Niliwahi Kushika Pesa Kuliko Msanii Yoyote , Ruge Hakuwahi Nidhurumu :-Chid

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini mabae kwa sasa amekuwa chini kutokana na hali yake ya kiafya kidogo kudhoofu CHID BENZ amefunguka na kusema kuwa tangu amekuwa msanii kwa zaidi ya miaka 10 sasa yeye no moja ya wasanii wenye historia ya kuwa na pesa nyingi kuliko msanii yoyote lakini hakuwahi kufanyiwa dhuruma na Ruge.

Chid benz ambae anasema kuwa yeye ni msanii aliyewahi kushika pesa sana kipindi cha nyuma kuliko msanii yoyote na alikuwa akisaidwa sana na bwana Ruhe lakini hakuwahi kufanyiwa yale ambayo baadhi ya wasanii wamekuwa wakizusha katika mitandao ya kijamii.

hata hivyo moja ya wasnaii DUDUBAYA amezua kashfa mbaya sana kwa marehemu Ruge mutahaba kwa kusema kuwa amekuwa akidhurumu sana wasanii hasa waliopitia mikononi mwake ilhali wasanii waliolelewa hapo wanasema hakukuwa na kitu kama icho.

Mpinzani Wangu Alikuwa Ngwea :-Chid Benz

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini Chid benz amefunguka na kusema kuwa katika maisha ya usanii kila msanii anakuwa na wimbo wake ambao unakuwa mkubwa na wa kumfanya atambulike sana kuliko wimbo mwingine na hakuna mtu anaweza kukataa hilo.

Hata hivyo Chid anasema kuwa pamoja na hayo kwa upand wae anaamini kuwa ngoma ambayo ilimfanya kukaa na kutambulika sana katika gemu ni ngoma ya Dar es salaam stand up ambao ulimfanya kupata mashabiki wengi sana,

Hata hivyo Chid anasema kuwa kwa anavyoamini yeye , hakuna msanii mwingine anaweza kulinganishwa na yeye zaidi ya marehemu Ngwe a ambae alikuwa anaona kuwa ndie aliekuwa akimkimbiza sana katika game la muziki kipindi hicho na hakuna mwingine anaweza kutokea.

 

Jux Amjibu Chid Benz Kuhusu Tuhuma Za Kutojua Kuimba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva  Juma Jux amemjibu Msanii mwenzake Chid Benz ambaye siku chache zilizopita alisema wazi kuwa hadhani kama Jux anajua kuimba.

Kama utakumbuka siku za nyuma Chid Benz na Jux wameshawahi kuwa na kabifu fulani Hivi baada ya Chidi kudai kuwa Jux alimpigisha shoo kwenye Ziara ya ‘In Love and Money tour’ bila kumlipa chochote kitu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Jux amefunguka haya kuhusiana na sakata hilo:

Chid Benz kusema mimi sijui kuimba sidhani kama kakosea maana huo ni mtazamo wake na sio dhambi maana ni uhuru wa kuongea, nilikosea kumwambia Chid Benz nitakucheki maana nilikutana nae kwenye Love and Money tour Dar backstage na aliomba kupanda kwenye stage na alipanda na alivyomaliza nilimshukuru na nikamwambia ‘nitakucheki’”.

Kesho na sikumcheki, kila alipokuwa akinitafuta nakuwa na mambo mengine na baada ya siku tatu nikaona anasema kwenye media nimlipe hela zake, na kiukweli ile show hatukuwa na sponsor na wasanii wote walifanya bure na kutuunga mkono, bado sijamcheki ila nitamcheki”.

 

Alichosema Chid Benz Kuhusu Mh Makonda

Msanii wa muziki Chid Benz amefunguka  na kuandika ujumbe mzito kwa mh mkuu wa mkoa wa jijini Dar es salaam kwa kusema kuwa mkuu wa mkoa huyo anatakiwa aachane na mambo ya muziki na wasanii na kudeal na mambo ya serikali sio kukaa kufanya vitu kwa kuichanganya serikali.

Chid benz anasema kuwa inawezekana kuwa makonda akawa na moyo wa kufanya yote kwa ajili ya watu wa Dar lakini nguvu ya kufanya hivyo hana kwa sababu yuko na mambo mengi ya kufanya hivyo anawez kupata lawama kutokana na yale anayoyafanya.

Chid benz anasema kuna mamb mengi ya kufanya katika jamii ukiachilia mbali na yale anayoyafanywa kwa sasa kwa wasanii .

Chid benz anasema kuwa mh makonda aache kutafuta kupigiwa kelele na wasanii badala yake aangalie mambo muhimu ya kufanya katika jamii kama kuleta madawa katika mahospitali, ukarabati wa vituo vya daladala  ili kupunguza lawama kwa wananchi.

 

 

Chid Benz Aomba Asivunjwe Moyo, Asipuuzwe.

Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Rashid Makwilo maarufu kama Chid Benz, amewataka watu kumsikiliza anayosema bila kumuhukumu kwa udhaifu wake.
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Chid Benz amesema kwamba mara nyingi amekuwa akiongea mambo ya msingi, lakini watu wamekuwa wakimpuuza na kumchukulia kama mtu aliyedata, huku vijana wengine wakiendelea kupotea.

Chid Benz ameendelea kusema kwamba hata kama wanamuhukumu kutumia madawa ya kulevya, lakini wasiangalie madawa anayotumia wala udhaifu mwingine, bali wachukue maneno anayoyazungumza ili kuokoa wengine.

Ukiskiliza interview zangu jinsi ninavyozifanya na mood zinavyonikuta, zimegeuzwa kama masihara ila kitu kama mtu anasikia na anasema huyu jamaa anaongea nini!?. Tuchukulie kavuta bangi, toa bangi zake, tuchukulie anakula unga, toa unga wake, ila fikiria anaongea nini!?”,  “Chid alikuwepo kama miaka 15 kwenye hii ‘industry’ nazunguka zunguka, wakati mwingine naona bora ninyamaze kwa sababu mimi nikiongea watu wanachukulia kama nimedata, lakini watu wengine wanazidi kupotea, wanazidi kufa wanazidi kukosa hela, wanazidi kuwa wajinga, wanazidi kuwa wapumbavu, wanakaa magetoni mwao wanasema Chid Mjinga, bangi tu”, amesema Chid Benz.

Hivi karibuni Chid Benz amekuwa akisema mambo mbali mbali kuwasema wasanii wenzake, jambo ambalo baadhi ya watu wamekuwa wakimdhihaki kutokana na uraibu ambao alikuwa nao miaka ya hivi karibuni.Pia aliwahi kusema tayari amefanya collaboration na 2pac

Chid Benz Kufuata Nyayo za Suma Lee

Msanii Chid Benz amefunguka na kusema kuwa kwa sasa  anampango wa kuachana na shughuli za muziki na kuamua kumtumikia mwenyezi Mungu, hatua ambayo imechukuliwa na baadhi ya wasanii katika muziki hapa  bongo.

Chid benz anasema kuwa ktendo cha kukutana na Abdulrazac kwake kimempa mawazo na kutaa kuchukua hatua thabiti ya kumtumikia mungu badala ya kuendelea na mambo ya kidunia.

Ikumbukwe kuwa shekh huyo ndie alietangaza hivi karibuni kuwa amekuwa na kiu ya kutaka kumbdilisha sana msanii huyo pamoja na alikiba li kumtumikia mungu na kuacha mambo ya kidunia, hsa kwa upande wa chid inakuja baada ya kiongozi huyo wa dini kuona kuwa mwanamuziki huyo amekuwa akiangaika sana .

kumtumikia mungu kwa wsanii kunaziid kuongezeka hasa baada ya wasanii kam Suma lee, mzee Yusuph na Saigon kuamua kujitoa katika sanaa na kumrudia Mungu.

 

Chid Benz Ataka Afande Sele Aombe Radhi Haraka

Baada ya mwanamuziki Afande sele kutangaza kuwa mtu yoyote anaevuta unga au kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya basi huyo ni shoga, msani Chid benz amefunguka na kumtaka msanii huyo kuomba radhi hadahrani  kwa kauli yake hiyo.

Kauli hiyo ya Afande sele imemuuumiza sana msanii Chid benz kwa sababu hata yeye pia ni moja ya waathirika wa madawa ya kulevya hivyo amemtaka afande sele kwa kumpa masaa 19 tu na kujitokeza ksiha kuomba radhi mbele ya watu la sivyo atajua cha kumfanya.

Kauli hiyo ilitolewa na  Afande sele alipokuwa stegini wikiend iliyopita  katika tamasha la Wasafi festival lililofanyika huko Morogoro.

Chid Benz ni Teja Hawezi Kupanda Kwenye Steji Ya Wasafi- Afande Sele

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Afande Sele amefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii mwenzake Chid Benz hawezi kupandishwa Steji ya Wasafi Festival kwa sababu ni teja.

Wiki iliyopita Chid Benz ambaye amekuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu sasa alilalamika kitendo cha kutoalikwa Kupanda Steji ya Wasafi na Kuperfom na kudai kuna wasanii wasio na vipaji wanapendelewa.

Afande Sele ameibuka na kudai Chid Benz hawezi kupandishwa katika Steji ya Wasafi Festival kwani ni teja hivyo mtu Kama huyo ataleta

Niseme tu ukweli ni kwamba Chid Benz ni Teja na wakati mwingine kumpandisha teja jukwaani ni kunajisi jukwaa maana teja ni Kama shoga tu kwaiyo kumpandisha Chid kwenye jukwaa la heshima Kama Wasafi Festival ni kuikosea heshima jamii”.

Lakini pia kwenye mahojiano hayo Afande Sele alifunguka kupotea kimuziki kwa 20 Percent ambapo alihusisha na Clouds kuwabania wasanii hivyo wengi wao kuishia kupata stress na kupotea kimuziki.

Chid Benz Amwaga Povu Baada Ya Kukosekana Kwenye Listi Ya Wasafi Festival

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip hop nchini Chid Benz amefunguka na kuwamwagia Povu zito timu nzima ya WCB Baada ya kukosa mwaliko wa kufanya shoo kwenye Wasafi Festival.

Chid Benz amefungukia ishu ya Diamond Platnumz na Timu yake nzima ya WCB kutumia wanamuziki Kama Dudubaya ambaye anaamini amechaguliwa kwa sababu ya umaarufu wa jina lake Konki Konki konki Master.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, Chid Benz amedai amesikiyishwa kuwa Msanii Kama yeye Anayeimba vitu vya maana hajachaguliwa kwa madai kuwa anatumia madawa ya kulevya ilhali ameshaacha.

Sisi wasanii tunaoimba nyimbo ambazo zinabeba ujumbe na maana hatupati nafasi kabisa utasikia wanasema achana na hao wakina Chidi Benz wanakula unga ila Dudubaya kisa anasema konki konki anajaza watu basi nasibu anampa tour kwenye Wasafi Festival”.

Diamond na timu nzima ya WCB ilimchagua Dudubaya Kama mmoja wa wasanii watakaoshiriki katika tamasha la WCB Baada ya umaarufu alioupata kupitia jina lake la utani la Konki Master.

 

Jux Ajibu Tuhuma Za Kumdhulumu Chid Benz

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux ameibuka na kujibu tuhuma nzito alizotupiwa na msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Chid Benz alipodai kuwa amemdhulumu pesa alizopigia shoo.

Siku chache zilizopita Chid Benz alimtuhumu Jux kwa utapeli baada ya kudai kuwa aliperfom Kwenye shoo ya ‘In Love and Money Tour’ lakini hakumlipa hata senti pamoja na kwamba mashabiki waliikubali shoo yake zaidi.

Katika mahojiano yake na Enews ya EATV, Jux amefunguka na kudai kuwa Chid hakuwepo Kwenye listi ya wasanii ambao walitakiwa kuperfom bali alimfuata backstage:

Kwanza kabisa Chid Benz hanidai pesa yoyote kwa sababu ile Show kabla hata ya kufika Dar tulikuwa tumeshapanga wasanii watakaotumbuiza  hatukuwa na mdhamini kwaiyo hata wale wasanii waliotumbuiza Kuna vitu tuliwafanyia lakini hatukuwalipa hela na wengine walikuja kutusapoti tu kama wasanii wenzao.

Chid alinifuata backstage akasema anataka kufanya kitu kwa mashabiki na mimi nikamuheshimu kama braza mkubwa akapanda stejini akapiga shoo lakini kesho yake ananipigia simu ananiambia amelogwa shoo lakini hajapata kitu nikamwambia nitampa kitu kutoka mfukoni kwangu lakini haikuwa lazima nashangaa ameenda Kwenye vyombo vya habari”.

 

 

Chid Benz Alalamika Kutolipwa na Jux.

Msanii wa muziki wa hip hop nchini , Chid benz amefunguka na kulalamika sana kitendo cha Jux kushindwa kumlipa pesa yake baada ya kuperfom katika tamsha lao la Love and Money Tour ambalo lilikuwa likifanya katika mikoa mbalimbali akiwa na mpenzi wake Vannesa.

Chid benz anasema kuwa Jux ni msanii mkubwa na ana haki ya kuwasaidia wasanii wnegine kama yeye kwa sababu wote ni wana mzuki lakini haikuwa poa kama anaweza kumuomba mtu kufanya nae kazi kwa malipo alafu ghafla ashindwe kumlipa pesa waliokubaliana,

Tour hiyo ya wapenzi hao ina zaidi ya miezi sasa tangu kuisha kwake na wasanii mbalimbai walinufaika na tamasha hilo kwa sababu walipata pia fursa za kutembeala na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii na kukutana na amshabiki wapya .

Hata hivyo kwa kitendo icho, Chid benz anamtuhumu Jux na kusema kuwa haono mchano wa wasanii wengine katika muziki na ndio maana anafanya hivyo.

Chid Benz Akana Kuiga Staili Ya Nywele

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Radhi Makwiro maarufu kama Chid Benz amefunguka na Kukana kabisa tuhuma za kuiga staii yake mpya ya nywele.

Wikiend iliyopita Chid Benz aliibukia pande za Tandale ambapo alipiga shoo Kwenye charity event ya Msanii Diamond Platnumz ndipo alipoonekana kapaka rangi nywele zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers,  Chid Benz ametajwa sababu ya kupaka  nywele zake rangi na sio kwamba anawaiga wasanii wanaotoka katika jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) bali wakati wake umefika wa kubadilika kichwani.

Unajua watu wanafikra tofauti na kupenda kuongea mambo mengi, mtu anapofanya kitu wanahisi tu atakuwa amewaiga watu wengine lakini mimi nimeamua kufanya hivi kwa kuwa wakati kwa upande wangu umefika”.

Lakini pia Chid Benz alimpongeza Diamond kwa kusema amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuufikisha Muziki wa Bongo Fleva mbali.

Namuombea Diamond aendelee kupenda kazi yake kwani Muziki wa Bongo Fleva unafanya mengi mazuri tuu, kwa hatua alioifanya namuombea kwa Mungu azidi kufika mbali, mbali zaidi“.

 

TID Afungukia Madawa Ya Kulevya na Ajitolea Kumnyoosha Chid Benz

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed aka TID amefunguka kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya na changamoto katika muziki wake.

Siku za nyuma TID ameshawahi kushika headlines kwa kutumia madawa ya kulevya na hata kukiri kuwa alikuwa muhanga wa madawa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, TID amefunguka na kusema kipindi anatumia madawa ya kulevya alipoteza vitu vingi sana na anatamani kukabidhiwa rungu la kuwarekebisha wanaotumia madawa ya kulevya na alimtolea mfano Chid Benz.

Mimi nikabidhiwe Chid Benz nikae naye maana amekuwa akitusumbua kwa muda sasa kwa sababu wanampeleka rehab akitoka anarudia yale yale lazima kutakuwa kuna kitu wanakosea kama kweli wananmjali wafanye kitu tofauti kama hawamjali wamuache tu kama wanavyomuachaga.

Chid Benz is true talent and was a successful guy halafu tumekorofishana tu alivyoingia kwenye vitu hivyo halafu mimi namuona kama bado ana nafasi kama binadamu hakuna mtu ambaye anafeli akafurahi”.

Siku za nyuma TID ameshawahi kushauri Chid Benz akanatwe na achapwe ndio atasikia na kuacha madawa kwani watu kadhaa wameshajatibu kumpeleka rehab lakini amekuwa akirudia madawa wakati wote.

Nina Sifa Zote za Kuwa Mke wa Chid Benzi:- Mariam

Watu wengi walikuwa wakiamini kuwa msanii Chid Benz hana mke wala familia inayomtegemea wala kuwa nayo karibu zaidi ya mama yake mzazi na kwamba msanii huyo amekuwa akiishi kwa mama yake miaka yote ya usanii na hata baada ya madhira anayomkumbana nayo kila siku.

Lakini kumbe sio kweli kwa sababu msanii huyo anakaa na mke wake ambae amekuwa nae bega kwa bega tangu kipinid hicho cha zamani mpaka matatizo yanayomkumba Chid amekuwa ane hakuwahi kumuacha na hii yote ni kuahakikisha kuwa Chid yuko salama.

Wakiwa mkoani morogoro, chid benz alionekana nawatu mbalimbali hata waandishi wa habari akiwamweny afya na furaha sana na mke wake huyo pamoja na kwamba hapo katikati kulikuwa na picha zilizosambaa kwamba msanii huyo kwa sasa hali yake ni mbaya.akiongea na waandishi mariamu anasema

Ni mwanaume mwenye mapenzi ya dhai na amekuwa akinijali muda wote,huwa najisikia vibaya sana asipokuwa karibu na mimi na nimekuwa nikimsaidia sana  kutegemea na kipindi hicho kuna kuwa na kitu gani.ni mwanaume wa peke tofauti na vile watu wanavyomfikiria na kwakweli mimi ndio mkali wake, nawaoma mashabiki waendelee kumsapoti katika muziki wake.

Tumekuwa wachumba kwa takribani miaka 10 sasa na tumebahatika kupata mtoto mmoja na Mungu akipenda mwakani tutafunga ndoa, nina sifa zote za kuolewa na yeye.

 

Chid Benz Aitabiria Makubwa Bongo Fleva Ya Sasa

Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Dar Es Salaam Stand Up’ amefunguka na kudai anaona kuwa Bongo fleva ya sasa inazidi kufika mbali tofauti na zamani.

Chidi Benz amedai kuwa kwa jinsi anavyoona sasa wasanii wa Bongo fleva wamekuwa wanajituma sana tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma kwa wasanii wengi.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Chid Benz amesema kuwa, muziki wa Bongo Fleva una­piga hatua siku hadi siku kutokana na wasanii wanavyojituma, hivyo utafika mbali zaidi.

Muziki wa Bongo Fleva un­aweza kufika mbali zaidi kwa kuwa wasanii wanaonekana kujituma zaidi, kila siku ki­nakuja kitu kipya, wanaonye­sha uwezo mzuri wa kuhitaji kufika mbali“.

Kadri miaka inavyozidi Kisonga mbele ndivyo sanaa ya Bongo fleva imezidi kupiga hatua na Kusonga mbele zaidi kutokana na wasanii kupata changamoto kutoka kwa wasanii wengine.

Chid benz Akanusha Kuwa na Bifu na Harmonize, Aongelea Mahusiano Yake na Wasanii Wenzake.

Msanii wa muziki wa siku nyingi Chid benz amefunguka na kuongelea mahusiano yake na msanii anaefanya vizuri sasa hivi katika sanaa ya bongo fleva Harmonize na kusema kuwa hakuna tatizo kubwa kati yake na Harmonize .Na hata kama litakuwepo , anaogopa hata watu watamshangaa na kumuona kuwa yeye ana wivu.

Hakuna tatizo kati yangu na harmonize na sdhani kama kutakuwa na tatzio lolote,na kama kutakuwa na tatizo kati yangu na harmonize lazima watu watanishangaa.kama kutakuwa na ugomvi  kati yangu na yeye basi ujue kuwa watu wanaweza hata kusema kuwa mimi nina mawivu yangu tu.

Lakini pia ninachoshukuru  ni kwamba karibia wasanii wote  wananipa respect sana mimi,mimi sinaga ubaguzi na mtu yoyote , kwa sababu mimi naongea na kila mtu, na nina heshimu kila mtu pia. 

Lakini pia Chid benz amefunguka na kusema kuwa yeye ni moja ya wasanii wasiopenda unafiki hata siku moja na ndio maana kila mtu anapofanya kosa huwa anataka kuonana na mtu husika na kumwambia moja kwa moja na wala hana kujificha wala kusema nje na pale ulipo.

Chid anasema kuwa pamoja na kwamba wasanii wengi wamekuwa na tabia ya kuchukuliana poa na kudharauliana lakini kwake hiyo hana na siku zote mtu akifanya kinyume na vile inavyopaswa kuishi basi na yeye hana budi kumwambia ukwlei kwa sababu hawezi kuficha ukweli.