Diamond ni Kama Taifa Stars :-Afande Sele

msani wa muziki mkongwe kutoka Morogoro Afande sele amefunguka na kusema kuwa amekuwa aiumisana anapoona kuwa msanii mkubwa na mwenye mafanikio kama Diamond platinumz anakuwa akitukanwa na kudhalishwa katika mitandao ya kijamii,

Akiongea na waandishi wa habari, Afande Sele amefunguka na kusema kuwa kwa thamnai aliyonayo Diamond Tanzania ni kama timu ya taifa inapokuwa inawakilisha nchini hivyo kwake yeye anapoona watu wanamuandama Diamond anakuwa  anaumia sana.

Afande sele anasema “Diamond ni kama taifa stars, akitukanwa mimi anaumia sana ”

 

Chid Benz ni Teja Hawezi Kupanda Kwenye Steji Ya Wasafi- Afande Sele

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini Afande Sele amefunguka na kuweka wazi kuwa Msanii mwenzake Chid Benz hawezi kupandishwa Steji ya Wasafi Festival kwa sababu ni teja.

Wiki iliyopita Chid Benz ambaye amekuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu sasa alilalamika kitendo cha kutoalikwa Kupanda Steji ya Wasafi na Kuperfom na kudai kuna wasanii wasio na vipaji wanapendelewa.

Afande Sele ameibuka na kudai Chid Benz hawezi kupandishwa katika Steji ya Wasafi Festival kwani ni teja hivyo mtu Kama huyo ataleta

Niseme tu ukweli ni kwamba Chid Benz ni Teja na wakati mwingine kumpandisha teja jukwaani ni kunajisi jukwaa maana teja ni Kama shoga tu kwaiyo kumpandisha Chid kwenye jukwaa la heshima Kama Wasafi Festival ni kuikosea heshima jamii”.

Lakini pia kwenye mahojiano hayo Afande Sele alifunguka kupotea kimuziki kwa 20 Percent ambapo alihusisha na Clouds kuwabania wasanii hivyo wengi wao kuishia kupata stress na kupotea kimuziki.

“Wasafi Festival ni Tamasha Kubwa Halijawahi Tokea Tanzania”-Afande Sele

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva nchini Afanse Sele ameibuka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hakuna msanii mkubwa Kama alivyokuwa Diamond na hivyo tamasha lake la Wasafi Festival ndio litafunika.

Suala hili limekuja kutokana na sakata linaloendelea kupamba moto hivi sasa la mabishano ya Nani zaidi kati ya Wasafi Festival na Tamasha la Clouds la Fiesta.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo kimoja cha habari, Afande Sele ameibuka na kusema hivi sasa Tamasha kubwa sana Tanzania ni Wasafi Festival na halina mpinzani kumaanisha Fiesta linakalishwa na Wasafi.

Unajua hivi sasa Wasafi ndio Real Madrid ya Tanzania ndio tamasha bora  na linaonekana kuja kuwa kubwa kuliko yote kwaiyo kushiriki katika tamasha la Wasafi ni fahari na pia naunga mkono juhudi za wadogo zetu ambao wameamua kukata minyororo ya watu waliokuwa wanatufanya watumwa na kutunyanyasa kwaiyo Wasafi ndio mapinduzi ya burudani kwanza inaongozwa na wasanii wenyewe”.

Lakini pia Afande Sele amewatolea Povu zito Clouds Fm na kuwatolea tuhuma za kutumia nguvu zao na cheo chao kuwanyanyasa wasanii na kuwataka wafanye vile wanavyotaka wao.

Afande Sele Awapa Makavu Wanaume Vibenteni

Mwanamuziki Mkongwe wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap Afande Sele amewatolea uvivu wanaume wote wanaopenda kulelewa na wanawake.

Vijana wa kiume wamekuwa na mtindo wa kutafuta wanawake waliwazidi umri na kulelewa kwa majina wanaitwa Marioo au Vibenteni.

Afande Sele amewatolea uvivu wanaume hao na kudai wanaume wote wanaopenda kulelewa wanaishia kupoteza nguvu zao za kiume.

Tabia ya vijana kupenda kulelewa inawanyima uhuru binafsi, uwezo wa kufikiria unapungua kwa sababu unajikuta muda mwingi unawaza kumfurahisha mtu mwingine na ndio maaan unaweza kukuta hata kufanya mapenzi hujisikii na Kitendo hiko kinasababisha kwa asilimia kubwa kwa kukosa nguvu za kiume na matokeo yake inapelekea kununua dawa za kuongeza nguvu za kiume”.

Kwa sasa imekuwa jambo la kawaida hasa kwa hapa mjini vijana masharobaro wasiopenda kufanya kazi huamua kujitafutia mashuga mama wa kuweza kuwapa huduma mbali mbali.

Afande Sele Atoa Wosia Siku ya Kifo Chake kwa Watoto Wake

Msanii mkongwe kutoka Morogoro Afande Sele ametoa wosia kwa watpto wake kuwa undapo atakufa wasiamamie maiti yake isizikwe bali achomwe moto kwa sababu anataka kubaki majivu.afande sele amewaomba watoto wake ilo ikiwa kama zawadi ya watoto hao kwa baba yao kwa sababu ya malezi anayowapa wakati huu yuko hai.

kila muda ninapopata nafasi ya kuongea na hawa mabnti zangu wawili huwa nataka kuwakumbuka kuwa yote ninayoyatenda chini ya jua ni jukumu langu, na pia ni haki yao lakini kitu kikubwa wanachoweza kunilipa ni kuhakikisha kuwa siku yangu ya mwisho nikifa wasiruhusu kivyovyote mwili wangu kuzikwa au kufukiwa  udongoni bali zawadi kubwa  na iliyobora wanapaswa kunipa ni kuhakikisha mwili wangu unateketezwa kwa moto na kubaki majivu ambayo ndio watayazika ardhini na kubaki alama pale nilipolala mimi usingizi mizto usiokuwa na ndoto…maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua..usiofu tufanane.

Hi sio mara yake ya kwanza msanii huyo kusema hivyo na sasa ameonekana kutilia mkazo huku akisema kuwa kwa upande wake yeye hana dini.

Afande Sele Aukacha Upinzani na Kujiunga na CCM

Mwanamuziki mkongwe na rapa wa muziki wa Bongo fleva Afande Sele ajivua rasmi upinzani siku ya leo na kuhamia chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM).

Afande Sele amejiunga rasmi leo na CCM mbele ya mwenyekiti wa Chama hicho na Raisi wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli leo Machi 15, 2017.

Afande Sele amefunguka na kudai kuwa sababu kubwa iliyompelekea  kuhamia Chama tawala ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli katika kupambana na rushwa na kuwajali wanyonge.

Lakini pia Afande Sele amewaomba wanachama wa Chama hiko kumpokea kwa mikono miwili na kumuonyesha ushirikiano katika kujenga nchi yetu na kuonyesha sapoti kwa raisi na serikali kwa ujumla.

Afande Sele kabla ya kujiunga na CCM alishawahi kuwa mwanachama wa CHADEMA na Chama cha ACT Wazalendo ambapo mwaka 2015 alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo.

Afande Sele Aipongeza Serikali kwa Kuwafungia Wasanii.

Msanii mkongwe wa muziki  bongo ambae kwa sasa ameacha kufanya kazi za muziki Afande Sele leo amefunguka na kuipongeza serikali kwa hatua waliochukua ya kuwafungia wasanii ambao wanatoa nyimbo ambazo hazina maadili katika jamii.

Afande Sele alisema  kuwa kuna wasanii ambao alikuwa akiwaona alijua kuwa watakuja katika tasnia kuendeleza muziki huu vizuri lakini kitu cha ajabu ni kwamba wamekuwa wa kwanza kuimba nyimbo za matusi na kuuharibu muziki kabisa.

Wasanii wa sasa hivi wanaimba sana mapenzi, ngono, kubakana,pombe ,ndoa kuvunjika, na mambo ya kunajisiana tu.

Nasikitika sana kuona kuwa wasanii ambao nilidhani watakuja katika tasnia  kuwa warithi wetu kwenye vipaji  vya hip- hop lakini   wamebadilika leo ndio wanaimba  matusi ya kijinga.

Pongezi za Afande Sele zimekuja  baada ya serikali kupitia naibu waziri wa habari kuwafungia baadhi ya wasanii na nyimbo zao kutokuchezwa katika vituo mbalimbali vya habari kutokana na kutokesana kwa maadili .Hata hivyo baraza limesema kuwa halitaishia hapo katika kufungia wasanii wanaoimba vitu visivyo na maaadili badala yake wapo kwenye mhkato wa kuchunguza nyimbo zingine zenye mapungufu pia.

“Afande Sele Ana Stress Zake Anatafuta Pa Kutokea”- Vanessa Mdee

Mwanamuziki wa Bongo fleva Vanessa Mdee anayefanya vizuri kwenye gemu amefunguka na kudai kuwa msanii mkongwe wa Bongo fleva Afande Sele ana stress zake binafsi ndio maana anatokwa na povu.

Wiki chsche zilizopita Afande Sele akiwa kwenye interview na kituo cha redio alimtaja msanii Vanessa mdee kama msanii anaefanikiwa sio kwa sababu ya kipaji chake au kujua kuimba bali kudai anabebwa na kiki lakini pia anabebwa na penzi lake na msanii Jux. Hii haikuwa mara ta kwanza kwa Afande Sele kumponda Vanessa ameshawahi kumtaja kwenye listi yake ya wasanii wasojua kuimba.

Vanessa alimtolea uvivu Afande Sele kwenye interview aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio ambapo alisema kuwa kitendo cha Afande Sele kumponda na kusema kuwa anabebwa alichukulia poa kwa sababu anaelewa Afande Sele alitafuta pa kutokea na stress zake.

Mimi binafsi nilimuelewa niliangalia anazungumzia kwa upande gani nikagundua in few seconds kama nimetumika kama punching bag, sikuchukulia personal, nikaona fresh kabisa, nikajua anhaa alikuwa na yeye anataka kusikika anatafuta pa kutokea kihivyo ila mimi ni shabiki yake Mkubwa akawa ameniua kihivyo yaani amenitathimini kaniona hivyo ila kiukweli yule ni legend pia”.

Lakini pia Vanessa amesema kuwa anaelewa kuwa Afande Sele ni mkongwe kwenye game ila huenda alikuwa na stress zake binafsi, hivyo alikuwa anatafuta pa kumalizia hasira zake ndipo alipoangukia kwa Vanessa.

Sam Misago Amefunguka Baada ya Afande Sele Kudai Alimkatisha Tamaa ya Kuendelea na Mziki

Mtangazaji wa East Africa Tv na redio Sam Misago amejikuta kikaangoni baada ya Mkongwe wa mziki wa Bongo fleva Afande Sele kudai aliacha kufanya mziki kwa sababu alikatishwa tamaa na Sam Misago.

Afande Sele ni moja Kati ya wasanii wa kitambo sana ambaye hajaingia studio siku nyingi sana na alitaja moja ya sababu ya yeye kutoingia studio na kutoa nyimbo mpya ni kukatishwa tamaa na wadau mbali mbali wa muziki na mmoja kati ya wait hao ni Sam Misago.

Afande Sele amedai kuwa mara ya mwisho kutoa nyimbo yake ya ‘Amani na Upendo’ alishauriwa na Sam kuwa nyimbo aina ile hazina soko tena badala yake watu wanapenda nyimbo zenye swagga Kama anazoimba Diamond na wasanii wngine kitendo alichodai kilimkatisha tamaa kwani yeye anapenda kuimba nyimbo za kuelimisha watu.

Baada ya tuhuma hizo Sam Misago amefunguka kwenye interview aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Africa radio:

Naweza nikasema kilichotokea ni kwamba Afande Sele alinielewa tofauti alidhani niliongelea ujumbe wa nyimbo yake sikuongelea ujumbe ulikokuwa kwenye nyimbo ujumbe ulikuwa mzuri tu  ila niliongelea uwasilishwaji wa ule ujumbe wake ila ninamwambia Afande Sele akaze asikate tamaa maana gemu limebadilika tangu alipoliacha na asikatishwe tamaa kabisa na kauli yangu”.

Afande Sele aliweka wazi kuwa anarudi kwenye gemu lakini kamwe hawezi kuimba nyimbo ambazo hazina ujumbe kwa jamii hasa hawezi kuimba nyimbo zinazoongelea mapenzi, kulewa na anasa nyingine.

Gigy Money Amtolea Matusi Mazito Afande Sele

Mwanamuziki wa Bongo fleva Gigy Money anayetamba na wimbo wake wa ‘Papa’ ameibuka na kumtolea matusi ya nguoni Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Afande Sele.

Siku chache zilizopita Afande Sele alifanya mahojiano na kituo cha redio cha East Africa ambapo aliongelea mmomonyoko wa maadili katika mziki wa Bongo fleva na kudai kuna baadhi ya wasanii wapya ambao wanakuja na kuharibu muonekano wote wa mziki wa Bongo fleva.

Afande Sele aliongeza na kudai kuwa Gigy Money hamfahamu kwa sura na wala hajawahi kumuona machoni lakini anasikia kuwa anapenda kuvaa uchi na kufanya vitendo vya ajabu ambavyo vinapelekea mmonyoko wa maadili.

Gigy Money anaonekana hakufurahishwa na maneno yale kwani kea kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtolea Afande Sele povu zito;

Wasanii wa Zamani naomba mnipumzishe midomoni mwenu maana kwenye kila interview zenu mnanitaja taja tena mnikomee….Mnafikiri mkinitaja mimi indio interview zenu zitamfikia Trump Marekani? new taarifa yenu mnanipa kiki tu kama hamjui alafu makorodan**  yanawaning’inia au madada nyie? Mnikome kabisaa maana akili zangu sio nzuri ntawaharibia wengine badala ya wakate nywele zao eti wanatoa ushauri mxiuuu embu pelekeni bangi zenu maskani hukoo”.

Afande Sele alidai kuwa nyimbo ya Gigy Money inayojulikana Kama ‘papa’ haina maadili na pia msanii mwingine aliyemtaja Kama anaimba nyimbo zenye mmomonyoko wa maadili ni Zaiid anayetamba na wimbo wak unaoitwa ‘Mwanaume mashine’.

Mrisho Mpoto Amjia Juu Afande Sele Kisa Kesi Ya Lulu na Mauaji Ya Kanumba

Msanii wa Muziki Tanzania, Mrisho Mpoto ameshindwa kumvumilia msanii mwenzake Afande Sele na kumpa makavu baada ya Afande Sele kudai maiti ya Kanumba ifukuliwe na ichomwe moto kwa sababu ni mbakaji.

Baada ya kifungo cha Lulu siku mbili zilizopita wasanii mbali mbali walikuwa na maoni yao mmoja wapo kati ya watu hao ni mwanamuziki Afande Sele ambaye aliweka wazi hisia zake na kumjia juu Mama Kanumba kwa kitendo chake cha kufurahia Lulu kufungwa huku akisisitiza kuwa Kanumba ni mbakaji ambaye alikuwa anatembea na mtoto mdogo kama Lulu hivyo hastahili kupewa heshima bali ilitakiwa afukuliwe makaburini na kuchomwa moto.

Baada ya Kuongea maneno hayo ambayo yalionekana kutokumfurahisha Mrisho Mpoto alimjia juu Afande Sele na kufunga haya:

Afande Sele wewe ni kaka yangu na mwandishi ambary sijawahi kuacha kuheshimu maandishi yako…..Nimesoma mara 30 maandishi ulioandika kuhusu Kanumba naomba kujua ile barua uliomuandikia Marehemu Kanumba ulitaka imfikie au ulitaka wanaokuja nyuma yake wamfikishie? Ulitaka wanaokuja nyuma yake wajifunze kupitia waraka wako? Mbona nimepata kusikia marehemu halaumiwi kwa kuwa hana uwezo wa kujitetea? Umesema ulikuwepo Sinza kwenye msiba lakini hukutaka kusogea kuzika kwa sababu umesema we we sio mnafki kama Watanzania walioenda kuzik…ikiwa watu wote wangekataa ile maiti ingekuwaje? Nini hasa lengo la movies za kibongo kuziita maigizo yanayokwenda kwenye kanda? Una ugomvi na Bongo movie au uliandika ukiwa Una jazba kidogo? Mimi ndugu yako Mrisho Mpoto”.