Nini Ajutia Kuchanganya Mapenzi na Kazi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kufanya vyema amefunguka na kusema wazi kuwa sio vizuri kuchanganya mambo ya mapenzi na kazi kwani utapotea kimuziki.

Nini aliwahi kuwa kwenye mahusiano na ya kimapenzi na msanii mwenzake Ney wa Mitego ambaye pia alikuwa bosi Wake kwani alikuwa amesainiwa chini ya Label yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Nini amesema wazi kuwa kuna madhara makubwa sana endapo Msanii wa kike atasimamiwa na Mpenzi Wake kwani inaweza ikasababisha Msanii huyo kupotea kwenye gemu.

Kuna madhara kwa mtoto wa kike kusimamiwa na mpenzi Wake kwani tumeona wasanii wengi wa hivyo wameishia kati na hawajafikia malengo yao kwaiyo kama inaweza ikaepukika ni vizuri zaidi lakini cha muhimu wa wasichana kujitambua na kutambua wanataka nini”.

 

“Bado Nampenda Nini, Akitaka Kurudi Niko Tayari”- Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nay wa Mitego amefunguka na kuweka wazi kuwa bado anampenda sana aliyekuwa mpenzi wake na msanii mwenzake Nini.

Wiki chache zilizopita Nini aliweka wazi kuwa Mahusiano Yake na Nay wa Mitego yamefika mwisho na alidai ameamua kumuacha rapa huyo kwa madai amekuwa na michepuko mingi.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Nay amefunguka na kudai bado anampenda sana Nini na kama atakuwa tayari kuwa naye Tena basi yeye Yupo Tayari.

Nay wa Mitego amekiri kuwa ni kweli alifanya makosa ambapo alikuwa ana michepuko kadhaa na Nini alipogundua alimpiga kibuti na hata alipomuomba msamaha hakutaka kumsamehe.

Nay amesisitiza kuwa bado anampenda sana Nini na kama atakuwa tayari kumsamehe hata leo hii basi Yupo Tayari kuwa naye Tena.

Nay amekiri kuwa ingawa yeye na Nini walikataa kuwa hawakuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini walikuwa pamoja kwa miaka zaidi ya miwili na hata kudai walianza Mahusiano kabla hata hajajua kuwa Nini anaimba.

Daxo Chali Yuko Tayari Kufanya Kazi na Nini, ni Baada ya Kuachana na Nay

Mtayarshaji maarufu wa muziki nchini Daxo Chali amefunguka na kusema kuwa yeye hana kinyongo na kufanya kazi na mwanadada nini ambae hapo awali alikuwa akifanya nae kazi lakini alihama kwake na kwenda kufanya kazi na nay wa mitego.

Daxo Chali ambae ndie aliona vipaji vya Nini na Hytham mara ya kwanza na kuanza kufanya nao kazi lakini baadae walikuja kukorofishana sana baada ya Nini kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na Nay wa mitego hivyo kutokuwa na nidhamu na kuwa akifanya yale anayojisikia hivyo kushindwana katika swala la kufanya kazi pamoja.

ata hivyo, baada ya muda Nini na Ney hivi karibuni walijitangaza kuwa wameacana huku sababu kubwa nini akisema kuwa wanawake wengi alionao nay wamemfanya aachane na Nay, Daxo Chali alipoulizwa kuhusu mahusinao hayo alijibu kuwa hajui swala la kuachana kwao kama ni kweli au kiki kwa sababu hata kipindi wapo katika mahusiano walikuwa wakikataa sana.

Daxo Chali aliulizwa kama angeweza kumpokea Nini tena kama atarudi kwake na yeye hakusita kusema kuwa kama nini atakuja kufanya kazi kwake atamokea kama wasanii wengine wanavyokuja na kulipa kiwango kinachotakiwa basi hana kinyongo cha kufanya nao kazi.

Daxo Chali anasema kuwa anafurahi kuwasaidia wasanii na kufikia muda wa kujitambua na kuamua kufanya kazi kama wao hivyo kwa Nini hakuwa na shida nae hata kidogo na ndio maana alimuacha aende.

Nini Akiri Kuvunjika Kwa Penzi Lake na Nay Wa Mitego Kisa Michepuko

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nini amefunguka na kuweka wazi kuwa penzi lake na msanii mwenzake Nay wa Mitego limefikia ukingoni hivi karibu.

Nay wa Mitego na Nini walidaiwa kuwa Kwenye Mahusiano kwa muda mrefu lakini walikuwa wanakataa kila wakiukizwa walidai kuwa ni marafiki tu lakini wamethibitisha walikuwa wapenzi baada ya kuachana.

Nini ameibuka na kukataa tetesi zinazoendelea kusambaa kuwa kisa chao wao kuachana ni baada ya familia yake kumlazimisha Nay amuoe baada ya kumchukua mtoto wao na kuishi naye bila kujitambulisha wala kumuoa.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv,Nini amesema ameamua kuachana na Nay wa Mitego kutokana na kumchukulia poa na kuwa na mahusiano na wanawake wengine.

Ni kweli nimeachana na Nay na niweke hili sawa sijawahi kuishi nyumba moja na Nay na hata hiyo ishu ya wazazi wangu kwenda kwa Nay sio kweli.

Unajua kwenye mahusiano kuna mambo mengi sana na mtu kama mwanaume unaweza ukampenda, ukamuheshimu akawa anakuchukulia poa, anakufanyia drama anakuletea wanawake“.

 

Nay Wa Mitego Adaiwa Kuvunja Mahusiano na Nini Baada Ya Familia Yake Kutaka Ndoa

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amedaiwa kuvunja Mahusiano na mpenzi wake Nini baada ya familia ya Nini kutaka afunge ndoa na binti yao.

Shilawadu wanaripoti kuwa Nay wa Mitego na mpenzi wake Nini wamejikuta katika wakati mgumu baada ya familia ya Nini kumkalia kooni Nay na kumtaka amuoe Nini.

Nay na Nini wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa muda kidogo Lakini sasa inadaiwa Familia ya Nini imekuja juu na kumtaka Nay amuoe binti yao baada ya kukaa naye nyumbani kwake.

Inadaiwa Nini alihamisha makazi yake nyumbani kwa Nay na kila Familia yake ilikuwa ikimtafuta arudi nyumbani alikuwa anagoma ndipo walipoamua kumsaka na kumtaka afunge ndoa.

Lakini inasemekana kuwa Nay alikuwa anawapiga chenga kila wakimtafuta anajificha hataki kabisa kuonana na Familia ya Nini.

Siku ya leo Nay wa Mitego Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kumtosa Nini na kudai yupo single ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alisema “It’s Official I am Single”.

“Daxo Chali Alikuwa Aliniimbisha Muziki Siujui”- Nini

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya Kolo, Mwanadada Nini ameibuka na kudai Daxo Chali alikuwa hajamjulia mziki wake wa kufanya kwani alikuwa anaimba nyimbo za ajabu.

Kama utakumbuka Nini alikuwa yupo chini ya label ya MJ Records chini ya Producer Daxo Chali lakini aliishia kutimuliwa baada ya kudaiwa kuwa na utovu wa nidhamu.

Baada ya kuondoka Kwa MJ Records, hivi sasa Nini yupo chini ya uongozi wa Nay wa Mitego ambapo amedai ndipo alipopatia umaarufu zaidi na muziki wake kujulikana zaidi kwani anafanya muziki mzuri.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Nini amedai kuwa mziki aliokuwa anaimba chini ya uangalizi wa Daxo CHali haukuwa muziki sahihi kwake na wala alikuwa haujui wala haupendi.

Mashabiki zangu wameongezeka kwa sababu mziki ninaoinba sasa ni tofauti na niliokuwa naomba kwa Daxo Chali kwa sababu mziki ninaoinba sahivi ni ule mziki ambao Watanzania wameshazoea kuusikia na kuupenda na  mimi nafurahia zaidi kuimba stabilizer hii ya hivi sasa”.

Kumekuwa na tetesi kuwa Nini anatoka kimapenzi na Nay wa Mitego, taarifa ambazo mwenyewe amezikataa kabisa.