Professa Jay afunguka kuhusu jumba lake la kifahari kuwekwa alama ya kubomolewa (Picha)

Mbunge wa Mikuni Joseph Haule maarufu kama Professor Jay ni miongoni mwa watu ambao nyumba zao zimewekewa alama ya X kuashiria zipo katika hifadhi ya barabara.

Professor Jay amejenga jumba lake la kifahari pembezoni mwa barabara ya Morogoro maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es Salaam.

Jumba la Professor Jay

Hivi karibuni Tanroads imetangaza kuwa muda wowote itaanza utekelezaji wa kubomoa nyumba zilizowekewa alama ya X katika barabara hiyo kupisha ujenzi wa barabara kubwa ya kisasa.

Professor Jay amefunguka kuhusu jumba lake kuwekwa alama ya kubomolewa;

“Wanasema kupanua ni meta 121.5 ni upana mkubwa sana na upande mkubwa sana na watu wengi wataarithirika na wataumia. Kwa sababu tunaamini haki inapatikana mahakamani ndio maana tukaenda kuweka zuio, kuangalia ni jinsi gani tunaweza kupata haki yetu ya msingi lakini kitu kikubwa tunachozidi kusisitiza hakuna mtu anayekataa kuhama kwa ajili ya maendeleo.

“Wengine tumejenga kwa muda mrefu sana, nakumbuka hii nyumba nimejenga kupitia muziki, unapata lakini mbili unatoa elfu hamsini unanunua misumari halafu laki na nusu unakula bata, kwa hiyo unapoona kwamba inabomolewa kwa siku moja na hakuna fidia serikali inatakiwa iangalia kwa jicho pevu,” Professor Jay ameimbia XXL ya Clouds FM.

 

Profesa Jay atajavitu ambavyo vilimpendeza katika harusi yake

Msanii na mbunge kutoka bongo Profesa Jay alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Grace – huku akiwavutia wengi kutoka Tanzania.

Sherehe ya harusi yake ilihudhuriwa na wasanii kama Diamond Platnumz, AY na wengi waliotumbuiza wageni na wazazi wa Profesa Jay na Grace.

Hata hivyo hivi karibuni msanii huyu alifunguka kutaja mambo matatu yaliyomvutia Profesa Jay katika harusi yake. Akizungumza na FNL ya EATV Profesa alisema,

“Chakwanza ni support kubwa ya watu wangu wa mtaa, nikaona watu wote wapo pale especially wasanii wenzangu walikuwepo sana sana, wengine walishindwa kuja kwa sababu mbali mbali,”

Aliongeza kusema;

“Pili media ime-play part yake vizuri sana, lakini kikubwa mbacho namshukuru Mwenyenzi Mungu mbele za haki nimejitahidi hata kuungainsha siasa zetu za Tanzania. Viongozi wote waliopata kuongea  walisema huyu jamaa ametuunganisha, watu wa vyama vyote walikuwa pale, watu wa dini zote walikuwepo pale, ni kitu kikubwa namshukuru Mungu,”

Diamond azua utata kwasababu ya zawadi aliyompa Professor Jay kwenye harusi yake

Professor Jay na mpenzi wake Grace Mkonja walifanya harusi wikendi iliyopita katika kanisa la Katoliki la St. Joseph jijini Dar Es Salaam.

Diamond alijiunga na shamrashamra za harusi ya Professor Jay kwenye ukumbi wa maakuli, staa huyo wa Wasafi aliwatumbuiza wageni kabla ya kumpa Jay zawadi aliyoleta.

Baba Tiffah aliwashangaza wengi kwa kumpa Professor Jay boksi tano za Diamond Karanga na manukato yake ya Chibu perfume kama zawadi.

Diamond akimpea Professor Jay zawadi zake

 

“Nimekuletea hizi boksi unajua uko kwenye ndoa, ndoa nayo inataka uongeze mwili ili watoto watoke wengi,” Diamond aliambia Professor Jay akimpa zawadi zake.

Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond alitumbuiza wageni kwa harusi ya Professor Jay:

Hivi ndivyo alivyofanya Steve Nyerere baada ya Professor Jay kumpigania Bungeni

Professor Jay alitetea haki ya wasanii wote Bungeni aliposimama kuchangia mapendekezo yake katika bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mbunge huyo wa Mikumi alisema TRA na mamlaka zingine za serikali zinawanyanyasa wasanii kwa kuwatoza kodi na ada zingine ambazo wasanii hawazi kumudu.

Tazama video hapo chini:

Kufwatia hatua ya Professor Jay kupigania haki za wasanii Bungeni, muigizaji wa filamu za Bongo – Steve amesema aliamua kummiminia sifa mbunge huyo.

“Mwenye akili anaanza kuelewa nalilia nini kwenye sanaa yetu..Sina haja ya kutukanana ni wajinga wanao tukana. Ukweli unadumu kuliko kitu chochote, ukweli huzaa amani..Asante Mhe. Haule kwa kuongea ukweli”. Alisema Steve kupitia ukurasa wake wa instagram

 

Professor Jay aongelea hatma ya Diamond Platnumz bungeni

Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amefikisha hatma ya Diamond na wasanii wengine kataka Bunge la Tanzania.

Professor Jay alieleza bunge changamoto zinazowakumba wasanii aliposimama kuchangia mapendekezo yake katika bajeti ya Wizara ya Habari, utamaduni, sanaa na michezo kwenye bunge la Bajeti linaloendelea.

Alisema TRA na mamlaka zingine za serikali zinawanyanyasa wasanii kwa kuwatoza kodi na ada zingine ambazo wasanii hawazi kumudu.

“Juzi msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya milioni mia nne, kwa hivyo unaweza ukajiuliza kwamba amekabiliwa milioni mia nne kwa kiasi gani alichoingiza. Lakini dangozi ambazo zinafanyika munaweza mukaona kwamba sasa hivi wasanii wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa wasanii kitu ambacho bado hawajakibandikiza,” Professor Jay aliambia bunge.

Tazama video hapo chini:

“Diamond and Ali Kiba wanazuia mziki wa Tanzania kuenda mbali” Professor Jay asema

Ingawa Professor Jay ni rafiki yake Diamond na hata washawai toa kolabo “Kipi Sijasikia”, msanii huyo anasema beef kati ya Diamond and Ali Kiba inazuia mziki ya Tanzania kuenda mbali.

Professor Jay na Diamond

Professor Jay anaamini mziki wa Bongo ingeenda kwenye level nyingine iwapo mashabiki wa Diamond na Ali Kiba wangekuwa pamoja ili kuipigania Tanzania.

Jay alisema haya alipokua akiongea kwenye Ayo TV.

‘Kitu kikubwa ukiongelea beef iliyopo kwenye bongo fleva ni hii ya Diamond na Ali Kiba nadhani mashabiki wa Diamond na Ali Kiba wangekuwa pamoja ili kuipigania Tanzania kwenda kwenye level nyingine nadhani muziki wetu ungeenda  mbali, kwa hiyo moja kati vitu ningependa kushuhudia siku moja Diamond na Alikiba wakiwa pamoja ikifanikiwa tu hiyo naamini muziki wa Bongo unakuwa level nyingine” Professor Jay alisema.

Professor Jay azungumzia wimbo wake mpya na uanasiasa

Professor Jay (Joseph Haule) ametoa wimbo mpya. Msanii huyo ambaye aliteuliwa mbunge wa Mikumi kwa tikiti cha Chadema miaka mbili iliopita, alizungumzia wimbo yake mpya “Kibabe” and uanasiasa alipohojiwa kwenye redio.

Jay alifunguka kuhusu kazi yake kama mbunge na kuandika wimbo.

“Kitu kikubwa ambacho namshukuru ni kwamba am blessed, yani hii vitu vipo. I am blessed kwa sababu situmii muda mwingi. Mr. T tayari yuko njiani anaweza akaja kwa muda sio mrefu… atakwambia jinsi amabvyo nifanya hii kibali. Yani mara mingi nikipewa pen na karatasi kitu kinaisha kwa sababu huwa ni migodi unaotembea… ni kisima cha mashairi. Kwa hivyo no problem kwa maana tunafanya kazi na wanainchi sana tunapata muda kidogo tunatupiatupia vitu kama hivi,” Professor Jay alisema.