Huu ndio ujumbe ambao Shamsa Ford aliwapa wanaume hawapendi kufanya kazi!

Staa wa muvi za Bongo Shamsa Ford hivi karibuni alichukua muda wake kuwa shauri wanaume amabao hawapendi kujitegemea – haswaa wale ambao huchagua kazi za kufanya.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Shamsa alionekana kukerwa na wanaume ambao wanategemea kufugwa na wanawake wazee kuwashinda.

Shamsa Ford

Katika ujumbe wake msanii huyu alitaja kuwan I vizuri wanaume kujituma na kufanya kazi kwa mikono yao badala ya kutamani maisha ya haraka yasiyo na utamu wowote. Aliandika kusema;

“Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,”

Akaongeza;

“Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa. Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

Diamond Platnumz asema haya kuhusu muziki wa Bongo

Ikiwa umekuwa ukijiuliza kuhusu muziki Wa bongo unaendelea wapi, basi Diamond Platnumz amejibu swali lako. Msanii huyu wa nyimbo za Bongo Fleva, amefunguka kusema kuwa nyimbo za kibongo zimekua na hii ni kutokana na bidii za wasanii kutoka bongo.

Diamond Platnumz alisema kuwa muziki Wa bongo Fleva wetu umeweza kufika sehemu mingi huku akiongeza kuwa tu si muziki bali pia mbuvi. Akizungumza na Bongo 5, Diamond Platnumz alisema,

“Muziki wetu unazidi kukua kwa kwa sababu mpaka Watu wa nje wanakuja kufanya kitu nyumbani lazima tasnia yetu iwe imekua, kwa hiyo tasnia yetu imekua sio tu kwa Wasanii hata Industry nzima Vyombo vya Habari, Wadau kila mtu anayehusika na burudani, tumepiga hatua“

Tazama mahojiano yake na Bongo 5.