Zari Atoa Ruhusa ya Hamisa Kuzaa Hata Watoto Kumi.

Mwanamama Zari the Bossy amemwaga povu lake huko katika ukurasa wake wa instagram baaada ya moja ya mashabiki zake kumwambia kuwa pamoja na kwamba yeye anataka kurudiana na Diamond lakii akae akijua kuwa mwanamke mwenzie ambae ni Hamisa kwa sasa ana mimba nyingine.

Kwa kuonyesha kuwa hata yeye hajali kwa hilo, Zari aliandika na kumnibu shabiki huyo kuwa huyo hamisa hata kama anataka kuzaa watoto kumi azae.

Zari kuwa makini maana kuna tetesi huko mtaani kwetu kuwa Hamisa ameshanasa mimba nyingine, Lisemwali lipo kama halipo laja.

Lakini kitu cha  kushangaza zari alijibu tu kwa kifupi na kusema ‘azae tu hata watoto kumi’ 

Wikiendi iliyopita Diamond alioneka akiwa Afrika ya Kusini akiwa na watoto wake aliozaa na zari ,  hii ilithibitisha tetesi kuwa inawezekana wawili hao kwa sasa ni wapenzi.

 

 

Mange Kimambi Aivaa Familia ya Diamond, Awaomba Wampumzishe Hamisa Mwezi Mtukufu.

Baada ya mama yake mzazi na Hamisa Mobeto kufunguka na kulalamika huku kiwaomba familia ya Diamond kuacha kumuandana mtoto wake, mange nae aangukiwa upande wa familia ya Hamisa kumpa moyo na kuwaonya familia ya upande wa pili  kuacha kumdharau Hamisa.

Mangekimambi_ – Unapoona familia ya kiislam hata mwezi wa Ramadhan hawana uwoga nao. Yani hata mwezi wa Ramadhan bado wanaendelea na visa, matusi, kejeli, chuki, husda, fitna, roho mbaya, dharau basi mtu inabidi uelewe unadili na watu wa aina gani.
Seriously mwezi wa Ramadhan wale bado wanachamba na kumdhalilisha mwanamke mwenzao. Yani hawana hofu ya Mungu hata mwezi huu ambao hata sisi tulioshindikana tumekituliza..Yani nashindwa hata kuwasema the way natamani niwaseme
Kutwa kuwapambanisha watoto wa wenzao huyu anajua kupika, huyu hajui, huyu mchafu, huyu msafi wao wanajua kupika? Wao wasafi? Mbona wao hawanyanyaswi au kudhalilishwa na ndugu za waume zao? Ila Mungu ni mkali sana @mama_mobetto siku hizi zilizobaki za mwezi mtukufu kazana na dua, mlilie Allah siku hizi zilizobaki. Wakabidhi kwake!! Usiwaombeee mabaya ila wakabidhi tu. Hizi dharau zote kwa wanawake wenzao sababu tu Allah kamwonyesha Neema ndugu yao?? Allah asingempa mafanikio ndugu yao je wangekuwa na dharau hizi? Hawa wanamletea nuksi ndugu yao. .
Pia Mungu keshaanza kujibu, Esma yuko busy na mahusiano ya kakake alafu mume wake laki moja hana mpaka anaweka passport rehani. Hizo zote ni fimbo Mungu anawachapa. Imagine kutwa mtoto wa mwenzenu yuko mdomoni alafu waume zenu laki hawana huo muda si mngeutumia kwa waume zenu ili wasiathirike? Kama nilivyosema nifimbo ya Mungu. Wao si wamemdhalilisha Hamisa sasa wao wanadhalilika mara mbili ya Hamisa.
Ila wale jamani sijui waislamu wa wapi wale. Yani hawana woga na mwezi mtukufu. Wengine hata kuandika shenzi hatuwezi ila wale wakavuuuuuuuu tena kwenye macamera, yani hawajali. Ndio sisi wote ni watenda dhambi so we cant judge each other ila muislam ambae hata mwezi mtukufu anaendelea na matendo yake ya kila siku huyo sio mzima

Alichojibu Fey Kuhusu Maumivu ya Mama Mobeto.

Mwanadada mwenye vituko katika mitandao ya kijamii Fey anmbae pia ni msanii wa nyimbo za bongo fleva amejibukwa kumpa moyo mama wa mwanadada Hamisa Mobeto baada ya mtoto wake kutukanwa sana katika mitandao ya kijamii hasa kuhusu mahusino yake na Diamond ambayo  familia ya mwanaume huyo inasema kuwa analazimisha na wala hawamtaki.

Hamisa na familia ya Diamond wamekuwa wakimuanda sana mwanadada huyo na kumtaka kuachana na mwanafamilia yao huku wakisema kuwa wifi yao mkubwa ni zari na hawataki mwanamke mwingine katika familia yao.

Fey ameandika katika ukurasa wa mama mobeto baada ya mama huyo kuwka picha yenye maneno makali ya  kuwaomba familia ya diamond kumpumzisha mtoto wake  kwa sababu wamekuwa wakimuandama na kumtukana aachane na kijana wao.

 

Faiza Ally Amwita Mtoto wa Mobeto Fake.

Mwanadada hasiye isha drama katika mitandao ya kijamii Faiza Ally amefunguka na kumjibu shabiki alitoa maoni ya kumshauri Faiza Ally hakumremba mtoto wake kama wanavyofanya wasanii wengine, lakini kitu cha ajabu wakati wa kumjibu shabiki Faiza Ally aliongea wazi kuwa hawezi kufanya hivyo kama anavyofanya Hamisa kwa watoto wake.

Katika maoni aliyoamua kujibu shabiki, faiza alisema kuwa hawezi kum-edit mtoto wake kama anavyofanya hamisa kwa mtoto wake na kumvalisha mawigi kwa sababu mtoto wake hivyo ndivyo alivyo.

siwezi kum-edit mtoto wangu mpaka apoteze uhalisia kama huyo wa mobeto , we are comfortable for who we are , na hizo nywele ndio asili yake ya uafrika , siwezi kumuweka dawa wala kumpachika viwigi …she born to be a star , she doesnt have to fake it , tunaishi maisha yetu kabisa.

Haijulikani kama kuna chochoko yoyote kati ya Hamisa na Faiza Ally mpaka afikie hatua ya kumuandikia hivi kuhusu mtoto wake.

 

 

Hamisa Ataka Watoto wa Zari na Mtoto Wake Kuwa na Umoja, Akiri Kuingilia Penzi la Zari.

Mwanadada hamisa mobeto amefunguka na kusemakuwa pamoja na kwamba kumekuwa na mgongano kati yake na zari the bozzy lakini mwisho wa siku watoto wote ni wa baba mmoja kwaio wale ni kama ndugu lazima kuwe na umoja kati yao.

Akijitahidi kufafanua hata maisha aliyoishi yeye pamoja na kwamba alikuwa akilelewa na baba wa kambo lakini aliweza kuwa-connect na watoto wa babahuyo lakinipia kuwa karibu na watoto wengine wa baba yake ambao hawakuwa  wa mama yake.

Lakini pia hamisa amekiri kuwa ni kweli yeye ndio aliingilia mapenzi ya Naseeb na Zari na hicho ni kitu hawezi kukikataa kwa sababu niukweli hata kama aliwahi kumjua Diamond kabla ya Zari lakini hawakuwa wapenzi

tutake tusitake, tupigane wale watoto ni  ndugu na mwissho wa siku nnaweza kuwa nimemjua naseeb kabla yazari lakini mimi ndio niliingila mapenzi yaok kwa sababu nimekuja wakiwepo pamoja tayari na hiyo ni fact kwa sababu sikuwepo nimekuja kutokea wakiwa pamoja na nikapata mimba na bahati nzuri nikajifungua …sio kitu kibaya kwa sababu inabisi mwanangu awajue na kuwatembea ndugu zake au wakaja tanzania inabidi waonae , kwaio tufanye tunavyofanya lakini wale ni ndugu lazima kuwe na njia ya kuwaweka pamoja.

Hamisa Afunguka Kuhusu Ndoa, Akanusha Kuwa Single Mother

Kumekuwa na habari nyingi sana kuhusu Hamisa kufunga ndoa na Diamond kwa sababu tu wawili hao kwa sasa wamekuwa wakionekana pamoja na kwamba kutokana na ukweli kwamba Diamond alishatangaza kuwa mwaka huu lazima aoe na kwamba mwanamke aliyenae katika mahusiano kwa sasa ni Hamisa basi inawezekana kabisa hamisa ndio mwanamke wa ndoa wa Diamond.

Lakini pia kumekuwa na habari za Wema Sepetu kutoa baraka nyingi sana kwa Hamisa na Diamond endao watafunga ndoa  na kusema kuwa wawili hao wanapendeza wakiwa pamoja, sasa basi mwana dada Hamisa Mobeto amefunguka na kusema kuwa anpokea ushauri wa Wema lakini kuhusu swala la ndoa hawezi kulizungumzia kwa sababu mwisho wa siku mwanaume ndio anaeamua mwanamke wa kuoa.

Alipoulizwa kuhsu swala la ndoa hamisa alijibu kwa mkato”siwezi kujibu swali hilo” lakini pia hamisa aliulizwa kuhhusu watu wanomwita yeye single mother na ndipo alipoamua kutoa chche na kusema

u cant call yourself a single mother kama watoto unasaidiwa kulea na baba zao,so hiyo sio facts kwa sababu mimi sio single mother kwa sababu baba watoto wananilelea watoto wao , siwezi kuwa single mother.

Hamisa amebahatika kupata watoto wawili ambapo mmoja amezaa na dj maarufu Majizzo na mwingine amezaa na Diamond Platinumz.

 

 

Mama Mobeto Ataka Mtoto Wake Aolewe na Mzungu

Mama mzazi wa mwanamitindo na video vixen hamisa mobeto alifunguka hivi karibuni na kusema kuwa alitamani sana mtoto wake kuolewa na mzungu .mama huyo anasema kuwa lengo kubwa la yeye kuolewa na mwanaume wa kizungu ni kutokana na kuamini kuwa wanaume wengi wa kiafrika hawana mapenzi ya kweli.

Akiongea na MCL Digital, mama mobeto anasema kuwa anaamini kuwa mtoto wake ni mrembo na ana sifa za kuolewa na mwanaume mwenye kumjali na kumpenda.

unajua mtoto wangu mzuri, mrembo na anashingo ndefu nataka mwanaume atakae muoa amwangalie kama malaika, amwangalie kama malaika kwa sababu ni mwanamke mwenye msimamoyake na ametulia sio kama watu wanavomfikiria.

wazungu hawana stress, wanajua kujali na kumpenda mwanamke , hawanaga longolongo hasa linapokuja swala la mapezni tofauti sana na wanaume wa kiafrika.

Akiongelea swala la mtoto wake kuzaa na wanaume tofauti tofauti, mama mobeto anasema kuwa kwake haina shida kwa sababu yeye alibahatika kumzaa mtoto mmoja tu na hivyo anaona kabisa kuwa bora amleteee watoto wengi maana hao ndio ndugu zake.

Familia ya Diamond Yaamisha Mapenzi kwa Mobeto.

Wanasemaga huu mchezo hautaki hasira, na kweli maana hii inadhihika katika familia ya msanii mkubwa bongo Diamond Platinumz na familia yake mabo kipindi cha kwanza walikuwa hawaonyeshi mapezni yoyote kwa mtoto wa Diamond aliyekuwa amezaa na Hamisa Mobeto lakini siku za hivi karibuni mambo yameanza kuiva.

Kipindi Diamond ana mahusiano mazuri na Zari the Bossy , katika akaunti yake ya instagram alikuwa akiweka picha za watoto wake wawili Tiffa na Nilan ambao amezaa na Zari na ikafika muda hata mashabiki zake walikuwa wakimuandana na kumsema kwanini hakuwahi kumpost Dully ambae ni mtoto wa Hamisa.

Ukienda kwa mama yake na Diamond pia , alishawahi kugombana na mshabikizake hata kuwajibu vibaya kwa sababu tu ya kuwa haweki picha za mjukuu wake upande wa Hamisa.

Hivi karibuni Diamond Platnumz aliweka comments aktika picha ya mama yake huku akimsifia mamayake na kutaja jina la dully , mtoto aliyezaaa na hamisa.Diamond aliandika “mama yangu mama…mama nasubi mamaaa..bibi dully  bibii..

Hapohapo kwa chini Esma pPlatinumz aliandika kwa kuongezea” alafu @diamondplatinumz dully kafanana nae mdomo@mama_dangote.”

Hii inaonyesha kuwa wawili hao hata kama hawajarudiana lakini wamekuwa na maelewano na kuamua kulea watoto wao wakiwa pamoja na kuwa na familia yenye furaha ingawa watu wengine wamekuwa wanahoji kwanii haya yote yatokee kipindi hiki ambacho Zari ametangaza kuachana na Diamond.Je ni kweli kuwa wawili hao wamerudiana.

Hamisa Mobeto Akumbuka Wema wa Mange Kimambi.

Ikiwa  siku ya tarehe 4 March ni siku ya kumbukumbu ya mwanaharakati wa kimitandao Mange Kimambi , amepokea salamu nyingi sana kutoka kwa watu mbalimbali huku yeye mwenyewe akisema kuwa hata baadhi ya upinzani wake waliweza kumtakia kheri ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.

Moja ya watu maarufu wanao-trend sana katika mitandao kwa sasa Hamisa Mobeto pia alikuwa ni mmoja walimtakia dada huyo kheri katika siku yake ya kuzaliwa lakini hii haitoshi kuelezea hisia zake hadi pale alipoamua kutoa shukrani zake za moyoni kuhusu mwanaharakati huyo na kwa jinsi alivyosimama nae kipindi cha matatioz yake.

Hamisa alimpongeza mwanadada huyo kwa siku hiyo lakini pia alimwambia kuwa anamshukuru sana kwai kipindi anapata matatizo ya kugombana na Zari na Diamond kila siki yeye hakuwahi kuonyesha kuchukia zaidi ya kumsapoti na kumtia moyo na hata wakati mwingine kutoa ushahidi wa ukweli kwa watu.

Happy birthday da mange @mangekimambi …wakati wengi waliniacha ulisimama nami  na pia wakati wngi walivyokuwa  hawaniamin you did..napenda kusema ahsante sana.

Mwenyezi Mungu ndo pekee anajua jinsi gani ulivyonipa nguvu  na ujasiri my dada.May Allah guide and protect you mama… na asante sana.-Aliandika Hamisa Mobeto katika ukurasa wake wa instagram.

Tukumbuke kuwa shukrani yake kwa Mange inakuja pale ambapo Hamisa alipokuwa akigombana sana na Diamond pamoja na zari kuhusu nani ni mmiliki halali wa mimba aliyokuwa nayo Hamisa, na hata mtoto alipozaliwa mange kimambi alishawahi kusema wazi kuwa mtoto ni wa Diamond Platinumz, siku zote ya vita kati aya pande hizi mbili Mange kimambi alikuwa akiandika posti za kumtia moyo Hamisa na ilipobidi kutoa ushahidi kwa kukandamizwa kwake Mange Kimambi aliweka ushahidi hadharani.

 

Hamisa Akataa Darasa Alilopewa Na Maimartha Wa Jesse

Mwanamitindo Hamisa Mobeto amemjibu kwa kashfa mwanadada Maimartha wa Jesse ambae alimshauri Hamisa kuachana na kutukanana na kushindana na Zari katika mitandao bali ajiwekeze zaidi katika swala zima la kufanya maisha yake na kuacha kusikiliza maneno ya watu katika mitandao.

Katika darasa ambalo Maimartha alimpa Hamisa kupitia ukurasa wake wa instagram, alimwambia kuwa Hamisa hapaswi kabisa kusikiliza  maneno ya team yake kwa sababu wanamuharibia sana yeye na familia yake , lakini pia swala la kuwa na  team linafanya familia yake kudharirika pia.

ZKatika ushauri huo Maimartha alimwambia Hamisa kuwa ni bora kuungana  na Zari na kuwa nae kitu kimoja na kwa sababu  wote ni wazazi ni bora kuwe na mahusiano mazuri kati ya Mama Mobeto na Mama Diamond ili kuileta familia pamoja na pia awapende  watoto wa Nassibu na kuwachukulia kama watoto wake.Pamoja na yote Maimartha alitoa pia tathmini ya show aliyoifanya Zari Uganda na kumwambia Hamisa kuwa show yake ilikuwa ni kama alienda kujidharirisha tu kwa sababu show yake haikuendana na hadhi yake.

Katika ukurasa wa maoni, Hamisa alimua kumjibu Maimartha na kumwambia kuwa ushauri huo yeye wala hauitaji labda angeufanyia kazi yeye mwenyewe na familia yake ungemsaidia.

Huu ushauri un gejishauri wewe dada yangu na kizazi chako ungekusaidia sana lakini ndo hivyo tena.

 

Kidoa Amtetea Hamisa Mobeto Mitandaoni

Moja ya wauza nyago wanaofanya vizuri kwa sasa katika video za wasanii bongo  Ssha salumu mwenye jina la umaarufu kama Kidoa amefunguka na kumtetea mwanamitindo na video queen Hamisa Mobeto kwa wasanii wengine wa kike ambao wamekuwa wakimsema na kumsimanga kutokaa na nyingi  skendo   anazopitia hasa hili kubwa la kuzaa na msanii mkubwa Diamond Platinumz na mambo yote yanayoendelea kuhusu kesi iliyokuwa imepelekwa mahakamani kuhusu malezi ya mtoto huyo.

Mwanadada huyo anasema kuwa anakuwa anachukizwa na kuumiza na baadhi ya wasanii wenzie wa kike ambao kutwa kukaaa katika mitandao na kuwa wanamsema Hamisa bila kujua ni kitu gani mwenzao anapitia katika kipindi hiki kigumu na badala yake walitakiwa wamsaidia na kumpa sapoti ya ushauri na sio kumsema kila kukicha katika mitandao ya kijamii.

Kidoa ambae alishinda taji la  Ijumaa Sexiest Girl kwa mwaka 2015 anasema kuwa kinachomshangaza ni jinsi wadada wamekuwa wakimsaidia Zari katika kumkandamiza Hamisa bila kujua kuwa maneno yao yanamwathiri mwanadada huyo kisaikolojia ukizingtia ni mbongo mwenzao.

Sio sawa wasanii wenzangu wanavyokaa wakimnyanyapaa hamisa hata kidogo, kutwa kumoiga vijembe wanatakiwa kukaa wakikumbuka kuwa hakuna ajuae kesha yake ,huenda  hata yeye mwenyewe hakuwaza kama yanaweza kumfika hayo yote. -Alisema Kidoa

Hamisa amekuwa ni moja ya wanadada gumzo katika mtandao kwa kipindi cha takribani miezi mitatu sasa tangu mtoto wake wa pili kuzaliwa na hii yote ni kutokana na kujulikana kwa baba wa mtoto kuwa ni wa Diamond Platinumz ambae tayari anafamilia nyingine yenye watoto wawili na Zari The Bossy Lady mwanamama tajiri kutoka Uganda.Hata hivyo Hamisa amekuwa akitajwa karibia kila kona katika mitandao huku wengine wakimkashifu kwa kujitegesha na kufanya makusudi kuzaa na msanii huyo ili aweze kupata pesa

Alichofanya Hamisa Ni Zaidi Ya Ubinadamu

Ni wengi tunaonekana kuwa na furaha tena hasa pale ambapo unaoona kama  mtu uliyekuwa haulewani nae au upo nae katika ugomvi kwa muda mrefu anapata matatizo na kuumia.Pengine miaka miwili ni mingi sana kwa Lulu kuona haya ambayo wasanii wenzie wameyaandika juu yake lakini pia Mungu ndie anaepanga kila kitu inawezekana pia ikawa ni bahati na akaweza kuyaona majonzi ya watu walikuwa wakimlilia hivi karibuni.

Hamisa alikuwa ni moja ya watu ambao hawakuwa katika maelewano mazuri na Lulu  kwa muda mrefu kidogo kama miaka miwili hivi, kwanza kabisa ni kutokana na msanii Lulu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baba mzazi wa mtoto wa kwanza wa kike wa Hamisa, lakini pia hivi karibuni lilipotokea sakata la Hamisa na Diamond kuhusu mtoto wake wa pili ,Lulu  alionekana kwa kiasi fulani kuwa upande wa Zari.

Lakini yote hayo hayakumfanya Hamisa jana kuonyesha hisia zake za kuumia baada ya Lulu kupata hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela.Pamoja na yote bado Hamisa alitambua mchango mkubwa aliokuwa nao Lulu kwa mtoto wake Fantancy ambae alizoea kumwita aunty kutokana na uhusiano wa karibu wa Lulu na baba wa mtoto huyo,

Ukiachana na post aliyoweka instagram, lakini pia Hamisa alifanya interview jana na televisheni ya Clouds plus, na hakusita kuelezea maumivu yake kwa kile kilichomkuta Lulu. Na kusema kuwa bado hakuwahi kumuona Lulu kama mtu mbaya kwa sababu alikuwa ni mama mzuri kwa mwanae.

Namjua Lulu, naujua upande wa mama Kanumba na upande wa Lulu pia, lakini ukirudisha  nyuma two years ago mimi na Lulu tulikuwa na mambo fulani, everybody knows sio mpaka niyaseme,na inapofika kwenye jambo ambalo ni tatizo its not good, na unajua watanzania  hata ukifanya kitu kwa nia nzuri, as much as i would love to kwa sababu mwisho wa siku  she is not a bad person kwangu especially kwa mwanangu , she has been a very good aunty, ni mtu ambae nilikuwa naweza kumuamini kwamba akiwa na mwanagu yuko safe ingawa nilikuwa najua ni mwanamke mwingine wa baba yake lakini nilikuwa najua yuko stable.-   Alifunguka Hamisa Mobeto.

Lulu alikiuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzazi mwenzie na hmaisa mobeto na hata mara nyingine mtoto huyo alikuwa akikaa kwa lulu kama kwa mama na alikuwa akimtunza vizuri kwa mujibu wa Hamisa mwenyewe.

Hamisa akiwa na mwanae  Fantancy, mtoto aliezoea kumwita Lulu aunty

Lulu akiwa  Majizzzo ambae pia ni  mzazi mwenzie na Hamisa Mobeto.

 

Baada Ya Mahakama Kutupilia Mbali Kesi Ya Mobeto, Wakili Wake Afunguka

Kesi ya mwanadada Hamisa Mobeto na mzazi mwenzie Diamond Platinumz iliyopelewa mahakamani mwezi uliopita ikihusisha hati ya madai ya mwanadada huyo kwa mzazi mwenzie kuhusu matunzo ya mtoto huku mwanadada huyo akitaka kulipwa milion tazo kama matunzo kwa mtoto iliyotupiliwa mbali na kusemekana kuwa mshtaki wa kesi hiyo alikosea baadhi ya masharti ya ufunguzi wa kesi hiyo hivyo mahakama kuitupulia mbali .

Hata hivyo watu wengi walidhani kuwa baada ya mahakama kutupilia mbali kesi hiyo basi ndio itakuwa mwisho wa madai hayo kutoka kwa upande wa mashtaka lakini kitu cha ajabu ni kwamba baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali , wakili wa mwanandada Hamisa Mobeto amefunguka na kuongelea swala hilo ni kusema kuwa kesi hiyo bado iko palepale.

Hata hivyo hilo alibadilishi chochote kwa sababu kesi ya msingi iko palepale, na jana baada ya mahakama kufuta kesi hiyo tulibadilisha haraka  na kurekebisha yale yote yaliyokosewa na  kuifungua upya ikiwa na marekebisho hivyom kesi ya msingi bado iko palepale.

Akiongezea wakili huyo amesema kuwa hata hivyo baada ya process hizo wanachosubiri kwa sasa ni kupangiwa tarehe nyingine upya ili waweze kwenda tena kusikiliza kesi hiyo mahakamani,

kwaiyo kwa sasa tunachosubiri ni kupangwa kwa tarehe mpya ya kusikilizwa kwa kesi hiyo mahakani,

Akimtetea mteja wake wakili Walter alisema kuwa watu wengi wamekuwa wakilaumu kuhusu kiwango anachodai Hamisa Mobeto kwa baba wa mtoto wake lakini ukweli ni kwamba Hamisa anaweza kuwa sahihi kwa sababu ya vitu fulani fulani,lakini pia kesi kama hizi huwa ni za muda mfupi na makwazo kama haya utokea ili kupoteza muda.

kwa kawaidia haya mapingamizi huwa yanawekwa kwa ajili ya kupoteza muda tu lakini kesi za madai kama hizi huwa hazitakiwi kuchukua hata miezi sita.

Hamisa alifungua kesi hiyo zidi ya Diamond huku akidai kupewa hela ya matumizi ya mtoto wake aliezaa na msanii huyo kiasi cha shilingi milioni tano kwa mwezi, hii ni baada ya msanii huyo kuonga kwenye media kuwa amekuwa akimuuhudumia mtoto huyo huku mwanadada huyo akikanusha usemi huo

Mobeto Afunguka Swala La Kuugua Uchizi Na Tetesi Za Kunyang’anywa Mtoto

Hamisa mobeto  ni moja ya warembo ambao kwa sasa wamekuwa wakisemwa  sana katika mitandao kila kukicha kutokana na drama za hapa na pale na hasa pale ambae mwanadada huyo alipoanza kujihusisha na familia ya msanii mkubwa maarufu Tanzania na Duniani kwa ujumla Diamond Platinumz, amefunguka na kuongelea maneno yaliyokuwa yakisemwa katika mitandao ya kijamii kuhusu yeye kuugua uchizi na kwamba baada ya kuugua uchiz mzazi mwenzie aliezaa nae mtoto wake wa kike wa kwanza aliamua kumchukua mtoto wake na kwenda kuishi nae.

Tukijikumbusha nyuma  kidogo siku chache zilizopita   kulikuwa na tetesi kuwa Hamisa Mobeto amekuwa akikaa ndani kwa sabau ameugua ugonjwa unaosemekana kuwa ni uchizi , ugonjwa ambao pia ulimfanya ashindwe kutekleza majukumu yake kama mama kwa watoto wake.

Hata hivyo katika kutafuta ukweli wa maneno hayo gazeti la  jumaa liliamua kutafutwa watu wa karibu wa Hamisa na ikibidi kumpata Hamisa mwenyewe ili aweze kudhbitisha tuhuma hizo. Na mtu wa kwanza kupatikana kwenye simu alikuwa ni mama yake na hamisa ambae alipoulizwa taarifa hizo alisema kwa jazba’Wewe ndie uliyeleta huo uchawi hapa nyumbani” na kisha kumkatia simu mwandishi huyo wa habari.

Hata hivyo baada ya muda namba ya Hamisa iliweza kupatikaa ndipo alipopokea simu na kuweza kujibu tetesi hizo. Hamisa alionyeshwa kushangazwa na taarifa zilizoendelea katika mitandao ya kijamii kwa sababu habari hizo ni za uongo ingawa ni kweli alikuwa akiumwa lakini sio magonjwa yanayozushwa katika mitandao.

Aisee!mitandaoni kuna mambo.ni kweli nilikuwa ninaumwa lakini sio uchizi,na nilikaa ndani kwa siku kama mbili hivi na ilikuwa kawaida tu kama ambavyo angeweza kuumwa mtu mwingine wa kawaida lakini hilo swala la uchizi mimi wala hata sielewi kwakweli.

Hata hivyo alipoulizwa habari za kunyang’anywa kwa mtoto wake wa kike aliezaa na mmoja wa  ma-dj maarufu nchini Hamisa alisema kuwa mtoto wake alienda kwa baba yake kutembea tu lakini sio kweli alichukuliwa kwa sababu ya matatizo hayo yanayosemwa katika mitandao.

Hivi karibuni Hamisa Mobeto alishindwa tuzo  kutoka Afrika ya Kusini.

 

Hamisa Kuingia Kwenye Fani Ya Uigizaji

Anajulikana zaidi katika uuzaji wa nyango katika video za wasanii mbalimbali ikiwemo ile ya Salome kutoka kwa msanii Diamond Platinumz, kumbe anaweza kufanya kazi nyingi tofauti na hizo.Video queen  mwenye maarufu  wake ambae kwa sasa anazidi kuwa maarufu zaidi kutokana na scandal nyingi ziinazomkabili  hasa katika mambo yake ya kifamilia na mahusiano ,Hamisa Mobeto  amethibitisha kuwa na kipaji kingine cha kuigiza baada ya kushirikishwa katika filamu mojawapo inayotegemwa kutoka hivi karibuni.

Katika ukurasa wake wa instagram, Hamisa mobeto aliposti picha ya movie iyo inayoitwa Zero Player na kusema kuwa yeye pia atakuwa mmoja wa mastaa wataoshiriki filamu iyo inayotegemewa kuchezwa na wasanii wengine wakubwa kutoka Afrika ya Kusini, Ghana,Nigeria na Cameroon huku ikiwa na mazingira ya kuigizia kutoka Tanzania na Afrika ya Kusini.

Uzinduzi wa filamu mpya iliyofanyika South Africa na tanzania ,ikinishirikisha mimi na mastaa wengine kutoka Afrika ya Kusini ,Ghana, Nigeria, & Cameron….Inaatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.Tukae tayari kwa mkao wa kula” aliandika Hamisa Mobeto na kuwaomba mashabiki wake wake mkao wa kula wakisubiri kumuona nini anaenda kufanya humo ndani. Hii pia itakuwa ni moja ya nafasi nzuri kwa Hamisa kuonyesha kipaji chake icho.

Hamisa ni mama wa watoto wawili mmoja wa kike aliyezaa na boss ya stesheni moja ya Radio na Tv, na wa pili akiwa amezaaa na Diamond Platinumz , ambae bado wana migogoro mpaka hivi sana kuhusu mtoto huyo.

Hamisa kwa sasa amekuwa katika scandal ya kugombana na mwanamke wa mwanaume aliyezaa nae(Zari) ambae pia ni msanii mkubwa Tanzania Diamond Platinumz, lakini pia hivi karibuni amekuwa na majibizano ya kimtandao na mwanadada mrembo kutoka Kenya anaejulikana kama Queen V.

Pamoja na kukumbwa na mambo mengi katika mtandao, Hamisa Mobeto bado anaonekana kuwa imara kabisa na kuendelea na kazi zake, ambapo wiliendi hii alikuwa na sherehe ya mwanae mdogo wakiume na baada ya hao aliwasili nchini kenya kwa ajili ya ‘special appearance’ katika event aliyoalikwa ikiwa ni kama moja ya kazi anazofanya kwa sasa.

Alichojibu Linah Kwenye Comment ya Hamisa Ni Utata

Instagram sasa imekuwa mtandao usiokuwa na siri , watu wanaotumia mtandao huo wanazidi kuongezeka siku hadi siku, hivyo mambo mengi yanayofanyika yanakuwa yanaonekana kwa watu wengi, mara nyingine unaweza kuhisi hakuna hatakaeona, au watakaona ni wachache kuhusu kile unachoandika au kupost lakini si kweli.

kuna screenshot zinazosambaa katika mtandao wa instagram zikionyesha comments za Hamisa na Linah katika moja ya picha Linah alizopost hivi karibuni akiwa na baba wa mtoto wake,katika posti hiyo ambayo inaonekana kama kama kuna siri chini ya kapeti kuhusu uwepo wa mwanamke mwingine mjamzito mwenye mahusiano ya kimapenzi na mzazi mwenzie na Linah.

Katika post hiyo Hamisa aliandika”lv unajua kuwa kuna mwenzio ana mimba$$$ mdomo koma lakini” maneno haya yanayoonyesha kama kuna kitu Hamisa anajua kuhusu mwanamke huyo mwingine mwenye mimba hivyo inakuwa kama anatoa tarifa kwa Linah.

Lakini kitu cha kushangaza ni jinsi Linah alivyamua kumjibu Hamisa kuhusu taarifa hizo ambapo anaonyesha kujua kwa taarifa hizo na anaonekana kutokujali kuhusu maneno hayo” @ hamisamobetto, Najua, tulishayaongea kuna lingine” alijibu linah

Linah Sanga ambae miezi michache iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kike mwenye jina TracyParis aliezaa na mpenzi wake  , alisikika hivi karibuni akisema kuwa yeye na mzazi mwenzie huyo wanategemea kufunga ndoa ukiachalia mbali tofauti zao za kidini .

Comment ya Hamisa kwa Linah.

Hata hivyo bado kunakuwa na mishangao kwa baadhi ya watumiaji wa mtandao huu wa kijamii , tena wengine wakimtolea mapovu mwanadada Hamisa mobeto kwa kitendo chake cha kuandika kitu kama hicho ambacho pengine ilipaswa kuwa siri ya familia tu, hii ina maanisha nini kuwa watu hawa wawili wapo katika , je Hamisa alishindwa kuongea na mwanadada Linah nje ya hapo.Je swala hili linapokelewaje na mwanaume aliyehusika katika jambo hili?

Hamisa Mobeto ambae hivi karibuni alikuwa na kashfa nzito ya kuvujisha picha za faragha na msanii mkubwa Tanzania na Duniani kwa ujumla Diamond Platinumz, baada ya msanii huyo kukataa katika vyombo vya habari kuwa mimba na mtoto aliyejifungua Hamisa sio wake , lakini baada ya hapo msanii huyo aliamua kukiri hadharani katika media na kusema kuwa mtoto huyo ni wa kwake.