TID Atangaza Kulikacha Jina La ‘Mnyama’

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khaleed Mohamed maarufu kama Top in Dar ‘TID’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kuanzia Hivi sasa hataki kutumia jina la ‘Mnyama’.

Kama utakumbuka siku za nyuma moja ya majina ya TID (a.k.a’s) ilikuwa ni jina la Mnyama Lakini TID aliingia kwenye mgogoro na baadhi ya wasanii huku kisa kikiwa ni jina hilo.

TID amewahi kugombania jina na Diamond Platnumz ambaye alikuwa anajiita simba Lakini pia aligombania jina na Dudubaya ambaye anajiita Mamba Lakini pia aligombania jina Mr. Blue.

Lakini hatimaye TID kaweka siku zake za kugombania jina nyuma yake kwani ametangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kuanzia Hivi sasa hataki hata kulisikia jina hilo:

Proudly Tanzanian music straight from the roots of Bongo fleva…..Naitwa TID kuanzia leo sitaki kuitwa mnyama kila mtu kawa mnyama sasa hivi sina unyama wowote I am a changed person…Niiteni Top tu kama zamani please tusije gombana mimi sio mnyama wowote ni binadamu wa kawaida tu”.

 

“TID Sio Baba Wa Mtoto Wangu, Prezzo Ndiye Baba”- Shekha

Mwanamke anayejulikana Kama Shekha ambaye Wiki iliyopita alitengeneza headlines Baada ya kudai    msanii mkongwe wa Bongo fleva T.I.D sio baba wa Mtoto Wake ingawa amekuwa aking’ang’ania hivo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa Wikienda, kwa njia ya simu akiwa nchini Ujeru­mani, Shekha alisema kuwa anam­shangaa T.I.D anavyokomaa kwamba mtoto ni wa kwake wakati baba halisi ni mwanamuziki wa nchini Kenya, Joseph Makini ‘Prezzo’.

Nimenyamaza kwa muda mrefu lakini sasa nimeshindwa kabisa kuen­delea kuvumilia ndiyo maana naweka wazi na TID ajue kuwa mtoto siyo wake bali ana baba yake.

Uzuri ni kwamba Prezzo ambaye ndiye baba wa mwanangu naye ni mwanamuziki hivyo kama TID anataka amuulize mwenyewe atapata jibu kuhusu nani anastahili kuitwa baba wa mtoto”.

Lakini pia Shekha alimtaka T.I.D kuendelea na maisha yake na yeye aendelee na maisha yake pamoja na mtoto wake kwa sababu hata baba yake ambaye ni Prezzo anamuhitaji pia hivyo waachane kwa usalama hataki malumbano kwani yeye ndiye alisababisha mpaka mambo hayo yakafikia hapo yalipo sasa.

Haya mambo yasingefika huku ila TID ndiye aliyesababisha maana anang’ang’ania vitu ambavyo siyo vyake, naomba aniache jamani na mai­sha yangu huyu mtoto ni wa Prezzo nimemaliza“.

 

TID Afungukia Sekeseke La Kudhulumiwa Mtoto

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khaleed Mohamed maarufu kama T.I.D amefunguka na kuweka wazi kuwa taarufa zinazosambazwa na mzazi mwenzake kuwa Mtoto sio Wake sio za kweli.

Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la shekha ametengeneza headlines siku chache zilizopita baada ya kumkataa TID kama baba wa Mtoto Wake na kumtaka Msaniii kutoka Kenya Prezzo kama baba Watoto Wake.

Shekha amemtaka TID kukaa mbali naye na Mtoto Wake kwani anajua wazi kuwa yeye sio baba wa Mtoto huyo hivyo aendeleee na maisha yake na amuache yeye na Prezzo wamlee Mtoto wao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, TID ameendelea kushikilia  msimamo wake kuwa mtoto huyo ni wake hata aje nani anachojua ndiyo hicho na si kitu kingine chochote.

Jamani hata aseme nini mtoto ni wa kwangu yeye ataongea mpaka basi lakini ajue mtoto ni wangu hata mtoto atakuwa anajua, huyo Shekha anajidanganya nafsi yake mwenyewe”.

 

 

TID na Mzazi Mwenzake Vitani Kisa ‘DNA’ Ya Mtoto

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva khaleed Mohamed ‘TID’ na mzazi mwenzake Shekha Small wamejikuta katika vita ya maneno Baada ya kutofautiana katika suala la DNA (vinasaba) vya Mtoto wao.

Global Publishers wanaripoti kuwa Wawili hao wameingia kwenye mvutano baada ya kila mmoja kutoa msimamo tofauti kuhusu unasaba wa mtoto wao huyo, ambapo TID anasema ni mtoto wake, wakati mama mtu akikanusha vikali.

Kwenye mahojiano na Gazeti hilo, Shekha ambaye kwa sasa anaishi Ujerumani, alisema kuwa  anachukizwa na namna TID anavyotangaza kuwa mtoto huyo ni wake, wakati siyo kweli.

Unajua huyu TID nahisi hayo madawa anayotumia (hajafafanua ni dawa za nini) yameshaanza kumuharibu, huyu mtoto sio wake kwa sababu nilishapima mpaka DNA na baba mzazi wa mtoto huyu ambaye makazi yake yapo hukohuko Bongo na majibu yakaonesha kwamba mtoto sio wa TID sasa kinachomfanya amng’ang’anie ni nini?”.

Kiukweli mimi ninachoomba TID amtoe kabisa huyu mtoto akilini mwake, kwa sababu kwanza mwanangu hajui hata kama ana baba anaitwa TID na tulishaondoka huko Tanzania tangu binti yangu akiwa na umri wa mwaka mmoja na miezi kumi… na sasa ana miaka mitatu, atakuwa ameshamsahau kabisa.”

Kwa upande wa TID alifunguka na kusema kuwa anachokifahamu na hakitabadilika akilini mwake ni kwamba Tania ni mtoto wake.

Huyu mwanamke ananishangaza sana, kwa sababu mimi ninachojua huyo mtoto ni wangu na mpaka kuondoka kwake hapa mimi ndio nilikwenda ubalozi kusaini ndio mtoto akapata Visa ya kusafiri.

Sasa simuelewi anavyosema nikae mbali na yule mtoto, isitoshe mimi nina mpaka ushahidi wa vyeti. Tania ni mwanangu na atabaki kuwa mwanangu siku zote”.

TID Ajikanyaga Kutoa Majibu Kuhusu Ushirikina

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama Top In Dar, TID amejikuta akipata kigugumizi pale alipotandikwa maswali kuhusu mambo ya kishirikina.

Siku za hivi karibuni topic ambayo imekuwa ikitrend Kwenye mitandao ya kijamii ni suala zinasambaa la uchawi ambapo watu maarufu wamekuwa wakinyosheana vidole kuhusu ushirikina.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari, TID alipoulizwa kuhusu uchawi alishindwa kutoa jibu la moja kwa moja na kuishia kupata kigugumizi na kudai haamini uwepo wa masuala ya ushirikina katika muziki hususani kwa wasanii, kwa sababu hajawahi kuona wala kuletewa ushahidi kuhusu mambo hayo.

Nikiulizwa swali kama hilo, mnanichanganya maana mimi sina utaalam wa hayo mambo. Nitafutieni ushahidi niufanyie upembuzi ili niweze kujua kama kweli washirikina wapo au laa”.

Lakini pia Msanii mwingine wa Bongo fleva Dayna Nyange alipotandikwa swali hilo hilo aliweka wazi kuwa uchawi upo kwa sababu hata kwenye vitabu vya dini imeandikwa hivyo.

Uchawi upo kiukweli, itabidi nimtafute TID ili niongee naye kwanini hajui masuala ya ushirikina”.

Siku mbili hizi zilizopita Hamisa Mobetto ametrend sana Kwenye mitandao ya kijamii kwa kutuhumiwa kuwa anafanya mambo ya kishirikina.

TID Afungukia Madawa Ya Kulevya na Ajitolea Kumnyoosha Chid Benz

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed aka TID amefunguka kuhusu matumizi ya madawa ya kulevya na changamoto katika muziki wake.

Siku za nyuma TID ameshawahi kushika headlines kwa kutumia madawa ya kulevya na hata kukiri kuwa alikuwa muhanga wa madawa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, TID amefunguka na kusema kipindi anatumia madawa ya kulevya alipoteza vitu vingi sana na anatamani kukabidhiwa rungu la kuwarekebisha wanaotumia madawa ya kulevya na alimtolea mfano Chid Benz.

Mimi nikabidhiwe Chid Benz nikae naye maana amekuwa akitusumbua kwa muda sasa kwa sababu wanampeleka rehab akitoka anarudia yale yale lazima kutakuwa kuna kitu wanakosea kama kweli wananmjali wafanye kitu tofauti kama hawamjali wamuache tu kama wanavyomuachaga.

Chid Benz is true talent and was a successful guy halafu tumekorofishana tu alivyoingia kwenye vitu hivyo halafu mimi namuona kama bado ana nafasi kama binadamu hakuna mtu ambaye anafeli akafurahi”.

Siku za nyuma TID ameshawahi kushauri Chid Benz akanatwe na achapwe ndio atasikia na kuacha madawa kwani watu kadhaa wameshajatibu kumpeleka rehab lakini amekuwa akirudia madawa wakati wote.

TID Awashukia Diamond na Wasanii Wengine Wanatumia Jina La Mnyama

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amewatolea povu Wasanii Wenzake kama Diamond na wasanii wengine wengine ambao wamekuwa Kwenye mgogoro juu la majina ya wanyama na kudai yeye ndiye mwanzilishi.

Siku za nyuma ulishawahi kutokea mgogoro wa majina baina ya wasanii ambapo baada ya Diamond kujiita simba wasanii kadhaa walidai wao ndio walikuwa simba kabla yake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, TID amefungukia wasanii wanaojiita wanyama na kudai wao wamemuiga yeye kwani alipewa jina la Mnyama miaka kumi iliyopita:

Mimi jina la mnyama nimepewa miaka kama kumi iliyopita ndio maaana sasahivi unaona kuna wanyama wengi wanajitokeza tokeza because they like the swagg, they feel the swagg, they feel the talent.

Walikuwa wanataka kuwa mimi huko nyuma na wanataka kuwa kama mimi mpaka leo, so Mnyama is my brand yaani nikitokea watu wanajua Mnyama halafu ndio wengine wanakuja sijui petty anaimals sijui domestic animals”.

 

Bill Nas Hawezi Kumfikia Ngwea- TID

Mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva khalid Mohamed na maarufu kama TID ameibuka na kuweka wazi kuwa marehemu Ngwea alikuwa msanii mkali hata Bill Nas hawezi kumfikia.

Ikiwa ni siku chache tangu Ngwea atimize miaka kadhaa tangu Kifo chake TID ambaye alikuwa rafiki yake mkubwa ameweka wazi kuwa pengo lake halitaweza kuzibwa na msanii yoyote.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari TID amesisitiza hata Bill Nas hajaweza kumfikia Ngwea kwa kipaji alichokuwa nacho enzi za uhai wake:

Hakuna msanii anayeweza kumfikia Ngwea that man was special Ngwea alikuwa blessed alafu umfananishe na nani? Bill Nas anaweza kuwa a half of it lakini hawezi kuwa kama Ngwea, Ngwea can rap Ngwea can sing Ngwea can give you melody halafu unataka kumfanisha na mtu? Hakuna wa kufanana naye”.

TID na Billnas walishawahi kuwa Kwenye bifu zito miaka ya nyuma lakini bifu hilo lilimalizika baada ya kutoa pamoja wimbo unaoitwa ‘Ligi Nzito’.

TID- Kuna Watu Wanataka Kumshusha Diamond

Mkongwe kwenye muziki wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amefunguka na kuwatolea povu baadhi ya media ambazo zinadai a kumshusha staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

TID amedai kuwa kwa muda mrefu kumekuwa kuna utaratibu wa wadau wa muziki wa Bongo fleva kujaribu au hata kumshusha kabisa msanii pale anapothubutu kudai maslahi yake jambo ambalo amedai linaua muziki.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, TID amejilinganisha na Diamond na kudai hata yeye ilishawahi kumtokea Kwenye muziki wake ambapo kuna baadhi ya vyombo vya habari vilijaribu kumshusha.

Na kweli anaweza because he has a media, yaani yeye ndio kama Mungu anajiona but mimi hapana. Nilifanya kosa hilo lakini kosa hilo ndilo limewasanua wasanii wengine, unaona msanii kama Diamond naye amekataa.

So Diamond was me lakini wakasema wewe siunajifanya mjanja sasa tunamleta Diamond tukushushe wewe. At the end Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani,” TID ameiambia Wasafi TV“.

Diamond ni moja kati ya wasanii ambao wamekuwa Kwenye migogoro na baadhi ya vyombo vya habari kama Clouds Fm na East Africa Tv ambavyo havipigi kabisa nyimbo zake.

Tangu Mangwea Amefariki Sijawahi Kupata Rafiki Wa Kweli-TID

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kama TID amefunguka na kuweka wazi kuwa hajawahi kupata rafiki kama aliyekuwa msanii mwenzake Marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’.

TID amefunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv ambapo alisema mwaka huu hakufanya Tamasha la kumkumbuka kwa sababu imekuwa katika mwezi Mtukufu wa ramadhani.

Ni kweli kila mwaka huwa tunafanya tamasha hilo kwa sababu tunakuwa na sababu na pia na uwezo lakini mwaka huu kitu kilichotufanya mpaka hatufanya tamasha letu ni Ramadhani ambayo imetubana na kusema kweli tupo kwenye swaumu.

Lakini pia TID aliwatolea povu watu ambao amewaita Masnich ambao walijitokeza wakati Mangwea alipofariki:

Mangwea alipofariki watu kibao walijitokeza na wengine kabisa wapo frontline wanachangisha wakati Ngwea yupo hai hawakumpa tamasha hata siku moja haya leo hii Ngwea hayupo hakuna hata mtu mmoja aliyesema tumuenzi Ngwea watu wana roho mbaya na masnich .

Wasanii kibao unaowaona leo ni masnitch tu nawaangalia sana ndio maana siwezi hata kuwa na ukaribu nao sina marafiki sahivi wala sitakuja kupata rafiki kama Ngwea”.

Mangwea alifariki dunia miaka mitano iliyopita na alikuwa rafiki wa karibu sana wa TID.

TID Amtupia Dongo Diamond Kwa Kujiita Simba

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Khalid Mohamed maarufu kwa Jina la usanii kama Top In Dar (TID) amedai yeye ndiye mwanzilishi wa jina la mnyama.

Hivi siku za karibuni kumekuwa na ugomvi wa marina baina ya wasanii kama juzi tu Afande Sele kamaliza mgogoro na Diamond kisa jina la Simba ambalo kila moja alidai la kwake.

TID ameibuka na kudai yeye ndiye mwanzilishia wa kutumia jina la Simba na hata kudai jina hilo alipewa na mashabiki zake kwa sababu ya kazi zake anazofanya akiwa stejini.

Kwenye mahojiano na kipichi cha On The Street cha ETV, TID amefunguka haya kuhusu jina hilo la mnyama:

Kwa mfano mimi perfomance zangu wanasema ni kali, yaani za kinyama, kwahiyo mimi nilikuwa nafanya kinyama ndipo mashabiki walipo amua kunipa jina la mnyama, mpaka sasa mimi ni mnyama kutoka unyamani.

Lakini sio mbaya sasa hivi nasikia kuna wengine wanajiita Simba, nimewa-inspire kuwa hivyo, kuna wengine ni wakufungwa, lakini ndio mnyama wenyewe”.

TID hana uhusiano Mzuri na WCB kwa ujumla kwani wiki chache tu zilizopita alitoka kutoa povu kwa Wasafi baada ya kudaiwa alikuwa anaomba kazi.

Wasanii Wengi Wanaoa Ili Kutafuta Kiki- TID

Msanii mkongwe wa Bongo fleva TID amewatolea povu zito wasanii wenzake wanaotangaza ndoa na kuoa ili mradi tu watengeneza kiki kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na trend ya wasanii wengi wa kiume kuoa hasa nje ya nchi kwa wasanii kama AY ambaye ameoa Rwanda na Ali Kiba ameoa Kenya, TID amedai hawana lolote zaidi ya kutafuta kiki.

Lakini pia TID amewatolea uvivu wasanii ambao wamekuwa wakitangaza kuwa wanataka kuoa lakini kiuhalisia hamna kitu mpaka leo hawajao zaidi walipata kiki za bure na katika hilo TID hakusita kumtaja swahiba wake Q chief ambaye alishawahi kutangaza ndoa siku za nyuma.

TID amefunguka hayo Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews ya  EATV baada ya kupita takribani siku 24 tokea msanii huyo kutangaza wazi kuwa yupo katika mahusiano na mwanadada mmoja ambae alikuwa nae nchini Germany jambo ambalo wengi wao walitarajia kuoa ndoa ikifuata katika siku za usoni.

Sijasema kama ninaoa mwezi wa sita (Juni) ila tulikuwa tunajifurahisha mimi na rafiki yangu usingizi katika ‘comment’ instagram ilikuwa utani tu sijafikilia kuwa hivyo. Unajua sasa hivi watu wanataka kutengenezea kama kiki kitendo cha kuoa, kwa hiyo mimi sio mtu kutafuta kiki kwa kutumia ndoa”.

 

TID Amwaga Povu Zito Baada Ya Kuhojiwa Kuhusu Mpenzi Wake Aliyemvisha Pete

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva TID ametoa povu zito mara baada ya Kuhojiwa kuhusu Mahusiano Yake na mwanamke wake aliyemvisha pete miaka nane iliyopita.

TID na Kinana walikuwa Kwenye Mahusiano ya miaka mingi na siku ya wapendanao mwaka 2010 TID alimvisha Pete mchumba wake huyo mbele ya mashabiki zake kwenye shoo aliyokuwa anapiga.

Mwanamuziki huyu anayetamba na ngoma ‘Wewe Dada’ katika mahojiano na E-Newz ya EATV alisema hapendi kuzungumzia mambo ambayo tayari yameshapita.

Hiyo sasa it’s very long time, i am not here to discus about my past, you should know that, usipenda kufuatilia mapenzi ya watu hilo ndio tatizo lako“.

Siku za hivi karibuni TID amekuwa akirusha picha Mtandaoni akiwa na mwanamke mwingine huku a kuweka wazi kuwa wapo Kwenye Mahusiano ya kimapenzi.

Ben Pol Arudisha Mapigo Kwa TID na Kudai Amemkosea Heshima

Wasanii wa mziki wa Bongo fleva TID mnyama na Ben Pol wamejikuta kwenye bifu zito baada ya TID kumtolea povu zito Ben Pol baada ya kuimba nyimbo yake kwenye tamasha la Fiesta lililofanyika wikiend iliyopita.

TID alimjia juu Ben Pol baada ya kuimba kiitikio cha wimbo wake wa ‘Nyota yangu’ katika tamasha la Fiesta bila ruhusa yake ambapo TID alikiambia kituoa cha redio cha East Africa kuwa ana mpango wa kuzungumza na wakubwa wake pamoja na wanasheria ili kumchukulia Ben Pol hatua za kisheria kwa kuiba nyimbo yake.

Kwenye mahohiano aliyofanya na Bongo 5, Ben Pol amemtaka msanii huyo mkongwe kumuomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa:

Unajua kilichotokea ni kwamba wimbo wangu wa moyo mashine unaendana na nyota yangu kwa sababu zote zina miondoko ya Zhouk kwaiyo yaani pale nilikuwa kama nampa heshima fulani hivi yeye na mziki wake. Kwanza kiukweli kabisa TID ni msanii aliyeni-insipire mimi mpaka nikaanza kuimba mimi nipo shule ya msingi nasikiliza albamu ya sauti ya dhahabu naiimba yote yaani pale ndipo Ben Pol alipozaliwa kwaiyo nilishangaa yeye kuwaka mimi kuimba kionjo cha nyimbo yake wakati yeye ni staa na ni msomi kama nsanii anaelewa hizo mambo zipo lakini sikutegemea msanii mwenye heshima yake Kama yete anaweza kufanya kitu kama mile kusema kweli I am very confused”.

Lakini pia Ben Pol amekiri kuwa hawezi kumlaumu sana TID kwani hawezi jua wakati anafanyaile interview alikuwa katika hali gani na anaamini akikaa akitulia amtafute Ben Pol amuombe  radhi kwa kitendo alichofanya kwani yeye anajua hakikuwa sawa kabisa.

T.I.D Kuingia Kwenye Siasa Mwaka 2020

Msanii mkongwe wa bongo fleva nchini  Mohamed Khalid mwenye jina la umaarufu kama T.I.D amefunguka na kusema kuwa kwa sasa anafikiria kuingia katika siasa na mwaka ujao wa uchaguzi anampango wa kugombea ubunge.

Msanii huyo amesema kuwa mwaka 2020 anampango wa kugombea ubunge katika jimbo la Kinondoni, jimbo ambalo kwa sasa linaongozwa na Maulid Mtulia.Hata hivyo  akiongelea sababu za yeye kutaka kugombea ubunge msanii huyo alisema kuwa kitu cha kwanza ni kwamba yeye ni mzawa wa jimbo hilo la Kinondoni hivyo amekuwa akijua matatizo yanayotokea na yanayoendelea kutokea jimboni hapo.

Hata hivyo T.I.D anasema kuwa msukumo mkubwa wa yeye kugombea ni kwa sababu anaona kabisa kuwa mbunge aliepo sasa hajaweza kutimiza na kutatua matatizo ya wananchi,T.I.D  anasema kuwa atakapogombea na akashinda  anaamini kabisa kuwa atatimiza na kutatua matatizo ya wananchi wa jimbo ilo.

T.I.D alipokuwa akiongea na chombo kimoja cha habari alisema kuwa moja ya tatizo linalomfanya awe na hamsa ya kugombea ubunge ni tatizo la vijana kujiingiza katika madawa ya kulevya, tatizo analoliona kuwa ni sugu na anatamani kuliondoa.Msanii huyo ambae pia  kwa muda mrefu alikuwa kimya katika muziki kwa sababu ya matumizi ya madawa ya kulevya alikuja  kuachana nayo   baada ya kukubali kupata msaada kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam aliyeanzisha vita ya kutokomeza madawa ya kulevya, hivyo kwa msanii kama yeye ambae alipitia huko na akatoka na  anaona vijana wengine wanavyoendelea kuharibika ni dhahiri kuwa anaumia na ana nia ya kusaidia wengine.

Wasanii wengi sasa wamekuwa wakijitokeza kujiingiza katika siasa na wamefanya vizuri katika swala hilo, wasanii kama Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya Mjini na Joseph Haule mbunge wa Mikumi wamekuwa chachu na amasa kwa vijana hasa wasanii ambao pamoja na kuwa katika tasnia ya muziki lakini pia wanaweza kufanya vizuri katika siasa. Hivi karibuni , msanii Nikki wa Pili kutoka kundi la Weusi pia alisikika akitangaza kuhusu nia yake ya kugombea ubunge kwa mwaka ujao wa uchaguzi, hii inaonyesha ni jinsi gani vijana wamekuwa na chachu ya maendeleo

 

Bifu ya wasanii wakongwe: Q Chief amchana TID

Q Chief anadai kuwa msanii mwenzake mkongwe – TID ako na matatizo ya kisaikolojia. Chief amesema haya baada ya kugadabishwa na tabia ya TID.

Akiongea na Times FM, Q Chief alieleza kuwa chanzo cha bifu yake na TID ni tabia ya msanii huyo kufwatilia maisha ya watu wengine huku akiacha kupambana na hali yake.

Q Chief

Chief alimshauri TID kuwa ni bora angejitahidi kuangalia jinsi ya kurudi kwenye muziki badala ya kujishugulisha kuzungumzia vitu visivyomuhusu.

“Mimi naona kama watu wazima kila mtu angelia na hali yake na kuangalia jinsi gani anaweza kurudi kwenye sehemu yake, Kwahiyo mimi huwa nachukulia kwanini niwe tatizo kwa mtu mwingine? nahisi kuna kitu special umekiona kwangu na hutaki kuniambia utakuwa unamatatizo. TID anamatatizo ya kisaikolojia hivyo anatakiwa ajitathmini kiundani, kama mpaka waheshimiwa wameamua kukusaidia lazima uoneshe muelekeo ili waendelee kukusaidia,” amesema Q Chief