Gigy Money Adai Akipewa Nafasi Atawamaliza Ali Kiba na Hemed PHD

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai kuwa endapo akiambiwa awagonge wanaume wowote ambao amewahi kuwa nao Kwenye Mahusiano basi atakuwa Ali Kiba na Hemed PHD na Rich Mavoko.

Gigy Money ambaye alianza kuongia Kwenye ulimwengu wa kisanaa kama Video vixen Mpaka sasa Msanii wa Bongo fleva amekiri Kuwahi kuwa Kwenye Mahusiano na wasanii wengi.

Gigy amekiri hapo nyuma kutokana na kufanya kazi za video na wasanii wengi basi pia ameshawahi kuwa nao Kwenye Mahusiano wengi sana na baadhi yao ni Rich Mavoko, Ali Kiba, Hemed PHD na wengineo.

Kwenye Interview moja aliyofanya hivi karibuni Gigy Money aliulizwa ni Ex gani wake staa ambaye leo hii akipewa ruhusa ya kumgonga na gari na kummaliza atamchagua nani?

Ikitokea nimepewa pesa niwagonge wapenzi wangu wa zamani, nitaomba nipewe fuso kabisa tena nitawasaga haswa nikianza na Hemed PHD, Ali Kiba na Rich Mavoko maana waliniumiza sana”.

 

“Mwenyezi Mungu Ndio Muumbaji Wa Wanyonge na Wajanja”- Ujumbe Wa Ali Kiba Kwa Ommy Dimpoz

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amemtumia salamu za Birthday njema Msanii mwenzake na rafiki yake Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz.

Siku ya leo ni siku ya kuzaliwa ya Ommy Dimpoz na rafiki yake na mtu wake wa karibu kabisa Ali Kiba kamuwish Birthday njema na ujumbe mzito.

Ali Kiba amemtaka asijali sana wala asiyawaze yale magumu aliyopitia Miezi michache iliyopita baada ya kulazwa hospitali kwa Miezi karibia mitano badala yake amshukuru tu Mwenyezi Mungu.

https://www.instagram.com/p/Bnp-7T9ll_E/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1azp61dlmsurf

Kwenye posti yake ya leo ya birthday Ommy Dimpoz amemshukuru sana Ali Kiba kwa kuwa naye kipindi chote cha ugonjwa na hata kuweka wazi kuwa amemuuguza.

Ali Kiba alisimamisha kuachia kinywaji chake  cha Mofaya Miezi michache iliyopita baada ya kukizindua kutokana na maradhi ya Ommy Dimpoz.

Ali Kiba Afunguka Baada Ya Kusainiwa Coastal Union

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka mara baada ya kucheza mchezo wake  wa kwanza ndani ya Coastal Union ya jijini Tanga.

Miezi michache iliyopita iliwekwa wazi kuwa Ali Kiba atatanua ujuzi wake na kuanza kucheza soka la kulipwa ndani ya Coastal Union.

Baada ya kuwa mkimya kwa muda kuhusu kuasajiliwa chini ya timu hiyo kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa hatimaye Ali Kiba anafunguka na kuweka wazi nafasi yake ndani ya Coastal Union.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ali Kiba ameandika maneno haya:

https://www.instagram.com/p/BnlkBF0nUCa/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=6bd15aapslui

Ali Kiba, Millard Ayo na Faraja Nyalandu Watajwa Kwenye Listi Ya Vijana 100 Wenye Ushawishi Afrika

Mastaa mbali mbali kama vile Ali Kiba, Millard Ayo, Faraja Nyalandu, Herieth Paul, Jennifer Bash, Jumanne Mtambalike, Mbwana Samatta na Yusuf Bakhresa wametajwa Kwenye listi ya vijana 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika.

Taasisi inayojishughulisha na tafiti mbalimbali zinazohusu vijana wenye ushawishi zaidi walio chini ya miaka 40  barani  Afrika ya The Africa Youth Awards, imetangaza orodha ya majina ya vijana 100 ya vijana wenye ushawishi kutoka kwenye mataifa 26 barani Afrika kwa mwaka 2018, na Tanzania ikiwemo.

.

Wasanii wanaowekwa Kwenye Orodha hii wanakuwa wameleta Mchango chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla hasa kwa dunia hii ya utumiaji wa mitandao ya kijamii tunaweza kusema ‘Role Models’.

Tazama orodha kamili hapa chini na kusoma zaidi kwenye website ya The Africa Youth Awards.

 

Wolper- Mapenzi na Ali Kiba Yalikuwa Bora Zaidi

Staa wa filamu za Bongo Movie na mjasiriamali Jacqueline Wolper ameibuka na kudai hakuna mwanaume ambaye alikuwa mpenzi bora kwake kama ilivyokuwa kwa staa wa Bongo fleva Ali Kiba.

Wolper ambaye siku za nyuma amewahi kukiri kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi kwa muda mrefu na Ali Kiba ingawa hawakuyaweka hadharani na kujulikana na mashabiki.

Kwenye mahojiano aliyiwahi kufanya na East Africa Television, Wolper amefunguka na kuongea haya:

Katika Mahusiano yangu yote ambayo nimewahi kuwa nayo, ambayo naweza kuyapa namba moja na yalikuwa mazuri na ni the best ni yale nilipokuwa na Ali Kiba. Lakini sio kwamba namiss hapana ila tu ninasema yalikuwa Mahusiano bora niliyowahi kuwa nayo”.

Mbali na Ali Kiba, Wolper ameshawahi kuwa Kwenye Mahusiano na mastaa wengine kama Harmonize, Juma Jux na wengineo.

Waziri Mwakyembe Kulifungia Kazi Bifu La Diamond na Ali Kiba

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kuhaidi kulimaliza bifu linaloendelea kati ya wasanii wawili wakubwa wa Bongo fleva.

Dkt. Mwakyembe ameweka wazi kuwa kama Mlezi wa wasanii Tanzania ameamua kulimaliza kwa kulishughulikia bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwani linaonekana kutoleta picha nzuri  kwenye Muziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano na Kampuni ya Global Publishers, Waziri Mwakyembe alisema kuwa, yeye hadhani kama kuna tofauti kubwa kati ya wasanii hao bali anaona kwamba mashabiki ndiyo wanaolikuza bifu hilo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Nahisi mashabiki wa hawa wasanii wawili ndiyo wanaolikuza hili bifu. Lakini pia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vikishaandika ndipo inaonekana kuna shida lakini kumbe siyo hivyo.

Labda niseme tu kwamba, kuna kitu naandaa na hivi karibuni mtawaona pamoja na hiyo itawafanya muamini kuwa hawana bifu kama inavyojaribu kukuzwa”.

Diamond na Kiba kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye bifu kubwa ambapo mbali na mara kadhaa kurushiana maneno makali pamoja na kwamba wamekataa kuwa Kwenye bifu.

 

Gigy Money Adai Yeye na Ali Kiba Wako Level Moja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money amefunguka na kudai yeye kama ilivyo kwa Msanii mwenzake Ali Kiba wanaweza kuhit na nyimbo moja kwa mwaka mzima.

Gigy Money amefunguka na kudai hapendi kutoa nyimbo back to back kama wasanii wengine kwani inaweza kuua brand yake bali hupendelea kutoa nyimbo mara moja moja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa East Africa amefunguka haya:

Siku si nyingi nakaribia kuachia kazi yangu mpya, watu wakae tayari naamini wimbo wangu utatingisha kinoma. Sipendi kutoa ngoma mpya mfululizo kwasababu huwa napenda kujikuta Alikiba kidogo, maana ninaweza ku-hit bila ya kutoa ngoma mwaka mzima”.

Lakini pia Gigy Money Anna mtazamo tofauti na wasanii wenzake pale linapokuja suala la kutoa Albamu kwani amedai hana mpango huo:

Sio kila msanii atakuwa na ubavu wa kuingia studio na kurekodi nyimbo 10 ili atengeneze albamu, kwangu mimi watu watasubiri sana katika hilo ila kama watu wanataka kuni-enjoy basi waendelee kunisikiliza kwenye ‘single’ moja moja, kwa maana sina hiyo pesa ya kutengeneza albamu kiukweli, halafu siwezi kujifungia studio muda wote kufanya kazi wakati mwanangu ananitegemea”.

 

Hakuna Bifu Kati Ya Ali Kiba na Diamond- Sallam Sk

Meneja wa Staa wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz, Sallam Sk amefunguka na kuweka wazi kuwa hakuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba.

Sallam amedai kuwa viongozi wa WCB wanakutana mara kwa mara na uongozi wa Alikiba na kuzungumza mambo mbalimbali.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za kuwepo kwa bifu kati ya Diamond na Ali Kiba ingawa kila mmoja amekuwa akikataa na kusisitiza kuwa hakuna bifu.

Kwenye mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Sallam alifunguka mambo mengi huku WCB pamoja na muziki ambapo pia alifunguka kueleza kwamba sio kweli kwamba Diamond ana bifu na Alikiba huku akienda mbali zaidi kwa kudai viongozi wa label hizo mbili hukutana mara kwa mara.

Kati ya Ali na Diamond hakunaga bifu, na haijawi kutokea, na uongozi wa Alikiba na WCB huwa unakutana mara kwa mara kuzungumza,” alisema Sallam. “Bifu ilitengenezwa na sisi baada ya kuona watu wanapenda hivyo vitu tukavitumia kwaajili ya kupromote wimbo wetu”.

 

“Nina Kipaji na Ninaweza” Ali Kiba Afunguka Kucheza Soka La Kulipwa

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amefunguka na kuongelea kitendo chake cha kujiingiza katika soka la kulipwa ambapo hivi sasa ni mchezaji rasmi wa Coastal Union.

Wiki chache zilizopita Ali kiba alitangazwa rasmi kama mchezaji wa timu ya Coastal Union yenye makazi yake mkoani Tanga.

Kwenye mahojiano na Azam Tv, Ali Kiba anafunguka juu ya njia mpya aliyochukua na kueleza kuwa ana kipaji cha kucheza mpira na uwezo pia anaamini kuwa anao:

Mimi kwa kipaji changu binafsi nimeona kwamba ninaweza na ndio maana nikajiunga na Coastal Union sababu ya kipaji nilichokuwa nacho”.

Lakini pia ALi Kiba amefunguka kuhusu uwezo wa timu yake hiyo mpya na malengi waliyokuwa nayo:

Coastal Union wanajutahidi na ni wapambanaji na tunatafuta title msimu huu japokuwa kuna timu kongwe lakini mpira wanasemaga unadunda kwaiyo ni kupambana tu tutafika”.

Ali Kiba pia ameweka wazi kuwa kinywaji chake cha Mo Faya ndiyo kitaidhamini timu hiyo.

Ali Kiba Kuidhamini Timu Yake Ya Coastal Union Kupitia Mo Faya

Staa wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema na ngoma yake ya ‘Mvumo wa Radi’ Ali Kiba ameweka wazi kuwa yeye ndio mdhamini Mkuu wa timu yake ya Coastal Union Kupitia kinywaji chake cha Mo Faya.

Wiki chache zilizopita timu ya Coastal Union ilitangaza kumsaini Ali Kiba katika kikosi hicho na siku chache baadae KIba ametangaza Neema kwa timu hiyo.

Kupitia mahojiano yake na Azam Tv msanii huyo anayetamba na kibao cha Mvumo wa Radi  amesema kuwa ameamua kuidhamini Coastal Union ili kuisaidia kurudi katika ubora wake, kwa hiyo kupitia udhamini huo anaamini utaisaidia kufikia malengo.

Nitakuwa mchezaji wa Coastal Union Lakini pia nitakuwa mdhamini Mkuu Kupitia kinywaji changu cha Mo Faya ili watu wakiwa wanakuja kuangalia mpira wawe wananunua na vinywaji vitakavyokuwa vinapatikana uwanjani na kuisapoti Coastal Union”.

Ali Kiba alizindua rasmi kinywaji chake cha Mo Faya Miezi michache iliyopita lakini hakijaweza kuingia sokoni mpaka leo kwa sababu ya kuugua kwa Ommy Dimpoz.

Ndoa Ya Abdu Kiba Yadaiwa Kupumulia Mashine

Ndoa ya staa wa Bongo fleva Abdu Kiba ambaye ni Kaka wa Ali Kiba imedaiwa kuwa katika hali mbaya na kuwa mbioni kuvunjika.

Global Publishers wanaripoti kuwa Ndoa hiyo na Abdu Kiba na mkewe Rwahida imeendelea kuwa matatani ambapo imesemwa kuwa Abdul Kiba mara nyingi amekuwa ni mtu wa kurudi nyumbani usiku na mara nyingi anashinda maskani maeneo ya Ilala Mtaa wa Arusha, kitu ambacho mkewe huyo amekiona kama sio sawa na pamoja na hayo bado anaona hakuna upendo ndani.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilimsaka Abdu Kiba ili kupata ukweli wake lakini mara moja aliwataka wazungumze na Meneja wake ambaye mara moja alifunguka:

Hizo habari hata sisi tumezisikia kwamba watu wanasema hivyo lakini naomba kukuhakikishia hakuna ukweli wowote.

Unajua Abdul ni tofauti sana na Ally, yeye mara nyingi anapenda sana kuwa huru sana hivyo watu wakimuona pekee yake wanafikiria hivyo lakini sivyo au wengine wanasema kwa nini hamposti mkewe…”.

Lakini pia na mke wa Abdu Kiba, Rwahida amefunguka na kusema:

Hakuna ukweli wowote mimi na mume wangu tupo vizuri tu kama kawaida hakuna kitu kama hicho“.

 

Matukio Ya Harusi Ya Zabibu Kiba Kwenye Picha

Zabibu Kiba ambaye ni dada wa staa wa Bongo fleva Ali Kiba ameolewa siku ya jana na Staa wa Taifa Stars na mchezaji wa Baroka FC ya Afrika Kusini Abdi Banda.

Ndoa hiyo imefungwa katika msikiti wa Sanene Tabata jijini Dar es Salaaam baada ya shamra shamra za sherehe za wiki nzima ambapo Ali Kiba alionekana kama mtu ambaye amemuoza dada yake.

Hizi ni baadhi ya picha za matukio ya ndoa hiyo iliyofungwa alfajiri na mapema:

Ali Kiba Avunja Ukimya Kuhusu Uteuzi wa Jokate

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amevunja ukimya na kufunguka kuhusu uteuzi wa aliyekuwa mpenzi wake Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Ali Kiba ambaye alikuwa mpenzi wa Jokate amefunguka Kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv,  kusema anamtumia salamu za pongezi na kumtakia kila la Kheri;

Siwezi kulizungumzia sana hilo lakini kwa ufupi tu ni kwamba nimefurahi na nampa hongera sana”.

Lakini pia kaka wa Ali Kiba, Abdu Kiba ambaye pia alikuwa na ukaribu na Jokate amefunguka na kumpongeza Jokate:

Namtakia kila la heri na aweze kuongoza vyema Kwenye uongozi wake. Sijapata nafasi ya kuongea naye kwa sababu naamini yuko bize lakini pia sijawahi kuwasiliana naye kwa kipindi kirefu lakini Kupitia hii Interview namtakia kila la kheri Kwenye maisha yake”.

Jokate aliteuliwa siku chache zilizopita na Raisi John Pombe Magufuli kuwa mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Ali Kiba Huenda Akakosa Mechi Ya Kwanza Ndani Ya Coastal Union

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vyema kabisa na ngoma yake ya ‘Mvumo wa radi’ Ali Kiba amedaiwa anaweza akakosa mechi muhimu kabisa ndani ya Coastal Union.

Ali Kiba ambaye alitangazwa kusajiliwa na timu hiyo ya mkoani Tanga wiki iliyopita, anasemekana kuwa ana aweza akakosa mechi yake ya kwanza ndani ya timu hiyo kutokana na shoo yake ya muziki.

Global Publishers wanaripoti kuwa Ligi Kuu imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22 lakini ratiba ya shoo ya Alikiba inaonyesha itaanza Agosti 17, 18 na 25, mwaka huu huko Toronto, nchini Canada katika shoo iliyopewa jina la The All Star Music.

Ratiba inaonyesha Coastal Union wataanza ligi, Agosti 22 dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hivyo Alikiba hatokuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza mechi hiyo.

Meneja wa Coastal Union, Said Hilal ameweka wazi kuwa wanatambua majukumu ya kimuziki ya Ali Kiba hivyo hawana tatizo juu ya kukosa kwake mechi.

Tunajua AliKiba ana majukumu yake mengi na sisi kama klabu hatuwezi kumzuia kwenye hilo pale ambapo atakuwepo atafanya kazi na wenzake hivyo hakuna tatizo”.

 

Uongozi Wa Coastal Union Utamruhusu Ali Kiba Kuendelea na Ratiba za Kimuziki

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Ali kiba amefanikiwa kusajiliwa rasmi katika kuichezea soka la kulipwa timu ya Coastal Union ya mkoani Tanga.

Uongozi wa klabu ya Coastal Union umethibitisha kukamilisha usajili wa Alikiba ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili  kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Championi Ijumaa, meneja wa timu hiyo, Said Hilary alisema Ali Kiba ni mchezaji mzuri na ameenda kwenye timu ya mpira na lengo lao kubwa ni kuitangaza Coastal.

Tumemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja na tunafahamu yeye ni mwanamuziki kwa hiyo akiwa na shughuli zake za kimuziki ataendelea na shughuli zake kama kawaida na akiwa yupo huru basi atacheza kuisaidia timu maana tuna uamini uwezo wake ndiyo maana tumemsajili“.

Ali Kiba Asajiliwa Rasmi Kuichezea Coastal Union

Staa wa muziki wa Bongo fleva Ali Kiba amekuwa muwazi juu ya mapenzi yake kwa mchezo wa mpira wa miguu na hata kudai kuwa endapo asingekuwa msanii wa muziki basi angekuwa mchezaji wa mpira.

Baada ya Tetesi za muda mrefu hatimaye Uongozi wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga umethibitisha kutarajia kumsajili msanii wa muziki wa Bongo, Alikiba kwaajili kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania Bara.

Kupitia kipindi cha Esports kinacho ruka kwenye radio ya E FM, Mwenyekiti wa klabu ya Coastal Union, Steven Mguto amethibitisha kuwa kwenye mazungumzo na msanii huyo ili kupata huduma yake ya kukipiga katika kikosi cha wagosi hao wa kaya.

Kiukweli siku zimebaki kidogo lakini na sisis kama zoezi letu limefikia ukingoni nafikiri mpaka kesho tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kueleza nani na nani tumemsajili.

Kwa sababu kwa sasa ndiyo tunamalizia watu wengine maswala ya mikataba sasa sirahisi kuweza kumtaja mkataba bado haja saini mwisho wasiku anaweza akageuza nia na ikawa kitu kingine.

Kwa kiasi kidogo kuna ukweli wa kutaka kumsaini Alikiba lakini pia mambo haya jakaa sana sawa lakini wenyewe mnamuona naye ni mchezaji ingawaje si wa kiwango cha juu kwasababu hana mazoezi ya mara kwa mara ya kucheza mpira hivyo kuwa katika mazungumzo ni kweli“.

Alikiba amvaye anafanya vizuri na wimbo wakeboard wa Mvumo wa Radi huwenda akaanza kuonekana kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu kupitia na timu yake ya Coastal Union endapo usajili huo utakamilika.