Nisha Awatolea Povu Wanaoisakama Shepu Yake

Msanii wa filamu na muziki wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ameibuka na kuwajia juu watu ambao wamekuwa wakimsema kuwa shepu yake ni feki.

Sakata hilo lilijitokeza siku chache zilizopita baada ya Nisha kuweka picha katika ukurasa wake wa kijamii iliyomuonyesha akiwa na shepu na umbo namba nane ambayo hakuwa nayo kwenye picha zake nyingine.

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nisha alisema watu wamekuwa wakichonga sana hivyo amewaachia nafasi waendelee kwani hawamuongezei wala kumpunguzia chochote.

Hao mashabiki nimewaacha tu wazidi kushambulia kwa sababu bando ni lao, simu ni zao, mimi sijali chochote maana kujibishana na watu ni kupoteza muda kwenye vitu ambavyo siyo muhimu wala havina faida kwangu”.

 

Nisha- Sijawahi Kuvaa Kigodoro Hili Umbo Nimepewa na Mungu

Muigizaji wa Bongo Movie Salma Jabu maarufu kama Nisha amefunguka na kudai umbo lake watu wanaloliona Kwenye picha ndio halisi na wala hajawahi kuvaa vigodoro.

Siku chache zilizopita Nisha alipata skendo ya kuvaa vigodoro vya kumuongezea shepu baada ya picha aliyoweka Mtandaoni kumuonyesha akiwa na maumbile makubwa tofauti na uhalisia wake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nisha amefunguka kuwa alichukua futi na kujipima makalio na matiti yake na kuwaangalia mastaa wanawake wenzake ambapo aligundua kwamba anawazidi sana na anamshukuru Mungu kwa kumpa zawadi hizo nzuri za kudumu.

Najikubali mwenyewe hata kama watu wakinishambulia, sijavaa kigodoro kwenye picha niliyoweka mtandaoni bali ni jinsi Mungu alivyonijaalia na hakuna staa wa kike anayenifikia, najivunia sana kwa kweli“.

Nisha ameshawahi kumwaga povu siku za nyuma baada ya mashabiki zake kumsema kuhusu kukosa shepu ambapo alidai aliyonayo imemtosha kabisa hivyo hahitaji mchina.

Nisha: Sitoweza Msahau Mzee Majuto Maishani

Msanio wa filamu za kibongo na msanii wa Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha amefungukia Kifo Cha Msanii mwenzake mkongwe wa Bongo movie na comedy Mzee Majuto aliyeaga dunia wiki iliyopita.

Nisha amefunguka na kudai yupo katika majonzi mazito katika kipindi hiki ambacho Msanii huyo Nzee Majuto amefariki dunia kwani pengo alilomuachia haliwezi kuzibika katu.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Nisha alieleza kuwa, kifo cha Mzee Majuto kimemuumiza kupitia kiasi na pengo alilomwachia moyoni mwake ni kubwa kwani mashabiki wa filamu hasa za vichekesho wasingemjua.

Mzee Majuto nilikuwa namwita baba kwa sababu amenitoa kisanaa, yaani alikuwa ni kiungo muhimu sana maishani mwangu, machozi na maumivu yangu havitafutika, nashindwa kuamini na pengo lake halifutiki maishani mwangu”.

Mzee Majuto alifariki dunia siku chache zilizopita katika hospitali ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Nisha- Wasanii Wanapenda Kiki Sababu Watanzania Wanasapoti Kiki Kuliko Kazi Zao

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ameibuka na kuwatetea wasanii wanaofanya kiki sana na kudai Watanzania wanapenda sana kiki.

Wiki iliyopita Nisha alishika headlines sana baada ya kusambaza picha Kwenye mitandao ya kijamii akiwa na mzungu ambaye alidai ni mume wake ambaye baadae ilikuja kujulikana kuwa ni mtu aliyefanya naye video tu.

Baada ya mashabiki kumjia juu na kumtuhumu kwa kupenda kiki Nisha amewatolea povu na kudai yeye pamoja na wasanii  wengi wanapenda kiki kwa sababu mashabiki wanafuatilia umbea unaowahusu kuliko kazi zao.

Nisha alimwaga povu hilo Kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuandika:

Watanzania wengi wanawasema wasanii wengi kuhusu kiki, Ila wanasahau kuwa wao ndio namba moja wanapenda umbea kuliko kazi zetu.

Tazama tukitoa umbea tunavyosapotiwa kuliko kazi, Yeye ni wimbo ulionifunza mengi”.

Mara ya mwisho Nisha alitoa wimbo wake wa kwanza ambao ulisindkizwa na kiki ya kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Ex wa Wolper Brown.

Nisha Atolewa Povu na Mke wa Mzungu

Msanii wa Bongo movie aliyegeukia tasnia ya Bongo fleva Salma Jabu maarufu kama Nisha ametokewa povu zito na mke wa mzungu Anatoly Shmakov aliye trend naye Kwenye social media wiki iliyopita.

Mwanamke huyo amejitambulisha kwa jina la Felista ambaye amedai ni mke wa mzungu ambaye alionekana Kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita akiwa na Nisha ambapo Nisha alidai ni mpenzi wake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Felista amedai ameshangaa kumuona Nisha anamuita mzungu yule mpenzi wake wakati yeye ni mume wake halali wa ndoa kabisa:

Kwanza mimi sikuona picha hizo mwanzo, ila nilipigiwa simu na rafiki yangu yupo Zanzibar na kuniuliza kama nimeziona hizo picha mtandaoni.

Kwa kweli nilishtuka sana baada ya kuziona picha hizo kama mke na yule ni mume wangu imeleta shida sana kwenye familia.

Nilijaribu kumuuliza mume wangu kuhusiana na picha hizo na yeye ilimshangaza kwani alipokuja Nisha nyumbani kwangu, alimuomba awe kwenye video ya wimbo wake na zile picha zipo kwenye video ya huo wimbo lakini haikuwa makubaliano ya kutangaza vile mitandaoni kuwa ni mwanaume wake. Sijapenda kwa kweli alivyofanya”.

Lakini mwanamke huyo ameweka wazi kuwa yeye na mume wake sasahivi wako vizuri:

Sasa hivi tupo sawa tumeyamaliza kifamilia maana ilikuwa ni tatizo sana“.

 

 

Nisha- Biashara Zimenipa Mafanikio Kuliko Filamu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Salma Jabu maarufu kama Nisha amedai biashara zake za nguo zimeweza kumpatia mafanikio ya haraka ambapo mpaka sasa tayari ameshanunua nyumba na magari ya kutembelea.

Nisha amefunguka Kwenye mahojiano na Bongo 5 na kuweka wazi kuwa alipokuwa anafanya Bongo Movie alikuwa anapata pesa ndogo ndogo sana ambazo aliziweka na kuanzisha biashara yake kuuza nguo ambayo amekiri kuwa imempa mafanikio mengi sana.

Mimi filamu nimeanza kucheza kama hausegirl nikilipwa sana labda elfu ishirini lakini pesa hiyo hiyo ndio imenipa leo hii biashara yangu ya nguo ambayo inanifanya mimi kila siku niende benki kwenda kuweka pesa”.

Lakini pia Nisha ameanika mali zake alizozipata Kupitia biashara zake.:

Kwa kweli mimi nina nyumba nina magari kama unavyoona nimepaki jingine pale nje kwaiyo namshukuru Mungu biashara zangu ndio zimenipa mafanikio sana”.

 

 

Nisha Adai Anataka Mahusiano na Mwanaume Mwenye Pesa Kuliko Yeye

Muigizaji wa Bongo movie Salma Rajabu Nisha maarufu kama Nisha Bebe ameibuka na kuweka wazi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi ambaye amemzidi uwezo kipesa zaidi.

Nisha amefunguka kuwa inakuwa ngumu kwake kutembea na mwanaume ambaye hana pesa kwa sababu wengi wao aliokuwa nao na wakawa hawana kitu walikosa shukrani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Bongo 5, amedai wanaume wengi waliopita kwake walikuwa wanampenda kwaajili ya pesa lakini sio mapenzi ya kweli.

Nimeshadate tayari na watu ambao hawana mtonyo lakini mwisho wa siku hawana shukrani,” Nisha aliimbia Bongo5. “So kwa sasa hivi siwezi kudate na mtu ambaye nimempita kipato, lazima awe amenipita.

Wanaume wengi ambao walikuwa wanakuja kwangu walikuwa wanataka mpaka kununuliwa nguo, kila wiki wanataka shopping ya nguo, baby sijui nimeona kitu fulani kizuri, sijui nataka kile halafu mwisho wa siku hawana mapenzi wa kweli”.

Wiki iliyopita Nisha alianika Mahusiano Yake na Mzungu ambaye alikiri anajiweza na kipato cha kutosha na hivyo y hatahitaji kumlea.

Mzungu Wa Nisha Anadaiwa Kuwa Mume wa Mtu na Familia Yake

Msanii wa filamu za Kibongo aliyegeukia na Bongo fleva Nisha Bebe amedaiwa kuwa amemchukua mume wa mtu na kisha kumtambulisha kama mpenzi wake.

Siku mbili hizi Nisha ametengeneza sana headlines Kwenye mitandao ya kijamii baada kurusha picha na video zilizomuonyesha akiwa na mzungu ambaye amemtangaza kama mpenzi wake.

Lakini mara moja taarifa zimeenea kuwa mzungu yule hana uhusiano na Nisha kwani ni mume wa mtu na ana Familia yake na watoto na mwanamke mwingine ambaye picha zake zimesambaa Mtandaoni.

Hizi ni baadhi ya picha zinazomuonyesha mzungu wa Nisha akiwa na mwanamke anayesemekana kuwa ni mke wake:

 

 

 

Baada ya Tetesi hizo kusambaa kuwa Nisha kumuona mume wa mtu na kuharibu familia ya watu alifunguka na kukataa tuhuma hizo ambapo alisema:

Walimwengu huwezi kuwakataza kuongea, kama wana ushahidi wa vyeti vyake vya ndoa waniletee“.

Nisha pia amekataa taarifa kwamba huna uhusiano na mwanaume huyo bali ni kiki tu ya ngoma yake mpya ambayo anategemea kuitoa hivi karibuni.

“Uhusiano Wangu Mpya Sio Kiki ni Mapenzi Ya Kweli”- Nisha

Muigizaji wa Bongo movie aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva hivi karibuni Nisha Rajabu maarufu kama Nisha Bebe ameibuka na kuweka rekodi kuwa mzungu aliyeonekana naye hivi karibuni mpenzi wake wala sio kiki.

Siku za hivi karibuni Nisha alimuanika Mwanaume mwenye asili ya Kizungu na kuonyeshana naye mahaba kupitia ukurasa wake wa Instagram lakini ghafla ilisemekana mzungu yule tayari ana Mke wake na kuwa ni Nisha ilikuwa ni kiki ya wimbo mpya.

Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi Nisha aliweka wazi kuwa yule jamaa ni mpenzi wake na ameamua kujaribu kuwa na mzungu baada ya kusalitiwa na wanaume wa rangi nyingine zote:

Ndiyo yule ndio mpenzi wangu, Nimeamua kujaribu kwa Mzungu maana nilishakuwa na Waafrika na Wahindi lakini niliambulia maumivu”.

Lakini pia Nisha alikuja juu alipoulizwa kuhusu suala la mpenzi wake huyo kuwa na mke halali wa ndoa kabisa:

Walimwengu huwezi kuwakataza kuongea, kama wana ushahidi wa vyeti vyake vya ndoa waniletee.  Hii siyo kiki bali ni mpenzi wangu halisi, wamekuwa wakinisema kwamba nakuwa na wanaume wadogo lakini kwa sasa nimempata saizi yangu lakini cha kushangaza hata huyu wanamsema kwamba ni babu sijui hawa walimwengu wanataka nini/?“.

 

Nisha Akana Skendo Ya Kumtongoza Young Dee

Muigizaji wa Bongo movie anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.

Siku ya jana msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha alikuwa anamtongoza Young Dee.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku alikiri kuwa Nisha ni fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.

Baada ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:

Mimi sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka ni kuingia kwenye muziki hivyo  Young Dee kama msanii wa Bongo fleva alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.

Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.

 

Diamond Amliza Nisha Bebe.

Msanii wa muziki nchini Diamond Platinumz amemtoa machozi mwanadada Nisha baada ya kusikiliza wimbo wak wa sikomi.

Nisha amepost  video katika ukurasa wake wa instagram akiwa anasikiliza wimbo wa Sikomi huku akitoa machozi kama ambavyo wimbo huo umekuwa ukitoa maudhui ya majonzi kwa mtu aliyeumizwa na mapenzi.

Nisha ni moja ya wasanii wa kike ambao mara nyingi wamekuwa wakilalamika sana kuuumizwa na mapenzi tena kwa kukimbiwa na wapenzi wao na kwenda kutoka na watu wengine.

Hivi karibuni , Nisha aliingia katika mgogoro na Snura baada ya kusemekana kuwa Snura alimuibia aliyekuwa mpenzi wake nisha kwa makusudi huku akijua kabisa kuwa ni mpenzi wa Nisha.

Nisha Hataki Tena Wanaume wa Bongo

Msanii wa maigizo  na vichekesho Salma Jabu maarufu kaa nisha amesema kuwa kwa sasa hataki tena kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume wa kibongo kwa sababu wana mapenzi ya kuigiza  ambayo kwake anaona yanampotezea muda na kumuumiza.

Nisha anakiri kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa katika mapenzi na wanaume wa kibongo tofauti tofauti na amekuwa akiumizwa kila kukicha hivyo amechoka kuumizwa kama anataka kuingia katika mapenzi sasa hivi atataufua mwanamue wa nje ya nchi na sio mbongo tena.

hivi sasa naanzaje kutoka kimapenzi na mwanaume wa kibongo, walivyowaongo na walaghai hivyo.nimepoteza muda mwingi sana katika kuwapenda wanaume wa kibongo  na kuwathamini lakini ninachoambulia kwao ni maumivu na fedhea.

Nisha amekuwa ni moja ya wasanii wa kike wanaoandikwa sana katika vyombo vya habari kwa maneno ya kuachwa na kuumizwa sana na mapenzi, wanaume wengi anaokuwa nao wanaibiwa na wanawake wenzake na kubaki mpweke,hivyo nisha ameamua kuachana na mapenzi ya mawazo na stress hivyo ameona ni bora kuachana na wabongo kabisa.

Nisha Kulia Na Wanaoiba Mabwana Za Watu

Nisha amekuwa ni moja wa wasanii wa kike ambao kila siku wanalalamika kutokana na wanawake wenzake kumtesa kwa kumuibia wanaume anaokuwa nao kwenye mahusiano.Sio mara ya kwanza  Nisha amekuwa akilalamika kuwa kuna nyakunyaku mjini wamekuwa wakiharibu usingizi wake kila kukicha kwa kumuibia wanaume.

Hivi karibuni alikuwa katika mahusiano na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la ,inu ambapo baada ya kukaa katika mahusiano kwa muda, zilizuka tetesi kuwa mwanaume huyo na Nisha wameachana ambapo baada ya Nisha kutafutwa na vyombo vya habari alikana na kusema kuwa hizo tetesi ni za uongo na kwamba hawajaachana na mpenzi wake huyo.

Lakini kama kawaida mitandao ya kijamii huwa haina siri, hivi juzi Nisha alishindwa kuvumila hilo na kuanza kuposti baadhi ya captions zilikonyesha kuwa tayari alishaumizwa na mwandani wake kutokana na kulalamika kwa kutesa na mapenzi.

Nisha ambae alilalamika katika ukurasa wake wa insta na kusema kuwa kila siku yeye amekuwa ni mtu wa kuibiwa mabwana na kwamba ameshachoka na kitendo hicho na kumalizia kuwa kwa sasa hana haja ya kumuanika mpenzi wake katika mitandao ili aweze kuficha watu wasimjue wasijewakamuiba tena kama alivyoibiwa yule aliyepita.

Lakini moja ya vitu vya kuajabisha ni kwamba mwanaume aliyekuwa nae katika mahusiano , Minu alijibu kwa kusemakuwa ‘”Mwanamke akimwga mbona wewe usimwage ugali, chukua dekio ufute“‘

Hata hivyo Nisha alipotafutwa na gazeti moja kuhusu vijembe hivyo na malalamiko yake  aliishia kucheka na kusema kuwa ‘”jamani kwani hapo ndo nimesemakuwa nimepata mwingine, hahaha‘”