Ruge Amekuwa na Nafasi Nyingi Sana Katika Maisha Yangu :-Nandy

Msanii wa bongo fleva nchini NANDY,  amefunguka na kusema kuwa  Mkurugenzi wa Clouds media , Ruge mutahaba amekuwa aki-play party kubwa sana katika maisha yake kiasi kwamba hata ugonjwa na magumu anayoyapitai sasa hivi yamekuwa yakimuumiza sana.

Nandy ameongea hayo alipokuwa akihojiwa na Clouds Media leo na kusema kuwa Ruge amekuwa ama bosi, kama kaka na kama baba kwake kwa sababu katika kazi zae za muziki bila Ruge basi hajui yeye mpaka sasa angekuwa wapi.

Hata hivyo haya yote yanakuja bada ya nandy kugombana na kujibizana na  msanii mwenzake Dudu baya ambae aliamua kusema kuwa kama Ruge ni mgonjwa na anahitaji msaada hakuna haja ya kumsaidia kwa sababu alishadhulumu wasanii wengi sana.

Amekuwa akiplay party kubwa sana katika maisha yangu sio kimuziki tu , lakini hata katika maisha.tukiangalia hapa nilipo sababu ni yeye, ukiacha nafasi ya wazazi wangu nafasi inayofuata ni yeye, kwangu yeye ni kama bosi, kaka na kama baba.

Akiongea huku analia, Nandy anasema kuwa mara nyingi amekuwa akikwama na anawaza kabisa kuwa tatizo kama hili angekuwepo Bosi Ruge angeweza kulitauta lakini anaona kabisa kuna kitu kinapotea.

 

 

Nandy na Lulu Diva Wawatatiza Mashabiki

Mwanadada Nandy na msanii mwenzake wa kike  Lulu Diva wamewaacha mashabiki katika njia panda baada ya wawili hao kila mmoja kwa nafasi yake kuonekana akiwa na lebo inayotatizza huku watu wakihisi kuwa lebo hiyo ni ya  mwannaume mmoja.

Hapo nyuma , Nandy alikuwa akihojiwa na mashabiki hasa kutokana na kuvaa kofia iliyoandikwa Joho 001, ambapo ni lbo ya rafiki mkubwa na alikiba anaekaa huku nchini mombasa.

Lakini wikiendi hii picha moja ya Lulu diva ilisambaa katika mitadao ya kijamii ikimuonyesha msanii huyo wa kike akiwa amechra tatoo yenye jina kama hilo la Joho katika mkono wake.

Hata hivyo mashabiki wamekuwa wakihoji juu ya nembo hiyo kwa wadada hao wawili kama imekuwa ikiashiria kitu kimoja au la.

Wazazi Wa Nandy Wafungukia Video Ya Utupu Ya Nandy

Wazazi wa Msanii wa Bongo fleva Faustina Charles Mfinanga maarufu kama Nandy wamefunguka na kuiongelea video ya utupu ya Nandy ambayo ilivujishwa mwaka jana kwenye Mitandao ya kijamii.

Baba mzazi wa Nandy amefunguka na kusema video hiyo ya binti yao iliwatia aibu sana kama Familia kiasi cha kumtaka Nandy aachane kabisa na kufanya muziki.

Katika interview aliyofanya Baba Nandy alisema kwamba siku iliyovuja video hiyo alikuwa akipigiwa simu kila dakika kumlaumu kwa kitendo chake cha kumuacha mtoto afanye sanaa, licha ya ndugu zake wengi kutofurahishwa na suala hilo.

Nilikuwa ofisini kwangu napigiwa simu nyingi nyingi wananilaumu vipi mtoto, yaani kama vile kitendo alichokifanya Nandy ni kama nimekifanya mimi, kwa jinsi wanavyotoa shutuma, nikawa najiuliza kumetokea nini, katika kuchunguza ndio nikaambiwa, mimi sijaiona hiyo picha, niliambiwa tu, nilichokifanya nikasema huu ndio mwisho wa huyu mtoto, mwisho wake wa kuimba umefika, sababu yale niliyokuwa nayaogopa naona yameshakuja”.

Lakini pia Mama mzazi wa Nandy amesema kwamba tukio lile lilimpa wakati mgumu, kwani alishindwa hata kula na kumfanya akae njaa kwa siku tatu, na kusema kwamba iwapo atarudia kufanya vile basi huenda akapoteza maisha kabisa.

Nilikuwa sipokei simu kwa sababu nilikuwa najua nitakachoulizwa, nilikosa raha nilikaa siku tatu sijala kitu zaidi ya kunywa chai tu, alipokuja kuona alizimia akashtuka yuko hospitali, lakini ni mateso, sikufichi ni mateso, Nandy siku akirudia naweza nikafa kabisa”.

Mwaka jana video iliyomuonyesha Nandy na Mpenzi Wake kwa wakati ule Billnas wakiwa chumbani faragha kabisa ilivuja kwenye Mitandao ya kijamii na kuzua kizaazaa.

Mimi na Ruby Hatuongei na Wala Sio Marafiki.:-Nandy

Mwanadada Nandy amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwanadada mwingine ambae aliwahi kuigva na kutamba sana katika muziki ambae kwa sasa pia anajitahidi kurudi kwa kasi kutokana na kazi zake.

Mwanadada Nandy anasema kuwa hakuna ukweli kuwa yeye na Ruby wamekuwa wakigombana kisa mafanikio na jina kwa mashabiki kutokana na muziki lakini wamekuwa tu hawaongei kwa sababu hawakutana mara kwa mara wala kufanya kazi pamoja.

Tetesi zelizowahi kusamba baada ya nandy kuwa anfanya vizuri katika muziki ni kuwa , wawili hoa wamekuwa maadui wakijaribu kugombia mashabiki tena hasa kutokana na kuwa wawili hao kidogo wamekuwa wakiimba muziki unaofanana.

Akiongea na Mzazi Mtuva wa mambo mesto jijini kenya Nandy anasema “mimi na Ruby hatuongei lakini tujo poa kabisa, na sio marafiki na wala sijui mara ya mwisho kumuona ilikuwa lini, lakini tuko poa na tukionana tutasalimiana.

Wazazi wa Nandy ni Zaidi ya Marafiki

Wazazi wa mwanadada Nandy leo wametinga mjengoi clouds tv katika kipindi cha clouds 360 huku lengo lao kubwa ikiwa ni kutaka kutambulisha wimbo mpya wa mtoto wao ambapo yeye ameshindwa kuhudhuria kwa sababu ya kutokuwepo nchni.

Wazazi wa mwanadada huyo wamekuwa wakimsapoti sana mtoto huyo karibia kwa kila kitu na hata kazi zake zimekuwa zikieda sawa kutokana na sapoti kubwa anayoipata kutoka kwa wazazi wake.

Nandy ambae  amekuwa hata akitumiwazazi wake kama model katika baadhi ya nyimbo zake amekuwa pia akioenekana kuwa karibu sana na baba yake mzazi kutokana na mapenzi yanayoonekana katika mitandao ya kijamii.

Wazazi hao ambao hivi karibuni walikabidhiwa nyumba mpya na mtoto wao huyo wa kike kutokana na mafanikio yake katika muziki anasema kuwa  wamekuwa na furaha siku zote kutokana  na mafanikio ya binti yao.

Nandy Aomba Asifananishwe Kiuchumi na Wasanii Waliotangulia

Mwanadada Nandy amefunguka na kusema kuwa amekuwa akikerwa sana pale anapofananishwa kimafanikio hasa ya kiuchumi na wasanii wakubwa waliotangulia katika muziki kabla yake kwa sababu hawezi kulingana nao kwa kuwa wao walishatagulia.

Kauli ya nandy inakuja baada ya mashabiki kuanza kumshindanisha na wasanii wengine waliotangulia hasa baada ya kupost katika mitandao kuwa ameweza kuwajengea wazazi wake nyumba huku akionyesha baadhi ya magari ya bei gari ikiwemo BMW.

mimi nina miaka miwili katika hame la muziki na kuna watu wanamuda mrefu sana katika game, kwaio nimekuwa nikiheshimu sana uwepo wao,  kwaio sidhani kama ni sawa kunifananisha nao kwa sababu na waowalianza kupokea mkwanja wa show  kama mimi .

 

 

Siri Ya Mafanikio Yangu ni Juhudi Kwenye Kazi-Nandy

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameibuka na kuanika Siri ya mafanikio yake ambapo ametangaza kuwa mali  nyingi ikiwemo kumiliki magari manne ya kifahari na nyumba ikiwemo nyumba aliyowajengea wazazi wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy ambaye anamiliki magari manne ya kifahari na ameweza kuwajengea wazazi wake mjengo wa kifahari alisema hakuna mwanaume yeyote anayemuwezesha kama watu wanavyodai, bali mafanikio yake ni juhudi zake katika kazi pia menejimenti aliyonayo ipo makini ndiyo maana amefika hapo alipo.

Siri ya mafanikio yangu inatokana na juhudi zangu. Pia nina menejimenti nzuri ambayo ipo siriazi sana linapokuja suala la kazi, ndiyo maana imenifanya niwe na mafanikio haya na hivi karibuni natarajia kufungua kampuni yangu mwenyewe ila siwezi kusema ni ya nini kwa sababu kuna mambo ambayo bado tunayaweka sawa, yakikamilika basi kila mtu atajua”.

Mwaka jana kulikuwa na tetesi kuwa Nandy amemuopoa pedeshee aliyekuwa wa Wema na ndiye anamtunza huku marcedes Benz aliyopewa siku ya birthday yake ilisemekana kutoka kwake.

Nandy Afunguka Baada Ya Kuwapa Wazazi Wake Nyumba

Staa wa muziki wa Bongo fleva kutoka Nyumba ya vipaji Tanzania (THT)  Faustina Charles maarufu kama Nandy Amefunguka mara ya Baada ya kutangaza zawadi yake kwa wazazi Wake.

Siku chache zilizopita Nandy aliweka wazi Nyumba ambayo amewanunulia wazazi wake  Kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka kipande cha video na picha ambazo zinaonyesha nyumba hiyo na maelezo yanayosomeka:

“Mungu wangu na Baba yangu najua nakukosea sana kama binadamu na kama kijana ila nikipiga goti unajua namaanisha kutoka moyoni mwangu na unajua hakuna ninayemtegemea zaidi yako… Asante kwa kunipa uvumilivu, unyenyekevu, katika maisha yangu hasa kipindi hiki cha mwaka 2018!! Asante kwa hii zawadi ndogo ya wazazi wangu najua hii ni ndoto ya kila kijana mwenye kutafuta!!! Ni kila ndoto ya mwanadamu yeyote duniani kuona wazazi wake wako na furaha na ndiyo baraka zenyewe” .

Nashukuru media zote , blogs zote, ma producers wote, mapromoters wote, familia yangu ya THT, familia yangu ya clouds, management yangu, Team yangu, marafiki zangu, Baba yangu wa kiroho Mtumishi MWAMPOSA , na mafans wangu wote ,bila kusahau na hatters wote kwa kunipa nguvuu na supports kwa namna moja au nyingine uwepo wenu ndio mafanikio yangu……..
Nilijipa nguvu kabla sijapewa
Nilijipa moyo kabla sijapewa
Nilijiamini kabla ya kuaminika
Nilijikubali kabla ya kukubalika
Popote ulipo kijana mwenye ndoto yoyote ile jua inawezekana ukiweka nia ukikubali mazuri na mabaya yote yakufikie sababu ni daraja na nguzo ya mafanikio yako bila kusahau MUNGU ndiye kila kitu. Nawapenda
HAPPY NEW YEAR IN ADVANCE ?
#DADAMWENYENYUMBA”.

Nandy Afuata Nyayo za Dogo Janja.

Mwanadada Nandy ameamua kufuata nyayo za msanii mwenzake Dogo Janja baada ya kuonyesha mafanikio yake ya kujenga nyumba mpya kwa ajili ya wazazi wake jambo ambalo anashukuru ameweza kulifanikisha kwa mwaka uliopita 2018.

Mwanadada huyo aliamua kuweka nyumba hiyo katika ukurasa wke wa instagram , ikiwa kama moja ya shukrani zake kwa mwaka 2018 kwa mafanikio yake aliyoyapata.

Mwanadada huyo anasema kuwa ameamua kujenga nyumba hiyo kwa ajili ya wazaiz wake ikiwa kama njia ya mafanikio kwa kazi zake.

Nyumba alionyesha Nandy kuwa ni zawadi kwa wazazi wake kwa mwaka 2018

 

 

 

Nandy na Diamond Platnumz Wang’ara Tuzo za AEAUSA

Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz kutoka WCB na Faustina  Charles maarufu kama Nandy na wasanii wengine kutoka Tanzania wameng’ara katika tuzo za African Entertainment Awards USA (AEAUSA).

Mbali na wasanii hao wa Kitanzania kushinda tuzo lakini pia kuna wasanii kutoka katika nchi za Afrika Mashariki waliofanikiwa kushinda tuzo.

Wasanii waliofanikiwa kushinda tuzo ni pamoja na Diamond Platnumz ambaye ameshinda tuzo mbili, ikiwemo tuzo ya Msanii bora wa mwaka ( Best artist of the year pamoja na Best Collaboration akishirikiana na Omarion kutoka nchini Marekani.

Msanii Nandy ameshinda katika kipengele cha Best Female Single kupitia wimbo wa Kivuruge, huku Rayvanny akishinda tuzo ya Best Vocalist na Dj wa Diamond Rom Jones akishinda tuzo ya best DJ in Africa.

 

Nandy Kupanda Steji Moja na Hamisa Mobetto

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ametangaza habari njema kwa mashabiki Wake wanaokaa nje ya nchi kwani anatarajiwa kupanda steji moja na Hamisa Mobetto.

Nandy ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Aibu’ ameweka wazi kuwa mwezi huu baadae anatarajia kuungana na Hamisa Mobetto kwa ajili ya your yake ya nchini Marekani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Nandy ameweka wazi kuwa yeye na msanii mwenzake Aslay wanatarajia kuungana na Hamisa Mobetto nchini Marekani.

Natarajia kusafiri siku ya tarehe 25 mwezi huu kuelekea Marekani kwa ajili yakufanya ziara nikiwa na msanii mwenzangu Aslay na Hamisa kisha nitarudi Bongo tarehe 10, Desemba tukiwa wote watatu, pia hii kwangu itakuwa ni mara ya kwanza kufika huko kwa sababu sijawahi kwenda kabisa”.

Hamisa Mobetto amekuwepo nchini Marekani kwa zaidi ya mwezi sasa ambapo ameonekana akiwa anafanya matamasha katika majimbo mbali mbali katik nchi hiyo.

Nandy Atupwa Kando Kwenye Listi Ya Wasanii 29 Watakaoperfom Fiesta

Clouds Media Group limetangaza Listi ya majina 29 ya wasanii ambao wanatarajiwa kuperfom katika tamasha la Fiesta 2018 litakalofanyika siku ya Jumamosi katika Viwanja vya Leaders Club.

Kwenye orodha hiyo ndefu, wapo wasanii Kama Rostam, Weusi, Maua Sama, Wakazi, Ben Pol, Chege, Fid Q na wengineo, huku wasanii chipukizi nao wakipewa kipaumbele.

1. Weusi  2. Rostam 3. Fid Q 4. Wakazi 5. Rich Mavoco  6. The Mafik 7. Ben pol 8. Rosa Ree 9. Marioo 10. Barnaba  11. Billnass 12. Chege Chigunda 13. Dogo Janja 14. Msami 15. WhoZu  16. Mimi Mars  17. Lulu Diva  18. Zaiid  19.Mesen Selekta 20. Maua Sama 21. Tid 22. Qchief 23. Juma Nature 24.Jolie 25.Benson 26.Jay Melody 27.Mabantu
28.Brian Simba 29.Amber Lulu”.

Suala la kukosekana kwa Msanii Nandy ambaye yupo ndani ya THT limeshangaza watu wengi huku tetesi za chini ya kapeti zikidai kuwa huenda kitendo cha Nandy kuonekana akila bata na Diamond Platnumz Dubai kinaweza kuwa chanzo.

Baada ya tetesi nyingi kusambaa Baada ya jina la Nandy kukosekana Clouds wametoa kauli na kusema kuwa List nyingine ya kambi ya upinzani itatangazwa baadae

N.B kuna Listi ya kambi ya Upinzani bado.  Kama vipi Jumamosii hii tukutane Leaders Club. Kiingilio 10,000/- Ukinunua kwa Tigopesa master-pass QR, na shs 15,000 Kawaida!“.

Nandy Adaiwa Kumnyakua Bwana Wa Wema

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Aibu’ Faustina Charles maarufu Kama Nandy amedaiwa kumchukua Mwanaume aliyekuwa kwenye mahusiano na muigizaji Wema Sepetu.

Gazeti la Risasi linaripoti kuwa Mwanaume mmoja anayejulikna Kama Rajabu ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza alikuwa ndio anamuweka Wema mjini lakini Baada ya skendo ya Wema na PCK kutokea inadaiwa bwana huyo alimtosa Wema na kuhamisha majeshi kwa Nandy.

Gazeti hilo linaendelea kuripoti kuwa mara tu baada ya mwanaume huyo kutua kwa Nandy alimpangishia nyumba Masaki jijini Dar na kumnunulia gari la kifahari aina ya BMW X 1 na pia siku ya birthday yake mwanaume alimwagia pesa chafu ukumbini.

https://www.instagram.com/p/Bp9dZByBMxh/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=pqpdgwd4nx78

Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Nandy ili kupata ukweli wake juu ya ishu ambapo alikana kabisa taarifa hizo na kukana kumjua jamaa huyo.

Mh! Waja wana mambo sana, kwanza niseme nashtuka wewe kuniambia mambo ya bwana wa Wema, mimi yule bwana alinipa kama milioni tano hivi nilipozihesabu na nilishangaa kwani sikuwa nikijua kuwa nitapewa pesa hizo lakini si mpenzi wangu, wala sijawahi kujua kama anatoka na Wema.

Ukweli ni kwamba nilimualika kwenye pati yangu akanipa pesa kama mlivyoona lakini sina uhusiano naye wa kimapenzi na wala gari hili hajaninunulia yeye, mimi nimejinunulia mwenyewe kwa kazi zangu tu. Kuhusu nyumba nimepangishiwa na mpenzi wangu ambaye siwezi kumtaja kwa sasa ila ni mtu maarufu tu.

Lakini Nandy alipobanwa zaidi kuhusu jamaa huyo alisema:

Alinipigia simu na kuniambia kuwa anataka kufanya biashara na mimi, akaniambia atakuja Dar, huwezi kuamini alikuja Dar na ikawa ndio imefika siku ya sherehe yangu ya kuzaliwa, nikamualika kwa bahati nzuri akaja”.

 

 

Nandy Amtaja Aslay Kama Msanii Alimtungia Nyimbo Kwa Ajili Ya Albamu Yake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva nchini kutoka katika Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) Faustina Charles maarufu kama Nandy amefungukia Albamu yake mpya.

Albamu mpya ya Nandy ambayo hivi sasa iko sokoni inaitwa ‘The African Princess” Kiowa ni albamu yake ya kwanza kuingiza sokoni tangu aanze Sanaa yake ya kimuziki.

Nandy ameweka wazi kuwa Albamu hiyo imemchukua Kama mwaka mzima kuiandaaa tu huku nyimbo zake akiandikiwa na msanii Kama Jay Melody na staa mkubwa wa Bongo fleva Aslay.

Kusema ukweli Albamu yangu imechukua muda mrefu kukamilika kwa sababu nimekuwa nikitungiwa nyimbo na wasanii Kama Aslay na Jay Melody”. 

Kwneye mahojino na kituo kimoja cha habari Nandy amefunguka haya kuhusu muziki wake na albamu yake hiyo:

Imenichukua mwaka mzima kutengeneza albamu yangu ili kupata Kitu kizuri hii imekuwa kwa sababu ya kusafiri kwa ajili ya kufanya shoo mbali mbali ambazo zimechukua muda wangu mwingi”.

 

Nandy Afunguka Baada Ya Kuonekana Tena na Billnas

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ na msanii mwenzake anayefanya muziki wa hip hop William Lyimo ‘Billnas’ walirudi kwenye headlines tena na kuzua gumzo Baada ya kuonekana pamoja.

Gumzo hilo lilizuka wiki iliyopita Baada ya Nandy kiposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ilimuonyesha akiwa pamoja na Billnas na msanii mwenzao Dogo Janja.

Baada ya kuposti picha hiyo maneno mengi yalisemwa ikiwemo tetesi as kwamba huenda wawili hao wamerudiana ama vipi huku baadhi ya mashabiki kuonekana kufurahia wawili hao Kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Nandy alisema hana kinyongo kabisa Billnas kwani walishamaliza tofauti zao tangu zamani hivyo kwa sasa wao ni washkaji tu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

Mimi na Bill sasa hivi ni washkaji tu, hakuna chembechembe yoyote ya mapenzi kati yetu, tulishaachana muda mrefu na kila mtu ana maisha yake, sioni tatizo kuwa naye karibu”.

Wawili hao walishawahi kuwa kwenye mahusiano siku za nyuma lakini walikuja kuachana na hata video yao ya faragha kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Nandy Azima Tetesi Za Kuwa Mjamzito

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy amefunguka na kukataa kata kata tetesi zilizombaa Kwenye mitandao ya kijamii kuwa hivi sasa ni mjamzito.

Nandy ambaye hivi sasa anafanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Aibu’ amekataa tetesi za kuwa hivi sasa amejazwa kibendi na Kigogo mmoja na kudai ni uzushi tu.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy alisema watu huwa wanaamua tu kuzusha mambo yasiyokuwa na ukweli wowote ule ndani yake, ili mradi tu wafurahishe mioyo yao kitu ambacho kinaumiza.

Hizo tetesi zinazosambaa mitandaoni kwamba nina mimba siyo za kweli, ila naona watu wameamua tu kuzizusha ili wafurahishe mioyo yao, sina mimba jamani naomba waniache“.