Nisha Aongea Na Wanaomkashifu Lulu Michael

Msanii wa bongo movies Salma Jabu maarufu kama Nisha  bebe, amefunguka na kuwaonya baadhi ya watu ambao tangu kesi ya msanii lulu michael ianze kusomwa katika mahakama jijini Dar Es Sallam wamekuwa mstari wa mbele kumuongelea mwanadada huyo.Msanii huyo amesema kuwa kwa kipindi kama hichi ambacho Lulu anapitia wakati mgumu sio muda wa kumnanga bali ni muda wa kumpa faraja na kumuombea apite katika kipindi ichi kigumu.

“tangu kesi ya Lulu ianze kusikilizwa upya, kuna watu wamekuwa wakimkashifu kila kukicha, kwa maneno ya ajabu bila kujua kuwa  hakuna ajuaye kesho yake, ni vyema tukampa faraja rafiki yetu, katika kipindi ichi kigumu anachokipitia” alifunguka Nisha

kwa kipindi cha muda mfupi ambacho Lulu amekipitia , akiwa anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia kumekuwa na maneno mengi katika mitandao yanayomsema vibaya mwanadada huyo,inawezekana kwa kukusudia au bila kukusudia lakini iki ni kipindi ambacho  mashabiki na watu wa karibu na Lulu wanapaswa kuwa na maneno ya kumpa  faraja ili aweze kushinda kesi hiyo, maamuzi mengine  na hukumu hutolewa na mahakama hivo watu wa mitandaoni hawapaswi kumuhuku msanii huyo.

Hata hivyo,imekuwa ni kama desturi kwa baadhi ya watu ambao wanakuwa haweleweki wamelalia upande gani, wanapoona mtu amefanya vizuri hujitokeza kumpongeza na anapopata matatizo wanaanza kumsema vibaya, huu ndio wakati ambao Lulu anapaswa kuiona nguvu kubwa ya mashabiki wake.

Kesi ya Lulu ambayo ilianza kusikilizwa Oktoba 19 , imeendelea jana ambapo Lulu alipata nafasi ya kuongea na kujitetea kwa nafasi yake,huku mashahidi wengine wakiwa tayari wameshatoa ushahidi wao kuhusu kifo cha marehemu kanumaba ambae alikuwa mpenzi wake na Lulu.Kifo icho kilitokea baada ya msanii huyo wa kike na mpenzi wake kuwa katika ugomvi uliosababisha purukushani za Kanumba kudondoka na kufa papo hapo.

Wapo baadhi ya watu maarufu na wasanii walionyesha kuwa karibu na Lulu Michael katika kipindi hiki kigumu kwa kutokea mahakamani na kumpa maneno yenye faraja mwanadada huyo akiwepo Dr.Cheni, na Muna love ambao muda wote wamekuwa nae mahakamani.

“Sina Mimba mie” Nisha kaweka mambo wazi

Nisha hana mimba kamwe ndio ujumbe uliotufikia leo na kuweka mambo yote kwa wazi.

Akizungumza kwenye Millard Ayo, Staa huyo wa filamu anayejulikana kama Salma Jabu alieleza ya kwamba yeye hana mimba kamwe na picha aliyoieka kwenye mitandao ilikuwa yeye kwenye harakati za kikazi.

Kama balozi wa watoto wanao ishi katika mazingira ya ufukara, aliamua afanye uchunguzi ndio akuje kutoa filamu mpya na ndipo akabuni huyo character aliyeonekana kana kwamba alikuwa na mimba.

Mtazame kwenye hii video akiongelea jambo hilo kwa unenepa:

 

Staa wa bongo movie Salma Jabu maarufu Nisha Bebee asema ukweli kuhusu mimba aliyopata baada ya kubakwa

Akiongea katika AyoTV, Salma Jabu alisema kuwa hana mimba. Staa huyo alieleza kuwa watu hawajui kutafautisha Salma na Nisha.

“Kwanza kabisa kila kitu kinatokea kwasababu. Kwa wale ambao wametokea kuwa wananichunguza au kunifwatilia tangu nlianza safari ya sanaa mbaka hapa nimefika, Nisha sio mtu wa kumwakilisha Salma katika media. Unapomzungumzia Nisha humzungumzi Salma. Ninacho maanisha ni kwamba Yule ambaye ana mimba sio Salma, ni Nisha. Ndo maana nkasema kila kitu kinatokea kwa sababu Nisha huwa hapendi kumrepresent Salma katika media,” Salma alisema.

Alifafanua kuwa alimvaa mtu anayeitwa Mariana ile kumpresent katika jamii kama mtu aliyepata mimba baada ya kubakwa.

“Ahhh! Sina mimba, mimi ni balozi wa watoto waishio katika mazingira hatarishi. Kwa hio kama balozi nliamua nifanye uchunguzi. Katika uchunguzi huo nliamua kutengeneza filamu ambayo ndo chanzo cha watoto asilimia sabini na tano wanaoishi katika mazingira hatarishi. Kuna wazazi ambao walibakwa wakaja wakajifungua watoto wakawatupa wakaja wakaokotwa, kuna wazazi ambao …mambo mengi amboya mwanamke amekua akiyapita kwa maisha yake yakasababisha kuja kuzaliwa wale watoto wa mitaani. Kama nlivyokuambia apo awali napenda kufanya uchunguzi katika filamu zangu, nliamua kumvaa mtu anaitwa Mariana na nikampresent katika jamii alafu nkisema story yake kwa ufupi katika mtendao wa kijamii, nkaandika story ya ule mtu lakini the way ambavyo watu walipokea, ilinipa shauku ya kutaka kubeba ule uhusika zaidi na kuja kujua maumivu ambayo ntakuja kuyapata au Yule mtu ambaye amepitia kubakwa vitu kam hivyo ambavyo anaweza akazipata,”