Bilnass kufanya kolabo na alikiba

Msanii anaetamba kwa sasa na wimbo wake mpya wa funga geti  BILNASS amefunguka na kusema kuwa ile kolabo aliokuwa akisubiri kuifanya kwa muda mrefu  kati yake na Alikiba kwa sasa imekwisha kamilika na iko mbioni kutoka.

Akiongea na Times Fm , Billnass anasema kuwa  wimbo huo uko tayari lakini hawezi kuutoa kwa sababu ya Alikiba yuko chini ya uongozi ambao ni lazima kufuata utaratibu fulani kabla ya kuachia ngoma , hivyo taratibu hizo zikikamilika basi wataweza kuutoa.

kolabo na Alikiba tayari tulishafanya bado tu kutoka kwa sababu ya taratibu zao na hii ni kwa sababu alikiba yuko chini ya Sony na wamekuwa na utaratbu wao, Hivyi ninasubiria utaratibu wao tu kama itatoka mwakani au mwaka huu.

 

Nandy Afunguka Baada Ya Kuonekana Tena na Billnas

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ na msanii mwenzake anayefanya muziki wa hip hop William Lyimo ‘Billnas’ walirudi kwenye headlines tena na kuzua gumzo Baada ya kuonekana pamoja.

Gumzo hilo lilizuka wiki iliyopita Baada ya Nandy kiposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ilimuonyesha akiwa pamoja na Billnas na msanii mwenzao Dogo Janja.

Baada ya kuposti picha hiyo maneno mengi yalisemwa ikiwemo tetesi as kwamba huenda wawili hao wamerudiana ama vipi huku baadhi ya mashabiki kuonekana kufurahia wawili hao Kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Nandy alisema hana kinyongo kabisa Billnas kwani walishamaliza tofauti zao tangu zamani hivyo kwa sasa wao ni washkaji tu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

Mimi na Bill sasa hivi ni washkaji tu, hakuna chembechembe yoyote ya mapenzi kati yetu, tulishaachana muda mrefu na kila mtu ana maisha yake, sioni tatizo kuwa naye karibu”.

Wawili hao walishawahi kuwa kwenye mahusiano siku za nyuma lakini walikuja kuachana na hata video yao ya faragha kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Billnas Amtaka Steve Nyerere Afungue Biashara Ya Mambo Ya Misiba

Msanii wa Bongo fleva anayetamba na kibao chake cha Labda Bill Nas amempa ushauri wa bure msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka afungue kampuni yake ya binafsi itakayoshughulikia mambo ya misiba.

Steve Nyerere siku za hivi karibuni amekumbwa na skendo ya Kula fedha za rambi rambi zinazochangwa na watu kwa ajili ya kuwafikia wafiwa.

Steve Nyerere na Billnas waliingia Kwenye bifu zito mapema mwezi huu baada ya Steve kumwambia maneno kuhusu yeye na Nandy jambo ambalo halikumfurahisha kabisa Billnas.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv, Billnas ameibuka  kumtaka Steve kuweka ugizaji wake wa vichekesho pembeni na badala yake ajikite kwenye biashara ya kuandaa misiba maana ndio anayoiweza:

Steve badala ya kutumia pesa zake kuandaa comedy shoo kubwa sijui anaweza kufungua kampuni ya kushughulikia mambo ya misiba na inaweza kuwa kampuni kubwa tu na akatengeneza hela na akatumia mtaji huo huo mdogo akanunua magari ya kubebea maiti na akafanikiwa zaidi”.

 

Billnas Afungukia Tuhuma Za Kuwa Mariooo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kurap, Billnas amefunguka na kukataa kata kata tuhuma alizorushiwa na Steve Nyerere kuwa ni mariooo.

Hivi karibuni Billnas na Steve Nyerere walijikuta katika vita kali ya maneno Kwenye mitandao ya kijamii baada ya Steve kumtuhumu Billnas baadhi ya mambo ikiwemo kuwa Marioo.

Billnas ameibuka na kukana taarifa hizo sio tu kwamba sio Marioo bali pia amemnyooshea kidole Steve na kudai inawezekana yeye ndio marioo maana anaonekana tu.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemwagia povu hili Steve Nyerere:

Mimi siwezi kuwa marioo halafu ukishawahi kusikia msemo “Anayesifia mvua ujue imemnyeshea” basi ndiyo yule ukiona mtu amezidiwa anakimbilia umarioo basi ujue yeye ana fanya huo umarioo.

Kwanza sina hiyo lifestyle ya kimarioo na siwezi kuwa Marioo ndio maana nina vitu kama Tagi Ubavu kwaiyo asiongee kitu ambacho hakijui”.

 

Billnas Amtolea Uvivu Steve Nyerere na Kumtaka Apeleke Komedi Zake Majukwaani

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva ambaye anafanya vyema na ngoma yake mpya ya ‘Labda’ amemtolea uvivu msanii wa Bongo movie Steve Nyerere na kumtaka apeleke komedi zake majukwaani.

Bifu kati ya Billnas na Steve Nyerere lilianza juzi baada ya Steve kumtolea maneno Billnas na kumuita Mariooo na maneno mengine ambayo yalipelekea wasanii hao kujibizana Kwenye Instagram.

Lakini sasa Billnas amemtolea maneno Steve na kumtaka aache kumfuatilia na kama nia yake ilikuwa ni kuchekesha watu kumpitia yeye basi amekosea ni bora angefanya komedi zake kwingine kwani alivuka mipaka ya utani.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Billnas amemtolea povu hili Steve Nyerere:

Komedi zake asilete Kwenye vitu vyangu mimi ile ni kazi yangu yeye kama anataka kufanya komedi si yapo majukwaa ya komedi?.

Halafu isitoshe mimi sio mtu ambaye nina Vibe naye yaani sina ukaribu naye kihivyo mambo hayo angefanya mtu kama Idris ingawa hata yeye kuna mipaka hawezi kuvuka”.

Lakini pia Billnas ametoa onyo kwa watu ambao wamekuwa wakimtania tania kuhusu ishu yake na Nandy tangu itokee:

 Hata kama mtu anakutania isiwe too much maana siku hizi naona watu watu wanapenda kunivaa vaa yaani unashangaa mtu from nowhere anamuandika Billnas”.

 

Mdogo wa Billnas Afunguka Kuhusu Mstari wa ‘Tag Ubavu’ Unaomkana Baba YaO

Mdogo wake na Billnass ambae walishare baba mmoja amefunguka na kuzungumzia huzuni yake na baba yake pia hasa baada ya kusikia wimbo wa tag ubavu ambao kuna mstari katika wimbo huo unaelezea kuwa billnass  hamjui baba yake na wala hataki kusikia stori zake.

Katika wimbo wa tag ubavu kuna sehemu inayosema “DINGI HAMJUI NA HATA SRORI ZAKE HAZIKUSUMBUI’ , Mstari ambao umeibua stori na huzuni kwa familia yak kwa sababu hata kama kweli baba wa billnass hakuhusika katika kumlea billnass lakini kuna baadhi ya maswala yanabaki kuwa ya kifamilia.

Steve ambae ni dogo wake na Billnass anamhoji kaka yake alijisikiaje kuimba sehemu hiyo huku akijua kabisa baba yake yuko hai na kwamba hata kama baba hakumlea lakini bado hakupswa kuongea hivyo kwa sababu kuna siri zingine za familia huwa zinabaki katika familia tu, hivyo katika ukurasa wake wa instagram aliandika:-

loh Billnas sijajua kama uliwaza baba atajisikiaje pindi ulipouwa ukiandika  na kurekodi dingi haumjui na hata stori zake hazikusumbui,wengi sana wapona tunajua kuwa hawajalelewa na baba zao lakini walibaki kuwaheshimu kwa sababu ukweli wa nani ni mkosaji kati  ya baba na mama  ni siri yao wazazi hivyo inabaki kuwa hivyo na sio vyema kuwakashfu wazazi , maana atabaki tu kuwa baba yako hata kama utamzidi kwa kipato au elimu  bila kujali amekutunza au hajakutunza  kiukweli mzee ameumia sana  na hajapenda lakini tukuombee tu kwenye muziki wako.

Billnas Afunguka Kuhusu Ndoa Yake na Jinsi Ali Kiba Alivyohusika

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas amefunguka na kuweka wazi kwa nini alitangaza ndoa yake mapema mwaka huu.

Bill Nas aliungana na wasanii wengi ambao wametangaza wanatarajia kuuaga ukapera hivi karibuni na kufunga ndoa.

Kwenye Interview yake na Wasafi Tv, Bill Nass amesema kuwa anaamua kuoa kutokana anapenda familia, pia wasanii wanatakiwa kuwa kama watu wengine kwani kufanya hivyo haimaanishi msanii atashuka kimuziki.

Niliposti kuhusu kuoa na pia kuhusu nani nitamuoa nitaamua mimi sio mtu mwingine. Mtu kama Alikiba anaweza kuoa na game yake bado ipo strong kuna kila haja, na pia inatambulisha kwamba ndoa ni jambo muhimu lakini pia sisi ni wasanii na ni watu kama wengine”.

Lakini pia Bill Nas ameweka wazi kuwa siku aliyohudhuria Harusi ya msanii mwenzake Ali Kiba alizidi kupata morali ya kuoa baada ya kuona jinsi mtoto wake alivyokuwa na furaha:

Mtoto wake alikuwa happy sana kwenye ile harusi kwa hiyo ile ilini-impress zaidi”.

 

Billnas Afungukia Mahusiano Yake na Ali Kiba

Mwanamuziki wa Bongo fleva Billnas amefunguka na kuweka wazi kabisa uhusiano wake na staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Billnas amerudi Kwenye headlines huku safari hii Ikiwa ni uhusiano wake wa kikazi na Ali Kiba. Siku chache zilizopita kuna taarifa za sintofahamu zilisambaa kumuhusu Billnas na Ali Kiba.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Billnas amefunguka kuhusu tetesi zilizodai kuna ngoma kati yake na Alikiba inakuja.

Nina Mahusiano mazuri na Ali Kiba na huwa ananishauri mambo mengi katika kazi zangu na hata muda mwingine huwa tunataniana naamini anakubali kazi zangu maana huwa nikiachia ngoma ananiambia mdogo wangu hapo freshi au kazia buti sehemu fulani.

Sitaki kuliweka sana hilo mbele ila watu wajue tunayo mahusiano mazuri kama nilivyo na mahusiano mazuri na wasanii wengine“.

Billnas anayefanya Muziki wake katika miondoko ya kurap anafanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Tagi Ubavu”.

 

Billnas Atangaza Kufunga Ndoa Mwakani

Mwanamuziki wa Bongo fleva William maarufu kama Billnas amefunguka na kutangaza nia yake ya kufunga ndoa mwakani.

Billnas amekuwa Kwenye headlines sana wiki tatu hizi kuanzia kuhit kwa wimbo wake wa ‘Tagi bovu’ mpaka skendo yake ya video ya utupu na msanii mwenzake Nandy.

Billnas amerudi Kwenye headlines baada ya kutangaza kuwa ana mpango wa kuoa mwakani na kusisitiza kuwa uwezo wa kuoa anao.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Billnas aliweka wazi mipango yake ya kufunga ndoa ndipo msanii mwenzake Chege alipomjibu na kumwambia woe mara ngapi maana amekwisha oa:

Mwakani nisipofunga ndoa sio mimi…. Yaani mimi nisioe kweli???”.

Uamuzj huu wa Billnas umekuja baada ya kuhudhuria ndoa ya msanii mwenzake wa Bongo fleva Ali Kiba.

Bill Nas Amefungukia Tuhuma Za Kupenda Kufanya Kolabo na Wasanii wa Kike Tu

Mwanamuziki wa Bongo fleva Bill Nas anayefanya vema kabisa kwa hivi sasa na wimbo wake wa ‘Tagi bovu’ amefunguka na kuongelea tuhuma zinazomkabili ya kwamba anafanya sana Kolabo na watoto wa kike kwa sababu ana Mahusiano nao.

Billnas amefanya Kolabo nyingi sana na wasanii wa kike kuliko hata kiume na kuna madai kuwa wasanii hao wa kike kuliko hata wa kiume na kuna madai kuwa wasanii hao wa kike aliofanya nao collaboration kuna ambao amekuwa nao kimapenzi.

Billnas ameshafanya kolabo na wasanii mbali mbali wa kike kama vile Rosa Ree, Dayna Nyange, Nandy, Linah na Mwanadada Nazizi kutoka Kenya na hivi karibuni ana Kolabo mpya na Mwasiti insyoitwa ‘Bado’.

Billnas amefungukia tuhuma hizo wenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews ya EATV ambapo amekataa tetesi hizo na kusema hazina ukweli wowote:

Habari hizo sio za kweli kabisa kwa sababu mimi nimefanya Kolabo na wasanii wengi wa kike Kasoro wachache tu lakini sina Mahusiano nao hawa wote ni dada zangu tu alafu isitoshe mimi sina dada kwenye familia yetu”.

Lakiji pia Billnas amesema aneshafanya kazi na wasanii wa kiume wengi tu kama Country Boy, Mwana FA, TID, Edu boy na amesema anategemea kupiga kazi na Ben Pol na Gnako.

 

Billnas Achoshwa na Skendo za Mapenzi Kila Siku Juu Yake

Msanii wa muziki bongo anaetamba na kibao chake kipya cha tag ubavu , Blnass amefunguka na kuongelea jinsi mitandao ya kijamii inavyokuwa inamharibia kazi na mahusiano yake kwa kumsambazia habari ambazo sio za kweli hasa katika swala la mahusiano.Bilnass anasema  kuwa hakuna kitu kinamkera na kumnyima amani  kama anapopata skendo hizo  za kuwa na mahusinao na wasanii wenzake kwa sababu vitu hivi sio vya kweli na vimekuwa vikimkosesha amani kabisa.

Bilnass anasema kuwa inamfanya anashindwa kufanya  kazi zake kwa sababu amekuwa akisingizia  kuwa na  mahusiano na watu ambao yeye yupo nae karibu kikazi tu na wala sio vinginevyo.Lakini pia skendo hizo mara nyingi zinamfanya anakosa amani katika mahusiano yake ya kweli kwa sababu mpenzi wake wakati mwingine anaamini kuwa ni kweli anatoka na wasanii wenzake.

sipendi sana pale ninapozushiwa kuwa natoka kimapenzi na waanii wenzangu kwa sababu niakosa amani na mahusiano yangu ya kweli.hizi skendo zinakuwa zinaniharibia sana kwa sababu hata yule niliyenae katika mahusiano kuna muda mwingine anahisi kuwa maneno hayo ni ya kweli kuwa nina mahusiano na watu waliotajwa ukiangalia nina ukaribu nao, hi inaniharibia sana.-Bilnass anatoa dukuduku lake alipokuwa akifanya mahojiano na  Ful shangwe ya GPL.

Katika mitandao, Billnass amewahi kuzungumziwa kuwa na mahusiano ya kimapezni na Dayna Nyange kutokana na ukaribu waliokuwa nao kipindi wanatoa wimbo wa Komela, ikaja tena akazushiwa kutoka kimapezni na Nandy na sasa hivi katika mitandao amepata skendo nyingine ya kutoka kimapenzi naip-hop mwana h Rosa ree kwa sababu ya kazi yao mpya iliyowafanya kuwa karibu.

Billnass Afurahia Petit Man kuondoka LFLG

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchi Billnass amesema kuwa kuondoka kwa aliyekuwa meneja wake wa zamani Petit Man kumempa unafuu kidogo ukizingatia kuwa kuna vitu alivyovifanya meneja huyo ambayo vilileta athari kubwa saa kwake kuliko kwa mtu mwingine yoyote katika lebo yao ya lflg.

Akiogea leo katika XXL ya Cloud Tv, wakati akitambulisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Tagi ubavu (self made) , Billnass anasema kuwa Petit Man aliamua kuondoka siku zzi nyuma kidogo lakini haweiz kusema chochote kuhusu kuondoka kwake kwa sababu hata wakati anaingia na kupokelewa hakuna aliyejua wala hakuna aliesema  kwanini aliingia katika lebo hiyo.

 Siwezi kusema kwanini ameondoka kwa sababu hata wakati anaingi hakuna aliyesema kwanini ameingia.Kuondoka kwake hakujaniathiri chochote kwa sababu hata wakati yupo kuna kitu alikifanya na kiliniletea damage kubwa sana kwa upande wnagu kuliko kwa mtu yoyote,kwaio imekuwa sawa maana ni kama vile nilikuwa namsubiri aondoke tu.

Hata hivyo billnass alipoulizwa kuhusu uhusiano wao kwa sasa na kwanini anaonekana kama anafurahia kuondoka kwa aliyekuwa meneja wake petit, bill nass alisema hawajagombana na wako poa kabisa.

Mimi na Petit tunaongea poa tu na tunawasiliana  hatujagombana kabisa ila tu hatuko pamoja tena kama zamani.

Bilnass na Petit Man walikuwa ni watu wanaofanya kazi pamoja na hata baadhi ya sehemu walikiwa wakionekana pamoja kama meneja na msanii wake hata baadhi ya ngoma za bill nass kama ile ya chafu pozi na petit man alionekana akitokea katika video hiyo.mpaka sasa hakuna aliye tayari kati yao kuweka bayana ni kitu gani kimewatenganisha au ni damage gani aliingiza kwa Billnass.

Bilnass ametoa wimbo mpya na ameufanya chini ya producer na menaja T-Touch

Billnas: Sijashuka Kwenye Muziki

Mwanamuziki wa Bongo fleva Billnas ambaye ametamba sana na kibao chake cha ‘Sina jambo’ amefunguka na kusema taarifa zinazodai kuwa yeye amefulia sio za kweli kabisa kwani hajatoa nyimbo yeyote tangu alipotoa ‘Sina jambo’.

Baada ya kukaaa kimya kwa muda mrefu  fununu zimeanzq kuzagaa kuwa mziki wa Billnas umeanza kushuka huku wengine wakidai Petit Man Wakuache kuondoka LFMG ndio kumesababisha hayo yote.

Billnas yupo chini ya uongozi unaoitwa LIve Fast LIve good (LGLF) na kwa muda mrefu Petit alikuwa manager wake lakini baada ya mikwaruzano na manager mwingine mwishoni mwa mwaka jana Petit aliondoka kwenye label hiyo na kusababisha Billnas kuwa chini ya uongozi mwingine kitu kilichowaaminisha wengi kuwa ndio Chanzo cha Billnas kushuka kimuziki.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Billnas amekana tuhuma hizo na kufunguka yafauatayo:

Huwezi kusema nimepanda au nimeshuka kimuziki kwa sababu so far kwa sababu sijatoa ngoma yoyote at least wangesema hayo kama ningekuwa natoa nyimbo zinakataa bado naaamini niko juu na material ambayo niko nayo ni nyingi lakini anayeitwa hayo ni mawazo ya watu wengine siwezi kuwakataza kusema “.

Lakini pia Billnas amesema ukimya aliokuwa nao kwenye kutoa nyimbo ni kawaida yake sio kwa sababu hayuko na Petit Man lakini pia amesema ukimya huo kwenye game unatokana na majukumu mengine aliyokuwa nayo ambapo anajishighulisha na biashara zake nyingine sio muziki tu.