“It hurts to think that you are not here” huu ndio ujumbe ambao Raphael alimwandikia baba yake Ivan Don

Familia ya Zari Hassan inaomboleza kifo cha Ivan Don aliyefariki Jumanne baada ya kuugua kwa maradhi ya moyo.

Zari alimwandikia Ivan ujumbe huku akiomboleza kifo chake na pia kumsheherekea kwa kuwa mfano mzuri kwa Watoto wake muda wote aliokuwa hai.

Hata hivyo Raphael ambaye ni mmoja wa watoto wa Ivan aliandika ujumbe kwenye Instagram yake huku akimuomboleza babake ambaye kwa sasa amewaondokea wakiwa bado wadogo. Raph aliendika kusema,

“It hurts to think that you are not here anymore. Although I can’t help but smile with tears in my eyes to think of how we cherished each and every moment of our lives together; I will miss you Dady and I cant stop crying anymore when i think of you Dady @ivandon may your souls rest in peace.”


Mungu aiweke roho yake pahali Pema.

Ni kweli kuwa aliyekuwa mpenzi wa Zari, Ivan Don alitiliwa sumu kwenye chakula?

Fununu mitandaoni inadai kuwa Marehemu Ivan Don alifariki baada ya kutiliwa sumu chakulani chake pale ambapo alikuwa akikula na marafiki wake wa Karibu.

Ripoti hizi zilisambazwa na gazeti moja la Uganda liloandika kudai kuwa kuna ushahidi wa maneno haya. Hata hivyo kulingana na tulichoambiwa na familia yake ni kuwa Ivan Don alifariki baada ya viungo vyake vya mwili vilipoanza kufaili kwa kuwa alikuwa anapumua kupitia usaidizi wa machine.

Familia yake imenyamaza na hakuna aliyechangia kwenye ripoti za Ivan Don kupewa sumu na adui yake ambaye ni mmoja wa marafiki wake wa karibu.

Gazeti hilo liliandika kusema,

“Zari anaumia kumuona Ivan akiwa kwa hali maututi” Diamond Platnumz asema

Diamond Platnumz hivi karibuni alifunga kusema sababu ambazo hajaweza kumpost aliyekuwa mpenzi wa Zari wa zamani, Ivan Don kumtakia kupona haraka.

Akizungumza na kipindi cha Clouds FM Diamond Platnumz alisema Kuwa anaona watu watasema kuwa anatafuta kiki kwa kumuweka Ivan Don kwenye Instagram yake kwa sababu wengi hudhania kuwa wawili hao hawapatani baada ya Diamond kumchukua Zari Hassan ambaye alikuwa mke wa Ivan kabla ya wao kuachana.

Hata hivyo Diamond Platnumz amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na Zari kila wakati anapoenda kumuona Ivan Don hospitalini. Aliendelea kwa kusema kuwa Zari anaumia kumuona baba ya Vijana wake akiwa kwenye hali hiyo. Lakini kwa sasa wote wanamubea ili apate nafuu nataka.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda,” Diamonda alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM. Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,