Mimba Yamtoa Lulu Gerezani

Kwa sasa amekuwa akitumikia kifungo cha nje kinachomfanya baadhi ya watu wamuone kipindi anaingia na kutoka katika eneno lake husika analifanyia adhabu, hata hivyo kwa waliomua lulu wanadai kuwa mwana dada huyo anaonekana katika hali sio ya kawaida kutokana na mwili wake ulivyo.

Kwa waliomzoea Lulu wanasema kuwa mwanadada huyo ni mjamzito kwa sababu tumbo limekuwa kubwa kidogo lakini pia hata mwili wake hasa vidole vimevimba na pia mara nyingi amekuwa akionwa na watu akitema sana mate kitu kinachowafanya watu wengi kuamini kuwa inawezekana mwanadada huyo ni mjamzito na ndicho kilichomplekea kutoka gerezani.

Jitihada za kumtafuta ziligonga mwamba hasa baada ya lulu kukataa kuongea na waandishi wa habari kwa sababu bado hajamaliza kifungo chake ;lakini pia hataki kuongea na waandishi wahabari kwa sababu anataka kuanzia sasa maisha yake yawe ya kwak bil kushirikisha mitandao.

Waandishi hawakuishia hapo wakaona bora kutafuta  wazazi na watu wa karibu wa Lulu   kuuliza kuhusu taraifa hizo ndipo walipojibu kwa lulu sio mjamzito lakini hiyo ni hali ambayo anweza kuwa nayo mtu yoyore hasa mtu aliyezoea kufanya mazoezi kisha akaacha kwa muda kama walivyoambiwa na daktari.

kutokana na hali hiyo sasa , watu wengi wamekuwa wanajipa majibu kuwa inawezekana msamaha wa lulu   kutoka kwa rais pia ulianagalia sana hali yake ya kiafya.

Mama Kanumba Asononeshwa na Kitendo Cha Lulu Kutolewa Jela Mapema

Mama mzazi wa aliyekuwa muigizaji wa Bongo movie Steven Kanumba, Florah Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba ameeleza machungu yake baada ya Lulu kuachiwa gerezani jana.

Siku ya jana Jeshi la Magereza lilitangaza rasmi kuwa Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameachiwa rasmi kutoka gerezani baada ya kukaa ndani kwa miezi mitano ambapo alitajwa kwenda kuendelea na kifungo chake nje.

Tangu Lulu afungwe Mama Kanumba aliweka wazi kuwa alifurahia kifungo cha Lulu na hata kudai kuwa kifungocha miaka miwili kilikuwa kidogo kwa mauaji ya mtoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na MCL digital, Mama Kanumba amefunguka kuwa tangu amepata taarifa kuwa Lulu ameachiwa amekuwa akikosa usingizi na hata presha kupanda kwani ameumizwa sana na taarifa hizo.

Tangu nilipopata taarifa hizi nimejikuta nakosa usingizi na kuumwa presha hivyo leo imenibidi niende kwenye maombi kwa ajili ya afya yangu.

Lakini siku zote naamini Kuwa maskini hana haki”.

Lakini Mama Kanumba amewashukuru wote walioshiriki katika kumtoa na kuongeza kuwa anaamini hiyo yote ni kwa sababu yeye hana hela.

Yasemekana Lulu Michael Aachiwa Huru

Habari zilizosambaa sana kwa siku ya tarehe 13 May zinasema kuwa mwanadada Elizabeth Lulu Michael ameachiwa huru na kwamba inasemekana kifungo chake kimepatiwa msamaha wa raisi hivyo mwanadada huyo yuko huru.

Ingawa habari hizi hazinathibitika bado , lakini chanz cha habari zinasema kuwa siku ya jana  Lulu Michael alitolewa gerezani na kusemakana kuwa kwa sasa yuko huru.

Bado kumekuwa na mkanganyiko wa maneno kuhusu kuac hiwa kwake ingawa hakuna picha ya karibuni iliyomuonyesha msanii huyo akiwa huru lakini sababu za kutoka kwake gerezani zimekuwa nyingi huku wengine wakisema kuwa ni msamaha wa raisi, wengine wakisema kuwa rufaa yake imefanikiwa huku wengine wakisema kuwa ameatiwa kifungo cha nje.

Baada Ya Jaji Kutoa Hukumu,Kumbe Lulu Alikataza Watu Kukata Rufaa

Ni dhahiri kuwa baada  ya hukumu ya Lulu kutolewa na jaji wengi waliumia sana hasa kuondokewa na ndugu, rariki na mwanafamilia wa tasnia ya filamu Tanzania tena ikiwa nyota yake inaanza kungaa kwa style ya ajabu.Wakili Msomi na mtetezi wake aliyekuwa nae kwa kipindi chote cha kesi Bw. Peter Kibatala na  alisimama mbele za watu na kuwatia moyo kuwa inawezekana kabisa Lulu kutoka kwa dhamana huku akiendelea kukata rufaa ya kutokurizika na hukumu hiyo.

Lakini kumbe faraja ambayo ilikuwa mioyoni mws watu inaweza kuanza kuyeyuka hasa baada ya kusikia taarifa kwamba tangu siku ya kwanza baada ya hukumu mwanadada mwenyewe Elizabeth Lulu Michael alikataa kata kaat ndugu zake wasifanye jambo lolote linalohusiana na kukata rufaa ya hukumu hiyo kwa sababu anataka kuheshimu maamuzi ya mahakama na kutumikia adhabu yake lakini pia alitaka kutumikia kifungoi hicho alichopewa na mahakama ili anapotoka huko awe huru na jamii inayomzunguka.

Akisimulia mambo yote yaliyotokea siku ya tukio, baba mlezi wa Lulu  ambae alikuwa nae bega kwa bega katika kipindi chote hicho na ndie aliyemkuza katika tasnia ya filamu Dr.Cheni alisema kuwa

kwakweli Lulu ni kama alijua lolote linaweza kutokea siku ile,ingwa ilo la kufungwa hakulipa kipaumbele sana.jaji alipomaliza kusoma hukumu lulu alishtuka kama sisi lakini yeye aliekuwa wa kwanza  kurudi katika hali yake ya kawaida na akaanza kutoa kauli za ujasiri. -Alisimulia dr.Dheni

sipingani na maamuzi ya mungu na haya ni maamuzi yake kabisa, na ana makusudi yake kunipa hiki kilichotokea leo,acheni miaka miwili ipite sio mingi sitaki kupingana na maamuzi ya mahakama.nayaheshimu sana maamuzi ya mahakama acheni nikatumikie kifungo changu.– Aliongea Dr.Cheni akiwa anarudia maneno aliyosema Lulu mahakamani siku ya mwisho ya hukumu yake.

hivyo basi kwa namna moja ama nyingne hata kama hakujua ilo litatokea lakini hakuwa mtu wa kuonyesha kukata tamaa kwa kile kilichomkuta siku ile.Elizabeth Lulu Michael anawekwa katika orodha ya wasichana wadogo Tanzania waliowahi kupata mafanikio kwa kupitia misukosuko mingi alkini bado hakuwahi kuteteleka.

Tazama Picha na Video Za Lulu Akiwa Mahakamani Kwaajili Ya Kesi Ya Kanumba

Msanii wa bongo movie Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ amewasili leo mahakama kuu ya Tanzania kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi yake ya kumuua bila kukusudia muigizaji wa bongo Movie marehemu Steven Kanumba.

Kesi ya Lulu imeanzwa kusikilizwa leo kwenye mahakama kuu ya Tanzania amewasili mahakamani hapo leo asubuhi akiwa ameambatana na mama yake Lucresia Kalugila. Huku marafiki wa karibu wa Lulu kama Muna Mapenzi akiwepo pia.

Mapema wiki hii iliwekwa wazi kuwa kesi ya Lulu iliyokuwa kimya kwa miaka kadhaa sasa itaanza kusikilizwa Alhamisi tarehe 19 kwenye mahakama ya kanda ya Dar es Salaam.

Hizi ni video zinazomuonyesha Lulu akiwasili Mahakamani leo asubuhi

 

 

Baada ya kesi ya lulu kusikilizwa kwa masaa kadhaa ambapo shahidi mmoja alitoa ushahidi kesi ilitangazwa kuendelea kisomwa siku ya kesho. Lulu alionekana akiondoka maeneo ya mahakama kwa kupanda gari la mwanasheria wake Peter Kibatala.