Siendi kwenye show bila milioni 5:-Shilole

Mwanadad shiloleh amefunguka na kusema kuwa katika muziki wake hawezi kufanya show bila kuwa na makubaliano ya malipo ya kiasi cha shilingi milioni tano na yule anaemuhitaji la sivyo hawezi kwenda.

Shiloleh ameyasema hayo siku ya leo alipokuwa katika kipindi cha leo tena akiwa na mume wake wa ajili ya kutambulisha wimbo wake mpya.

Shiloleh anasema kuwa amekuja kutafuta pesa hivyo hawezi kufanya kazi bila kuwa na makubaliano ya pesa hiyo labda iwe ni tamasha wa ajili ya kuwasaidia na kusapoti wanawake wenzake.

Bila milioni tano mimi sifanyi show. siendi kwenye show kwa sababu ya maisha,mimi ni brand kubwa hivyo tukikubaliana naenda ila  ila siend kwenye shoo bila milioni tano.Na hii inajulikana kabisa labda wanawake wenzangu ndio ntawasaidia  ambao  ambao wanajituma kwa kuandaa matamasha.

 

Shiloleh Afunguka Swala la Kumzalia Uchebe.

Mwanadad Shiloleh amefunguka na kuelezea kuhusu swala lakutaa kumzaliwa mume wake Uchebe ambae kwa sasa wanatimiza zaidi ya mwaka tangu kufungwa kwa ndoa hiyo lakini hakuna dalili ya Shiloleh kuwa mjamzito.

Hata hivyo wawili hao pamoja na kwamba wameoa , lakini tayari kila mmoja tayari alikuwa na watoto wawili hivyo kufanya familia yao kuwa na watoto wanne  tayari.

Shiloleh anasema kuwa hata yeye amekuwa akitamani sana kumzalia mume wake huyo mtoto kama zawadi lakini anaamini kuwa muda utakapofika basi kila kitu kitakuwa sawa.

 

Shilole aelezea Mh. Rais alivyosaidia ujenzi wa Nyumba yake.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni mjasiriamali wa chakula, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa Rais Magufuli amechangia kukamilisha ujenzi wa nyumba yake.

Shilole amesema kuwa moja kati ya pesa alizopata na kuziwekeza katika ujenzi wa nyumba hiyo, zilitokana na kampeni za urais mwaka 2015 wakati wakimnadi mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM), ambaye ndiye rais wa sasa Dkt. John Magufuli.

“Nyumba yangu imejengwa na muziki pamoja na kampeni za kumnadi Rais Magufuli, maana tulikuwa tunalipwa na tulilipwa pesa nyingi ndipo niliamua kuwekeza kwenye nyumba yangu”, amesema Shilole.

Shilole ameongeza kuwa, “Mimi ni mnyamwezi nimetoka Tabora kuja mjini kutafuta sijaja kuangalia maghorofa ya Dar, nilivyopata ile hela tu nikasema naenda kununua kiwanja moja kwa moja lakini wapo walionunua magari”.

Shilole ni miongoni mwa wasanii wa kike waliofanikiwa kumiliki mjengo na kuuonesha kwenye ukurasa wake wa ‘Instagram’ mwaka uliopita, ambapo amesema kuwa mjengo huo aliujenga kidogo kidogo na unapatikana maeneo ya Majohe, Gongo la mboto jijini Dar es salaam.

Shiloleh Amkumbuka Sharo Millionea

Mwanadada Shiloleh amefunguka na kusema kuwa moja kati ya watu anaowakumbuka sana katika maisha yake  ni msanii sharo millionea ambae amefariki miaka mingi nyuma kuwa ndio alikuwa alimpenda na kumchukulia kama ndugu yake katika sanaa.

Shiloleh ambae aliongea na ilifika sehemu alishindwa kuendelea kuongea anasema kuwa , Sharo Millionea alikuwa hawezi kukaa mbali na yeye kiasi kwamba hata alipokuwa akitaka kwenda kulala alikuwa radhi alale sebleni .

Ikumbukwe kuwa shilole  na Sharo Milionea walikuwa marafiki sana kiasi kwamba ikifikia hatua baadhi ya mashabii walikuwa wakihoji sana mahusiano yao kutokana na ukaribu wao.

Shiloleh Atoa Angalizo kwa Wanaomuwinda Mume Wake.

Msanii wa muziki Bongo, Shilole amechimba mkwara kwa wale wote anaoamini kuwa wanamnyemelea mume wake, Uchebe.

Muimbaji huyo ameeleza kuwa toka mwanzo aliridhika na hali ya mume wake lakini sasa watu wanapoona anang’aa ndipo wanamnyemelea. Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

“Nililizika na hali yako tangu mwanzo mpaka sasa unashaine Ila wadangaji msivyo na haya mnaanza
kumwambia Mume wangu Uchebe Umekuwa Handsome, Mkome Namtunza! zamani mlikuwa wapi??,” ameeleza Uchebe.

Shilole na Uchebe walifunga ndoa December 07, 2017 na mwaka jana Uchebe alioonekana kwenye video ya muimbaji huyo inayokwenda kwa jina la Mchakamchaka

Chid ni Msanii Mkubwa Anapaswa kupewa Hesima Yake :-Shiloleh

Mwanadada Shilole amefunguka na kusem kuwa sabau kubwa iliyomfanya yeye kumshirikisha Chid benz katika wimbo wake mpya ni kwa sababu Chid benz ni msanii kama walivyo wasanii wengine na wala sio vinginevyo.

Akiulizwa kuhusu baadhi ya wasanii kuwa wakimsema na kumuweka katika makudi mabaya shiloleh anasema kuwa watu wanatakiwa kungalia aliotoka Chid Benz na kitu alichowahi kufanya katika muziki wa bongo fleva na sio kumdhaurau kwa sasa kwa sababu ameshuka.

watu hawaelewi tu, chid benz ni msanii mkubwa sana na anapswa kuoewa heshima yake kwa sababu ameweka mchango  mkubwa sana katika kuisimamsiah bongo fleva,  kwanini watu wanasema kuwa sio msanii? Na mimi nilimchukua yeye kwa sababu chid ana uweoz wa kuandika ngoma kuliko hata wanavyofikria wao.

Shiloleh anakiri kuwa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha chid benz yeye hakuiandika bali iliandikwa na chid benz mwenyewe.

Nyumba Mpya ya Shiloleh Yampa Jeraha.

Mwanadad Shiloeh amefunguka na kusema kuwa nyumba yake mpya ambayo amehamia siku za hivi karibuni ilimtoa ngeu baada ya kudondoka katika nyumba hiyo usiku alipokuwa narudi katika kazi zake.

Akionekana kama mtu aliyepigwa kutokana na majeraha makubwa aliyokuwa nayo hasa sehemu za usoni na hata watu kuhisi pengine labda ampigwa na mume wake alipokuwa katika siku ya mwanadada Nandy , Shiloleh alikanusha taaarifa za kupigwa na kuesma kuwa ni baada ya kuhamia katika nyumba yake ndipo alipopata hayo majeraha.

Shiloeh anasema ‘unajua kuwa juzi juzi ndio nimehamia kule kwenye nyumba yangu majohe sasa nilikuwa nimerudi usiku na nilikuwa nimerudi nimechoka na hakuna umeme bado basi niliporudi nikawa nimejigongwa kwa sababu ya giza.Nyumba yenyewe nilikuwa bado sijaizoea na hii pati nimealikwa na nilimwaidii nandy kuwa nitakuja kwaio nisngeweza kuacha kuja.

Hata hivyo majeraha hayo hayakumfanya shiloleh kuwa mnyonge katika pati hiyo ambayo nandy alikuwa pia anafanya uzinduzi wa album yake ya kwanza.

Shiloleh Apiga Marufuku Mumewe Kutumika Katika Video.

Mwanadada Shilole amefunguka na kusema kuwa hataki kusikia mtu yoyote anataka kumtumia mume wake katika video yoyote kwa sababu wamekuwa wakimsumbua kila maa hasa baada ya mwanaume huyo kuonekana katika mja ya video ya shiloleh mwenyewe.

Akiongea na waandishi wa habari wikiendi hii alipokuwa katika uzinduzi wa albumu ya msanii Nandy , Shiloleh anasema kuwa inawezekana kwli wengine wanataka kufanya nae kazi kwa nia nzuri lakini yeye hataki  kumuona mume wake katika video za watu wengine.

no nilishamwambia kabisa dont do that, unajua kuwa kuna muda wamekuwa wakimtafuta tu lakini mimi nilishakataa kabisa kufanya nao kazi, ingawa wanaweza kutaka kumchukua kwa nia nzuri lakini sitaki kabisa, na ninatangaza kabisa kuwa sitaki msanii yoyote kumtumia mume wangu

Shiloleh na uchebe wamefunga ndoa mwanzoni mwa mwaka huu na mpaka sasa wanaingai katika idadi ya wasanii wachache walioweza kukaa muda bila kuwa na mikwaruzano ya hadharani

Ngoma ya Champion Nimepewa na Chid Benz ;-Shiloleh

Mwanadada Shiloleh amefunguka na kusema kuwa wimbo wake mpya wa champion ulikuwa ni kama zawadi kutoka kwa Chid benz kwa sababu alimpigia simu na kumwambia kuwa amemtayarishia wimbo na alipomtumia  aliupenda na kuingiza vocal zake ambazo sehemu nyingine anaimba akiwa anachana.

Shiloeh anasem hayo alipokuwa akitambulisha wimbo huo wa champion alipokuwa clouds media , na kusema kuwa katika wimbo huo amekuwa togfauti kwa sababu anachana.

ngoma yangu ya champion humo ndani nimechana na ngoma hii nimeandikiwa na kaka yangu Chid benzi, nakumbuka alinipigia simu usiki na kuniambia kuwa kuna zawadi anataka kunipa na kweli alinitumia na mimi nikaingia coko na  hata alivyokuja alishangaa.

Shiloleh aliwahi kufunguka na kuwaomba mashabiki kuacha kumsema na kumchukulia vibaya Chid benz kwa sababu kwa sas ameazna kubadilika na hayupo kama vile alivyokuwa zamani zaidi sana anachohitaji ni maombi ili aendelee kuwa sawa.

Shishi Awashangaa Wanawake Wanaotukana Katika Mitandao ya Kijamii.

Mwanadada shiloleh amefunguka na kusema kuwa amekuwa akwashangaa sana wasichana wanaokaa kutwa kutykana na watu katika mitndao ya kjiamii kama hawana kazi za kufanya wakati kuna mambo mengi ya kushughulika nayo.

Shiloleh anasema kuwa aina hiyo ya wanawake wanakera na pia wanatia aibu sana wanawake wenzao , hivyo waache mara moja na kufanya vitu vingine vya maana.

Akiongea  katika mahojiano, shiloleh anasema “nashangaa kuona watoto wa kike wako busy kutukana  katika mitandao ya kijamii, wakumbuke kuwa hata bibi pia alikuwaga msichana kwaio waache hayo mambo na waanze kufocus katika mambo ya muhimu katika maisha”

Kwa kuongea hapo, shiloleh pia anasema kuwa watu waache kumsema vibaya msanii Chid Benz kwa sababu kwa sasa hayuko kama alivyokuwa zamani na kwamba amebadilika sana.

Mi Siwezi Kugombania Jina, Ninagombania Hela.;-Shiloleh.

Mwanadada Shilole amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake anaona hakuna maana sana ya kukaa na kugombania jina ambalo unaweza kutafuta la kwako na kulitengeneza na likawa kubwa .

Shiloleh anasema kuwa kwa wema sepetu kuitwa Tanzania sweethaert ni jina lake alilopewa na watu hivyo ni lazima watu wengine wakae wakiliheshimu jina hilo lakini pia hakuna haja ya kugombana kwa sababu ya hilo.

Shiloleh anasema kuwa kwa upande mwingie anawao watu hao ni wajinga kwa kugombania jina  badala ya kugombania ela kwa sababu kwa upande wake yeye anawaza ela na sio jina.

hayo ni maneno tu yanayokuwa yanaongelewa kama mimi ninavyosemaga shishi trumph lakini trump mwenyewe yuko huko, mwenye jina atabaki kuwa mwenye jina tu kwa

sababu tayari watu walishampa, kwanza mimi nitaona ujinga kama wanabaki kugombania majina.mimi nagombania ela i dont need to kugombania jina, why cant you choose another name.

Wema na hamisa wamekuwa wakirumbana katika mitandao kwa sababu ya jina la Tanzania Sweetheart.

Shiloleh Amtupia Bango Diamond Kuhusu Tetesi za Kulogwa na Wanawake.

Ikiwa katika mitandao ya kijamii kumekuwa na habari za kuwa mwanamuziki Diamond Platinumz amekuwa akilogwa na mama wa mtoto wake mdogo anaejulikana kama Hamisa Mobeto, habari ambayo ime-trend sana ktaika mitandao wikiend hii na wiki hii yote kwa ujumla mwanadada shiloleh nae ameamua kupigilia msumari wa moto kutoka katika habari hiyo.

Katika ukurasa wake  wa instagram, Shiloleh aliandika  baada ya kuweka picha ya Diamond Platinumz huku akimtania kuwa muonekano wake mpya unavutia kufuatia kusuka kwake nywele huku akisema kuwa na ndio maana wanawake wamekuwa wakimloga.”kakangu diamond umedamshi na ndio maana wanawake wanakuloga”

Hata hivyo tangu kumesambaa kwa maneno hayo katika mitandao ya kijamii mwanadada Hamisa Mobeto hajataka kuongea kitu kuhusu hilo zaidi ya kuonyesha shughuli zake zikiendelea kufanikiwa.

Shiloleh Amsifia Uchebe Kwenye Mambo ya Chumbani.

Mwanadada abaesifika kwa kupika chakula kitamu katika mgahawa wake wa shishi food , Shiloleh amefunguka na kusema kuwa amekuwa akiwaponda sana wanaume wa Dar kutokana na tabia zao za kupenda kula chipsi mayai na kuwaita kuwa hao sio wanaume halisi.

Shiloleh anasema kuwa pamoja na hayo anaona kuwa wanaume hao wanaopenda chipsi hawawezi kumpata kwa sababu mume wake sio legelege kama wanaume wa aina hiyo kwa sababu mume wake  sio mla chipsi kama mwanaume mwingine.

Akimsifia mume wake Shiloleh anasema kuwa hawezi kumfananisha mwanaume wake na mwanaume mwingine yoyote kwa sababu ya shughuli kubwa aliyonayo chumbani haifanani na mwanaume yoyote.

Shiloleh na Uchebe wameoa mapema mwaka huu na ndoa yao imekuwa ni ndoa tulivu isiyokuwa na migogoro na kuwa shiloleh anasema kuwa mume wake ni mume halisi aliyekuwa akimuhitaji siku zote.

Shiloleh Awatolea Povu Walimshambulia Baada ya Kumuomba Sapoti Rais.

mwanadada Shilole hivi karibuni alituma salamu zake kwa rais wa Tanzania na kumuomba aje kujaribu kula chakula chake katika mgahawa wake wa shishi food , Shiloleh alisema kuwa moja ya ndoto zake ni kumuona rais akila chakula chake na anatumaini kuwa Rais atamsikiliza ombi lake na kumjibu kwa kujongea mgahawani hapo.

Hata hivyo wapo waliomua kama anaigiza au anatafuta kiki hivyo kuanza kumshambulia kwa uamuzi wake huo, basi shiloleh nae hakuona uvivu kuwajibu kwa kuwatolea povu katika ukurasa wake wa instagram na kusema

Niombe radhi kwa walionilelewa vibaya maana mimi huwa si-fake masha kabisa, naishi maisha yangu.sina utajiri huo kama mnaosema na hata nyumba niliojenga nilijenga kwa kujiwekea kidogo kiodgo kama mam ntilie na msanii, na ndio maana hata nilipofanikiwa niliona bora kushare na nyie ili kuwaonyesha ni jinsi gani mnaweza kunisapoti na kufika hapa nilipofika.

Nilichoomba juzi kwa baba magufuli ni sapoti na kuendelezwa kwa wanangu katika vipaji wanavyosomea,mimi napambana sana ili wanangu wapate kusoma lakini natamani sana kuwapa zaidi ya kile ninachowapatia, kwaio nikaona kwanini nisiweke kilio changu kwa mheshimiwa rais wakati yeye ni mtu anajali sana elimu ya watoto wa kike.

Mwanadada shiloleh ambae kila siku amekuwa akipambana kufikia malego yake hakuona aibu kuweka wazi kwa mba anatamani sana kupata sapoti ya elimu ya watoto wake kwa mheshimiwa rais kwa sababu anatamani watoto wake wafike mbali na pale anapooona yeye kwa sasa wanaweza kufika.

Shiloleh Atuma Meseji kwa Rais Magufuli.

Msanii wa muziki shiloleh ametuma salamu zake  kwa Mh rais Magufui na kumtaka aende nyumbani kwake ambapo anafanya shughuli zake za upishi kwa ajili ya kufanya shughuli zake za uuzaji wa chakula.

Shilole anasema kuwa kwa jinsi alivyo na matumaini na Mh rais anaamini kuwa akipata salamu hizo basi anajua kuwa atakuja kwa sababu ana matumainai hayo.

shiloleh ni moja ya wasanii ambao wamekuwa na uhamasishaji sana kuhusu maswala ya jamii na watu wengi wamekuwa wakitamani mafankio yake ukizingatia kuwa mwanadada huy ni moja ya wasanii walipitia maisha magumu kabla ya kufanikiwa.

Namuomba mh rais magufuli aje kwangu aje kula chakula changu pale shishi food ilo ndo ombi langu kubwa kwa mh rais , na ninaona kabisa kuwa matumaini yapo.

Tukinyimwa Tiketi Tutaaandamana, Nampenda Sana Zari.-Shiloleh

Mwanadada Shiloleh amefunguka na kusema kama endapo watanyimwa ticket ya kwenda kusherekea sherehe ya mtoto wa diamond huko Afrika yaKusini basi wataandamana kwa sababu walishapewa ahaadi ya kwenda nchini humo.

Akiongea na waandishi wa habari, shiloleh anasema kuwa kwake hana wasiwasi kwa sababu Diamond tayari alishamwambia amtumie paspoti yake ya kusafiria hivyo wala hana wasiwasi na safari lakini ikitokea kuwa hajapata tiketi basi ataandamana.

Hata hivyo , Shiloleh anasema kuwa kwake haoni sababu ya kumchukia Zari kwa sababu kama atamchukia basi atakuwa na wivu wala sio kitu kingine.lakini pia anasema kuwa watu wanaojifanya kumpenda sasa hivi walikuwa wapi pindi Diamond akitafuta mtoto.

tiketi ya nini wakati tayari tulishawekwa kwenye tiketi ya pamoja, na safari haijawa-cancelld, wewe nani kakwambia, tutaandamana.

wakati Nasibu alipokuwa anangaika kupata mtoto hakuna aliyejitokeza kumpa mtoto, dada wa watu katoka huko kaja kampa watoto wawili.mimi nitasema namchukia huyo dada kwa kipi, huo ni wivu wa maendeleo tu, yule dada ana akili sana na mimibado nitaendelea kuwa team zari kwa sababu nampenda , ana akili sana.