Profesa Jay Awatolea Povu Wanataka Sapoti Yake Bila Kurudisha Fadhila

Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini Profesa Jay amefunguka na kutoa dukuduku lake la moyoni baada ya kuona kuwa kuna wimb kubwa la wasanii wamekuwa wakimsumbua katika simu yake wakitaka kupata sapoti kutoka kwake lakini wao wamekuwa hawasapoti muziki wake kabisa.

Profesa Jay anasema kuwa watu hao wamekuwa katika kumsumbua kila inayoitwa leo ili aweze kuwatangazia kazi zao lakini wao wanapoona nyimbo yao wanashidwa kutoa sapoti kama ile anayoitoa yeye katika nyimbo zake, hivyo Profesa Jay anasema kuwa hataki kusumbuliwa tena.

Alindika :ATTENTION PLEASE..hii ni kwawasanii wenzangu ambao kila nikitoa nyimbo wamekuwa wakika kimya wanauchuna, ..hawaoni na wala hawataki kunisapoti lakini wao kila kukicha wapo katika INBOX  yangu wakiomba niwapost na kuwafanyia hivyo mara kwa mara, kuanzia sasa hivi msije inbox kwangu maana mnakoelekea mtapata  na hilii….

Profesa Jay Anafaa Kuitwa Mkongwe Katika Huu Muziki;-Roma

Msanii wa hip-hop nchini,  Roma  amefunguka na kusema kuwa katika wasanii anaona wanafaa kuitwa wa kongwe kwake anaona kuwa ni Profesa  Jay kwa sababi ndio anafanya vizuri na kupigania sana haki za wasanii kwa kipindi kirefu sana.

Roma amesema kuwa hata kipindi anaanza muziki mpaka sasa, msanii ambae kwake ni role model ni Profesa Jay na wala sio mwingine kwa sababu amekuwa mfano wa kuigwa katika hilo.

Profesa jay anafaa kuwa mkongwe kwenye huu muziki, kwa sababu ni miongoni mwa wasanii waliopigania sana huu muziki kwangu mimi profesa jay ndio role model wangu.

Alichosema Profesa Jay Kuhusu Wasafi Tv

Kufunguliwa kwa kituo cha televisheni cha wasafi tv imekuwa moja ya stori kubwa mjini hasa baada ya kuona kuwa wasanii wengi wanaonekana kupata matumaini kuhusu kuwepo kwa kituo hicho kipya kama kauli mbiu yao inavyosema kuwa  ni televisheni ya’ kwetu sote’

Diamond amepokea pongezi nyingi sana kutoka kwa wasanii na watu mbalimbali na pia moja ya wasanii wakubwa na wakongwe Profesa Jay hakuwepo nyuma kuzungumzia swala hilo pia.

hili ni jambo jema sana ambalo kwa kila mpenda maendeleo na burudani  nchini ni lazima alifurahie,hongersa sana mdogo wangu @diamondpaltinumz  na timu yako nzima ya WCB #YAMETIMIA TUKO PAMOJA SANA.- Aliandika profesa jay katika ukurasa wake wa Twitter.

 

Profesa Jay Kumtembela Lulu Gerezani

Mwanamuziki mkongwe wa bongo hip -hop ProfesaJay anasema kuwa siku yoyote kuanzia sasa yuko mbioni kwenda  kumtembelea msanii wa bongo movie lulu michael ambae ayupo gerezani akitumikia kifungo chake cha miaka miwili baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

                                                 

Profesa Jay anasema kuwa anaamini kabisa kuwa lulu ana mengi ya kuongea hivyo anatamani sana kuongea nae ili aweze kumwambia yalitopo moyon mwake na pia kumfariji kwa kila analopitia kwa sasa.

Ninatamani sana kuonana na lulu niweze kuzungumza nae,ninafahamu ana mengi ya kuzungumza na hivyo ninajipanga  na muda pia  na ikiwa tayari nitawafamisha ni lini ninakwenda kumuona.-  Alisema Profesa Jay ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake kipya cha Pagamisa alichomshirikisha Mr.T-Touch

 

Profesa Jay Afunguka Tetesi za Kuacha Muziki

Msanii Joseph haule amefunguka na kusema kuwa kamwe hatoacha muziki kwa sababu muziki ndio uliomfanya kujulikana na mashabiki zake wa miukumi na kumpeleka bungeni, hivyo kuacha muziki ni kama kuwasaliti wananchi wake waliomwamini kupiyia muziki huo..

Joseph Haule kwa jina maarufu Profesa Jay ni wasanii wa kwanza mbao sasa hivi ni wakongwe katika sanaa, lakini pamoja na kwamba aliamua kujiingiza katika siasa, anasema kuwa kazi ya muziki ndio iliyomfanya kujuliakna tanzania na kot ulimwenguni na inawezekana kama sio muziki basi hasingeweza kuwa mbunge wala kujuana na wananchi wa mikumi.

pagamisa ni kazi nzuri ambayo imepokelwa vizuri tu na mashabiki wangu,miaka yote ya muziki wangu nitaendelea kutoa kazi nzuri za muziki wangu  na kamwe siwezi kuacha kazi ya muziki kwa sababu ya kufanya hivyo ni kama kuwasaliti wananchi ambao wamenipeleka mjengoni kupitia muziki huu ambao naufanya.-Alisema Profesa Jay ambae alikuwa studio kutambulishwa wimbo wake mpya.

Profesa Jay Akiri Kuwasamahe Wote Waliomsaliti, Aelezea Maisha ya Sugu Gerezani

Mwanamuziki mkongwe nchini Profesa Jay , amefunguka na kusema kuwa ameamua kuwasamahe wasanii na watu wote wa karibu waliokuwa wakimsaliti kipindi cha kampeni na mpaka anafikia hatu ya kuwa mbunge.

Profesa jay anasema kuwa wasanii wengi sana hawana umoja na wamekuwa na tabia ya usaliti na kusemana sana ktika vitumbalimbai hivyo bsai kwa upande wake anaona kabisa kama atatumia kisasi na kuwachukia au kuwbabgua basi ndio itaendeleza chuki kati yao na kfanya muziki uzidi kufa wakati ili muziki ukue inabidi kuwe na umoja thabiti.

Profesa jay anasema kuwa kwa sasa hana kinyongo na mtu yoote aliyewahi kumkosea wala kumsaliti hasa katika kipind cha kampeni ila atajitahidisana kuweka umoja kati yake na wasnii wengine ili waweze kufika mbali katika kukuza muziki wao.

Hata hivyo akifunguka na kuelezea maisha ya mwanamuziki mwenzie ambae pia alijiingiza ktika siasa, Mh Sugu ambae kwa sasa anatumiakia kifungo chake cha miezi  gerezani baada ya kukutwana hatia ya kuongea maneno ya uchochezi na kutokumheshimu raisi, profesa jay anasema kuwa tangu sugu alipoenda gerezani alishawahi kwenda kumuona na kuambiwa kuwa mbunge huyo alikataa kabisa kukaa sehemu ya watu maalumu alipokuwa gerezani mpaka sasa.