Young Dee Aliniita Nikampelekee Chakula Nikamkuta Na Mwanamke- Amber lulu

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber lulu amefunguka na kueleza moja kati ya matukio yaliyomuumiza kwenye uhusiano wake na msanii mwenzake Young Dee ambapo amedai ameshawahi kumfumania na mwanamke mwingine ndani.

Amber lulu amekuwa muwazi sana kila inapokuja kwenye hisia zake na Young Dee kwani ni  mara kwa mara ameweka wazi kuwa ampenda sana hata Kama amemuumiza sana kwa kuchepuka na wanawake wengine.

Amber lulu amekiri kuwa pamoja na kwamba yupo na Prezzo lakini Young dee ni moja Kati ya mwanaume ambaye alimpenda sana lakini pia amekiri kuwa tukio ambalo hatokuja kulisahau kwenye maisha yake ni siku ambayo Kwani alimfumania live.

Kwenye interview aliyofanya na East Africa redio kupitia kipindi cha Planet Bongo, Amber lulu alifunguka mengi:

Yaani hata leo hii Young Dee akimposti demu mwingine Instagram mimi naumia ingawa siwezi kumkataza lakini pia ikitokea nimeachana na Prezzo naweza nikarudiana naye ingawa ameniumiza sana kipindi cha nyuma kama nakumbuka kuna Siku alinipigia Simu akaniambia yuko studio somewhere akaniambia hebu my baby nipikie kile chakula ninachokipendaga ambacho kilikuwa ni ugali na maini basi mwenyewe nikjipikilisha pale unyamwezi pembeni nimemaliza nimebeba kile chakula nimpelekee alikuwa kwenye hoteli Fulani hivii kufika pale namkuta na msichana mwingine kusema kweli niliumia sana”.

 

Yound Dee:Amber Lulu Hana Hadhi Ya Kutembea Na Mimi

Wasanii Amber Lulu na David Genzi maarufu kama Young Dee wamekuwa katika mgogoro wa muda mrefu huku ikisemekana kuwa wawili hao inawezekana bado wanapendana au wamekuwa wakioneana wivu tena hasa baada ya kuwa wapenzi kwa muda mrefu na kisha kuachana na wote kuendelea na maisha yao ya kawaida. Lakini swala linakuja palepale  ni aidha wawili hao watakuwa bado wanapendana lakini hakuna anaeweza kumuanza mwenzake ndio maana inakuwa ni vita kila siku katika mitandao ya kijamii.

Hivi karibuni Amber Lulu aliwaonya mashabiki katika mitandao kuacha  kumfananisha Young Dee ambae alikuwa mpenzi wake wa zamani na mpenzi wake wa sasa ambae ni Prezzo mwanamuziki kutoka Kenya na kusema kuwa Young Dee hana kiwango chochote cha kulinganishwa na Prezzo katika mambo yote.

Msanii Young Dee ameamua kumjibu na kuwajibu waandishi kuwa amekuwa anachoshwa sana na tabia ya waandishi wa habari kuwa na maswali yanayomuhusu Amber Lulu kwake, na amesema kuwa  Amber Lulu hana hadhi ya kuwa na yeye ana swala la kuwa wanamuuliza maswali ya Amber Lulu mara kwa mara yamekuwa yakisumbua uhusiano wake mpya.

Nimechoka kuulizwa maswali kuhusu mimi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Amber Lulu,hana hadhi ya kuwa na mimi na ninaomba nisiulizwe kwa sababu mnaniharibia sana mahusiano mapya na mpenzi wangu wa sasa.

Amber lulu ambae amejiingiza katika mahusiano na prezzo maekuwa akichukizwa na baadhi ya watu katika mitandao ambao wamekuwa wakimfananisha msanii huyona mpenzi wake huyo mpya .

Young Dee- Nimeiga Wimbo Wa Mr. Nice Kwa Heshima

Msanii wa Bongo fleva Young Dee ameibuka na kudai kuwa kitendo cha yeye kuiga wimbo msanii mkongwe wa Bongo fleva Lucas Mkenda maarufu kama Mr.Nice Ilikuwa ni kwa sababu ya heshima aliyonayo kwenye mziki wake na wala sio wizi.

Baada ya Young Dee kutoa wimbo wake mpya unaoenda kwa jina la Kiben10 ambao ndani yake ameweka kionjo cha wimbo wa Mr.Nice bila ruhusa, ndipo pale jasho lilimtoka kwani Mr. Nice alipousikia wimbo huo alimjia juu Young Dee kwenye mitandao ya kijamii na kudiriki kumuita mwizi wa kazi zake na kutishia kumchukulia hatua za kisheria.

Young Dee amemjibu Mr. Nice na amejitetea kuwa yeye kuimba wimbo wake haikuwa kwa nia mbaya bali alifnya vile kwa sababu alikuwa shabiki Mkubwa wa wimbo wa Mr. Nice.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kupitua kipindi Chao cha Enews Young Dee alifunguka:

Naomba niseme kuwa sikuwa na nia mbaya bali nia yangu ilikuwa ni kumpa heshima maana hawa ni kaka yangu aliyenitangulia katika gemu alafu ana mchango mkubwa kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kwaiyo lengi langi lilikuwq ni kumuonyesha heshima aliyoiweka kwenye mziki wetu wa Bongo fleva kiasi ya kwamba miaka mingi baada ya wimbo huo kuhit lakini bado Una ladha ya kipekee kabisa”.

Mr. Nice Amjia Juu Young Dee Baada ya Kuimuibia Wimbo Wake Wa ‘King’asti’

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyetamba kwa staili yake ya ‘Takeu style’ ameibuka na kumtolea povu zito msanii mwenzake Young Dee baada ya kusample wimbo wake wa ‘King’asti’.

Mr. Nice amezidi kukaa kwenye headlines kwa wiki hii kuanzia kurudi upya kwa bifu lake na aliyekuwa hasimu wake mkubwa Dudubaya mpaka kuingia kwenye vita ya maneno na Paka rapa Young Dee baada ya Young Dee ku-sample wimbo wake ulio-hit miaka ya nyuma ulioenda kwa jina la ‘king’asti’.

Young Dee ametoa wimbo wake mpya unaoitwa ‘kiben-10’ na amemshirikisha Dayna Nyange ambapo kwenye wimbo huo kuna kionjo na mashairi machache kutoka kwenye wimbo huo wa Mr. Nice ambao amechukua bila ruhusa ya mwenye wimbo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mr. Nice amemtolea Young Dee povu zito:

Nadhani ni wizi na ni aibu kuchukua kazi ya mtu na kuirudia tena kwa manufaa yako binafsi bila hata kuomba ridhaa yoyote kutoka kwa mwenye kazi yake, ni wizi ambao serikali na jamii nzima imekuwa ikipiga vita every day na ni kosa kubwa kabisa kisheria…..Huyo msanii anayeitwa sijui Young Dee mwelezeni asije kutafuta huruma yangu hapo baadae kwa maana haitakuwepo”.

 

Gigy Money Amshauri Young Dee Kubaki Na Amber Lulu

Msanii wa kike ambae kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha ‘nampa papa’, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, mwisho ni mwa wiki iliyopita alijikuta akitoa povu zito kwa msanii mwenzie wa kiume anaejulikana kama Young dee kutokana na muenendo mbaya alionao katika mahusiano.kwa mujibu wa Gigy Money, Young Dee ni shemeji yake kutoka kwa Amber Lulu ambae pia ni msanii wa Bongo fleva lakini pia aliyekuwa na anaendelea kuwa moja ya ma-video queen wanaofanya   vizuri katika videos za wasanii mbalimbali wakubwa  nchini.

Gigy Money  alisikika akisema kuwa katika wanawake wote aliokuwa nao Young Dee ni msichana mmoja tu Amber Lulu ndie mwenye mapenzi ya kweli kwake sio hao wengine wanamchukulia kama kikatuni .Maneno hayo yalianza baada ya wasnii hao wote watuatu walipokutana nje ya jengo la EATV, wakitoka katika mahojiano ya kipindi cha Friday Nite Live ambapo , Amber Lulu aliona baadhi ya alama za kucha na vidole katika shigo ya Young Dee na kuanza kumshangaa na kumtuhumu kuwa itakuwa alikuwa katika ugomvi na mwanamke mwingine,

Kutokana na tukio ilo Gigy Money alipewa nafasi ya kuongea na kusema kuwa “Young Dee apunguze mitandao ya wanawake, maana inamchanganya wakati ukimwangalia umri wake ni mdogo sana,atulie tu na Amber Lulu maana katika wanawake wake wote mia  Amber Lulu ana mapenzi ya kweli kwake,wengine wote wanafata jina tu ilo la bongo bahati mbaya ,wanamuona kama kinyani wanamtakataka” alifunguka  Gigy Money ambae aliweka wazi pia kuwa kumbe wawili hao walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi.

Amber Lulu na Young Dee walikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda kidogo uliopoita huku wakikataa kuwa katika mahusiano hayo, ilifikia hatua mpaka Amber Lulu aliamua kuchora tattooo ya jina la  Young Dee mkononi lakini walipogombana Amber Lulu aliamua kufuta tattoo iyo, hivi karibuni pia kuna picha zilisambaa za amber lulu na Young Dee , picha ambazo ziliwafanya wawili hao kupelekana polisi .

Bifu La Young Dee Na Dogo Janja,Chanzo ni Muna

Kwa muda sasa kumekuwa na chokochoko kati ya wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva yaani Young Dee na Dogo Janja ambapo katika kufatilia sababu inaonekana ni yale maneno ambayo Young Dee aliyaongea yaliyokuwa yanamuhusu Dogo Janja na Young Killer Msodoki kuwa yeye (Young Dee) ni mkubwa kimuziki hivyo hataki kabisa kusikia watu wakimfanisha na wasanii hao wawili ambao kwake anawaona bado wachanga hawajamfikia kiwango chake. Young Killer alinyamzaza na hajaonekana kuongea chochote kuhusu ili lakini Dogo Janja hakuweza kuvumilia na kuamua kujibu maneno ya Young Dee na kumwambia kuwa hata yeye hawezi kulinganishawa  msanii kama yeye ambae anavuta unga, kabisa hawezi kuongea na ‘mteja’.

Bifu limeendelea na kuwa kubwa mpaka baadhi ya wasanii waliamua kuingia nakuwashauri kuyamaliza mambo hayo, kati ya wasanii hao ni pamoja na Nikki wa Pili.Lakini jana msanii wa muziki wa singeli Sholo Mwamba nae aliamua kufunguka kuhusu bifu ilo huku akiamua kumwaga ubuyu hadharani kuhusu sababu ya wasanii hao kugombana ni mwanamke.

Akiongea na eNews ,Sholo Mwamba ambae alikuwa chini ya menejiment ya Muna Entertainment alifunguka na kusema kuwa kwa sasa yeye na Muna hawafanyi kazi pamoja na sababu sio kwamba yeye alichokwa na Muna bali yeye alimchoka Muna, alipoulizwa sababau ya yeye kumchoka meneja wake alijibu “Kitu ambacho mimi kiliniuzi na nilikichoka kwa Muda ni kitendo cha sisi wanaume kufanya kazi na kutafuta ela  afu tukienda pale  kwa muna tunakuta madogo wengune wamekaa kwenye makochi wamejiachia, sisi wahuni tunaenda kuimba visingeli vijijini tunaleta mpunga kwa bosi alafu bosi anatumia na wajinga”aliongea Sholo Mwamba

hapo wote vingasti tu, tunawakuta pale kwa bimkubwa wanajiachia achia tu, Dogo Janja, Young Dee, wanagombana wanagombania demu, ila sisi tunakuja kwa bosi tunawakuta hayo mambo ya kugombana ni miyeyusho tu” aliongezea Sholo Mwamba

Hata hivyo Sholo pia anaonekana ana wivu wa mapenzi kwa Muna Love na kufikia hatua ya kusema ” namshangaa bosi si angenipa hata mimi, akinipa sisemi, tunakula kimyakimya”

Dogo Janja Amwita Young Dee Teja

Ikiwa ni siku kadha zimepita na ugomvi kati ya wasanii wa Bongo Fleva Young Dee na Dogo Janja unazidi kuwa mzito huku kila mmoja akitaika kuwa juu zaidi ya mwenzie, ugomvi huu ambao ulianza kwa Young Dee kukataa kabisa kufananisha na wasanii wengine ambao hawapo kabisa katika level zake, kwa mujibu wa Young Dee anasema wasanii kama Dogo Janja  wa Arusha na Young Killer wa Mwanza ni wadodgo sana katika swala la muziki na yeye ndie kaka yao hivyo kwanza wanapaswa kumheshimu lakini pia vyombo vya habari havipaswi kumfananisha wa wasanii hao.

Hata hivyo Dogo Janja ameamua kumjibu rapper huyo  na kusema kuwa yeye hawezi kubishana na Young Dee kwa sababu Young Dee ni teja.Dogo Janja anasema kuwa ni sawa kabisa kwa Young Dee kukataa kufananishwa na yeye kwa sababau hata yeye pia hayuko tayari kabisa kufananishwa na Young Dee kwa sababu rapper huyo anatumia madawa ya kulevya na muda mwingi anaongea akiwa tayari ameshatumia madawa  , na kutokana na matumizi ya madawa hayo ndio maana anaongea mambo ya ajabu ajabu”Young Dee ni mteja,na hawezi kufanana na mim.Mtu mwenye akili timamu hawezi kutukana kwenye Media matusi makubwa kama alivyofanya Young Dee, akiacha unga ndo ninaweza kuzungumza,siwezi jua kama saivi ntakuwa nazungumza  au nabishana  na yeye au na mteja.Mtu mwenye akili timamau unamsamehe  tu maana inawezekana kashavuta mambo yake na yupo kwenye dunia yake nyingine” alifunguka Dogo Janja

Hata hivyo Dogo Janja anasema kuwa yeye hakatai kufananishwa na mtu lakini anaangalia mtu wa kufananishwa nae”mimi pia sipendi kufananishwa  japo pia sikatai kufananishwa, Young Killer nilishawahi kuwa Role model wake kwaiyo kufananishwa nae si kitu kibaya lakini kufananishwa na mla unga ni kukosea.. Young Dee akiacha kula unga tutakaa mezani tuzungumze  lakini kfananishwa nae kwa sasa hivi sitaki”

Baada ya Dogo Janja kuongea hivyo Young Dee  alimjibu tena msanii huyo na kusema kuwa wao kama wasanii wadogo wanatakiwa wamfate yeye kaka yao ili wajue sababu ya yeye  kusema hataki mkufananishwa nao,hata hivo Young Dee anasisitiza kuwa bila yeye wasanii wengine wadogo wasingekuwa hapo kimziki maana wote wamefunguliwa njia na yeye.