Zari adaiwa kupungua mwili Kisa na sababu, Hamisa Mobetto

Mrembo na mama watoto wa Diamond Platnumz, Zari Hassan anasemekana kuwa na mawazo mengi ambayo yamemfanya kupungua kimwili sababu ya kufikiria sana.

Habari hizi ziliwekwa wazi na chanzo kimoja kilichozungumza na Global Publisherz kueleza hali ya Zari inavyoendelea tangu Hamisa Mobetto kuweka wazi kuwa Abdul Naseeb ni mtoto wa Diamond Platnumz. Chanzo hicho kilisema;

“Zari kapungua mwili kweli jamani. Mobeto amemponza. Amemsababishia watu wamtukane sana Zari kiasi ambacho amekosa amani kabisa. Masikini mtoto wa watu kakonda kweli sasa hivi.Ukitazama picha za Zari sasa hivi si Zari yule aliyetoka kujifungua. Tena kwa kawaida tunajua mtu ukitoka kujifungua unanenepa lakini kwa Zari mambo yamekuwa tofauti. Ngoja niwatumie picha yake ya sasa muone,”

 

Hata hivyo maneno haya yanauwezekano ya kuwa ya kweli kwani kwenye picha za Sasa, Zari anaonekana kupugua mwili sana.

 

 

Zari
Zari

Lucy Komba awapasha mashabiki wa Zari wanaomtusi Hamisa Mobetto

Muigizaji wa bongo Lucy Komba amefunguka kwa mara ya kwanza kuwakomesha watanzania ambao wanamtukana Hamisa Mobetto kisa kuwa mtoto aliyezaa ni Diamond Platnumz.

Hii ni baada ya wengi kudai kuwa kunauwezekano wa mtoto huyu wa pili wa Mobetto kuwa wa Diamond Platnumz ambaye anasemekana aliwahi kutoka kimapenzi na Hamisa Mobetto.

Lucy Komba

Hata hivyo Lucy Komba aliwatoa wengi povu kwa kuandika;

“Samahani lakini kimenichoma. MABOGAS YA TZ YANAMPONDA MTZ MWENZIO YANAMSIFIA BOGAS MWENZIO sijui yanafikiri yatapewa ule urithi. Mbona waganda hawambabaikii acheni umasikini wa kujirahisisha. Au mnafikiri mtapitishiwa kila mmoja karanga moja moja ya bure,”

Aliongeza,

“Hongera mwanamke mwenzangu, wanajifanya roho ngumu tu kukuponda wakati roho zinawauma unatoa vitu hasa mwanamke unazaa huku unatabasamu. Wale wanaoniponda eti ningekuwa mzalendo nisingeolewa na mzungu, Yes nimeolewa na mzungu sababu sina ubaguzi wa rangi wala ukabila na tangu nimeolewa sijawahi kutukana kaka zangu wakisfrika kwa hiyo lazima mjue kutofautisha A na B. Pili anayewapa taarifa nimeachwa nahisi kama kachelewa kuwataharifu halafu mwambieni awape taarifa kamili maana huwa anaingia insta na kuzizungusha bado hajawapata taarifa za kunichamba huku mmesimaisha visimi. Ukweli unauma mmepewa ukweli wa huyo stranger wenu aliyenenepesha miguu kiuno kimeshindikana kukipunguza mnalia chambeni tu mniongezee followers maana nilikuwa sijaamka bado kujua kumbe umaarufu wa bongo unatokana na vichambo. GOODMORNING.,”

Zari Hassan na Diamond Platnumz washerehekea siku ya kuzaliwa ya mtoto wao, Princess Tiffah

Diamond na mpenzi wake Zari The Bosslady walisherehekea siku ya kuzaliwa ya Princess Lattifah Jumapili hii iliyopita kwa kumuandikia ujumbe ambao umewaacha wengi wakifurahia kupitia mitandaoni yao ya Instagram.

Hii ni baaad ya Zari alipojifungua mtoto wa kwanza wa miaka miwili iliyopita. Kupitia mtandao wa instagram, wazazi hao walionyesha furaha zao kupitia ujumbe wao.

Zari aliandika,

“It’s princess world…happy birthday my one and only princess_tiffah.”

Na akaongeza kusema;

“My Princess….. May God see you through with nothing but the best. May you be blessed from this day forward. Most of all, May you be a Godly child. Without God we are nothing. Happy birthday @princess_tiffah,”

Diamond Platnumz naye akaandika;

“Happy 2 years mama, Words Can’t express how much i love you my Tee….

Tiffah ni miongoni mwa watoto maarufu Africa yote.

 

Picha za Zari Hassan akiwa amevalia kama mwanamke anayefuata maadili ya dini ya Kiislamu

Japo sio mara mingi tunamuona Zari Hassan kama amejistiri, kuna picha zake kadhaa ambazo mrembo huyu ameonekana amevalia dera na buibui ambazo wanawake wa dini wa kiislamu huvaa.

Hapo awali mpenzi wake Diamond Platnumz alisema kuwa yeye hana shida na Zari Hassan kuvaa anavyotaka kwani hawezi kumchagulia wala kumbadilisha kwa kumtaka ajistiri.

Picha ambazo nimezipata mitandaoni, Zari anaonekana kupendeza kwa mavazi haya ingawa hii sio style yake.

Tazama picha hizi hapa chini;

“It hurts to think that you are not here” huu ndio ujumbe ambao Raphael alimwandikia baba yake Ivan Don

Familia ya Zari Hassan inaomboleza kifo cha Ivan Don aliyefariki Jumanne baada ya kuugua kwa maradhi ya moyo.

Zari alimwandikia Ivan ujumbe huku akiomboleza kifo chake na pia kumsheherekea kwa kuwa mfano mzuri kwa Watoto wake muda wote aliokuwa hai.

Hata hivyo Raphael ambaye ni mmoja wa watoto wa Ivan aliandika ujumbe kwenye Instagram yake huku akimuomboleza babake ambaye kwa sasa amewaondokea wakiwa bado wadogo. Raph aliendika kusema,

“It hurts to think that you are not here anymore. Although I can’t help but smile with tears in my eyes to think of how we cherished each and every moment of our lives together; I will miss you Dady and I cant stop crying anymore when i think of you Dady @ivandon may your souls rest in peace.”


Mungu aiweke roho yake pahali Pema.

Ni kweli kuwa aliyekuwa mpenzi wa Zari, Ivan Don alitiliwa sumu kwenye chakula?

Fununu mitandaoni inadai kuwa Marehemu Ivan Don alifariki baada ya kutiliwa sumu chakulani chake pale ambapo alikuwa akikula na marafiki wake wa Karibu.

Ripoti hizi zilisambazwa na gazeti moja la Uganda liloandika kudai kuwa kuna ushahidi wa maneno haya. Hata hivyo kulingana na tulichoambiwa na familia yake ni kuwa Ivan Don alifariki baada ya viungo vyake vya mwili vilipoanza kufaili kwa kuwa alikuwa anapumua kupitia usaidizi wa machine.

Familia yake imenyamaza na hakuna aliyechangia kwenye ripoti za Ivan Don kupewa sumu na adui yake ambaye ni mmoja wa marafiki wake wa karibu.

Gazeti hilo liliandika kusema,

“Zari anaumia kumuona Ivan akiwa kwa hali maututi” Diamond Platnumz asema

Diamond Platnumz hivi karibuni alifunga kusema sababu ambazo hajaweza kumpost aliyekuwa mpenzi wa Zari wa zamani, Ivan Don kumtakia kupona haraka.

Akizungumza na kipindi cha Clouds FM Diamond Platnumz alisema Kuwa anaona watu watasema kuwa anatafuta kiki kwa kumuweka Ivan Don kwenye Instagram yake kwa sababu wengi hudhania kuwa wawili hao hawapatani baada ya Diamond kumchukua Zari Hassan ambaye alikuwa mke wa Ivan kabla ya wao kuachana.

Hata hivyo Diamond Platnumz amesema kuwa amekuwa akiwasiliana na Zari kila wakati anapoenda kumuona Ivan Don hospitalini. Aliendelea kwa kusema kuwa Zari anaumia kumuona baba ya Vijana wake akiwa kwenye hali hiyo. Lakini kwa sasa wote wanamubea ili apate nafuu nataka.

“Ni kweli mzazi wake Zari anaumwa, na yuko serious. Na kila siku huwa namuhimiza Zari akamuone mzazi mwenzie kwasababu najiuliza asingekuwa anaenda familia yangu ingemuonaje, kwa hiyo maskini dada wa watu kila siku huwa anaenda,” Diamonda alikiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM. Sijawahi mpigia simu kwasababu yuko serious sana na pia sikuweza kumpost kwasababu watu waneanza kusema labda natafuta kiki maskini ya Mungu kumbe wala,