitulia amtafute Ben Pol amuombe  radhi kwa kitendo alichofanya kwani yeye anajua hakikuwa sawa kabisa.

T.I.D Kumshtumu Ben Pol Kwa Kutumia Nyimbo Yake.

Haijapita siki nyingi tangu kutokee kwa mgogoro kati ya msanii Ray C na Nandy baada ya Ray C kumshutmu na kumuonya Nandy kwa kutumia nyimbo zake na kuziimba katika matamasha ya Fiesta na kumuomba kuacha kutumia nyimbo hizo kwa sababu yeye hafaidiki chochote na swala hilo.Hivi juzi tena msanii mwingine ameibuka na kumshtumu msanii mwenzie kwa jambo jilo hilo tena.

Msanii tT.I.D ameibuka na kumtuhumu Ben Pol kwa kutumia nyimbo zake katika matamasha makubwa (bila kuyataja jina) lakini amelalamika na kusema kuwa hata sponsors wa tamasha ilo hajawahi kulewena nayo wala kufanya nayo kazi pamoja kwa sababu hawana mahusiano mazuri na sponsors hao.

Pamoja na kwamba hakutaka kusema wazi ni kampuni gani lakini maneno hayo yalikja baada ya Ben Pol kuimba wimbo wa T.I.D wa nyota yangu katika usiku wa tamasha la Fiesta uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club usiku wa tarehe 25 November.

Nina kesi na Ben Pol, huyo jamaa kwenye concert moja kubwa sana alafu ilikuwa sponsored na walimlipa ela kubwa sana lakini katika nyimbo nyingi alizoimba katika playlist yake kaamua kuweka wimbo wangu pia, and those sponsors they dont work with me, they don’t like me, because am not performing am not dead.Wao wanaimba unawalipa , so what about me, what about my copyright, ni makosa.-Alifunguka T.I.D

T.I.D hatokuwa msanii wa kwanza kutoa lawama kwa wasanii ambao wamekuwa wakitumia nyimbo za wasanii wenzao bila kuwashirikisha kwa chochote, wasanii wengi wamekuwa wakilalamika kwa nyimbo zao kuimbwa katika majukwaa bila kulipwa au kuwa -considered kwa kitu chochote,wasanii hao wanadai haki zao kwa sababu wanachoamini ni kuwa walifanya kazi kubwa kuinua muziki huo.

T.I.D ameongezea na kusema kuwa hata hivyo sio heshima kwa msanii kuimba wimbo wa msanii mwenzie ambae bado yuko hai, hivo anategema kutafuta mwanasheria ili kuzungumza na kujua watamfanya nini Ben Pol kupata haki zake kwa kitendo hicho.

 

Ben Pol Amfananisha Msaga Sumu Na Dr.Remmy

Ni wasanii wachache sana wanaokubali kazi za wasanii wenzao tena hasa wanapokuja katika swala zima la kazi za musiki kwa sababu wengi wanaamini kuwa ili kufanikiwa kimuziki basi lazima kuwe na ushindani.Hii imekuwa tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva anaejulikana kwa kufanya vizuri na kupewa jina la king of Rnb , msanii Ben Pol ambae ameibuka na kuusifia sna muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.

Akiongea na kipindi kinachorushwa na Clouds Radio cha XXL, Ben Pol ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘kidume’ alichomshirikisha mwanadada mrembo kabisa kutoka Nigeria Chidinma Chikere, Ben Pol anasema anavutiwa sana na ufanyaji muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.

Sijui kama Msaga Sumu ni upcoming artist au sio lakini  napenda sana muziki wake na jinsi  anavyokuja , ana-flavor , yake kama Dr.remmy  au sound flani hivi  ya kitofauti sana, na ninamuona jinsi atakavyofika mbali katika muziki wake’ alifunguka Ben Pol kuhusu Msaga Sumu

Ben Pol anaendelea kumuongelea Msaga Sumu na kusema kuwa ni msanii mwenye kipaji cha kuweza kubadilika badilika na kuimba nyimbo zenye radha tofauti tofauti”Alafu anaweza kubadilikabadilika kila mara, mara nyingine anaweza kuimba zilipendwa, au anaweza kuimba singeli, kama oya oya oya  lakini ni msanii mwenye vitu vingi sana” aliongezea ben pol

Msaga Sumu ni mmoja wa wasanii wanaochipukia na kufanya vizuri katika game la muziki hasa katika style hii mpya ya muziki wa kisingeli iliyopo sokoni kwa sasa, hata hivyo Msaga Sumu anaweza kuita mwanzilishi wa kisingeli na ndiO msanii alijitaidi hata kuhamamsisha wasanii wengine wadogo kufanya muziki wa kisingeli hivyo  kusababisha kukua kwa kisingeli.Msaga Sumu kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha singeli kinachojulikana kama  “mwanaume mashine” inayopendwa sana hadi na watoto kutokana na style yake ya kuimba na kucheza huku ikitaja baadhi ya majina maarufu ya wacheza mpira na timu kubwa nchini , hapo mwanzo alifanya vizuri na kibao cha “unanitega shemeji’.

Ben Pol Asema Hawezi Kutoka Na Wema Sepetu Wala Jokate

Msanii ambae kwa muda sasa amekuwa akifanya vizuri katika  musiki wa Bongo Fleva, na kupokea  shangwe la kutoka kila anapopandwa majukwaani tena hasa kwa kipindi hiki cha tamasha kubwa la muziki la Fiesta likiendelea Ben  Pol ameonekana kukubalika sana na mashabiki wake. Hivi karibuni mashabiki zake wamekuwa wakimwita ‘king of Rnb’  na kumfanya yeye kuanza kutembea na fimbo ambayo yeye mwenyewe anasema ni ishara ya ufalme wake. Ben Pol amefunguka na kusema kuwa kwa yeye hawezi kabisa kutoka katika uhusiano wa mapenzi na wema sepetu wala jokate mwegelo.

Ben Pol ambae kwa sasa amekuwa na scandal ya kuwa na mahusiano ya kumapenzi na msanii wa maigizo ya uchekeshaji anaejulikana kama Ebitoke.Katika tetesi izo  Ben Pol mwenyewe alikanusha na kusema yupo na Ebitoke  kwa sababu anataka kumsaidia katika kazi zake za sana na si kitu kingine.

Ben Pol alipokuwana akiojiwa na Jonijo,  wa onlinetv, alisema kuwa katika wasanii hawa wa kike wawili yaani wema Sepetu na Jokate Mwegelo hakuna hata mmoja ambae anaweza kutoka nae , lakini alipoulizwa sababu hakujibu nini kinamfanya asema kitu kama hicho.’Ikitokea natakiwa kutoka na Wema Sepetu au Jokate Mwegelo, sitatoka na mtu yoyote, ni bora nitoke mwenyewe’ huku akionekana kucheka, Ben Pol aliongea.Hata hivyo Ben Pol alisema kuwa mwanamke anaemtaka ni yule mwenye kujiamini hata wakiwa wanachart anakuwa anamuona huyo ni mwanamke anaejiamini

Tofauti kwa Ben pol, kunakuwa na wasanii kibao katika tasnia ya muziki waliowahi kutamka kutamani kuwa na mahusiano na wakinadada hawa wawili hasa Wema Sepetu, ilhali kila mwanaume ana sifa zake kwa mwanamke lakini wengi wanaonekana kuvutiwana warembo hawa waili huku kila mmoja akitoa sababu zake.

Tukiachana na historia ya kimuziki , Ben Pol ni baba wa mtoto mmoja wa kiume na kwa muda sasa umepita tangu kuwe na tetesi za yeye kuachana na mama wa mtoto wake ambae walikuwa wakiishi pamoja lakini taarifa hizo hazikuthibishwa na yeye mwenyewe , na baada ya hapo ndipo issue ya yeye(Ben Pol)  kutoka na Ebitoke ilipoanza kusambaa kwatika mitandao.

 

Napenda Mwanamke Anayejiamini- Ben Pol

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernad Paulo maarufu kama Ben Pol amefunguka kuhusu aina ya mwanamke anayempenda. Mwana muziki huyo amekuwa katika vichwa vya habari sana kutokana na kutajwa na mchekeshaji maarufu Anastazia Kisaveli ‘Ebitoke’.

Ebitoke amemtaja mara kwa mara kwamba anampenda kimapenzi Ben Pol lakini kijana huyo amepotezea. Katika mahojiano yake aliyoyafanya hivi karibuni Ben Pol aliweka wazi kuwa hana muda wa kumuongelea Ebitoke kwani kulitokea mvurugano baada ya Meneja wa Ebitoke kutoka Timamu tv kudai kuwa alimlipa Ben Pol kiasi cha shilingi milioni tatu ili tu aonekane na Ebitoke katika mitandao ya kijamii lakini Ben Pol amekataa tuhuma hizo.

Ben Pol ameweka wazi kuwa kitu pekee anachoangalia kwa mwanamke ili awe naye kimapenzi ni lazima awe najiamini pindi wanapokuwa kwenye maongezi.

“Endapo nikimpenda msichana kitu kikubwa ninachoangalia ni ‘confidence’ yake hasa pindi tukiwa tunachat, usmart, umakini na uharaka wa kujibu vitu unavyokuwa unaulizwa kwa wakati huo”.

Ben Pol ni moja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na wadada yaani mashabiki wake wengi ni wasichana kutokana na aina ya muziki anayoimba hata pia na muonekano wake . Hivi sasa Ben Pol anatamba na nyimbo yake mpya inayoitwa kidume aliyomshirikisha mwanamuziki kutoka Nigeria inayofanya vizuri sana katika stesheni nyingi za redio nchini.

Ebitoke: Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani

Siku chache zilizopita, Ben Pol alisema kuwa hataki aulizwe kuhusu mahusiano yake na mchekeshaji Ebitoke. Msanii huyo alieleza kuwa anajiusisha na mambo ya muziki kwa sasa na hangependa kuongelea mambo yake binafsi.

Ebitoke amedhibitisha kuwa yeye na Ben Pol bado ni wapenzi ila hawataki tu kuweka mapenzi yao hadharani. Akiongea na Times FM, Ebitoke alisema mipango walionayo kwa sasa ndio inapelekea kutoonekana pamoja kwa sasa na kupostiana kwenye mitandao ya kijamii.

Ben Pol na Ebitoke

“Mimi na Ben Pol sasa hivi tunafanya vitu vya ndani kwa ndani, hatutaki tuviweke hadharani. Hamna siyo vya unyago na siwezi kumuongelea vibaya Bentoke labda watu wanaona haniposti mimi kila siku lakini si hivyo. Tunamipango mingi, kwanza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika jambo lolote na ameniaidi lazima ahakikishe natimiza malengo yangu na ameona mimi bado ni mdogo ananifundisha kila kitu jinsi gani nikue kwenye hii tasnia na the way hii mitandao ya kijamii ilivyo na maneno ya watu yalivyo,” alisema Ebitoke.

 

Ben Pol aeleza kwanini hana majuto kuhusu picha zake za utupu

Ben Pol alizua utata picha zake za utupu zilipotokea kabla ya yeye kuwachia wimbo wake ‘Tatu’. Staa huyo alionekana akiwa uchi wa mnyama kama ameketi kwa kiti huku mikono zake zimefungwa na uso wake kufunikwa.

Ben Pol alisema picha zake za utupu ziko na mchango mkubwa sana kwa maisha yake, alieleza kuwa picha hizo ni sehemu ya vitu ambayo amepitia ili vimjenge katika maisha yake.

“Hamna majuto, ni mafundisho tu…hamna majuto…hakuna majuto sehemu yoyote ila kila siku tunajifunza vitu vipya maana mimi akili yangu nilivyo iset napenda kupokea vitu vipya kujifunza kila siku. Sijawai kuwa comfortable ata uimbaji wangu mimi mbaka leo naskiliza mbinu mpya za kuimba, mbaka leo nafanya mazoezi, mbaka leo nagundua muziki mpya. Kwa hivyo kila kitu ni kujifunza tu kinavyoenda unaimprove, saa ingine unakutana na reaction mbaya inakujenga unakua imara kwa hivyo ndivyo hivyo inavyokua,” Ben Pol aliambia Bongo 5 alipoulizwa kama yupo na majuto kuhusu picha zake za utupu.

 

Mchekeshaji Ebitoke afunguka kuhusu Ben Pol kushindwa kumuondoa ubikira

Mchekeshaji wa kike Ebitoke alipata umaarufu sana miezi michache zilizopita alipolia kwenye mahojiano kwa TV huku akitaka msanii Ben Pol afunge naye ndoa.

Ebitoke alisema anampenda sana Ben Pol na hata alitaka mwimbaji huyo amuondolee ubikira wake. Alisema alikua tayari kufanya lolote ili Ben Pol ampende.

Soma pia: Ben Pol amjibu mchekeshaji aliyelia na kumwomba amuoe

Ben Pol na Ebitoke hatimaye walikutana na kwa sasa inasemekana kuwa wawili hao ni wapenzi. Akiongea kwenye kipindi cha Friday Night Live (FNL) ya EATV, Ebitoke alisema kuwa Ben Pol hajafanikiwa ‘kufungua mlango wake’.

Ben Pol na Ebitoke

Mchekeshaji huyo alieleza kuwa bado hajawahi kulala na mwanaume yoyote yule katika maisha yake na alitaka Ben Pol ndo awe mwanaume wa kwanza kulala naye.

Hata hivyo kuna wale wanaodai kuwa Ben Pol na Ebitoke wanafanya tu utani ilhali wanazidi tu kujitangaza na kuzidi kupata kiki katika kazi zao.