Wakati Nampenda Diamond Hakuwa na Pesa Wala Huo Mwili :-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto ambae kwa sasa yuko nchi kenya kwa ajili ya show kubwa ya Chipukeezy inayofanyika nchini Kenya alipata nafasi ya kufanya interview katika television iliyompokea huku wakimuuliza sababu kubwa iliyomvutia kwa Diamond mpaka kuamua kutoka nae kimapenzi.

Hata hivyo mwanahabari huyo alimtajia baadhi ya vitu kama pesa, mwili au umaarufu ndio uliomkimbiza kwa diamond mpaka kuamua kuzaa nae.

siwezi kusema kiukweli ni kit gani kilinivutia kwake kwa sababu wakati nina kutana nae hakuwa na hivyo vyote unavyovitaja hata kimoja,yaan hakuwa na pesa, hakuna na mwili wala hakuna na umaarufu alionao sasa hivi.

Hata hivyo Hamisa pia anasema kuwa hata alipoamua kumuacha Diamond ni kwa sababu aliona kuwa ulikuwa ni muda sahihi wa yeye kumuacha na pia anaamini kuwa wapo wanaume wengine wengi wazuri kwa ajili yake.

Ikumbukwe kuwa pamoja na kuachana kwao lakini wawili hawa wanaonekana kuwa na agenda nyingi za siri za chinichini zinazoendelea kati yao pamoja na kwamba masgabiki wanakuwa hawajui.

 

Sitaki Kuolewa na Kijana , Nataka Mwanaume wa Kizungu Mzee ;-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto ameongea na kutoa dukuduku lake la moyoni kuhusu ndoa huku akisema kuwa hataki tena kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kijana kwa sababu vijana wamekuwa wakisumbua sana kuliko wazee.

Hamisa anasema kuwa amekuwa akiwaza kuolewa na mwanaume kuanzia miaka 45 kwa sababu amekuwa akiwafikiria sana watoto wake kwa sasa na jinsi ya kuwalea.

mimi hapa nataka mtu mzima au mzungu, awe tayari alishakuwa kwenye ndoa alafu akaachika au mgane,kwaio ndio hivyo lakini nikisema kijana kwakweli hapana hapo.Awe na kuanzia miaka 45 hivi kwa sababu ukisema kijana mi mwenyewe nina watoto tayari na yeye anakuwa anataka kuendelea kukua, sasa atawezaje kulea wa kwangu.

Hata hivyo Hamisa alikiri kuwa hata ile sauti iliyokuwa ikisambaa katika mitandao ya kijamii ilikuwa ni ya kwake kweli lakini hakuwa anaongea na mganga.

 

 

Mama Diamond Ampiga Hamisa Vijembe kwa Mafanikio Yake.

Mama wa msanii Diamond Platinumz ameonyesha kupinga vikali kila maendelea anayoyapiga  moja ya wanawake waliozaa na mtoto wake Hamisa Mobeto kutokana na vijembe  anavyoamua kumrushia katika mitandao ya kijamii .

Wikiend hii ilisambaa picha ya Hamisa Mobeto akiwa amesimama na mchina mmoja huku wakionekana kupenana mikono kama ishara ya tukio muhimu lililokamilika la kusaini mikataba fulani lakini kitu cha ajabu mama wa msanii Diamond ametupia dongo ilo huku akisema kuwa kuna watu wameeenda kupiga picha na wachina Kariakoo.

Katika post hiyo ambayo inamuonyesha mwanamke  akiimba wimbo wa Diamond huku ikisemekana kuwa huyo ndio mwanamke aliyenae sasa hiv Diamond kutoka Nigeria, Mama Diamond alifanya ku-repsost kutoka kwa diamond huku yeye akiandika maneno yenye hashtag ya #watuwameendakariakookupigapichanawachinatuonedeal

 

Siwezi Kugombana na Mwanamke Mwenzangu Kisa Mwanaume.

Ingawa mara nyingi wamekuwa wakirushiana sana maneno katika  mitandao ya kijamii hasa kuhusu ugomvi wako wakiwa wanagombania penzi la msanii diamond platinumz lakini moja ya wanawake hao mmoja amefunguka na kusema kuwa hana shida ya  mwanaume hivyo hawezi kugombana na wanawake wenzie  kisa mwanaume.

Wanawake kugombania mwanaume na mara nyingi huwa ni kawaida kwenye maisha tunayoisho lakini hili limekuwa tofauti kwa upande wa Hit Maker wa ngoma ya ‘MadamHero’ Hamisa Mobetto baada ya kuweka wazi kuwa hawezi kugombana na mwanamke mwenzie kisa mwanaume kwa madai wanaume wako wengi.

Hamisa amesema hayo akiwa kwenye interview alipokwenda kutambulisha nyimbo yake na alipoulizwa kama ana tatizo na Wema na Zari kisa Diamond mwanamitindo huyo akajibu “Siwezi kugombana na mwanamke mwenzangu kisa mwanaume na sina ugomvi na Wema wala zari” kwa upande mwingine Hamisa amekubali kuwa ile voice note iliyovuja ilikuwa ni yake na alikuwa akiongea na Sheikh kuhusu dua na sio mambo mengine ya kishirikina.

Nyota Ya Hamisa Mobeto Yazidi Kung’ara.

Pamoja na kwamba amekuwa akishambuliwa katika mitandao ya kijamii huku wengune wakumtuhumu vibaya hasa wale watu  ambao ni mashabiki wa upande wake wa pili ,mwanadada Hamisa Mobeto amezidi kuonekana akiwa na nyota yenye kungaa baada ya kupata deal lingine alilosaini hivi karibuni.

Akionekana katika picha  na moja ya mabosi wa kampuni fulani, mwanadada hamisa mobeto ameonekana mwenye furaha na mwenye kuonyesha sura ya mafanikio sana hasa baada ya kuweka picha hiyo akiwa tayari ameshasaini mkataba huo.

Hamisa ambae hivi karibuni alitoka kusaini mkataba mwingine  wa kampuni ya Prima Afro anaendelea kuonyesha mafanikio yake hasa baada ya hivi karibuni kutoa wimbo wake na kuonyesha kupokelewa vizuri.

Hamisa Atoa Sababu Kubwa ya Kumblock Diamond

Mwanadada Hamisa Mobeto wikiend hii amefunguka na kutoa sababu yake kubwa inayomfanya kuwa anam-block Damond katika kurasa zake za intagram lakini hata ile ya mtoto wake kama ilivyosemakana hapo awali tangu kwa shangazi wa mtoto huyo ambae alipowahi kuulizwa aliongelea swala hilo.

Hamisa ameongea hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Times Fm ambapo alisema kuwa amekuwa akifanya hivyo kwa sababu kuna maswala ambao mtoto wake hayamuhusu kabisa katika gomvi zao lakini mtoto huyo amekuwa akingizwa humo.

Kwenye page ya mtoto sio kumfuata tu lakini hata kum-block  pia kwa sababu amekuwa kama hajielewi vile,hata kama we have issues hakuna haja ya kumuingiza mtoto au hata mama yake, unajua kwetu wanasema mstiri mtu aliyekuzaliwa mtoto au kumheshimu yule ambae ni mke wako kwa sababu aibu yako ndio aibu yake.

Hamisa na Diamond wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume na kumfanya Diamond kutimiza idadi ya watoto watatu,

kijembe cha Steve Kilimlenga Hamisa Mobeto.

Kama siku mbili nyuma kuna habari ya Steve Nyerere kuongelea mambo ya uchawi na ushirikina ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii huku steve akisema kuwa mchawi mkubwa pekee ni mungu tu na wala sio binadamu kama watu walivyozoea.

Lakini katika kukaa saa na kuchunguza steve nyerere pia alisema kuwa ” wanawake wengi sana  wanaamini kuwa hawawezi kufanikiwa mpka wapate wanaume wenye pesa na wengine udirki hata kwenda kwa waganga wa kienyeji ili kupata wanaume hao wanaowahitaji

Kwa trending ya habari  ya wiki iliyopita habari kubwa iliyokuwepo katika mitandao ilikuwa ni swala la ushirikina ambalo alihusishwa hamisa mobeto na familia ya Diamond Platinumz huku ikisemekana kuwa hamisa amekuwa akimloga diamond ili aendelee kumpenda na kumpa pesa.

Swali linakuja je, kauli ya Steve nyerere haikuwa ni kijembe  kilicholenga kusistiza habar za uchawi za hamisa mobeto, na kwanini yamesemwa hayo baada ya kuvuma kwa skendo ya uchawi kwa hamisa Mobeto.

Yawezekana huo ni msumari wa moto steve nyerere aliamua kuupigilia kwa hamisa lakini bila kuwka wazi kuwa alikuwa akimlenga yeye.

Tangu Nikiwa Mtoto Nilikuwa Naongelewa, Mama Aliniambi kwa sababu Nina Kitu Special:-Hamisa

Mwanadada Hamisa Mobeto jana laipokuwa katika kampeni ya SMART na wasanii mbalimbali alipata bahati ya kuulizwa swali na waandishi wa habari  kuhusu yeye kuwa akiongelewa katika mitandao ya kijamii na ndipo aliposema kuwa kwake ni swala la kawaida kwa sababu amekuwa akiongelea tangu akiwa mtoto.

Hamisa anasema kuwa hata akitoka shule alikuwa kunyooshewa sana yeye vidole kuliko watoto wengine wote na alipokuwa akimuuliza mam ayake alikuwa akimjibu ni kutokana na utofauti wake aliopewa na Mungu ndio uliomfanya awe hivyo.

Hamisa anasema kuwa hakuwa anajibizana na watu tangu akiwa mtoto na hata sasa ni kutokana na malezi yale aliyoyapata kutoka kwa mama yake na maneno mazuri ndio yanayoendelea kumpa moyo wa kufanikiwa zaidi nakujikuta akifanikiwa kila siku.

nadhani kila mtu ana moyo na kwa upand wangu pia ni hivyo hivyo kila kukicha likija jipya unakuwa tu unasema na leo hili tena .hii ni kwa sababu nimekuwa na moyo mgumu kwa sababu tangu niko nasoma kablwa isjakuwa maarufu nilikuwa nasemwa pia.

na nilikuwa namuuliza mamangu kwa nini nikipita kutoka shule ninaongelewa tu yaani,lakini mamangu aliniambia ni kwa sababu nina kitu special na ndio maana ninaongelewa kuliko watoto wengine.lakini pia ni kutokana na moyo wa mtu na vile mtu ulivyolelewa.

Siku za hapo nyuma kidogo mama wa mwanadada Hamisa aliwahi kunakiriwa akisema kuwa hata Dunia imfanye nini lakini hatokaa aache kumsapoti mtoto wake Hamisa kwa sababu ndio mtoto wake wa pekee.

Pamoja na yote anayopitia na kutukanwa kwa hamisa baba yake ameonekana kuwa mstari wa  mbele kumsapoti na kumkingia kifua na hata kusimama mbele za watu na kusema anajivunia mtoto wake.

Gigy Money Atoboa Siri ya Aliyeimba I like It Kwenye Jibebe Ya Diamond ni Hamisa.

Kwa muda sasa tangu wimbo wa jibebe umeanza kusikika katika masikio ya watu na mpaka video yake kutoka katika television mbalimbali watu wamekuwa wakijiuliza ni nani aliyeimba wimbo huo na kwamba kwanini hata kwenye vide hajaonekana.

Basi siri imevuja baada ya mwanadada Gigy Money kuamua kutoa siri hiyo kuwa aliyeimba kasauti hako katamu ambako watu wengi wamekuwa wakiipenda na kumuulizia muimbaji kuwa ni Hamisa Mobeto mzazi mwenzie na Diamond.

hamisa na gigy money ni marafiki hivyo kwa asilimia fulani maneno ya Gigy Money yatakuwa na ukweli ndani yake . Gigy Money anasema ” Najua Hamisa anafanya muziki sio kwa biashara ila for funny , ila ile i like it ya jibebe  ameweka yeye , ana sauti nzuri ila siwezi sema kuwa atafika mbali kweye muziki.

Idris Aongea na Hamisa, Amsapoti Kama Maskini Mwenzake.

Mchekeshaji maarufu nchini idris sultani ameamua kuvunja ukimya baada ya kuamua kumpa maneno ya faraja mwanadada Hamisa Mobeto kutokana na biashara zake na mambo ya upinzani yanayoendelea katika mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, idris sultan aliandika maneno hayo ikiwa ni njia ya kumtia moyo  mwanadada huyo kutokana na safari yake ya muziki na ujasiriamali aliyoiazisha.

naomba niwe wa kwanza kabisa kukusapoti ili baadae unapoanza kuchukua matuoz usitusahau masikini wenzako.mwanzo sio mwepesi lakini kamamsiamamizi wa mpesa vodacom ninaweza kusema yajayo yanafurahisha.nitashangaa kuona watu wanakukejeli kwenye hii hatua yako , sijui wanataka utembee barabarani unauza naniliii.

katika hatua zako za mafanikio, jua sana kuchuja maneno, kama kweli umekubali kuanza muziki basi kazz na utatoboa tu kwani hao wengine ni wakina nani,wengine tulianza na wala hatukubaliki tutoe msaada wa nguo zetu tubaki watupu ila unakazaa tu baada ya muda unaanza kuokota fans  mmoja mmoja wawili mwishowe unajikuta una mamilion.

hamisa mobeto amekuwa moja ya wasichana wanaoandamwa sana katika mitandao ya kijamii kutokana na kila hatua anayoipiga na hayo yote yalianza baada ya kuzaa na Diamond platnumz.

Hamisa Mobeto na Zamaradi Hapatoshi.

Mwanadada Hamisa Mobeto na mwanamama Zamaradi Mketema wameingia katika bifu zito na kujibishana  maneno katika mitandao ya kijamii baada ya Zamaradi kumshushia maneno mazito hamisa Mobeto kwa kumsambazia habari za uongo kuhusu makubaliana yao ya kushonewa nguo kwa ajili ya 40 ya mtoto wa Zamaradi.

Katika kurasa za udaku , hapo awali kuna ukurasa uliandika mambo mengi kuhusu zamaradi ikiwa ni pamoja na kwamba nguo alivaa siku ya sherehe hiyo ilitakiwa kushonwa kwa hamisa lakini cha ajabu baada ya hamisa kumpa mshono zamaradi, basi zamaradi akakimbia kwa fundi mwingine , lakini pia kuwa sherehe hiyo ilichangishwa pesa kutokwa kwa wadau na mshabiki zake .

Baada ya maneno hayo ndipo Zamaradi naeo alipoamka na kutaka kuonyesha ushahidi wa yote yaliyokuwa yakiongelewa na kusema kuwa pesa hakuwahi kumchangisha mtu yoyote zaidi ya pesa ya zawadi ambayo wanakikundi waliamua kumpa siku hiyo na wala hakuwa anajua hilo.”tukija kwenye nguo naambiwa kuwa nilipewa mshono na mwingine na nikaenda kushona kwa mwigine, funny nimeattach hapo juu na picha muone kuwa mimi ndio nilietuma mshono wake na wala sio yeye.kutokana na kupishana na muda nikaona bora nikashone kwingine , kwanza ni uamuzi wangu kuamua kushona popote pale.”

Hata baada ya zamaradi kuongea hivyo, Hamisa nae aliamua kuja na kuongea  nakuweka picha za chat  zinazoonyesha mazungumzo yake na zamaradi na kwa jinsi gani mwanamama huyo alimtafuta na kuomba ushauri wa nini cha kushona siku hiyo.

 

 

Hamisa Mobeto Ajiingiza Katika Muziki, ni kwa Ajili ya Kinamama

Mwanamitindo maarufu nchini Hamisa Mobetto kwa mara ya kwanza ameachia Clip Fupi inayosikika ngoma yake ya Madam Hero kupitia ukurasa wake wa instagram ambayo ni Track Mojawapo Aliyoimba Kwa Ajili ya Foundation yake ya The Mobeto Foundation

Hamisa  amesema lengo kubwa la kuachia ngoma hiyo ni iwafikie wanawake wote as An inspirational Song kama nguvu ya kupambana na kutokukata tamaa .
.
Vilevile hamisa amesema pesa ya mauzo atakayoyapata kupitia wimbo huo wa Madam hero itaenda kwa Wakina Mama wote wanaowalea watoto wao kwenye mazingira magumu na kwa wanojifungua katika hali ngumu

Ninge beba Mimba Tena Lazima Ingetoka:-Hamisa

MWANAMITINDO maarufu na mzazi mwenziye mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Hamisa Mobeto amefunguka kuwa hana ujauzito kama watu wanavyoeneza uvumi huo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Akizungumza na Amani, wakati akitoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima cha CHAKUWAMA, kilichopo Sinza-Mori jijini Dar, Mobeto alisema haiwezekani akawa mjamzito kwa kipindi hiki sababu kwanza mtoto wake bado ni mdogo na maneno mengi ya kejeli yanatolewa dhidi yake mtandaoni.

“Watu naona wanachukulia kubeba mimba ni kitu rahisi sana lakini wangetambua mimi nina mtoto mdogo sana lakini kitu kingine waangalie kuwa hata kama ningeshika ujauzito lazima ungetoka maana kila kukicha ni kusimangwa ila muda wangu sahihi ukifika wa kuzaa mtoto mwingine nitafanya hivyo tu,” alisema Mobeto.

Nyumba ya Hamisa Yaleta Utata, Yasemekana ni ya Kupanga.

Inasemekana kuwa hiyo inaweza kuwa ni tabia ya msanii Diamond Platinumz kuwa na show-off kila anapofanya kitu na kuwaamisha watu kuwa kila anachokifanya  ni mali yake kumbe sio kweli, hii inaendelea kuonekana baada ya ku-trend sana katika mitandao ya kijamii kuhusu nyumba ambayo inasemekana kuwa ni nyumba ambayo Hamisa amenunuliwa na Diamond lakini habari za chini chini zinasema kuwa nyumba hiyo sio ya kununua ni ya kupanga.

katika moja ya kurasa za  instagram inayojulikana kama dalali kiongozi imeonyeshwa nyumba hiyo ilipokuwa katika matangaza ya kupangishwa hapo kipindi cha nyuma na hata kutajwa kiasi cha kupangishwa kwa nyumba hiyo.

Amber Lulu Amuonea Huruma Hamisa.

Mwana dada Amber Lulu amefunguka na kusema amekuwa akimuonea huruma sana  Hamisa Mobeto kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiandamwa na watu hasa familia ya ndugu wa Diamond mwanaume ambae amezaa nae mtoto mmoja wa kiume na kuonekana kuwa hapendwi na familia hiyo.

Anachokisema Amber Lulu ni kwamba anaamini kuwa Mungu yupo na Hamisa na ipo siku atamuona na kumpigania sana na kumtoa katika kifungo icho cha mateso anachopitia kwa muda wote sasa.

Mimi ninamuamini sana mobeto na nina jua ni mwanamke anaejiamini sana,kwaio hilo linalomtokea sasa ni changamoto tu za maisha , niseme tu yeye aendelee tu na biashara zake  na kazi zake kwa nguvu zake zote na kulea familia yake,achukulie hiyo kama chngamoto tu na kufanya kazi zake kwa bidii na kama mwanaume anampenda basi atarudi tu.

 

 

Hamisa Kulikwaa Penzi la The Game.

Habari izlizosambaa katika mitandao ya kijamii zinadai kuwa hivi karibuni moja ya wasanii wakubwa Duniani The Game amemtumia  mrembo Hamisa Mobeto meseji huko DM akimchombeza na kumsifia kwa urembo alionao huku akimkubali sana.

Hata hivyo siri hiyo imevuja baada ya mtu wa karibu wa hamisa kusema kuwa hamisa aliona meseji katika DM yake na kuona kama ni uongo au watu wa kawaida wa kimtandao lakini alipofatilia aligundua kuwa ni akaunt ya kweli kanisa ya msanii huyo.

Hata hivyo Hamisa alipata uoga sana kujibu sms hizo huku akionekana kutokuamini kwa kile anachokiona katika instagra, yake upande wa DM na kupatwa na kigugumizi  wa nini cha kujibu.

Hii ni habari njema kwa mashabiki wa mobeto, inawezekana msani huyo akataka kufanya kazi na Hamisa.