Nandy Afunguka Baada Ya Kuonekana Tena na Billnas

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ na msanii mwenzake anayefanya muziki wa hip hop William Lyimo ‘Billnas’ walirudi kwenye headlines tena na kuzua gumzo Baada ya kuonekana pamoja.

Gumzo hilo lilizuka wiki iliyopita Baada ya Nandy kiposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ilimuonyesha akiwa pamoja na Billnas na msanii mwenzao Dogo Janja.

Baada ya kuposti picha hiyo maneno mengi yalisemwa ikiwemo tetesi as kwamba huenda wawili hao wamerudiana ama vipi huku baadhi ya mashabiki kuonekana kufurahia wawili hao Kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Nandy alisema hana kinyongo kabisa Billnas kwani walishamaliza tofauti zao tangu zamani hivyo kwa sasa wao ni washkaji tu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

Mimi na Bill sasa hivi ni washkaji tu, hakuna chembechembe yoyote ya mapenzi kati yetu, tulishaachana muda mrefu na kila mtu ana maisha yake, sioni tatizo kuwa naye karibu”.

Wawili hao walishawahi kuwa kwenye mahusiano siku za nyuma lakini walikuja kuachana na hata video yao ya faragha kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Sina Urafiki Wowote na Billnas- Nandy

Msanii  wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake. Mpya ya ‘Aibu’ amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana Mahusiano yoyote na aliyekuwa mpenzi wake Msanii mwenzake Bill Nas.

Nandy na Billnas waliwahi kuwa wapenzi miaka ya nyuma wakaja kuachana lakini walipata fedheha mapema mwaka huu baada ya video yao chafu ya Kitandani kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nandy aliulizwa kuhusu urafiki wake na Billnas na kama waliacha kuongea baada ya video yao kuvuja Nandy alifunguka:

Hatuna ushikaji kiukweli tangu kipindi kile tatizo lilipotokea, hatujawahi kuwasiliana hata kwenye simu, ila nakumbuka mara ya mwisho tulionana central kituo cha Polisi, kwa hiyo sidhani kama kuna kitu chochote cha kuongea, japo najua tukikutana lazima tutapiga stori, tutacheka na kufurahi pia“.

Lakini pia Nandy amesema kwa sasa hivi amepata mpenzi mwingine na kama Mungu akijalia, hivi karibuni atafunga ndoa.

Bill Nas- Nandy ni Dada Yangu na Ninamuheshimu Sana

Msanii wa Bongo fleva aliyefanya vizuri na ngoma zake kama chafu pozi amefunguka na kusema Nandy ni dada yake na anamuheshimi sana.

Bill Nas na Nandy walishangaza watu wengi wiki chche zilizopita baadae ya kuitana dada na kaka huku Ikiwa wazi kabisa kuwa wawili hao walisha wahi kuwa Kwenye Mahusiano siku za nyuma.

Bill Nas ameiambia Enews ya EATV kuwa uamuzi wake wa kumuita Nandy dada unatokana na ukweli kuwa mapenzi yao yalipiita siku nyingi sana kwani baada ya kuachana na Nandy alikuwa Kwenye uhusiano na wasichana wengine wawili hivyo kwake sio Ex tena bali ni dada:

Kwa kweli kibusara Nandy ni dada yangu inaweza pia kiumri akawa dada yangu ingawa sina uhakika lakini ni dada kiheshima kwa sababu sijawahi kumvunjia heshima kwa namna yoyote ile ndio maana nikamuita dada lakini sio kindugu”.

Bill Nas na Nandy walizua gumzo mwezi uliopita baada ya video yao ya ngono kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Video Ya Ngono Yaendelea Kumtesa Nandy

Mwanamuziki wa Bongo fleva Faustina Charles maarufu kama Nandy ameendelea kuandamwa na video yake ya ngono na aliyekuwa mpenzi wake Billnas.

Nandy ambaye kwa hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ya Ninogeshe amekiri kuwa mpaka leo hii bado anapata kipindi kigumu kwa ajili ya ile video yake.

Nandy ambaye amekiri kuwa anatamani sana aweze kupanda usafiri wa umma maarufu kama daladala ili aweze kupata nafasi ya kukutana na mashabiki zake Uso Kwa Uso lakini ameweka iankuwa ngumu kutokana na ile video yake.

Kwenye mahojiano na Showbiz Xtra Nandy alisema kuwa, alipanga karibu mwezi mzima kufanya ziara hiyo ya kila sehemu atakayoenda atumie usafiri wa daladala ili aweze kupata nafasi nzuri ya kujua mambo mbalimbali ndani ya daladala na kuna wakati anazitamani stori za humo.

Nilipanga ndani ya mwezi mzima usafiri wangu uwe huo lakini mambo yakaingiliana na ya kusambaa ile video ya faragha kwenye mitandao ya kijamii, lakini bado dhamira yangu ipo nitafanya hivyo kwa sababu natamani kukutana na watu tofauti”.

Mwezi uliopita Nandy alipata fedheha hiyo baada ya video yake ya faragha na aliyekuwa mpenzi wake Billnas kusambaa Mtandaoni baada ya kukataa sio wapenzi kwa mara nyingi tu.

Baada Ya Video Ya Utupu Nandy na Billnas Waamua Kuwa Kaka na Dada

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy na aliyekuwa Mpenzi wake msanii mwenzake Billnas wameamua kuweka chuki na uadui pembeni na kuwa koa na dada.

Wiki chache zilizopita Nandy na Billnas wali trend vibaya mno baada ya video yao ya ngono kuvujishwa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha kizaazaa.

Baada ya video hiyo kuvujishwa Kwenye mitandao ya kijamii kila mmoja alianza kumbyooshea kidole mwenziye kwani Billnas alidai aliyerekodi ile video ni Nandy na sio yeye kwaiyo aliyeivujisha hakuwa yeye lakini na Nandy naye alikataa kuvujisha video ile.

Lakini hatimaye tangu sakata hilo litokee Nandy na billnas wameamua kuweka pembeni tofauti zao na Kusonga mbele na wameamua kuwa kaka na dada.

Jana Nandy aliachia ngoma yake mpya inayoitwa Ninogeshe na Billnas alikpa sapoti kwa kuposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kumuita dada yake na Billnas naye alimuita kaka.

 

 

Nandy Akana Kuvujisha Video Yake Ya Ngono

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amekana kabisa taarifa zilizoenea kuwa yeye mwenyewe kwa mkono wake ndiye aliyesambaza video yake ya ngono na Billnas kisa kiki.

Wiki chache zilizopita Nandy na Billnas wali trend vibaya mno baada ya kuonekana kwenye video iliyovuja Mtandaoni wakiwa kitandani wakifanya mambo yao.

Kwenye mahojiano aliyofanya leo na kipindi cha Leo Tena cha Clouds Fm, Nandy amekanusha kuwa video yake na Billnas haikuwa mpango wa kiki kama  wengi wanavyodhani na taarifa za kusambaa kwa video hiyo zilimuathiri kiafya kiasi cha kupoteza fahamu mpaka kukimbizwa hospitalini.

Ile video haikuwa kiki na wala sonata tabia ya kufanya kiki, wakati video inasambaa milioni huwa simu na meneja wangu kuniuliza na kiukweli baada ya kuiona ile video nilihisi sio mimi niliishiwa nguvu na uongozi wangu unasema niliishiwa fahamu kwa masaa kadhaa”.

Tangu video hiyo itokee nandy amekiri kuwa katika wakati mgumu kwani ni siku chache zilizopita kuna video iliyo trend ikimuonyesha akiangua kilio stejini hadi kushindwa kupiga shoo na meneja kumtoa stejini.

Nandy: Siyo Sahihi Kujirekodi Ukiwa Mtupu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amefunguka a kuweka wazi kuwa kuvuja kwa video yake ya mahaba chumbani na aliyekuwa mpenzi wake Bilnass imemfunza mambo mengi ikiwemo sio vyema kujirekodi ukiwa uchi.

Sakata hili lilimkuta Nandy wiki iliyopita baada ya video yake akiwa chumbani na mpenzi wake Billnas wakiwa wamevaa nguo za ndani huku wakiwa nikaona ya kimahaba kuvuja mtandaoni na kusababisha tafrani.

Nandy amefungukia majuto yake kwenye mkutano na waandishi wa habari aliofanya alipotoka katika ofisi za mamlaka ya mawasiliano Tanzania na kuweka wazi kuwa amejutia sana kitendo hiko na sasa yupo tayari kushirikiana na serikali kwa ajili ya kutoa elimu kwa watu:

Nipo Tayari kushirikiana na serikali kwa hilo lililotokea na kuelimisha wasanii, wanafunzi na jamii kwa ujumla najua watu wengi wanapitia hatua kama hizi na wengine hata hawajulikani lakini kwa kuwa limetokea kwangu Ilan najua kuna watu wengine wamefanya mambo kama haya na video zimeenda mitandaoni bila idhini yao”.

 

Nandy Aweka Sanaa Pembeni Baada ya Skendo Yake

Mwanamuziki wa bongo fleva kutoka Nyumba ya vipaji (THT) Nandy amejikuta katika wakati mgumu baada ya video yake ya ngono na msanii mwenzake Billnas kuvuja siku ya jana Nandy bado yupo katika wakati mgumu.

Tangu video hiyo ivuje  siku ya jana Nandy ameweka wazi hisia zake na amesema mara kwa mara kuwa hayupo vizuri na yupo katika wakati mgumu huku akielezea kuwa amelia sana na anaendelea kuomba radhi.

Mchana huu Nandy ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwagombanisha radhi Tena mashabiki zake familia na hata BASATA na serikali Lakini pia ameweka wazi kuwa anaweka sanaa kando kwa sasa mpaka atakapokuwa vizuri.

[ajax_load_more]

 

Baada Ya Video Yao Ya Utupu Kuvuja Mtandaoni Nandy na Billnas Watupiana Lawama

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy na rapa Billnas jana walitengeneza headlines za mitandao ya kijamii kwa kazi ya ajabu baada ya video yao ya ngono kuvuja mtandaoni.

Video hiyo iliwaonyesha wakiwa chumbani faragha nusu utupu wakifanya yao hali iliyomuonyesha taharuki kwa mashabiki zao.

Baada ya video ile kuvuja kila mmoja ameanza kumnyooshea kidole mwenzake kuwa anahusika na kuvujisha video hiyo.

Nandy amefunguka haya kuhusiana na kuvuja kwavideo hiyo:

Nilikuwa na mahusiano na Bill Nass mwaka 2016, nilikuwa na mahusiano na Bill Nas na tulikubaliana iwe siri, sasa sielewi kwa sababu gani kaamua kuvujisha, nimesikitishwa sana, ni video ambayo ilishutiwa kwa snapchat, sasa sielewi aliipataje hiyo video kwani ni lazima nimrushie ndio aipate, sijui niseme nini, Naomba radhi sana kwa familia yangu, kanisani kwangu, mashabiki serikali yangu kwa kweli video imenichefua sana mpaka hapa ninapoongea nimechefuka, ila adhabu ya maumivu ninayoipata sasa hivi ni kutokana na kumuamini mwenzangu”.

Billnas na yeye amemgeuka Nandy na kudai Nandy ndio anahusika nakuiweka video ile mtandaoni kwani yeye ndio aliichukua kwa simu yake na hakuwahi kumuomba amtumie:

 

Lakini Nandy na Billnas nao wameomba radhi kwa video ile kwani walikana kuwa na Mahusiano kwa kipindi kirefu sana.

Baada Ya Kuficha Mahusiano Yao Kwa Muda Mrefu, Hatimaye Nandy na Bilnass Wayaanika

Mwsnamuziki wa Bongo fleva Nandy anayetokea nyumba ya vipaji THT na mpenzi wake rapa Billnas hatimaye waneanika penzi lao hadharani baada ya kulificha kwa muda mrefu.

Kwa kipindi kirefu Kumekuwa na tetesi kuwa Nandy na Billnas wana mahusiano ya kimapenzi na bata picha zao wakiwa maeneno sawa kwa wakati mmoja zilisambaa lakini kila mmoja alikana mahusiano hayo na kusisitiza kuwa ni marafiki.

Lakini waswahili wanasema mapenzi kikohozi kwani baada ya kuficha kwa muda mrefu hatimaye wawili hao wameonekana wakiwa pamoja kwenye picha ambazo wameposti Kwenye mtandao wa Instagram.

Leo ni siku ya kusheherekea siku ya kuzaliwa ya Billnas kama ilivyo desturi Nandy kamtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nandy kamuandikia ujumbe wa heri na kusindikiza na picha yao: