“Nakupenda Sana, Kula Ushibe Halafu Kaza Chaga”-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameibuka na kumtumia ujumbe Mpenzi wake  Mpya anayejulikana kwa jina la Linah.

Dogo Janja alitangaza kuchana na aliyekuwa mke Wake Msanii Irene Uwoya mapema mwaka jana Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miezi kadhaa.

Dogo Janja Hivi sasa yupo kwenye mahusiano na Mrembo ambaye ni Mfanyabiashara kutoka Arusha ambaye anasemekana kuwa na pesa ndefu kutokana na Familia yake kuwa kwenye biashara za madini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja amemtumia ujumbe wa birthday mrembo huyo ambaye alizaliwa siku ya jana:

Hakuna neno linaloweza kutosha kuielezea furaha niliyonayo kwenye kufurahia siku yako ya kuzaliwa mpenzi wangu…..mengine nitakueleza chumbani…..kula ushibe kisha kaza chaga….nakupenda sana”.

https://www.instagram.com/p/BtlyFosFIt9/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1tdljljimtqu5

Dogo Janja- Mbali Ya Muziki Nafanya Biashara

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa mbali na kufanya muziki Lakini pia ni mfanyabiashara.

Dogo Janja ambaye anafanya vyema kwenye tasnia ya muziki nchini ameweka wazi kuwa pamoja na kuupenda muziki Lakini anaamini ni vyema Kuwa na kitu kingine cha kufanya.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Dogo Janja amesema kuwa amekuwa akifanya biashara zake nje ya muziki wake ambazo zimekuwa zikimwingizia kipato kizuri na kujivunia kuifanya kwa moyo mmoja.

Nafurahi nafanya biashara ambazo zinanilipa nje ya muziki wangu, nafurahia kile ninachokifanya kwa kuwa biashara zangu zimekuwa na manufaa makubwa kwenye maisha yangu”.

 

Dogo Janja Amuanika Hadharani Mpenzi Wake Mpya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja ameonekana kuendelea na maisha yake Baada ya kuachana na aliyekuwa mke Wake Irene Uwoya.

Dogo ameonekana akijiachia live na mwanamke mwingine anayetambulika kama Lina kwenye Mitandao ya kijamii ambapo walionekana wakiwa wanakumbatiana bila uwoga.

Wikiendi iliyopita Dogo Janja na mama yake mzazi walionekana kwenye party ya rafiki wa karibu wa Lina ambapo Dogo alikuwa anatumbuiza Lakini mara akaonekana akiwa anakumbatiana na Linah na mahaba hadharani.

Pamoja na taarifa za Dogo Janja kuwa kwenye mahusiano na linah Lakini Mpaka sasa hajathibitisha taarifa hizo.

Dogo Janja Aikana Familia ya Uwoya.

Msanii Dogo Janja ameonekana kuikana familia ya msanii Irene Uwoya ambae aliwahi kuwa mke wake na kuachana hivi karibuni huku akisema kuwa hajui kitu kuhusu familia hiyo na wala hana habari nayo hata kidogo.

Alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya waandishi anasema kuwa kwa upande wa familia yake wanandekea vizrui akimaanisha familia yake iliyopo Arusha ambako amekuwepo huko kwa mud mrefu sana lakini kuhusu familia ya msanii Irene huyo hajui chochote hivyo anaombwa hasiulizwe kitu.

Ikumbukwe kuwa Dogo Janja na Irene wamekuwa katika ndoa kwa muda mfupi sana , ndoa iliyofungwa mwanzoni mwa mwak 2018 na kuachana mwaka 2018 , huku sababu kubwa ni kushindwana kwa tabia kati ya wawili hao.

 

Dogo Janja Amponda Bilnass na Style Yake ya Nywele.

Msanii kutoka Arusha Dogo Janja amemtupia msanii mwenzake Billnass,  Dongo baada ya msanii huyo kuonekana akiwa na style mpya ya nywele akiwa ametengeneza dread, style ambayo wasanii weng ka sasa wamekuwa wakiweka kichwani.

Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa style hiyo haijampndeza kabisa msanii mwenzake huyo na kumwambia kuwa  hata waliupokutana katika After school bash wikiend iliyopita hakumtambua mara moja kwa sababu ya  upya huo.

Dogo janja amefunguka na kumwambia kuwa msanii mwenzake huyo hajapendeza kabisa na kuamua kubadili style hiyo.

Wasanii hasa wa kiume kwa sasa wengi wamekuwa wakivutiwa na kutengeneza nywele style ya nywele ndefu yaan dread , ingawa wengi hupendelea kusuka lakini  sio kichwa kizima, vado haijafahamika kama dogo janja alikuwa akitania kuhusu swala hili au lakwa sababu wawili hao ni marafiki pia.

 

Lynn Akiri Kuvutiwa na Rayvanny na Dogo Janja

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis maarufu kama Lynn ameibuka na kuweka wazi kuwa wasanii waliomvutia kwenye Sanaa ni Mastaa wa Bongo fleva Rayvanny na Dogo Janja.

Wiki mbili ziizopita Lynn aliingia rasmi kwenye tasnia ya Bongo Fleva kwa kutambulisha wimbo Wake Mpya ‘Chafu’.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Jumamosi, Lynn alisema kwa kipindi kirefu alikuwa na nia ila alikosa mtu wa kumshauri, lakini baada ya kuwasikilizisha nyimbo zake, Rayvanny na Dogo Janja walimtia moyo kuwa anaweza.

Muziki ni moja ya malengo yaliyokuwa ndani yangu, lakini ndoto zangu niliona kama zinakufa kutokana na baadhi ya watu kunikatisha tamaa. Lakini ilikuwa tofauti kwa Rayvanny na Dogo Janja ambao walinipa moyo kuwa naweza ndipo nikatoa wimbo wangu haraka”.

Lyyn ambaye ameachia ngoma inayokwenda kwa jina la Chafu na kusifia mapokezi kuwa ni mazuri kuliko alivyotegemea hivyo amepanga kuachia mwingine fasta.

 

 

Dogo janja Akumbuka Zamani

Msanii Dogo Janja Amerudi na kukumbuka kule alikotoka baada ya kuikabidhi shule aliyosomea darasa la kwanza mpaka la saba kwa kuwapa ndoo za rangi 20  pamoja na kuamua kukarabati shule hiyo kwa kuweka mabati.

Dogo janja mabae laisoma shule ya ungalimitied arusha, ameamua kurudisha fadhila na kukarabati mazingira hayo ili kuwasaidia wanafunzi waliopo sasa kusoma katika mazingira sala na safi.

Huu ni wakati mabao Dogo janja amekuwa akijitolea kwa jamii yake  kwa sababu tangu amekuwa Arusha ambao ndiko aliozaliwa , ameamua kujirudi kwa jamii yake na hata kujenga nyumba kwa ajili ya mama yak mzazi.

katika ukurasa wake wa instagra  Madee aliandika ; leo mapema @dogojanjatz alirudi kwenye shule #Ungalimited alisomalakwanza mpaka ka saba na kutoa ahadi ya kupiga rangi shule nzima na bila kuchelewa akapiga simu kiwandani na kuletwa ndoo kama zote … pia atapiga bati shule nzima

 

Dogo Janja Amjengea Mjengo Mama Yake Baada Ya Baba Yake Kufariki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chende maarufu kama Dogo Janja ameuanika mjengo ambao amemjengea Mama yake mzazi miaka miwili baada ya baba yake kufariki.

Siku ya jana December 4, 2018 Dogo Janja, amefanya dua ya kumuombea Baba yake ambapo pia ametuonyesha nyumba aliyomjengea Mama yake Mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha Mama yake anaishi sehemu nzuri.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Dogo Janja ameandika mjengo huo na kufunguka mengi:

Sisi tumekulia katika nyumba ya kupanga, Mimi na Kaka yangu tulikuwa tunalala sebuleni baada ya Baba kufariki Mimi nimebaki kama Baba wa familia, Mama angu anahitaji sana faraja, najitahidi sana kumpa faraja sababu siwezi badilishana na Mtu mama”.

Lakini pia Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dogo Janja amefunguka muhimu wa yeye Kama Mtoto wa kiume kumjengea Nyumba hiyo Mama yake:

Mimi ni Mfanyabiashara Sitakiwa Kuchagua Upande Kati Ya Wasafi Au Clouds-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini Abdul Chande Maarufu Kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye ni mfanyabiashara hivyo hawezi kufungamana na upende wowote.

Mgawanyiko huo kati ya wasanii ulitokea mapema Wiki iliyopita Baada ya sakata la Wasafi Festival na Fiesta lilopelekea wasanii waliokuwa wanaperfom kwenye Fiesta kushindwa kufanya hivyo na kuaababisha kukosa shoo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago TV, Dogo Janja ameweka wazi kuwa hawezi kujiweka katika upande wowote ule kwa sababu yeye ni mfanyabiashara hivyo kokote atakapoitwa kupiga pesa yeye ataona sawa tu.

Mimi matabaka sioni ninachoamini Mimi mfanyabiashara hivyo sitakiwa kufungamana na upande wowote ilimradi naenda huku napiga naenda kule napiga hela basi hicho cha maana kwangu”.

Dogo Janja alikuwa mmoja wa wasanii ambao walitakiwa kupiga shoo ya Fiesta jumamosi iliyopita lakini walishindwa Baada ya shoo hiyo kuhairishwa Baada ya serikali kuizuia kufanyika katika viwanja vya Leaders.

Maneno ya Dogo Janja Kuhusu kifo Chake

Msanii wa bongo flea Dogo Janja amefunguka  na kuwataka watu kuwa na upendo  na watu pale wanapkuwa hai na sio kusbiri mpak pale watakapokufa ndo waanze kulia na kusema kuwa walikuwa ni wapendwa wao.

katika kurasa wake Dogo Janja aliandika “siku nikifa utataoa machozi lakini mimi sitayaona,utaleta maua lakini mimi sitayapokea, utanisifai asna lakini mimi sitakusikia utanisamehe makosa yangu lakini mimi sitayajua , utanimisi sana lakini sitafahamu na utauzinika sana lakini sitakuona.

Dogo janja ametaka watu kuwa wakweli wa  wale wanaowapenda kabla hawajakufa na sio kujifanya mnafiki kuonyesha kuwa unampenda mtu akiwa tayari hajuia wala haoni kile unachokifanya.

Jibu la Dogo Janja Kuhusu Sababu ya Kumsaliti Irene Lina Utata.

Msanii Dogo Janja amejikuta akimjibu kwa kumtolea povu moja ya mashabiki zake walimuuliza kwa nii aliamua kumsaliti mke wake wa ndoa irene uwoya na kwenda kutembea na mwanamke mwingie.

Ikumbukwe kuwa siku za hapo karibuni kulizuka tetesi za msanii Dogo Janja kutoka kimapenzi na mwana dada wema sepet na kusababisha ndoa yao kuvunjika, ndoa ambayo ilikuwa aikizungumziwa sana midomoni mwa watu katika mitandao ya kijamii.

Moja ya mashabiki zake walimuuliza  sababu kubwa ya  kumsaliti mke wake ilikuwa ni nini lakini kitu cha ajabu dogo janja alijibu jibu ambalo kama vule kosa hilo alikuwa amesingiziwa hakuna na hatia yoyote

Shabiki aliuliza, Dogo janja why didi you cheat on your wife,  Dogo janja nae aliwajibu kwa kusema ‘”stress ya ukweli ni pale unapokutana na mama wa demu wako alafu anakwambia wewe ndio uwaga kila siku unakuja na gari usiku kumchukua  mwanangu , wakati wewe hata mkokoteni tu hauna.”

 

 

Dogo Janja Atangaza Zawadi ya Mjukuu kwa Mama Yake

Msanii Dogo Janja katika hali isiyo ya kuhaminika kwa mashabiki wake aliweka picha ya mama yake mzazi huku akisema kuwa ni muda muafaka sasa wa yeye kumletea mama yake mzazi mjukuu kwa sasa kwa sababu mama yake anaanza kuzeeka.

Dogo janja anasema hivyo ikiwa imepita siku chache tu tangu kuvunjika kwa ndoa yake na mwanadada Irene uwoya hivyo hii inazua gumzo kwa mashabiki wake kwa sababu kutangaza uwepo wa mjukuuu ni ishara ya kujiamini na jambo hilo huku ikitaka kujulikana mwanamke anamletea mama yake mzazi Dogo janja mjukuu.

Msanii huyo ambae tang kumekuwa na skendo za kuachan na mke wake amekuwa akionekna yupo karibu na nyumbani kwao Arusha huku ikisemwa kuwa nyumba aliyokuwa akikaa na me wake inaoneknana kwa sasa haina mtu.

 

Maneno ya Mashabiki Baada ya Dogo Janja Kukitana na Jenipher Kanumba

Wikiend hii wasani walipokuwa katika ziara ya shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro, msanii Dogo janja alikutana na msanii wa bongo movies Jenipher kanumba  na kupiga nae picha ya pamoja.

Kata hivyo wawili hao wote ni wasanii lakini kwa maelezo ya dogo janja anasema kuwa hakuwahi kukutana na msanii mwenzake huyo na ndio ilikuwa mara ya kwanza kwa siku hiyo.

Katika picha hiyo Dogo janja alisema kuwa hiyo iliwahi kuwa moja ya ndoto yake ya kutaka kukutana na msanii huyo na anashukuru ndoto hiyo imekamilika.

Kama kawaida kwa maneno ya mshabiki walianza kumpingeza huku wengine wakimwambia kuwa wasichana kama jenipher ndio saizi yake na sio kukimbilia wanamwake wakubwa wakubwa ambao  wamezidi umri kama uwoya.

Baadhi za commentsa za wadau zinaonekna azikisema hivi ”

Wema Afunguka Tetesi Za Kufaidi Penzi la Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuongelea skendo nzito inayomuandama hivi sasa ya kufaidi Penzi la Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku ya jana Mange Kimambi alidai kuwa  Wema  na Dogo Janja walikutana mkoani Arusha ambapo walikuwa nyumbani kwa rafiki yao lakini mambo yaliwazidi na kujikuta wanafanya yao.

Wema ameibuka kukataa tetesi hizo na kumtuhumu Mange kwa kusambaza taarifa ambazo hazina ukweli wowote.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wema ameandika maneno haya:

Wema amekana tetesi hizo na kumuanika mwanaume mwingine ambaye amedai atakuwa mume wake mtarajiwa.

Bill Nas Akana Bifu na Dogo Janja Baada Ya Kumwagiana Povu Zito

Msanii wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kuchana William Lymo maarufu kama Bill Nas amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Dogo Janja hawana bifu lolote.

Tetesi za Bill Nas na Dogo Janja kusemekana kuwa na bifu zilianza mara baada ya wawili hao kurushiana maneno ya kejeli Kwenye mitandao ya kijamii ambapo Dogo Janja alimtania Bill Nas kwa kuachwa na mwanamke wake kwa sababu ya mdomo  na Bill Nas alimchana kuwa ameolewa na Uwoya ili acheze na mtoto wake.

Global Publishers lilimtafuta Billnass ili azungumzie ishu hiyo ambapo alisema hana bifu na Dogo Janja bali maneno hayo yalikuwa ni utani tu.

Sina bifu na Dogo Janja, hayo maneno tuliyokuwa tunaandikiana yalikuwa ni utani tu, sisi tumeshazoea kutaniana kwa hiyo nawaomba mashabiki zangu wasichukulie kwamba tuna tofauti”.

 

Dogo Janja Akimbilia Kwa Mwanasaikolojia.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Dogo Janja ameanza kuonekana akitafuta msaada kwa kile kilichodaiwa kuwa anahitaji  msaada wa kisaikolojia kutoka na matatizo ya msongo wa mawazo unaomkumba hasa baada ya kushindwa kukubaliana na hali halisa ya mahusianoa yake.

Mwanamuziki huyo ambae aliweka picha yake akiwa na mwanasaikolojia Chris Mauki, imesemekana kuwa hali yake kwa sasa haiko sawa hivyo imembidi kutafuta msaada zaidi.

Kama utakumbuka basi wiki chache zilizopita, mwanamuziki huyo aliwahi kuripotiwa kuwa mgonjwa hospitali huku sababu kubwa ikisemekana kuwa ni msongo wa mawazo wa kusindwa kukubaliana na hali halisi ya mfarakano wake na  mkewe.

Hata hivyo Uwoya mwenyewe amekuwa akikanusha taarifa hizo ilhali kumekuwa hakua zile rapsha rapsha  za mapenzi kama ilivyokuwa hapo awali kati yao.