Shiloleh Kutoa Ngoma na Chriss Brown.

Mwanamuziki Zuwena Mohamed amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuusambaza na kupamnua wigo wa muziki wake anaofanya sasa hivi na kwa kulithibitisha hilo amesema kuwa ameanza kuchart na baadhi ya wasanii kutoka nje na mmoja wapo ni msaniiwa kimataifa Chriss Brown.

Akiongea na Lady Hahaa wa kipindi cha african wired kutoka Clouds Media, Shiloleh anasema kuwa alimtumia meseji Chriss Brown wiki hii na alipomuuliza kama anamjua msanii huyo wa kimataifa alikiri kujua na kwamba wanajianda kufanya nae kolabo.

Shiloleh anasema kuwa hata alipomtumia smsm DM , chriss brown alimpongeza kwa jitihada zake katika muziki na katika kujifunza lugha ya kingereza na pia wamekubaliana kutoa nyimbo ya pamoja.

 i was calling the message on DM on instagram, i went hii bro its me shishi baby and he say oooh youu, and i  say yeah its me.-aliongea shiloleh hukua akiojitahidi kuongea na kingereza chake cha kusuasua na kusema kuwa alipomuuliza chriss kuhusu kumjua alijibu kuwa anamjua na anaijua Tanzania.

Mimi na Shiloleh Atuongei kwa Sababu ya Mwanaume._Khadija Ziota.

Mwanadada kutoka mwanza anaejulikana kama Khadija Ziota aanaesadikiwa kuwa ni mwanamke anaemlea Harmorapa kwa sasa amefunguka na kusema kuwa yeye na Shiloleh ni ndugu lakini wamekuwa hawaongei wala kupatana kwa sababu ya mwanaume ndio aliewagimbanisha.

Mimi na shiloleh atuongei kabisa, hatupatani hata kidogo kwa sababu ya mwanaume.mimi na shiloleh ni mtoto wa baba mkubwa na mdogo.lakini kwa sababu ya mwanaume katusababisha kwa sasa hatuongei kabisaa,na hata tukikutana hatuna hata salamu kabisa na hata kupigiana simu hakuna na imeshakuwa muda mrefu sana sasa hivi.

Alipoulizwa kuhusu mwanaume huyo , mwanadada khadija alimtaja mwanaume huyo kuwa na Nuh mziwanda, ambae hapo awali aliwahi kuwa mpenzi wa shilolhe kabla hajaachana nae na kuolewa na uchebe.

Mwanadada huyo ambae kwa na mna moja ama nyingine amekuwa akiongea maneno mengi mitandaoni kuhusu wasanii mbalimbali huku akionekana kuwachafua, inasemekana kuwa anatafuta kiki ili kujulikana mjini.

Shiloleh Apata Deal la Kujifunza Kingereza .

Mwanadada shiloleh amepata dili la kusomeshwa na British Council baada ya kuonekana hawezi kuongea kingereza ingawa dhumuni lake kubwa limekuwa ni kutaka kuongea kingereza kila anapofanya interviews.

shiloleh ambae mara nyingi amekuwa akiongea kingereza pamoja na kukosea lakini amekuwa akiongea hivyo hivyo amesaini dili hilo la kujifunza kingerza mpaka pale takapojua kukiongea kabisa kwa udhamini wa taasisi hiyo.

Shiloleh amekuwa moja ya wanawake majasiri na wenye uhamasishaji mkubwa sana katika jamii kila siku kutokana na mambo mengi anayoyafanya yanayowapendeza jamii yake.

Sikutaka Mwanaume wa Kunilamba Lips :-Shiloleh

Mwanadada shiloleh amefunguka na kusema kuwa ndoa yake inaendelea vizuri na hata hakuna anayemaini kuwa ndoa ile iliyosemwa sana ingeweza kutulia na kufikia hatu ailiyofikia sasa hivi kama wengi walivyokuwa wakidhani.

Shiloleh anasema kuwa alipoanza mapenzi alikuwa akikuta na wanaume tofauti tofauti ambao hawakuwa wamefikia kiwango alichokuwa akikitaka yeye cha kutokubembelezwa kama  walivyokuwa wakifanya lakini alipokuata na Uchebe aliona kuwa uyo ndio mwanaume aliyekuwa akimtaka.

Shiloleh anasema kuwa alikuwa akitafuta mwanaume ambae akikosea anweza kumpa za uso na akamrekebisha na sio kumbembeleza au kumuogopa tu bila kuwa na ukali ndani yake na ndio maana tangu amefunga ndoa watu wamekuwa wakishangaa sana mafanikio yake.

sikutaka mwanaume wa kunilamba lips, nilitaka mwanaume ambae nikizingua nakula za  uso na anayesimama kama mwanaume na watu waliongea mengi sana kwanini uchebe  na sio mwanaume  mwingine lakini kwa  sasa wanashangaa mafanikio yangu.

 

 

Mange Kimambi Amtolea Uvivu Shiloleh

Mwanadada anaesifika katika mitandao kwa ajili ya kukososa na kutoa siri za wasanii na watu wengi marufu nchini Mange Kimambi amemtolea uvivu msanii wa bongo fleva Shiloleh  baada ya msanii huo kumkosoa Muna love kwa kufanya press conference na kuelezea scenario ya kifo cha mtoto wake.

Katika press hiyo ambayo muna aliamua kuweka wazi juu ya mahusiano yake na Peter ambae ndie iliyesemekana kuwa ndie baba wa mtoto na kusema ukweli kuwa mtoto ni wa Casto, aliwagusa watu wengi akiwemo shihsi ambae alianza kumtukana muna kwa kumwambia kuwa alipaswa kusubiri mpaka 40 ya mtoto wake ipite.

Hata hivyo Mange kimambi nae alikuja kuibuka na kuanza kumtolea mapovu shishi na kumwambia kuwa wasanii wengi wa bongo wamekuwa na tabaia ya kuchagua watu wa kuwakosoa kwa kuwaona kama wanaweza kubishana nao au la na ndio maana imekuwa raisi kwa shiloleh kumsema Muna.

kwa mujibu wa Mange kimambi anashangazwa na shiloleh kwa sababu mambo kama hayo yaliwahi kutokea huko nyuma kwa baadi ya wasanii lakini hakuwasema kama alivyomsema Muna sasa hivi.lakini pia sio kwa kumuonyesha kumschukia Muna au Shiloleh  Mange kimambi anasema inawezekana shilole akawa yuko sawa lakini kwanini hakuwahi kuwa-judge na waliowahi kufanya hivyo huko nyuma

Shiloleh Amtolea Mapovu Muna “Utapata Tabu Sana”

Baada ya kuongea na waandishi wa habari, mwanadada Muna alisema mengi huku akisema kuwa anao uthibitisho wa kutosha kuwa mtoto wake patrick ni mtoto wa Casto na wala sio vinginevyo, huku akisema kuwa  hakuwahi kuwa na mahusiano na peter hata siku moja bali alikuwa akimchukulia kama baba yake na mtu wake wa karibu.

Kila mtu ameyapokea maneno ya Muna kwa hali tofauti lakini shiloleh ni moja ya watu walionhea mara tu  baada ya mahojiano hayo kuisha na kumshangaa sana muna kuwa amepata wapi nguvu ya kusimama na kuwaita waandishi wa habari mpaka kuja nyumbani kwake na kuongea kile alichokiongea .

Shiloleh anasema kuwa hata kama alichokiongea kina ukweli lakini hakupaswa kuonyesha au ku-prove chochote kwa mtu yoyote kwa sababu hata 40 ya mtoto wake ilikuwa bado haijafika.

Muna unaenda kuita press conference,ufanyiwe interviw for what, unafurahia nini, unawaia unawaambia nini na juzi tu umetoka kuzika mtoto wako.unataka kuthibitisha kuwa huyo mtoto ni wa casto hatutaki kujua, we dont need it…mimi ni dada yako kama ungekuwa na shda ungenifata tu kama unavyonifataga kwenye mengine…muna utapata tabu sanaa.

Shiloleh ameonyeshwa kusikitishwa sana na kitendo cha muna kumkana mume wake ambae amefunga nae mpaka ndoa kwa ujinga wake mwenyewe.

Shiloleh Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph

Mwanadada Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema kuwa kadri siku zinavyokwenda anaona kama inawezekana yeyekufuta nyayo za moja ya msanii mkubwa wa taarab aliyepita ya kuachana na muziki na kufanya mambo mengine ya kijamii.

Akiongea katika futari iliyoandaliwa na msanii mwenzie Iren uwoya pamoja na mumewe dogo janja anasema kuwa kwa jinsi mwezi huu mtuklufu ulivyomfunza mengi anaona kabisa kuwa hana muda mrefu anaweza kupiga chini muziki na kufanya vitu vingine.

si unaona ninavyopendeza na vazi hili la kiislamu,basi kwa taarifa yako sina muda mrefu na mimi nitaacha muziki kama alivyofanya Mzee Yusuf

Kikubwa na kizuri ni kwamba nina vyanzo vingine vya kimapato,unajua kuwa nina ule mgahawa  na biashara zingine , hizo zinaweza kabisa kunifanya niendelee kuishi pale nitakapochukua huo uamuzi.

 

Mzazi Mwenzie na Shilole Afariki Dunia,

Mwana dada mpambananji , Zuwena Mohamed amefikwa na msiba wa kuondokewa na mzazi mwenzie walie bahatika kupata nae mtoto mmoja wa kike wa kwanza,mwanaume huyo aliekuwa akiitwa Elias makala amefariki leo huko Igunga Mkoani Tabora ambapo alikuwa haugui kitu chochote.

Shiloleh amethibitisha kifo icho cha mzazi mwenzie baada ya kusema kuwa marehemu hakuwa  anaumwa chochote ila alikuwa akitoka katika sherehe na kurudi nyumba na ndipo mauti yalipomkuta.

Shiloleh anasema kuwa marehemu alikuwa mzima na mara ya mwisho kuwasiliana nae ilikuwa miezi miwili iliyopita , Lakini kwa taarifa alizozipata kutoka kwa ndugu zinasema hakuwa na ugonjwa wowote uliomsumbua kabla.

Marehemu na msanii Shiloleh walifanikiw akupata mtoto wa kike ambae ndie mtoto wa kwanza wa shilole ambae sasa hivi ana miaka 14.

Shiloleh Akataa Watoto Wake Kufuata Nyayo Zake

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amesema mavazi anayovaa kwenye shoo au sehemu mbalimbali za starehe hayupo tayari kuwaona watoto wake wakiiga.
Mrembo huyo amedai kuwa watoto wake wanatakiwa kujua kuwa mama yao yupo kazini na si aina ya mavazi anayopenda kuyavaa

.
Amesema kuwa “Watoto wangu nawalea katika maadili siwezi kuwalea maisha ya kistaa kama ambayo mimi nayafanya, mavazi ninayovaa sehemu mbalimbali ni kutokana na kazi yangu na wanalijua hilo.

Pia amesema kuwa watoto wake hawana dalili za kuja kuwa mastaa, hivyo lazima wakae mbali na aina hiyo ya mavazi kwa kuwa wanalelewa mazingira ya dini,”.

Utani wa Idris kwa Shiloleh

Mchekeshaji Idris Sultan amemtania Shiloleh huku akimsifia kama mwanamke jasiri anaejiamini na kujituma kuliko wanawake wengine waliozoea kuletea kila siku.Hii inakuwa sio mara ya kwanza wa baadhi ya wasanii kugundua umuhimu wa Shiloleh katika jamii.

Pamoja na kwamba Idris aliandika maneno haya kwa njia ya utani lakini imeleta hamasa sana kwa vijana wengine na kuweka gumzo katika mitandao ya kjamii,

Ana nyumba, ana biashara kama tatu, ana watoto watatu na ameolewa  ni marufu na pia ni baby face .mimi nina kiingereza tu hapa , tuendelee kuendekeza ujinga tutajua nani anamcheka mwenzie.

Shiloleh Kuja na Kitabu cha Stori ya Mapenzi

Akiwa kama moja wa wasanii wapambanaji sana, mwanadada shiloleh ametangaza kuja na kitabu chake akishirikiana na mwandishi mmoja kitakachokuwa kikizungumzia histori yake ya mapenzi.

Shiloleh amekuwa ni moja wa wanawake na wasanii wachach wenye uharaka wa kuthubutu kila inapotokea

hey guys kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikianda kitabu changu na mwandishi chipukizi  ni romantic novel ambayo  inavutia kwa wapenzi wa vitabu  vya love story kama fans wangu naomba mkae mkao wa kula  kupakuwa kitabu hiki, kitazinduliwa baada ya mwezi mtukufu  kuisha.are you guys excited as i am?get ready  for heart broken.

 

 

Mimi Sina Competition na Shiloleh:-Esha Buheti

Mwanadada wa bongo movie esha buheti amefunguka na kuongelea uhusiano wake na shiloleh kama watu ambavyo wamekuwa wakiwashindanisha katika swala zima la mapisha na kusemekana wawili hao kwa sasa hawaelewani kwa sababu hiyo,

Akiongea na mwandishi wa habari, esga anasema kuwa kwa upande wake hana ushindani na mtu yoyote zaidi ya kwamba anachojua kila mtu anafanya kazi zake mwenyewe na kila mtu ana wateja wake lakini pia anshangaa kwanini watu wengi wamekuwa wakimshindanisha na yeye wakati kuna wasanii wengi tu ambao ni wapishi.

Competion gani, mimi si-compet na mtu yoyote na hakuna biashara mamabyo ni ya mtu  au kuwa hii imepangwa kufanywa na mtu fulani tu hapana,na hayo ni maneno ya watu nimekuwa nikiyachukia sana kwa sababu mimi sina competition na shiloleh , kwanini mbona watu wengi wanapika tu kuna open kitchen anapika , uwoya anapika lakini wao wamekazana na shiloleh tu kuna nini au vigezo gani vya kunilinganisha nae.

Siwezi kulinganishwa na shilole kwa sababu yeye nilishamkuta akifanya alafu hata menu zetu ni tofauti sana.

Baada ya Kupewa Tuzo,Shiloleh Atoa Shukuran kwa Aunty Ezekiel

Siku ya May 13 ilikuwa pia siku aalumu na muhimu kwa Shiloleh hasa baada ya kupokea tuzo kubwa ya kutambulika kwa machnago wake katika tasnia ya muziki na pia kama mwanamke mpambananji katika tasnia ya muziki na filamu pia lakini akiwa kama wanamke anaepambana kuhudumia jamii.

Aunty Ezekiel alimpa shiloleh tuzo ya kutambua mchango wake mkubwa wa kuhamasisha jamii kwa kile aanacho kifanya katika jamii na pia kuhamamsisha watu wengi waliokata tamaa.

Katika uzinduzi wa filamu yake ya mama, Aunty Ezekiel alitoa tuzo hiyo kwa shiloleh na kupokealwa na snura na kisha kumfikishia mwenye nayo.baada ya kupokea tuzo hiyo Shiloleh kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika

Naamini kuna wengi wanaostahili tuzo hiilakini siwezi kuwa na maneno mengi ya kutosha kushukuru  kwa heshima kubwa ulionipatia mama cookie, nashukuru sana  kwa zawadi nzuri.tuzo ya mama bora mpambanaji  bora kwa bongo fleva na movies katika uzinduzi wako wa filamu ya mama.lakini pia nakupongeza sana kwa kazi nzuri na product ya spray ulioizindua, wewe ni mwanamke shupavu.

Mama yangu aliniacha nikiwa mdogo sana kwaio nikaelewa mazingira magumu ya kuishi bila mama,na ndio maana siku zote nitapambana sana kwa ajili ya wanangu, ukiwagusa wanangu  umenigusa mimi.Hawa ndio watu pekee ninaoweza kusema nitakufa kwa ajili yao.

Shiloleh amekuwa akitambulika kama msanii na mwanamke mwenye moyo wa uthubutu na kujiamini sana ktikakufanya vitu na amekuwa moja ya wanawake wenye kuleta hamasa sana ukiangalia jinsi alivyoanza na mpaka sasa hivi alipofikia , watu wengi wanapata moyo kupitia yeye,.

 

Shiloleh Ajipanga Kurudi Shule Tena.

Mwanadada na msanii maarufu zuwena mohamed ambae siu chache zilizopita alikuwa amepata nafasi ya kwenda kutembelea chuo cha NCT ambapo alipata nafasi pia ya kuona kozi mbalimbali zinazopatikana chuon hapo na kuongea na baadhi ya wanafunzi alifunguka na kuhaidi kuwa atajipanga na yeye kurudi chuoni hapo kwa ajili ya kuongeza elimu kuhuusu mapishi.

Shiloleh ambae ukiachana na kazi ya muziki anayoifanya lakini pa ni mpishi mzuri wa chakula na amekuwa akiwalisha watu wengi jijini, amesema kuwa kuna haja ya yeye kurudi chuo na kusomea kozi hiyo ili kuongeza ujuzi zaidi.

kutoka katika chuo cha NCT waliandika haya baada ya shishi kuondoka chuoni hapo” siri imefichuliwa na shishi mwenyewe  mmiliki wa mgahawa wa shishi food kuwa kumbe mambo yanalipa sana , ila yeye hakusita kufika chuoni hapa NCT kuiongezea thamani ya chakula chke kwa kupata dondoo  juu ya ukarimu na ufahamu kuhusu  ujasiriamali lakini pia  utaalamu katika maswala ya food production.

alisema kuwa atakuja yeye na team yake kupata kozi fupi , ulikuwa ni wakati mzuri kukutana na anayeitumikia sekta ya ukarimu wake  na wale wanaojiandaa  nafasi bado ni nyingi , hataki  ujinga wa kupishana na fursa.aante sana shishi kwa kupata nafasi ya kutembelea hapa.

Shiloleh anawekwa katika list ya wasanii wanaojituma na kufanya kazi buoa kukata tamaa hasa  kutokana na kuamua kufanya muziki na mapishi kwa wakati mmoja.

Sio kwa Sababu Msanii Basi Ukae Ndani Kama Mtoto:-Shiloleh

Msanii wa kike nchini , shiloleh anaweza kuwa ni moja ya wanawake jasiri na wenye moya wa pekee,hii haimaanishi kuwa wengine hawapaswi kupewa pongezi hizi, lakini pale mtu anapofanya jambo zuri kwa jamii ni bora kumsifia na kumpa pongezi zake ili wengine waige na pia kuendlea kumtia moyo mhusika.

Katika msiba wa Agness Masogange, msanii Shilole aliwahi kufika kwenye msiba huko mbeya pamoja na kwamba alikuwepo pia Leaders Club kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu . alkini hata alipofika jijini mbeya shilole alionekana kuwa busy sana hasa upande wa jikoni,

Shilole mwenyewe anakwambia kuwa yeye ni mtoto wa kiek hivyo isngekuwa rahisi kukaa ndani tu wakati kuna kazi nyingi nje zilikwa zikitakiwa kufanyika hasa katika swala la kupika.Shilole aliweka umaarufu na usanii pembeni na kuamua kuingia jikoni kusaidia wanawake wengine.

hii ni kazi ya wanawake , ukiwa msanii sio kwamba lazima ukae ndani tu , wewe sio mtoto kwamba unatakiwa kukaa ndani tu lazima ujishughulishe na wanawake wenzio, kwaio mimi nilivyofika tu nikauliza jiko liko wapi,kabla ya kuzika inabidi watu wale na kuna wengine waliopoa hapa pia ni watu wanahitaji msaada.uUkiwa mwanamke ni lazima ukae na wanawake wenzio ufanye kazi.

Shiloleh Afikishwa Mahakamani Kwa Kosa la Utapeli.

Msanii wa mzuki wa kizazi kipya nchini, zuwena mohamed maarufu kama shiloleh amefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuchukua  pesa ya shoo  kiasi cha shilingi milioni 3 ikiwa ni  pesa aliyokuwa amelipwa kwa ajili ya kufanya shoo lakini siku ya tukio msanii Shiloleh alishindwa kuonekana katika shoo hiyo na kushindwa kutoa taarifa kwa waandaji wa shoo hiyo  kwa muda muafaka,hivyo kusababisha hasara.

Shiloleh amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo manispaa ya Kinondoni leo na kupewa hukumu ya shilingi mil 14, ikiwa ni pamoja na fidia ya kumsababishia hasara Mama  Mary Musa  aliyemlipa kwa ajili ya kufanya shoo siku ya pasaka mwaka 2017  Mbagala Kijichi ambapo baada ya kulipwa alishindwa kufika ukumbini hapo kwa muda hivyo mashabiki na wapenzi wa burudani kushindwa kuvumila na kupandwa nahasira iliyosababisha kuvuja na kuharibu mali.

Kwa mujibu wa GPL, shiloleh alipofanya kosa hilo alitakiwa kurudisha pesa hizo lakini alikuwa akipuuza agizo hilo la mahakama kwa muda wote ndipo mama huyo alipoamua kufatilia zaidi na hukumu kutolewa leo kuwa ndani ya wiki moja Shiloleh anapaswa kulipa fidia hivyo na kama hatashindwa basi mali zake zitashikiliwa na mahakama.

Shiloleh amefika mahakama hapo akiwa na mume wake uchebe lakini baadae alianza kuangu akilio baaada ya hukumu kutolewa.