Aika Afungukia Skendo Za Diamond Kuwadhalilisha Wanawake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetokea katika kundi la Navykenzo, Aikah Marealle ambaye hivi sasa pamoja na mpenzi wake Nahreel wanafanya vizuri na ngoma yao ya ‘Katika’ amefunguka na kumuongelea Diamond Platnumz.

Aikah na Nahreel wameonekana kuwa na ukaribu mkubwa na Diamond hii ni baada ya kumshirikisha katika ngoma yao ya Katika lakini kuna tetesi zilisambaa kuwa kundi hilo Lina mpango wa kusainiwa chini ya WCB tetesi zilizokataliwa na Navykenzo.

Lakini pia siku za hivi Karibuni Diamond amekuwa akinyoshewa sana vidole kwa tabia yake anayo tuhuma ya kumdhalilisha wanawake ambapo mashabiki walimjia juu kwa vitendo ambavyo vilimuonyesha kama hawaheshimu wanawake waliomzalia ambao ni Mobetto na Zari.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Aikah alihojiwa kuhusu tuhuma hizo za Diamond kudhalilisha wanawake ambapo alifunguka kwa kusema:

Mimi huwa siwezi kumhukumu mtu na maisha yake na kila anachoamua kukifanya, ila ni mtu ambaye nimekaa na Diamond kwa nyuma ya pazia ambapo naona jinsi anavyoishi na watu vizuri, hao wanawake wote mnaosema anawadhalilisha anaishi nao vizuri na anawajali“.

Lakini pia Aikah aliulizwa kuhusu mstari ambao umesikika Kwenye wimbo huo ambapo Diamond alimtaja Hamisa kuhusu uchawi na matunguli:

Tena huo ndio ubunifu ambao unatakiwa katika muziki maana kitu kinapokuwa kinaongelewa halafu ukakiweka katika muziki ili kuburudisha watu inakuwa sio kitu kibaya sisi tuliona kawaida na ni njia ya kufanyabiashara na nina uhakika hata muhusika mwenyewe alipokisikia alikifurahia”.

Aika amesisitiza kuwa hana tatizo na Hamisa na ni mtu wake ambaye anachat naye mara kwa mara.

Hamisa Mobetto Ataja Kilichomvutia Kwa Diamond

Mwanamitindo na Msanii wa Bongo fleva Hamisa Mobetto amefunguka Tena na kumuongelea aliyekuwa mpenzi wake na Baba watoto wake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya siku ya jana kwenye Chipukeezy Show nchini Kenya, Hamisa aliulizwa alivutiwa nini hasa kwa Diamond kama ilikuwa ni Sura, Mwili wake, Pesa au umaarufu?

Hamisa alifunguka:

Siwezi kusema kiukweli kipi kilichonivutia kwa Diamond kwa sababu mimi na yeye tulipokutana kwa mara ya kwanza hakuwa na hivyo vitu vyote unavyovitaji yaani hakuwa na pesa, hakuwa na mwili aliokuwa na sasa hivi wala hakuwa na umaarufu”.

Lakini pia Hamisa ameweka wazi kuwa aliamua kumuacha Diamond kwa sababu alihisi kabisa ulikuwa wakati sahihi kwake yeye kuendelea na maisha yake kwa sababu anaamini kuna wanaume wengine wengi kwa ajili yake.

Mobetto Kumburuza Diamond Mahakamani Baada Ya Tuhuma Za Uchawi

Msanii wa Bongo movie Mrembo Hamisa Mobetto anadaiwa kuingia kwenye vita ya kisheria na Mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz baada ya sakata la uchawi.

Global Publishers wanaripoti kuwa Baada ya kutuhumiwa kuwa ni mchawi na hata clips zake zainazodaiwa kuwa ni yeye kusambazwa Kwenye mitandao ya kijamii hatimaye inadaiwa kuwa timu Mobeto inayoamini kuwa mwanadada huyo hakurekodi clip hiyo, ilikuja na hoja ya kutinga mahakamani kutafuta haki.

Chanzo kinasema ni mtu aliyesambaza clip hiyo ya sauti sambamba na wale waliyoiamini akiwemo Diamond.

Mtu anayesambaza hiyo sauti ameshajulikana, lakini na Diamond naye anatakiwa kupelekwa mahakamani maana aliwaaminisha watu kuwa hiyo ni sauti ya Mobeto.

GPL limeripoti kuwa Kwa mujibu wa wanasheria, litakalomkabili Diamond ni ‘udhalilishaji’ na kwamba licha ya kwamba hakumtaja jina Mobeto lakini mazingira yanaonesha kuwa aliyekuwa anamzungumzia katika majibu yake alikuwa ni Mobeto:

Kama unavyojua udhalilishaji siyo kosa la jinai, lipo kwenye Sheria za Mwenendo wa Makosa ya Madai au Civil Procedure Code ya mwaka 1966 iliyofanyiwa marekebisho mara kadhaa“.

Sakata hilo lilitokea wik iliyopita ambapo Familia ya Diamond ilimtuhuma Mobetto kwa uchawi na baadae kusambaza voice notes ambazo zilidaiwa kuwa za Hamisa Akichonga na mganga huku akiwa anaomba awafanyie dawa

Kitendo Cha Diamond Kumuita Mobetto Mchepuko Chamliza Mama Hamisa

Siku chache zilizopita staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz aliwaacha watu midomo wazi baada ya kufanya Interview na Kwenye Interview hiyo kumuita Hamisa Mchepuko.

Kwenye clip hiyo ya Diamond inayodaiwa kuwa ni mahojiano yake aliyoyafanyia nje ya nchi, Diamond alisikika akijilaumu kuwa mwaka 2017 ulikuwa mbaya maishani kutokana na matukio mabaya yaliyomtokea. Alisema, mwaka huo ndiyo ambao aligombana na mpenzi wake wa muda mrefu, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aliyezaa naye watoto wawili, mmoja wa kike.

Alisema hayo yote yalitokea baada ya kuchepuka na Mobeto na kujikuta amempa ujauzito na hata Zari alipojaribu kuhoji baada ya kusikiasikia fununu, alijaribu kumficha ili kulinda uhusiano wake, lakini hata hivyo jipu lilikuja kupasuka baada ya Mobeto kuvujisha picha zao wakiwa kimahaba chumbani, jambo ambalo lilimharibia sana.

Baada ya clip hiyo kusambaa mashabiki wa Hamisa walimjia juu Msanii huyo na kumtuhumu kwa tabia mbaya ya kudhalilisha wanawake hasa ambao amekwisha zaa nao.

Baada ya sakata hilo Global Publishers lilimsaka mama mzazi wa Hamisa Mobetto, Shufaa Lutiginga ambaye alionyesha kutofurahishwa na Kauli hizo za mkwewe  dhidi ya mwanaye Mobetto:

Jamani inauma na kwa kweli nisingependa hayo mambo jamani kuyaongelea mimi… jamani naombeni sana mtafuteni huyo mwenyewe aliyesema au Mobeto tafadhali, niacheni mimi nipumzike”.

Lakini pia Kwenye Interview hiyo  Diamond alisikika akiwaasa vijana wote wenye wapenzi wao ‘serious’ au wenye wake zao, kuwa makini pindi wanapokuwa na michepuko ili kuepuka kupata watoto wa mchepuko kama ilivyomtokea yeye, jambo ambalo limekuwa baya maishani.

Mtoto wa Hamisa Uso Kwa Uso na Familia Ya Diamond (picha)

Mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Hamisa Mobetto Dylan ameonekana kwa mara ya kwanza aliwa na Familia ya upande wa Diamond baada ya mgogoro wa muda mrefu.

Tangu Hamisa azae na Diamond Kumekuwa na sintofahamu kwani wanafamilia upande wa Diamond hawajawahi kuonekana wakiwa na mtoto wa Hamisa kama ilivyo watoto wengine wa Diamond na Zari.

Mama Diamond ameshawahi kudaiwa kumshushia kipigo kizito Hamisa baada ya kuweka wazi kumchukia baada ya kumuitia Shilawadu ili waweze kumpiga picha.

Lakini wiki chache zilizopita Mama Diamond aliweka wazi kuwa pamoja na  kuwa na  tatizo na Hamisa lakini hana tatizo na mjukuu wake Dylan na amethibitisha hilo kwani siku ya jana picha zilizomuonyesha Diamond, mama Yake na dada yake pamoja na Dylan zilisambaa mtandaoni:

 

 

Kuna Muda Natamani Kuondoka Tanzania- Hamisa Mobetto

Muigizaji wa Bongo movie na mzazi  mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amedai kuwa kuna muda anatamani kuondoka Tanzania.

Hamisa ambaye ameendelea kushika headlines kwani tangu alivyotangaza kuwa ana ujauzito wa Diamond mwaka jana basi hajatoka midomoni kwa watu tena.

Hamisa siku ya jana alizuahgumzo baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kuondoka Tanzania lakini kila akifika airport anajuuliza Watanzania wataishije bila yeye.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa aliandika:

Sometimes, Natamani Kuondoka Tanzania nafika hadi airport ila najiuliza Watanzania Wenzangu Wataishije Bila Mimi“.

Hamisa amekuwa akiongelewa sana Kwenye mitandao ya kijamii siku hizi tangu arudiane na Diamond na kiukweli imekuwa burudani kwa mashabiki zao hasa ukimuweka Diamond huku Zari pale na Hamisa huku.

Mahaba ya Diamond na Hamisa Yazusha Gumzo Kwenye Tuzo za Sinema Zetu

Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz amerudi tena kwenye headlines baada ya kukumbatiana na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto mwishoni mwaka wiki hii kwenye tuzo za Sinema Zetu Film Festivals.

Diamond aliwaacha watu midomo wazi kwenye ukumbi wa Mlimani City ambapo shamra shamra hizo zilifanyika ambapo alikumbatiana na Hamisa na hata kushikana mikono name kupelekea kuibua tetesi za kurudiana.

Sio siri kuwa Diamond na Hamisa walikuwa kwenye bifu zito mwaka Jana baada ya Hamisa kuanika picha zao na video wakiwa faragha name baadae kuzaa mtoto wao Dylan ambapo Diamond alikuwa kwenye mahusiano na Zari.

Diamond na Hamisa walikuwa moja ya watu waliochaguliwa kuhudhuria tuzo hizo na kugawa tuzo hizo kwa washindi waliopigiwa kura lakini baada ya kufika pale mbele walianza kukumbatiana.

Diamond Amekataa Kumpa Hamisa Milioni Tano Kila Mwezi Kwaajili Ya Malezi Ya Mtoto

Mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa kwenye mgogoro na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto tangu Hamisa alipovujisha picha zao za faragha na kupelekea Diamond kukiri kuwa amezaa na Hamisa.

Baada ya sekeseke hilo kutokea Diamond alikata mawasiliano na Hamisa na kuacha kumuona mtoto wake huku Hamisa akidai kuwa Diamond aliacha kabisa kulea mtoto na hakuwahi kutoa hela ya matumizi kitendo kilichopelekea Hamisa kumfungulia Diamond kesi ya madai ya kumtelekeza mtoto na kudai alipwe shilingi milioni tano kwa mwezi kutokana na kipato kikubwa cha Diamond.

Baada ya kupokea tuhuma hizo Diamond aliiambia mahakama kuwa hana uwezo wa kumlipa Hamisa milioni tano kwa mwezi Kama gharama ya kumtunza mtoto. Diamond amewasilisha majibu hayo katika mahakama ya watoto Kisutu, mbele ya hakimu mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobetto kumfungulia kesi hiyo mwezi uliopita.

Katika majibu yake, Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa alipwe kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa na hawezi kuzimudu. Hamisa katika maombi yake kupitia kwa mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Goodluck wa kampuni ya uwakili ya Century attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond, kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama ilihairisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, Mobetto kwa kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya motto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezwa hivyo wakapeleka kesi yao mahakamani.

Christian Bella Amefungukia Ishu Ya Hamisa na Diamond

Mwanamuziki maarufu wa dansi, Christian Bella ameongelea habari ambayo bado inashika vichwa vya habari, uhusiano kati ya Hamisa Mobetto na mzazi mwenziye Diamond Platnumz.

Christian Bella aliyetumbuiza kwenye sherehe ya mtoto wa Hamisa, Kwenye mahojiano na Bongo 5 Bella ameongelea mawazo yake juu ya kinachoendelea kati ya Diamond na Hamisa:

Hamisa kwangu mimi ni mwanadada anayejituma ni model si unaona mpaka anapata tunzo za nje ya nchi, mi namuona ni mtu mzuri tu ambaye hana tatizo na piano suala la Hamisa na diamond kupelekana mahakamani mi sidhani kama Diamond anaweza kushindwa au anaweza kukataa kumlea mtoto wake ilimradi ameshakubali kuwa mtoto ni wa kwake”.

Pia Christian Bella hakuishia hapo aliendelea kuweka maneno:

Mi naona umefika wakati wawili hawa wakae chini wayaongee tu kistaarabu kwani Naseeb hawezi akashindwa au akamletea roho mbaya kwa sababu yule ni mtoto wake alafu isitoshe Naseeb mwenyewe kapitia maisha magumu kakulia Tandale kwaiyo anaelewa ugumu na Kama kweli hajatoa mi naaminmawa na misunderstanding hivyo wakae wayaongee mi naamini hapatatokea makelele yoyote”.

Kuhusu suala la kupelekana mahakamani Hamisa alielezea kuwa Diamond ndio aliyetaka iwe vile, yaani atafute mwanasheria na afungue kesi mahakamani ili wapate mwongozo wa kisheria wa jinsi Diamond ataweza kumtunza mtoto bila tatizo lolote.