Ali Kiba Amtumia Salamu Za Pongezi Jokate Mwegelo

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Saleh Kiba amemtumia salamu za pongezi Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo kwa kazi nzuri anayefanya.

Ali Kiba ambaye ameshawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Jokate katika siku za nyuma amefunguka kusema Jokate ni mmoja Kati ya viongozi wachapa kazi na kazi sake anazofanya zinaonekana.

Ali Kiba alifunguka hayo kwenye mahojiano na Big Chawa ambaye alimuuliza Kama anachochote cha kumwambia Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mrembo Jokate naye alifunguka:

Namwambia Afanye kazi na pia nimeona kazi zake anazofanya jinsi zinavyoenda vizuri kwa hilo ninampongeza”.

Lakini pia mahojiano hayo Ali kiba amekana taarifa kwamba nyimbo sake mbili alizozitoa mwishoni zimebuma na kudai anaona amefanya vizuri tu Kama siku nyingine.

Diamond Ampa Ali Kiba Ruksa Ya Kudhamini Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na msanii mwenzake Ali Kiba wameonekana kuelekea katika njia sahihi Baada ya Ali Kiba kuomba kuwa mdhamini kwenye Wasafi Festival na Diamond kukubali.

Kupitia, ukurasa wake wa Instagram, King Kiba ameshukuru kupokea mwaliko huo kutoka WCB na kudai kuwa hatoshiriki kwenye Tamasha hilo kwa sasa kutokana na kuwa na ratiba zake za uzinduzi wa kinywaji chake cha MoFaya na hivyo kusema atashiriki Tamasha hilo kwa kudhamini kupitia kinywaji chake hicho cha MoFaya.

Baada ya majibu hayo ya Kiba, Diamond Platnumz Baada ya kukutana na posti hiyo ya kiba aliamua kukomenti palepale kwa kumueleza kuwa uongozi wa WCB unaendelea kuwasiliana na uongozi wa RockyStar ili kuweka mambo sawa na kwamba tayari jambo hilo limeshapitishwa.

Limepita hilo Ally K@sallam_sk anamcheki Seven now… #DiamondKaranga#MoFaya#WasafiFestival2018 #NewBongofleva #BongoFlevaToTheWorld?@WasafiFM@WasafiFestival???????? “.

Baada ya Bifu la miaka Minho hatimaye Ali Kiba na Diamond wanaonekana kuelekea katika njia iliyonyoooka na kumaliza Bifu Lao.

Ali Kiba Akataa Mualiko Wa Diamond Badala Yake Ampa Ofa Kupitia Mofaya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kusema hataweza kushiriki katika tamasha la Wasafi Festival Kama alivyoonbwa na Mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz.

Siku chache zilizopita Diamond Platnumz alitangaza kumkaribisha msanii huyo kwenye tamasha hilo litakaloanza hivi karibuni Kama mmoja wa wasanii watakaopanda stejini.

Ali Kiba amefungukia mwaliko huo na kuweka wazi kuwa hataweza Kushiriki kwenye tamasha hilo kutokana na majukumu ya kinywaji chake cha Mofaya:

https://www.instagram.com/p/Bp374WbB5YB/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=165bmfx3zngd9

 

Jibu la Ali Kiba Baada Ya Kualikwa na Diamond Lazua Utata

Siku mbili  zilizopita Staa wa Bongo fleva na mkurugenzi wa WCB Diamond Platnumz alimualika hasimu wake Ali Kiba kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival litakaloanza siku za karibuni.

Lakini Ali Kiba amedaiwa kumjibu Diamond kimagumashi kwa kupost picha ya mchekeshaji maarufu duniani, Mr. Bean na kuandika maneno kadhaa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kiba amepost picha hiyo yenye maneno; ‘Thank you for listening, To my presentation’, halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”.

Mashabiki wengi walianza kuzungumza mitandaoni na kusema siyo rahisi kwa Alikiba kukubali kuungana na Diamond kwenye Wasafi Festival huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Mange pita aliweka wazi kuwa Ali Kiba hawezi kukubali kuperfom na Diamond kwani kwa kufanya hivyo itakuwa anajimaliza yeye kwani Bifu lake na Diamond likiisha tu basi na ndio mafanikio yake mwisho kwani anabebwa sana na Bifu na Diamond.

Mange Adai Ali Kiba Atapotea Kimuziki Bila Bifu na Diamond

Mwanaharakati wa mambo ya siasa kwenye mitandao ya kijamii Mange Kimambi amefunguka na kudai Bifu linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba linamfaidisha zaidi Kiba.

Sakata hilo limekuja baada ya msanii Diamond kutaka kumaliza Bifu lake na Ali Kiba Siku ya Jana Baada ya kumualika kushiriki katika tamasha lake la Wasafi Festival.

Mange amepima uzito ishu hiyo na kusema kuwa Ali Kiba Hatakiwi kupatana na Diamond kwani year ndio anafaidishwa na Bifu hilo Babu bila Bifu hilo ana hatihati ya kupotea kimuziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange Kimambi ameandika:

Sio kama nachochea ugomvi ila nimeongea fact tu. Tujikumbushe Ray na Kanumba. Mnalikumba beef lao? Siku Kanumba alipokosekana na lile bifu lilipokosekana Ray si alishuka na umaarufu ukapungua vibaya mno mpaka akapotea. .
So lile beef ndio lilikuwa linaibeba career ya Ray. Kwenye situation kama hizi yule ambae ndio msanii mkubwa zaidi huwa ana gain kiki kwenye beef ila anae gain sana ni yule mwingine. Beef la Ray na Kanuamba aliegain sana ni Ray ndo maana Kanuamba kukosekana akafulia.

Sasa naomba mu-ally hii concept to Diamond and Kiba. Then mtaelewa kwanini nasema hao wakipatana Diamond will win Kiba will loose. Diamond ndio ana benefit kwenye hili beef ila ana benefit kidogo mnoo anae benefit zaidi ni Kiba na ukijumlisha na dharau anazomfanyia ndio anazidi kupanda hata bila kutoa nyimbo ??. Ila wakipatana Diamond will gain everything and Kiba will loose everything. Wakipatana hao ndio utakuwa confirmation ya Diamond as the ONLY main artist wa Tz. Na Diamond is very strategic amelijua hili, keshajua kugombana na Kiba kuna faida ndogo sana kwake na faida kubwa sana kwa Kiba.Amestuka kuwa anamfaidisha Kiba. Na anajua akipatana na Kiba ni faida kubwa mnooo kwake na Kiba atapata faida ndogo. Ndo maana mnamuona Dai anahangaika staili izote ili mradi aelewane na Kiba. Anajua akielewana nae anampoteza mazima. Diamond sio mtu wa kujishusha kwa mtu kiasi hiki. He is very smart. Ana mahesabu yake. Ila na Kiba nae keshausoma mchezo ndo maana anampotezea tu ??. Na Diamond naamini amerealize hiki kitu kwenye seduce Me, maana alivyoleta ushindani ndio nyimbo ya Kiba ilinoga mara 1000 na watu waliisapoti kwa ushabiki na hasira ili wamkomeshe Dai. So So kaona bora amsogeze karibu ili ammalize kabisa abakie yeye ndio Konki Masta pekee wa bongo flava. .

Babu Tale-Tumeshaanza Kuwasiliana na Uongozi Wa Ali Kiba

Meneja wa msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Babu Tale amefunguka na kuweka wazi mipango yao ya kumpata msanii wa Bongo fleva Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye tamasha la Wasafi Festival.

Siku ya Jana kwenye mkutano na waandishi wa Habari Mkurugenzi wa WCB, Diamond Platnumz aliweka wazi mipango yao  ya kumpata Ali Kiba ili aweze kuperfom kwenye shoo yao.

Lakini sasa Meneja wa Diamond Babu Tale anafunguka kuhusu jitihada zao za kuwasiliana na Kiba ambapo amekiri kuwa hana mawasiliano na Kiba lakini anaelewana sana na meneja wake anayeitwa Seven.

Siongeagi na Alikiba kivile, mimi naongeaga na meneja wake maana alishawahi kunisaidia sana, lakini kuhusu inshu ya Wasafi Festival Sallam ameshaanza kuwasiliana na uongozi wa Alikiba”.

Baby Tale ameweka wazi kuwa siku ya uzinduzi wa Wasafi festival pamoja na wasafi fm mbali ya kuwepo kwa mipango ya kumpata Ali Kiba lakini pjs atakuwepo msanii Konki konki konki master Dudu baya katika tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Wasafi media.

Barakah The Prince Adai Ali Kiba Anampotezea

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Barakah The Prince ameibuka na kudai Msanii mwenzake Ali Kiba amekuwa akimpotezea na kukataa kujibu meseji zake anazomtumia.

Sakata kwa Ali Kiba na Barakah The Prince lilianza mara baada ya Barakah kuamua kujitoa katika label ya Ali Kiba Ya Rockstar 4000 kwa madai ya kutosimamiwa vyema na kazi zake kuthaminiwa.

Lakini baada ya kutoka kwenye Label hiyo Barakah aliitupia tuhuma nzito na pia kumtuhumu Ali Kiba kwa kufanya kila njia kumharibia muziki wake ikiwemo kumfutia Chanel yake ya Youtube na kufuta nyimba anazotoa ili asifike mbali.

Tuhuma hizo hazijawahi kujibiwa na Ali Kiba lakini Barakah baadae alienda kuomba radhi kwa maneno hayo, Lakini sasa Barakah ameibuka na kudai amekuwa akijaribu kumtafuta Ali Kiba lakini meseji zake hazijibiwi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo,Barakah amefunguka haya kuhusu jitihada zake za kutaka kumtafuta Ali Kiba.

Nilishawahi kumtext nikamwambia brother kuna hichi na hichi na haya ni maisha na haya mambo ambayo yanayoendelea tuachane nayo tudeal na maisha mengine, mimi bado ni kijana nahitaji muongozo wao ili nifanikiwe”.

Barakah amefunguka na kusema pamoja na kumtumia meseji Ali Kiba meseji na kutojibu Lakini pia alimtumia meseji ya msamaha Seven Mosha, Kidboy na Mgagulah ambao wote hawakujibu.

“Tangu Nimeoa Mabinti Wamepunguza Usumbufu”- Ali Kiba

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa tangu ameoa Miezi michache iliyopita anaona mabadiliko makubwa kwani mabinti wamekuwa hawamsumbui kama alivyokuwa single.

Kama ilivyo kwa wasanii wengi maarufu ni kawaida kwa warembo kujigonga kwao kutokana na labda umaarufu au hata pesa ambazo wanakuwa nazo na Ali Kiba aliwahi kukiri kukutana na changamoto kama hizo.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Enews cha EATV, Al Kiba amefunguka kuwa tangu amefunga ndoa amebadili tabia yake na kwa saaa anamuheshimu sana Mke wake.

Lakini pia Kiba amekiri kuwa usumbufu  aliokuwa anaupata kutoka kwa mabinti ambao walikuwa wanamtongoza umepungua kabisa kwa sababu wanajua hivi sasa ameoa.

Ali Kiba ameweka wazi hata kwa upande wake binafsi amebadilika kwani amekuwa akijiheshimu na kumuheshimu Mke wake tofauti na  alivyokuwa kabla hajaoa ambapo wasichana walikuwa wanamsumbua wakijua ya kwamba labda wanaweza  kupata nafasi ya wao Kuolewa kitu ambacho kwa sasa hakipo kabisa.

Ali Kiba Afungukia Tetesi Za Ujauzito Wa Mke Wake

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuongelea tetesi zinazoendelea kusambaa kuwa mke wake wa Miezi Sita Amina Khaleef ni mjamzito.

Taarifa za ujauzito wa Amina zilianza kusambaa tangu walipofunga ndoa  Miezi michache iliyopita lakini hijawahi kuthibitishwa kama ni kweli au uongo mpaka hivi sasa.

Kwenye mahojiano yake na kipindi cha Enews ya EATV, Ali Kiba ameweka wazi kuwa mke wake hana ujauzito ila huo ni ugumu tu uliotengenezwa Kwenye mitandao ya kijamii:

Kuna taarifa niliziona Kwenye mitandao ya kijamii kuwa mke wangu ni mjamzito lakini taarifa hizo sio za kweli, Kwenye ile picha iliyosambazwa mke wangu alikuwa amevaa koti  langu  ambalo lilitunishwa na upepo akaonekana kama mjamzito lakini hana mimba yupo sawa tu”.

Lakini pia Ali Kiba amesema watu hawamuoni mke wake akiwa naye kila wakati kwa sababu ni msomi ambaye anafanya kazi zake ambazo zibamuweka busy kila wakati na pia mkewe hapendi umaarufu na kujionyesha.

 

 

Ali Kiba Afungukia Tuhuma Za Kushuka Kimuziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka na Kupitia vikali tuhuma zinazoendelea Kwenye mitandao ya kijamii na kusema ameshuka Kimuziki.

Habari za Ali Kiba kushuka kimuziki zilianza kushika kasi Miezi michache baada ya kuachwa wimbo wake wa ‘Mvumo wa radi’ ambao mashabiki zake hawakuupenda Lakini pia baada ya kutoawwimbo siku chache zilizopita uliorudiwa ukiwatoa povu zito mashabiki zake.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali Kiba amepingana vikali na kauli hiyo ambapo amesema hajashuka kimuziki hata kidogo:

Sijashuka kimuziki ningekuwa nimeshuka basi wasingeniingiza kwenye hizo tuzo zao za Afrimma,halafu mimi sifanyi muziki ajili ya tuzo mimi pesa zangu nafanya kwa kuuza muziki wangu na kufanya Show,kwahiyo tuzo sizitilii maanani sana”.

Ali Kiba ameachia wimbo mpya unaoenda kwa jina la ‘Mwambie sina’ ambao uneshika namba moja kwa siku kadhaa Kwenye mtandao wa Youtube na mpaka hivi sasa una Jumla ya watazamaji milioni moja.

Ali Kiba- Sifanyi Muziki Ili Kupata Tuzo, Nafanya Muziki Kwajili Ya

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali salehe Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa anapokuwa anafanya anaangalia zaidi kuwafurahisha mashabiki na sio kupata tuzo.

Kauli hiyo ya Ali Kiba imekuja siku moja baada ya taarifa za kwamba yeye pamoja na wasanii kama Diamond na Wengineo waliokuwa wanawania tuzo za Afrimma kukosa na kuambulia patupu.

Kwa miaka miwili mfululizo Ali Kiba amekuwa akifanya vizuri katika tuzo za Afrimma ambapo hta mwaka jana alimbwaga Msanii mwenzake Diamond Platnumz na kuchukua tuzo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali Kiba amefunguka na kusema hajaumizwa sana na kukosa Tuzo kwani tangu Mwanzoni hakuwa alifanya ili kupata tuzo:

Unajua siku zote kuna kupata na kukosa na pia Tuzo lazima upromote lakini mimi sijawahi hata siku moja kuomba kupigiwa kura kwa sababu sijawahi kuzipa kipaumbele tuzo na pia sifanyi Muziki kwa ajili ya kupata tuzo nia yangu ni kuwafurahisha mashabiki zangu kwa muziki mzuri”.

Lakini pia Kwenye mahojiano hayo Ali Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna kitu kinachomuumiza kama akiona familia yake inakuwa inatukanwa Kwenye mitandao ya kijamii.

Mrembo Aibuka na Kudai Anatongozwa na Ali Kiba

Video vixen maarufu kunako gemu la Bongo fleva Sasha Kassim ameingia Kwenye headlines baada ya kudaiwa kuleta mtafaruku Kwenye ndoa ya Ali Kiba na Mke wake Amina Khalef.

Global Publishers wanaripoti kuwa Sasha Meseji hizo zilizovuja zilionekana kutoka kwa Kiba kwenda kwa Sasha usiku mnene, jambo ambalo ni hatari kwa jamaa huyo ambaye inasemekana mkewe alijifungua juzikati.

Rafiki wa karibu wa Sasha amefunguka kuhusu meseji za Ali Kiba na Sasha ameiambia

Hivi mnajua kuwa Sasha ana mawasiliano na Kiba na kuna wakati anawasiliana naye mpaka usiku mwingi? “Kama hamuamini, mimi nitawaletea ushahidi wa chatting zao kwani nimezinasa kutoka kwenye simu ya Sasha mwenyewe, hata hivyo Sasha hamtaki Kiba, mkimbana nyinyi kwa njia zenu, atawaeleza ukweli”.

Baada ya Tetesi hizo gazeti la Risasi lilimsaka Sasha na kumhoji kuhusu Tetesi hizo za mawasiliano na Kiba ilhali anajua ameoa Sasha alifunguka:

Sasa akijua kwanimimi najali? Sikia, mimi huyo Kiba simtaki yeye mwenyewe ndio ananisumbua. Tena kwa taarifa yako, sio Kiba tu hata wasanii wengine kibao wa Kibongo wananisumbua kweli siwataki, siwezi kutoka na msanii wa Bongo labda wa mantoni kama Chris Brown hivi”.

Baada ya Tuhuma hizo nzito dhidi ya yake Ali Kiba alisakwa ndipo alipofunguka haya kuhusu tuhuma hizo:

Samahani sina tabia ya kuchati na watu ovyo”.

 

 

Ali Kiba Ataja Sababu Ya Kufuta Nyimbo Yake

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kutaja sababu za kifua wimbo wake wa ‘Hela’ ambao ulifutwa Kwenye mtandao wa Youtube masaa machache baada ya kurushwa.

Siku ya jana Ali Kiba alikumbana na lawama na kejeli za mashabiki wake mitandaoni baada ya kufuta wimbo wake mpya wa ‘HELA’ aliouachia usiku kupitia mtandao wa YouTube kisha kuufuta asubuhi, amefunguka sababu za kufuta wimbo huo.

Siku yenyewe haikuwa siku yangu ambayo napenda ku-release nyimbo, ilikuwa siku ya Jumanne, so tukamwambia jamaa autoe, inatakiwa siku kama ya leo Alhamisi, ndiyo maana ulikuta umetoka kwenye YouTube, ila sasa hivi ukiingia utaikuta”.

Alikiba amelazimika kutoa maelezo hayo baada ya kushambuliwa na mashabiki kuwa ameutoa wimbo huo kwa kuwa ni mbaya huku wengine wakidai amerudia wimbo wake wa zamani.

Ali Kiba Afuta Video Ya ‘Hela’ Youtube Baada Ya Mashabiki Kumvaa

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amedaiwa kufuta video ya nyimbo yake ya ‘Hela’ aliyotangaza kuiachia siku ya jana baada ya mashabiki zake kumjia juu.

Ali Kiba  aliachia kazi hiyo usiku wa kuamkia Jumatano hii baada ya kukaa muda mrefu bila kuachia kazi hali ambayo iliwafanya mashabiki wake wachukizwe na kitendo hicho.

Ali Kiba alilazimika kuifuta video ya wimbo wa Hela baada ya mashabiki zake kumgeuka na kumtolea povu zito huku wengine wakidai kwamba wimbo huo ameuridia wimbo wake wa zamani.

Mashabiki walitawala koment na kumchana kuwa wanataka nyimbo mpya kwani hajatoa nyimbo mda mrefu na kipindi ambacho wamekaa wanasubiri nyimbo mpya yeye amefanya video ya wimbo wa miaka ya nyuma.

Baada ya povu hilo Ali Kiba alifuta video ya wimbo huo kutoka Youtube na hajatoa tamko lolote.

Makala: “Alikiba Unakua Kiumri Kimuziki Unadumaa Badilika Utapotea”

Wahenga walisema muda ni ukuta hauwezi kushindana nao, na hii inakuja kujionesha hata katika maisha ya kawaida kadri muda unavyozidi kwenda vitu kama mitindo, teknolojia na hata ladha ya muziki nayo inabadilika, lakini sio kwa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, King Kiba.

Alikiba bado anaamini kuwa nyimbo zake za zamani alizowahi kuziachia iwe kwa kuvujisha au kuziachia mtandaoni, kwa muda huo zinaweza kutumika tena na ku-hit jambo ambalo sio baya kwa msanii lakini kwa mtu mkubwa kama Alikiba huo ni uvivu.

Hebu turudi nyuma kidogo, Alikiba kwa miaka mingi alikuwa kimya kwenye muziki lakini mwaka 2014 aliporudi kwenye gemu na kuanza kutoa nyimbo kama Mwana (2014), Chekecha Cheketua (2015), Aje (2016), Seduce Me (2017) na Nagharamia watu wengi walianza kumuelewa na aliongeza mashabiki wapya ambao kwa miaka 2006 wakati anafanya vizuri wengi walikuwa ni wadogo kiumri.

Kutokana na ukubwa wa nyimbo hizo alizoachia kwa miaka mitatu mashabiki wengi wapya walianza kumfuatilia na kuamini kuwa wapo upande sahihi, lakini sio kwa mwaka 2018.

Kwa mwaka huu 2018 Alikiba umewakosea mashabiki wako wapya na hata baadhi ya mashabiki wako wa zamani, kwani nyimbo zote tatu hakuwa wimbo uliopokelewa vizuri kama zile ulizoachia miaka mitatu ya nyuma.

Wimbo kama Mvumo wa Radi sidhani kama unaweza ukaufananisha na Mwana, au wimbo kama Maumivu Per Day unaweza ukaufananisha na Aje au pengine wimbo wake mpya wa Hela unaweza ukaufananisha na Seduce Me.

Hii ni ishara tosha Alikiba kwa mwaka huu umewaangusha mashabiki wako, ngoma zote ulizotoa zimepokelewa kawaida sana.

Na, pengine huenda asiwe yeye peke yake aliyetoa nyimbo za kawaida kwa mwaka huu lakini, tunakuzungumzia yeye kutokana na ukubwa wa jina lake ‘KING KIBA’.

Achilia mbali, mashabiki wengi wa Alikiba ni wakubwa kimri kuanzia miaka 25 na kuendelea, lakini hiyo isimfanye Alikiba kubweteka na kutoa nyimbo za kawaida kama Mvumo wa Radi, Hela na Maumivu per Day.

Nyimbo kama Hela na Maumivu Per Day zote Alikiba alishawahi kuziachia mtandaoni miaka ya nyuma na zimesikilizwa hadi watu wakazichoka, sasa ni uvivu gani hadi akaamua kuziachia tena ile hali anajua muziki wa sasa unahitaji ubunifu wa hali ya juu ili usikilizwe zaidi.

Alikiba ni msanii mwenye kila sifa ya kuitwa msanii mkubwa, anauwezo wa kuandika nyimbo na kabarikiwa sauti, sasa ni kitu gani kinachomfanya mpaka arudie nyimbo kama Maumivu Per Day na Hii aliyoichia leo ya Hela? bila shaka ni uvivu.

Kwa jinsi muziki wa sasa ulivyo kiushindani, Alikiba usitegemee mashabiki wako wapya watashindwa kukushambulia endapo utaendelea kutowatendea haki kwa kuachia nyimbo za kawaida au kurudia nyimbo za zamani.

Leo, Alikiba ameachia wimbo wake aliyouita mpya wa ‘HELA’ ambao kiukweli sio mpya ni wimbo wa miaka mitatu iliyopita na hata kipindi hicho haukuwa mkali kivile, sasa kwanini unakuja kuurudia mwaka 2018?

Sitaki kuamini kama Alikiba ni mvivu kiasi hicho au ameridhika kiasi kwamba anashindwa kuumiza kichwa na kutunga nyimbo kali kama alivyozoeleka.

SOURCE: Bongo 5

Ali Kiba Ataja Sababu Za Kutoonekana Uwanjani na Coastal Union

Staa wa muziki wa Bongo fleva aliyegeuka mfanyabiashara na sasa mcheza mpira wa kulipwa kupitia timu ya Coastal Union, Ali Salehe Kiba amefunguka na kutaja sababu za kutoonekana Kwenye mechi yoyote mpaka sasa.

Pamoja na kwamba Ali Kiba alitangazwa kujiunga na kikosi cha Coastal Union Miezi michache iliyopita lakini mpaka sasa Ali Kiba hajaonekana Kwenye mchezo hata mmoja wa timu hiyo.

Ali Kiba amefunguka na kusema kuwa hana haraka ya kucheza kwa sasa na badala yake anausoma mchezo jinsi ambavyo unaenda pamoja na kukosa mechi za Coastal Union dhidi ya Lipuli FC, Biashara United, KMC na African Lyon.

Kwenye mahojiano aliyofanua na Spoti Xtra Ali Kiba amefunguka haya:

Ifahamike kuwa haina haraka ya mimi kucheza kwani mpira una njia na kanuni zake ambazo mtu unatakiwa uzijue”.

Ni lazima uzijue vizuri hizo na siyo unakurupuka na kuingia uwanjani, niko vizuri kabisa ila kwa sasa natafuta kuielewa timu kabla ya kuonekana uwanjani kwenye mechi zijazo za timu yangu”.

Wakati wa usajili wa Kiba, uongozi wa timu hiyo uliweka wazi kuwa Msanii huyo atakuwa huru kufanya shughuli zake za Kimuziki endapo atahitajika kipindi cha mechi.