“Usiogope maneno ya watu” Diamond Platnumz amwambia Harmonize

Wikendi hii iliyopita, Diamond Platnumz, Harmonize na warembo wao walifika katika klabu maarufu ya Nairobi, B Club kuwatumbuiza mashabiki wao wa Kenya katika show iliyowavutia wengi.

Wakali hao wawili wanaaminika kuwa marafiki wa karibu waliwapa wengi kitu cha kuongea hasa baada ya kuonekana na warembo wao, Zari na mpenzi mpya wa Harmonize anayetambulika kama Sarah.

Hata hivyo Diamond Platnumz aliwashangaza wengi baada ya kumuandikia Harmonize ujumbe kupitia Instagram huku akimsihi asiogope maneno ya watu kwani wamepata fedha na mali ya kutosha kupitia muziki wao.

Tazama picha hiyo hapa;

https://instagram.com/p/BXMcjb7FSgD/

Picha hii ya Diamond Platnumz akiwa mtoto ni dhibitisho tosha kuwa alitambua fashion kitambo

Diamond Platnumz na meneja wake Sallam_SK wanapenda sana kutaniana kupitia mitandao yao ya Instagram. Hivi karibuni msanii huyo mkubwa wa bongo aliweka picha ya yake huku akimtania meneja kuwa yeye alianza kupenda kuvaa jerseys tangu awe mtoto mdogo.

Platnumz aliweka picha hii kwenye mtandao wake wa Instagram huku akimchana Sallam kwa kuwa yeye hajaanza kuvaa shati za strips juzi kama who. Alindika kusema;

Don’t get twister @Sallam_sk I started this strip outfits and chains shit since…..!?
(Mi nawaona tu na nguo zenu za mistari pembeni, na macheni kuyamwaga kwa Shinzo…ila michezo tumeanza kitambo sana?)

Katika picha hiyo, Diamond Platnumz anaonekana akiwa kijana mdogo lakini kulingana na alivyokuwa amevalia, ni kweli kuwa alianza mambo ya fashion kitambo. Tazama picha hii hapa chini.

Chibu Dangote

Diamond Platnumz asema haya kuhusu muziki wa Bongo

Ikiwa umekuwa ukijiuliza kuhusu muziki Wa bongo unaendelea wapi, basi Diamond Platnumz amejibu swali lako. Msanii huyu wa nyimbo za Bongo Fleva, amefunguka kusema kuwa nyimbo za kibongo zimekua na hii ni kutokana na bidii za wasanii kutoka bongo.

Diamond Platnumz alisema kuwa muziki Wa bongo Fleva wetu umeweza kufika sehemu mingi huku akiongeza kuwa tu si muziki bali pia mbuvi. Akizungumza na Bongo 5, Diamond Platnumz alisema,

“Muziki wetu unazidi kukua kwa kwa sababu mpaka Watu wa nje wanakuja kufanya kitu nyumbani lazima tasnia yetu iwe imekua, kwa hiyo tasnia yetu imekua sio tu kwa Wasanii hata Industry nzima Vyombo vya Habari, Wadau kila mtu anayehusika na burudani, tumepiga hatua“

Tazama mahojiano yake na Bongo 5.