Chid Benz Alalamika Kutolipwa na Jux.

Msanii wa muziki wa hip hop nchini , Chid benz amefunguka na kulalamika sana kitendo cha Jux kushindwa kumlipa pesa yake baada ya kuperfom katika tamsha lao la Love and Money Tour ambalo lilikuwa likifanya katika mikoa mbalimbali akiwa na mpenzi wake Vannesa.

Chid benz anasema kuwa Jux ni msanii mkubwa na ana haki ya kuwasaidia wasanii wnegine kama yeye kwa sababu wote ni wana mzuki lakini haikuwa poa kama anaweza kumuomba mtu kufanya nae kazi kwa malipo alafu ghafla ashindwe kumlipa pesa waliokubaliana,

Tour hiyo ya wapenzi hao ina zaidi ya miezi sasa tangu kuisha kwake na wasanii mbalimbai walinufaika na tamasha hilo kwa sababu walipata pia fursa za kutembeala na kutoa misaada mbalimbali ya kijamii na kukutana na amshabiki wapya .

Hata hivyo kwa kitendo icho, Chid benz anamtuhumu Jux na kusema kuwa haono mchano wa wasanii wengine katika muziki na ndio maana anafanya hivyo.

Jux Afunguka Kutofanya Kolabo Kimataifa

Msanii wa muziki wa bongo fleva Juma Jux amefunguka na kutoa sababu yake kubwa kwanini kwa sasa yeye hafikirii kufanya kolabo na wasanii  wa nje.Jux anasema kuwa pamoja na kwamba ikitokea kolabo na msaniiwa nje ikawa nzuri inaweza kumpa mafanikio makubwa msanii lakini kwa sasa hafikirii hilo.

Jux anasema kuwa haiwezekani msanii kufanyua kolabo na msanii wa nje ambae unakuwa hauna mazoea nae wala hamjawahi kufanya kazi ya pamoja wala kujuana.Jux anasema kuwa madhara ya kufanya hayo ni kubembelezana sana katika kuitangaza kazi na pia kunakuwa na dharau sana kwa sababu hamjuani.

huwezi kufanya kolabo na msanii tu ambae hakujui na wala haumui unakuwa umemdandia tu , kwenye kufanya kazi kuna kua na dharau, kwenye ku-promote kuna kuwa na kubembelezana kwaio ni bora nifanye kazi byser ambae najua ngoma ita-hit na kufanya vizuri kabisa na kunifikisha mbali.

Kumfungia Nyimbo ni Kumuua Msanii:-Jux

Msanii wa bongo fleva juma jux amefunguka na kusema kuwa kitendo cha BASATA kufungia nyimbo za wasanii sio kitu kizuri na kimekuwa kikiwaathiri sana wasaniiwengine hata kama BASATA wanakuwa hawaobi nikwakiasi gani wanawaumiza wasanii.

jux ambae pia wimbo wake wa uzuri wako ulifungiwa , anasema uwa wimbo wake umefungiwa miaka kama mitano iliyopita hivyo alikuwa ameshafuta machozi na kidonda kimepona lakini walipoutoa tena katika lish]t mpya imekuwa kama wanatonesha kidonda na kuonyesha kuwa wanatilia mkazo maamuzi yao.

Wimbo wangu ulifungiwa miaka kama mitano iliyopita,nilijaribu kufatilia lakini hakuna feedback yoyte niliyopata ,na kisa ni maadili hayohayo.lakini pia kuitoa tena sasa hivi kunaonyesha kuwa wanataka kutilia mkazo lakini wanatonesha kidonda kilichopona.

Kuhusu kukosewa kwa jina lake katika list hiyo ya majina na nyimbo zilizofungiwa , jux anasema kuwa hajui kwa nini walikosea jinalake lakini anajua kuwa serikali inamtambua.

Kuhusu jina langu kukosewa hapo hata sijui ingawa kuna baadhi ya watuwalisema kuwa inawezekana sitambuliki na BASATA  lakini  sidhani kwa sababu nilishawahi kushinda hata tuzo.sasa inakuwaje wanakosea jina langu.

Maoni ya mwisho ya jux kwa BASATA ni kwamba kama wanaona kuwa kuna kitu cha kuzngumza na msanii ni bora kufanya hivyo kabla ya kufikia uamuzi wa kufungia nyimbo zao.

Kufungiwa nyimbo sio jambo zuri kabisa , hii ni kama kumuu msanii tu .na hii nadhani BASATA wanatakiwa wakae na wasanii kujua tatizo lao kwa sababu huu ndo muda ambao biashara ya muziki ndio inaanza kuamka.

 

Maneno ya Jux kwa Vannesa Yalivyowafurahisha Mashabiki.

Inaweza ikawa ndio couple bora katika mtandao kwa sasa bongo kutokana na ukaribu wao na mapenzi wanayoonyeshana wote wawili, inaweza kusemekana kuwa nguvu kubwa ya mashabiki inawafanya waendelee kudumu katika mahusiano hayo kwa sababu kipindi wamekosana mashabiki wengi walionyesha kuumia   na hata kupaza sauti ili wawili hao warudiane.

Kelele kubwa ya sasa kutoka kwa mashabiki sasa hivini wawili hao kuharalisha mahusiano yao na kufunga ndoa ili kuthibitisha kuwa wapo pamoja muda wote, kila wanapoweka picha katika mitandao mashabiki wamekuwa wakiweka maoni yenye kuonyesha kufurahi kuwaona pamoja wawili hao.

Wikiend hii Jux aliweka picha akiwa na vannesa mdee huku wakiwa katika pozi moja matata la kimahaba ambalo liliwakosha mashabiki wengi wa wasanii hao ambao ni wapenzi , lakini pia kikubwa kilichowavutia ni  maneno matamu Jux aliyoyaandika kwa Vannesa Mdee.

Ninachotaka kuona ni tabasamu  na furaha yako siku zote #bestfriend alafu don’t change your hairstyle  nazipenda saaana.-Aliadika Jux katikaukurasa wake wa instagram.

Balaa La Vannesa na Jux Jukwaa La Fiesta,Mapenzi Ni Mubashara.

Wakiwa bado wanakiri kuwa  hakuna mapenzi kati yao wasanii wawili Vannesa Mdee  pamoja na Jux wamewashangaza mashabiki kwa matukio yao ya kuimba pamoja katika matamasha mbalimbali ya Fiesta huku wakionesha kuwa hawana ugomvi wowote ilihali wamekuwa mbali katika mapenzi.wasanii hao ambao hata wamekuwa wakionekana waki-hang out pamoja katika mikoa mbalimbali tofauti na jukwaani wanaonekana kuwa bado na hisia kwa kila mtu kutokana na vile wanavyokuwa wakijiwakilisha jukwaan mbele ya mashabiki.

Tarehe 25, wikiendi iliyopita wasanii hao walipata bahati ya kutumbuiza katika jukwaa kubwa la Fiesta mkoani Dar Es Salaam ambapo waliwashangaza watu wengi baada ya kuimba kwa kuonyeshana mahaba na kuwa karibu zaidi.

Walipokuwa wakiimba mashabiki zao walikuwa wakishangilia na kupiga kelele za kuwataka wawili hao kurudiana, hata hivyo inasemekana kuwa wawili hao bado wanaendeleza mahusiano yao pamoja na kwamba wamekuwa wakikataa kuhusu kurudiana kwao.

Vannesa Mdee ni mmoja kati ya wasemaji katika kukanusha taarifa za kurudian kwao huku wakisema kuwa wamekuwa wasanii na wafanyabiashara kwa uda mrefu hivyo ugomvi wa kimapenzi hauwezi kuharibu kazi na biashara.

Vannesa na jux wakiimba kwa pamoja

Jux akimtengeneza Vannesa cheni kifuani kwake

Wakiwa pamoja jukwaani.

 

Vannesa Ajibu Tetesi Za Kurudiana Na Jux

Kumekuwa na tetesi nyingi mitandaoni kuhusu uhusiano wao wa karibu licha ya kuwa walikuwa wapenzi na wakaachana, wengi walitegemea watu hawa watakuwa maadui, wengine wakisema kuwa uwepo wao wa karibu unamaanisha kuwa wamerudiana kutokana na ahadi alizoweka Jux kuwa atafanya juu chini na watarudiana na Vanesaa Mdee.

Vannesa na Jux walikuwa ni moja ya couple iliyokuwa ukiwavutia watu wengi sana hasa muonekano wao walipokuwa pamoja, ukiachana na mapenzi lakini pia walikuwa wakifanya kazi ya muziki na biashara pamoja hiki ni moja ya vitu vilivykokuwa vikivutia zaidi.

Hata hivyo, baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu kurudiana kwao hasa katika msimu huu wa tamasha la Fiesta ambapo mara nyingi walikuwa wakionekana kuwa pamoja na kuwa wote jukwaani na hata kuonyesha vitendo vya kukwepana kimahaba walipokuwa wakiimba Vannesa Mdee amuamua kufunguka na kujibu tuhuma hizo.

Vannesa alisema kuwa ukiachana na mapenzi lakini pia wao walikuwa wakifanya kazi pamoja na biashara, hivyo hata kama wamegombana katika swala la mapenzi haimaanishi kuwa wamapaswa kuwa maadui na kushindwa kufanya kazi pamoja.Wao watabaki kuwa washikaji tu na kufanya kazi na hakuna mapenzi.

kitu ambacho watu wengi hawajui ni kuwa jux ni mshikaji wangu sana,ni mt ambae tunapatana sana na tunaffanya kazi pamoja,na hata vitu vingi sana nje ya muziki jux amekuwa akinipa sapoti sana,kwaio hatuwezi kukaa tukagombana sasa hivi kwanza tunakuwa tukihatribu biashara. -Alifunguka vannesa

Vanesa ana Jux mara ya mwisho walipoonekana kuwa pamoja katika jukwaa la fiesta Morogoro Jux alikuwa akiimba kwa style ya kuomba msamaha ambapo Vanessa alimjibu atamsamehe akifika katika jukwaa la Mtwara, na walipofika mtwara wawili hao walionekana kuimba pamoja na kuonyesha ishara nzito za mahaba zilizofanya  mashabiki wengi khpji kama wamesharudiana au la.

Endapo wawili hao watarudiana itakuwa ni moja ya mambo yatakayo walidhisha mashabiki kwa sababu kwa muda mrefu mashabiki wamekuwa wakivutiwa kuwaona wawili hao kuwa pamoja na  wakiwaomba kwa muda mrefu wawili hao kutaka kurudiana

Vanessa ana thamani kubwa kwangu- Jux

Msanii wa RnB nchini Juma Jux anayetamba na wimbo wake mpya wa “Utaniua” amefunguka juu ya uhusiano wake na mwanamuziki wa hapa nchini Vanessa Mdee, Kuwa kwake kwanza ni familia yake kisha Vanessa.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Vanessa alisema, “Nampenda Vanessa kuliko msichana yoyote niliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano na sitegemei kumuachia aende hivi hivi hata familia yangu inajua mapenzi yangu kwa Vanessa.

“Nikiwaga mbali na Vanessa kitu cha kwanza nikiamka asubuhi naingia Instagram namuangalia halafu nampigia simu, Siwezi kumpigia Simu bila kuangalia picha zake kiufupi ninampenda sana Vanessa”.

Kuhusu kuwa na Mtoto Jux alifunguka kuwa ” Sasa hivi natamani kupata mtoto na nina mpango huo, kwa sasa najipanga vizuri Mungu akinijalia basi hivi karibuni ntapata mtoto na nitapenda kumuita Karim na si jina jingine zaidi ya hilo.

Jux na mpenzi wake huyo Vanessa waliachana miezi michache iliyopita lakini Jux ameweka wazi kuwa bado a na mp end a.

Jacqueline Wolper aamua kurudi shule baada ya Jux kuitimu masomo yake nchini China

Juma Mussa maarufu kama Jux ameitimu masomo yake nchini China. Msanii huyo amepata shahada ya Computer Science aliyosomea kwa muda wa miaka minne.

Jacqueline Wolper amepata changamoto ya kurudi shuleni baada ya kuona picha ya Jux akisherekea baada ya kuitimu masomo yake nchini China.

“Nimekumbuka mbali kweli nilivyoiona hii picha, nakumbuka siku hizo mwenyewe ndo nakupeleka airport unaenda kuanza kusoma mpaka na mimi nilitamani kuwa mwanafunzi ili twende wote yaani naandika hii caption huku nasmile nikikumbuka hiyo siku ndo unaenda kusoma mwenyewe…am very happy for you mwanafunzi wangu! yani verrrrry happy…! Hongera sana siku hizi vijana wanafanya yote na shule ipooo ndo unazidi kuwa mnyamweezi, mimi mwenyewe hapa nataka nirudi shule ya kutafuta hela manake maisha magumu sana… Hongera sana kwa kuhitimu..!!nisaidieni kumtag mwanafunzi wangu,” Wolper aliandika.

“Unatisha sana Jux wewe hatari mnoo” Mashabiki watoa maoni yao baada ya Jux kuachia video mpya

Juma Mussa maarufu kama Jux ameachia video mpya wa wimbo unaitwa “Umenikamata”. Maoni ya mashabiki ni dhibitisho kuwa wimbo huo ni kali.

Fran k fran k:  niskize ninavyo imba na pia ninavyo piga gita naona watu wamependeza face zao zime jaa furaha najua ujui leo hii kita tokea nn I do this for u juma juma unajua bro much respect bro

frank msafiri: umenikumbusha napata raha nilikua naisikiza mpaka sio poa / nice work

George Lyimo: Unatisha sana jux wewe hatari mnoo….. Big up….

Iam Rogerz: all the way from USA watching Kali sana

Gilbert Boniphace:  Hujawahi niangusha …Much respect to you JUX. kill them all…nice and great job

Abdallah Juma: Kazi nzuri brother..nmependa uwepo wa akina benpol,barnaba,kamikaze.. dah na mashairi mazur sana asante hii namdedicate mu wife asee

Thobias Mwacha: kali mzee jux nakukubali balaaa hatari mzee baba

Georgina shi: my best musician  thanks for the good music dearest!???

Amisi Steven: umenikamata

Godfrey Yuvenali: video Kali nyimbo Kali wewe   mwenyewe mkali very good

Edward dixonfaithfull gichallu mlg: huyu ndiye jux nayemjua Mimi!

 

Tazama hapa chini video yake Jux uone kama utakubaliana na maoni ya mashabiki hawa: