Kimnana Kupatikana kwa Millioni Moja

Mwanadada Kimnana ambae amewahi kuwa video vixen katika baadhi ya nyimbo za wasanii hapa nchini amefunguka na kusema kuwa katika kazi hiyo kwa sasa imekuwa hailipi  na wala pesa yake haikidhi mahitaji ya maisha na brand ya video Vixen.

Kimnana anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwachukua katika video na kuwalia pesa kidogo bila kujali kuwa kazi zao zinaweza kuuzia sana kuliko hata pesa wanayolipwa katika kufanya kazi hiyo.

Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa kwa sasa kama kuna mtu anataka kufanya nae kazi basi dau lake la chini ni shilingi milioni moja na kama haipo basi ni bora kuacha kufanya kazi hiyo.

kazi hiyo kwa sasa sigfanyi kwa sababu hailipi,  kwa sababu hailipi kabisa, uklipwa sana basi shilingi laki tano hivyo mimi kufanya kazi hiyo chii ya milioi moja sifanyi.

Kimnana amepata umaarufu sana hapa kipindi cha nyuma kutokana na kuwa na mahusiano na msanii diamond platinumz.

Brownmauzo Anywa Sumu Kisa Kimnana

Moja ya wasanii marufu na wanaofanya vizuri nchini keny brown mauzo amekutwa na kashfa nizto inayohusisha mapeniz  baaada ya kujlikana kwamba alikunywa sumu kisa mapenzi.

Msanii huyo ambae hivi karibuni ilisambaa video yake akiwa Hoi amebebwa na watu akiwa anapelekwa hospitali na kusemekana kuwa alikuwa amepigwa risasi kumbe haikuwa kweli kuhusu taarifa hizo.

Msanii huyo aliyeshindwa hata kufanya mahojiano na waandishi wa habari akiwa analia anadaiwa kutaka kujiua kwa kunywa smu baada ya kugundua kuwa mwanamke huyo anaempenda yeye yuko katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingie.

Hata hivyo hakuna taarifa za wazi kutoka kwa mhusika ila watu wake wa karibu wamekuwa wakitoa hiyo taarifa na hata kusea kuwa msanii huyo alikuwa akija Tanzania kwa ajili ya Kimnana.

Na itakumbukwa kuwa wiki kadhaa zilizopita , msanii huyu aliwahi kusemakatika kurasa zake kuwa amekuwa akiishi under stress kutokana  na kuvunjika kwa mahusiano yake na msichana mmoja aliyekuwa akimpenda sana.

Kim Nana Afungukia Tetesi Za Bifu na Lynn

Video vixen maarufu kama Lilian Kessy ‘Kimnana’ amefunguka na kudai kuwa yeye na video queen mwenzake Irene Louis ‘Lynn’ hawana Bifu kama inavyodaiwa.

Tetesi za kuwepo kwa Bifu kati ya warembo hao zilizuka Baada ya warembo hao wawili wote kudaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Kim Nana amefunguka  kuwa watu wamekuwa wakizungumza mengi kuwa ana bifu na Lynn, lakini hawajawahi kuwa maadui hata siku moja na Lynn ni kama mdogo wake na hata wakikutana wanasalimiana vizuri na kuzungumza.

Lynn ni mshkaji wangu, hatuna bifu kabisa ndiyo maana hata hivi karibuni niliposti kipande cha video nikiwa naimba wimbo wake wa Chafu kwa lengo la kumsapoti hivyo wanaosema tuna bifu imekula kwao maana siyo kweli”.

 

Kimnana Atuliza Moyo Wake Kwa Otile Brown

Video vixen na aliyekuwa Mpenzi wa Staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Kimnana anasemekana kuutuliza moyo Wake Kwa msanii kutoka Kenya Otile Brown.

Kimnana alijizolea umaarufu Baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond miezi michache iliyopita lakini mahusiano hayo yaliingia shubiri Baada ya Diamond kumtosa Wiki chache zilizopita na kuanzisha mahusiano na mrembo kutoka Kenya Tanasha.

Baada ya kumalizana na Diamond, Kimnana amesonga mbele kwani hivi sasa anadaiwa kuwa kwenye mahusiano na Otile ambaye ni Ex boyfriend wa Socialite Vera Sidika kutoka Kenya.

Wawili hao walionekana pamoja nchini Kenya Wiki iliyopita na kuzua maneno kutokana na ukaribu wao  waliouonyesha kutokana na kukumbatiana na maneno mengine.

Otile Brown hajaweka wazi Kama Wapo kwenye mahusiano lakini amemuandikia ujumbe wa shukrani mrembo huyo kupitia ukurasa wake Wake wa Instagram:

Kimnana Adakwa na Otile

Mwanadada ambae alisifika na kuta umaarufu wa muda mfui sana hao nyakati za nyuma  kimnana ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond platinum anasemekana kuwa katika penzi zito na mwanakaka kutoka kenya Otile brown ambae na yeye pia ametoka katika kiumizwa kichwa baada ya kuachwa na mpenzi wake.

Wawili hao wanasemwa kuoneka apamona baadhi ya maeneo huku Otile akiweka baadhi ya pichakatika mitandao za mwanadada huyo.ikumbukwe kuwa otile alikuwa na mahusiano na mtu maarufu sana uganda, vera sidika na hata kim alikuwa na mahusiano na mtu maarufu sana Diamond  platinum, Otile na kim wote kwa sasa wamekuwa wakiugulia mauivu ya mapenzi.

Hata hivyo , msanii harmonize pia alimtuia ujumbe wa kum-miss kimnana , ujumbe unaomtaka kurudi huko alipokuwa huku ikisaidkiwa kuwa ni kweli mwanadada huyo atakuwa nje ya tanzania na mpeniz wake huyo

Harmonize am-miss Kimnana wa Diamond

Msanii kutoka katika lebo ya WCB Harmonize,  amefunguka katika ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa amekuwa akim-miss sana shemeji yake mpendwa Kimnana ambae kwa sasa amekuwa kimya hata baada ya kuachana na Dimaond platinuz.

Kminana alikuwa na mahusnio na diamond hivyo alikuwa karibu na wasanii wote wa lebo hiyo ukizingatia kuwa diamond ndio Bosi wa Lebo hiyo.

Wawili hao wanatajwa kuwa maadui sasa hasa baada ya kimnana kum-unfollow kabisa diamond kwa chuki ya kuachwa yeye na kutoka na mwanamke mwingine.

katika ukurasa wake, Harmonze alindika ‘……..SHEM LAKE,,SHEM LANGU MIE @officialkimnana  SEMA SIKUONI SIKU HIZI MBILI TAU UKO MJINI ? NAKUMBUKA MARA YA MWISHO ULIKUWA MTWARA,  UKO WAI JAMANI MIE MZALENDO BANA…

 

Picha ya Kimnana Yazua Gumzo Mitandaoni

Mwanadada aliye-trend sana hapa karibuni kwa sababu ya kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki mkubwa bongo na nje ya nchi Diamond Platinumz ameacha gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa instagram ikiwa tofauti na ile iliyopostiwa katika ukurasa wa designer wa nguo aliyokuwa ameiaa akiitangaza.

Wasanii wengi wa kike bongo wamekuwa wakisemwa kuwa wanatabia ya ku-edit picha zao na kuongeza maumbo au kubaidlisha rangi ba baadhi ya sehemu katika miili yao na hii inazidi kudhiirika kwa mwanadada huyo ambapo pivha hizo mbili zinaonekana ziko tofauti sana na kile kinachoonekana kuwa na ukweli .

Picha hiyo imezua guzo katika mitandao ya kijamii huku kila shabiki alihoji kwanini picha hzio zimekuwa na utofauti sana.

Picha moja ya kimnana yenye utofauti  wa muonekano.