Hemed Atangaza Wokovu, Ajutia Maisha Yake ya Nyuma

Msanii maarufu wa filamu bongo, Hemed Suleiman maarufu ‘Hemed phd’, ameweka wazi juu ya maisha yake ya sasa kwamba ameamua kuokoka na kubadilika kitabia.

Akizungumza kwenye DADAZ ya East Africa Televisio, Hemed amesema kwamba awali alikuwa na maisha ya kupenda kubadili wanawake, lakini sasa ameamua kutulia na kuwa na mpenzi mmoja, anayetengeneza naye maisha.

Akiendelea kuweka wazi maisha ambayo alikuwa nayo mara tu baada ya kuupata umaarufu, Hemed amesema kuwa aliachana na mpenzi wake ambaye alikuwa naye tangu akiwa darasa la tatu, lakini alimuacha mara tu baada ya kurudi kwenye mashindano ya Tusker Project Fame.

“Nilipoanza umaarufu, yule demu wangu niliyeanza naye tangu darasa la tatu mpaka napata ustar alikuja tu airpot kunipokea nilipokuwa narudi kwenye Tusker Project Fame, nilijiuliza huyu kafuata nini hapa!?. Yaani niliona ashakuja kuniharibia, maana siku ile totoz zilishaniambia sirudi nyumbani, nikawa ni mtu wa watoto tu, ila kuna muda unafika unasema nakua sasa nahitaji ‘future’, nikaamua kutulia na mmoja sasa hivi nimeokoka kabisa, sina mambo hayo”, amesema Hemedi.

Hemedi amesema kutokana na tabia ambayo alikuwa nayo, muda mwengine hata mtu ambaye yuko naye hamuamini, lakini ameamua kumuweka wazi kwa sababu ni kweli ametulia.

Hemed PHD Ataja Sababu Za Kukimbia Kuzaa na Mastaa Wenzake

Muigizaji wa Bongo movie Hemed Suleiman ‘PHD’ amefunguka na kutaja sababu za kukimbia kuzaa na Mastaa Wenzake na kuishia kuzaa na wanawake ambao sio maarufu.

Hemed ameweka wazi kuwa amlichagua kuzaa na wanawake ambao sio maarufu kwa sababu hakuona staa wa kike ambaye angeweza kuzaa naye na kisha kuwa mama bora.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Hemed amefunguka na kusema kuwa kwa sasa ana watoto sita ambao amezaa na wanawake tofauti, lakini hakuwahi kuona mwanamke staa mwenye kigezo cha kuzaa naye kwani anapenda wanawake wanaojiheshimu na wenye mapenzi ya kweli.

Ninamshukuru sana Mungu kwa kunijalia watoto sita kwa wanawake ambao hawana umaarufu hata mmoja maana wangekuwa mastaa tungesumbuana sana”.

Hemed ana jumla ya watoto sita na Wanawake tofauti tofauti lakini mtoto wake pekee ambaye amekuwa akimuanika ni wa mwisho ambapo amedai watoto wake wengine Hawaonekani kwa sababu mama zao hawataki.

 

Gigy Money Adai Akipewa Nafasi Atawamaliza Ali Kiba na Hemed PHD

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai kuwa endapo akiambiwa awagonge wanaume wowote ambao amewahi kuwa nao Kwenye Mahusiano basi atakuwa Ali Kiba na Hemed PHD na Rich Mavoko.

Gigy Money ambaye alianza kuongia Kwenye ulimwengu wa kisanaa kama Video vixen Mpaka sasa Msanii wa Bongo fleva amekiri Kuwahi kuwa Kwenye Mahusiano na wasanii wengi.

Gigy amekiri hapo nyuma kutokana na kufanya kazi za video na wasanii wengi basi pia ameshawahi kuwa nao Kwenye Mahusiano wengi sana na baadhi yao ni Rich Mavoko, Ali Kiba, Hemed PHD na wengineo.

Kwenye Interview moja aliyofanya hivi karibuni Gigy Money aliulizwa ni Ex gani wake staa ambaye leo hii akipewa ruhusa ya kumgonga na gari na kummaliza atamchagua nani?

Ikitokea nimepewa pesa niwagonge wapenzi wangu wa zamani, nitaomba nipewe fuso kabisa tena nitawasaga haswa nikianza na Hemed PHD, Ali Kiba na Rich Mavoko maana waliniumiza sana”.

 

Hemed PHD ni Chawa Wangu- Gelly Wa Ryhmes

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gelly wa Rhymes amefunguka na kudai kuwa msanii mwenzake wa Bongo fleva Hemed PHD pia ni chawa wake.

Hemed na Belly wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 11 wameshirikiana na kudhirikishana katika nyimbo zao mbali mbali lakini wameigiza pamoja filamu za bongo movie kadhaa na kwa nyakati tofauti wote wamesisisitiza kuwa wao kwa sasa ni zaidi ya marafiki wamekuwa kama ndugu kwa ukaribu wao.

Gelly amejibu fununu zilizopo mtandaoni zinazodai kuwa yeye ni chawa tu wa Hemed na hana mchongo mwingine wa maana hapa mjini, Gelly amesema yeye na Hemed ni zaidi ya ndugu hivyo watu wanaomuita chawa wake hawafahamu kuwa hata Hemed ni chawa kwake.

Gelly alifunguka hayo kwenye mahojiano na Enews ya EATV ambapo pia alizidi kuongeza:

Kwanza nilikuwa sielewi maana ya chawa mpaka uliponielezea kumbe chawa ni mtu ambaye yuko karibu na mtu basi kama ndio hivyo Hemed basi na yeye chawa wangu kwa sababu na yeye yupo karibu na mimi sana, anyway iko hivi mimi na Hemed sahivi tumevuka urafiki tuko kama brothers na ni watu tunaosaidiana kwenye kila kitu hata kutoa nyimbo lazima tushauriane kwaiyo tuko pamoja most of the time hasa hasa kikazi hata yeye akiwa na tatizo ananifuata ananiambia na mimi pia nafanya hivyo hivyo”.

Lakini pia Gelly ameongelea label yao pamoja naHemed inayoitwa Pappination lakini pia nyimbo yake aliyoitoa hivi karibuni inayoitwa ‘Vibenten’ ambayo ndani yake ameongelea vijana wa mjini ambao nivibenten lakini pia amedai amewataja kwa majina humo ndani.

Hemed Ajutia Maisha Yake ya Nyuma

Msanii wa muziki na filamu nchini Hemed PHD amekiri kuwa maisha yake aliyokuwa akiishi kipindi cha nyuma yalikuwa hayana mwenendo mzuri na yalikuwa machafu tena hasa katika kipengere cha mahusiano  kwa sababu alikuwa akipenda sana wanawake isivyo kawaida.

Hemed PHD, anasema kuwa amekuwa akiyajutia sana maisha hayo aliyokuwa akiishi kipindi cha nyuma na kwamba anawashauri hata vijana wengine waache kupenda starehe na kufanya maisha ya anasa.Hemed PHD anasema kuwa alikuwa ana uwezo wa kutembea kimapenzi hata na wanawake watano kwa siku moja na wala alikuwa haoni ajabu yoyote.

Sio kitu cha kujivunia kwa sasa hivi kwa sabau ni maisha niliyoyapitia tayari,lakini nisngependa vijana wengine wanaonisikiliza  wayapitie na kuyaishi kama mimi, lakini mzee mimi nilikuwa ninaweza kula hata mashine tano kwa siku.-Alisema Hemed PHD alipokuwa akiongea katika kipindi cha radio moja wapo nchini.

Akiendelea kusimulia , Hemed  PHD, anasema kuwa hakuwahi kuwa na makazi maalum ya kuishi na kuna muda alikuwa naweza kukaa hoteli na ikawa kama nyumba kwa ajili  ya kufanya ufuksa na wanawake tofauti tofauti. ‘sometimes nilikuwa najenga kambi mahotelini kwa ajili ya kufumua tuu.”

Jambo la kusikitisha na kushangaza kwa Hemed  PHDni kwamba hakumbuki na waka hajui kabisa alishajiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wanawake wangapi ingawa ansema kuwa idadi ni kubwa sana isivyo ya kawaida.

Hemedy PHD: Mimba ya Mapacha ya Girlfriend Wangu Imetoka ghafla, Lakini Ningekuwa na Watoto 8

Muigizaji wa Bongo movie na mwanamuziki wa Bongo fleva, Hemed PHD amefunguka kuhusu tuhuma anazorushiwa kwa kitendo kinachosemekana kuwa amewaacha solemba watoto wake watano na kumuweka wazi mmoja tu.

Hemedy ni moja kati ya wasanii anayesemekana kuwa na watoto wengi ambapo amesema kuwa ana watoto sita. Kwenye mahojiano aliyofanya hivi karibuni Hemed amekiri kuwa na watoto wengi kiasi kuwa wengine ni ngumu kuwatambua kwani kipindi cha nyuma alikuwa anakataa mimba nyingi.

Pamoja na kuwa na watoto wengi, kupitia ukurasa wake wa Instagram na mitandao mingine yote ya kijamii Hemed humweka wazi mtoto wake mmoja tu na hivyo kupelekea watu wengi kudhani kuwa ana mtoto mmoja tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa radio, Hemed alifunguka haya kuhusiana na tuhuma hizo na tetesi za kuwa na watoto sita:

Kwanza naomba niseme kuwa namshukuru Mungu kwa kila kitu kilichotokea kwenye maisha yangu kwa sababu wiki mbili zilizopita mpenzi wangu alipata miscarriage na ilikuwa mimba ya mapacha kwahivyo ningekuwa na watoto nane na mtoto wangu wa kwanza ana miaka mitatu na wanaofuatia wote watano wamepishana miezi miwili miwili na kila mtoto na mama yake”.

Pia Hemed alifunguka kuhusu tuhuma za kuwatenga watoto wake wengine na kumuonyesha mtoto mmoja tu ambapo amedai kuwa mama za watoto wake wengine hawapendi awaanike watoto wao kwenye mitandao ya kijamii hivyo anaheshimu maamuzi yao na kuwaweka private na pia kuna ugomvi wa kifamilia baina yangu na wamama hao.

Hemed Phd Akiri Kuwa Msanii Mwenye Watoto Wengi

Kuna tabia za wasanii hazibadiliki tena hasa Kwa wasanii wa kiume, wengi wamekuwa  wakikataa kuwa na majukumu  hasa ya kifamilia(watoto), kuwa na watoto sio jambo dogo , lakini pia sio jambo la mkosi, kuwa na mtoto ni jambo la kheri, kuna baadhi ya wasanii wakubwa tu nchini wamekuwa  wakikata majukumu ya kulea watoto hao na kuwaachia  wazazi wa upande wa pili kubaki wakiangaika na mizigo ya kulea peke yao.

Hemed Phd ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Mkimbie’ anasema kuwa amekuwa kimya kwa muda kwa sababu ya majukumu ya kifamilia”tunakuwa kimya kutokana na majukumu,majukumu ndio yanaweza kukubadilisha kutoka kwenye ujana kwenda kwenye ubaba, siwezi kusema kuwa ni mafanikio sana kwa sababu havikuja katika mipango kama nilivyotarajia,, hivi vitu vilihappen tu buubaa basi  Mungu akafanya yake lakini ninajivunia kwa sababu ninaweza kuwahudumia  watu ambao wananiangalia kwa kiasi kikubwa .Am proud to be a father'” alisema Hemed

Msanii Hemed  Phd , alikiri kuwa hata yeye alikuwa akichomoa pale alipokuwa akiambiwa kuhusu taarifa za wanawake wake kumwambia wanaujauzito lakini inapokuja kwenye swala la mtoto anatoka amefanana nae kila kitu hivyo ni lazima akubali”kiukweli mwanzo nilikuwa nazingua  kwa maana ya kwamba nilikuwa sizikubali mimba kabisa lakini copy zilivyotoka,wanangu wazuri sana,wanangu wamenizidi uzuri ivyo inabidid tu niwakubali maana wanafanana na mimi’ anaendelea kuongea

Hemed anasema kuwa hata hivyo , imekuwa tofauti kwa upande wake kwa sababu watoto wake wote hakuna ambae amebambikiziwa hata mmoja wote ni wa kwake na anawalea wote,kwa sababu hata matendo ya kupata mimba  anavyofanya anakuwa anajua kipi kinafanyika.

Hata hivyo kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa pamoja na kuwa na watoto wengi lakini amekuwa akimpost mmoja tu” ni kweli ,lakini katika familia kuna mambo mengi, na bado ninayaweka sawa, yakikaa sawa ntawaweka wote , ila kwa sasa naomba ijulikana kuwa huyo ndo mwanangu na ifahamike ivyo kwa sasa” aliongezea Hemed

Kuhusu kuwa na watoto wengi hemed alipoulizwa ana watoto wangapi alijibu”ngoja nikatafute daftari langu kwanza niangalie idadi, ila nashukuru mungu tumeambiwa tuijaze Dunia kwaiyo kuwa na  watoto wengi ni sawa tu’ aliongezea Hemed