Amber Lulu- Natamani Sana Kusainiwa WCB

Video vixen maarufu na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amefunguka na kuongelea mipango yake ya kutaka kusaini chini ya label maarufu Bongo WCB inayomilikiwa na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Amber Lulu ambaye alijulikana kutokana na kuuza Mushi kwenye video za wasanii mbali mbali wa Bongo fleva na vituko vyake. Hivi sasa Amber Lulu kwa hivi sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya jini kisirani.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Sam Misago Tv, Amber Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa anatamani sana kufanya kazi chini ya WCB:

Natamani hata kesho niweze kusainiwa WCB na naomba niseme kuwa namtegemea sana Diamond kwa sababu yeye ni kaka yangu ambaye amenitangulia kwaiyo kwa upande wangu nina mipango mingi sana na Diamond na WCB kwa ujumla ingawa najua yeye ana mambo yake na ni mtu mkubwa kumpata inakuwa ngumu lakini natamani siku moja nije kufanya naye kazi na ninatamani niwe msanii wa kwanza kusainiwa WCB baada Queen Darleen”.

Hivi sasa Amber Lulu anafanya vizuri na wimbo wake wa jini kisirani na amekiri msanii anayetamani sana kufanya naye kazi ni Rayvanny kutoka WCB.

 

Dimpoz Hana mvuto, Hajakaa Kama Mwanaume-Amber Lulu

Msanii wa muziki bongo Amber Lulu amefunguka na kusema kuwa msanii Ommy Dimpoz hana mvuto wa kuwa mwanaume anaeweza kumuona kwa sababu amekaa kama kongo au mtu hasiejielewa hivi.Akiongea katika online tv ya Jonijo, mwanamuziki huyo alifunguka hayo alipoulizwa kuwa ikitokea kati ya jux na ommy dimpoz wakataka kumuoa ni na atamchagua ndipo alipokuja na majibu haya.

Unanitafutia bifu za Vannesa lakini obviously nitamchagua jux na wala sio ommy kwa sababu kwanza ommy hana ule mvuto na hajakaa kama mwanaume,yaan hajakaa kivile ila jux ndo yule mwanaume ambae hata ukimwamnagalia kwa macho tu unaona , lakini Ommy Dimpozi hawezi kukaa sehemu moja na Jux ku-battle  ni zero yani hana mvuto sijaona kitu ambacho kimenivutia kwake.”

Amber Lulu: Simpendi Baba Yangu Hata KIdogo Na Wala Sitaki Kumuona

Video vixen maarufu aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Amber Lulu amekiri kuwa amemtosa Baba yake mzazi na hataki hata kumuona.

Amber Lulu amefunguka hayo wakati anaelezea changamoto alizozipitia katika maisha yake naada ya Baba yake mzazi kuwakimbia na kumuacha yeye kama mtu pekee ambaye alitakiwa kuiangalia familia yake hasa mama yake ambaye alikuwa mgonjwa.

Amber Lulu ameongelea uhusiano aliokuwa nao na Baba yake mzazi ambapo amekiri katika umri mdogo alianza kushika majukumu mazito ya kuielea familia yake hivyo ilimbidi ajiingize katika biashara mbali mbali ili aweze kupata pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Clouds Fm, Amber Lulu aliongea haya kuhusiana na changamoto alizozipitia:

Kipindi hiko nilikuwa bado niko shule lakini ilikuwa likizo hata ya wiki mbili nilikuwa nakuja Dar kufanya kazi maana tulikuwa tunahitaji pesa na kama Yangu alikuwa mgonjwa na ndio baba alikuwa kashatukimbia, nakumbuka msanii alikuwa anaitwa Pasha alinitumia kwenye video yake akanilipa shilingi elfu hamsini ambayo sikutumia hata senti nikaenda kumpa Mama yangu ambaye alikuwa anahitaji lakin moja na nusu ya matibabu”.

Lakini Pia Amber Lulu ameongelea uhusiano wake na Baba yake mzazi ambaye alimkimbia:

Wanasema mzazi ni mzazi lakini mimi Baba yangu alinitelekeza kaja kunitafuta nilivyotoa wimbo wangu wa Watakoma alafu ananiomba hela kusema kweli aliniumiza kwa sababu hajanitafuta kama miaka kumi halafu anakuja kunitafuta kwa sababu anataka hela , dah kusema ukweli simpendi baba yangu hata kidogo na sitaki hata kumuona”

.

Amber Lulu Amuanika Mpenzi Wake Mpya Baada ya Kumwagana na Prezzo

Video vixen na msanii wa Bongo fleva, Lulu Eugene maarufu kama Amber Lulu amemuanika live mpenzi wake mpya baada ya kumwagana na staa wa muziki kutoka Kenya, Prezzo.

Prezzo na Amber Lulu walikuwa kwenye mahusiano  kwa miezi kadhaa ambapo mara kwa mara pamoja na penzi lao kupondwa na watu kadhaa ikiwemo kama msanii TID, lakini walisisitiza penzi lao ni la kweli na litadumu.

Lakini baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kupostiana Kwenye mitandao ya kijamii tetesi zilianza kusambaa kuwa wawili hao wameachana ingawa hakuna aliyethibitisha hilo mpaka wikiendi iliyopita kwenye birthday party ya Amber Lulu.

Global Publishers wanaripoti kuwa siku ya Jumamosi Amber Lulu alifanya party ya birthday ambapo alialika watu kadhaa na moja kati ya wageni alimtambulisha mwanaume mmmoja kama Sam ambaye aliweka wazi kuwa ni mpenzi wake.

Amber Lulu na Mpenzi Wake Sam

Amber Lulu alimtambulisha mpenzi wake Sam kwa wageni waliohudhuria sherehe hiyo na kusema:

Jamani huyu ndio naniliuu wangu yeye ni mkurugenzi hapa mjini lakini sitaki kumpamba sana kwenye pati yangu hii nisije nikaibiwa buree na vidaka tonge vya mjini, naomba kwa leo mjue hivyo tu”.

Amber lulu- Nillan ni Mtoto wa Ivan sio Diamond

Msanii wa mziki wa Bongo fleva, Amber lulu amejikuta akivamiwa na kupewa vichambo vya maana na Team Zari baada ya kusema mtoto wa Zari Nillan sio mtoto wa Diamond.

Siku ya jana Hamisa aliweka picha za mtoto wake aliyezaa na Diamond Instagram na moja kwa moja zilizua gumzo huku kila mmoja akiibuka na kusema lake.

Amber lulu ambaye anajulikana wazi kuwa ni rafiki wa Hamisa aliweka picha ya Nillan huku ikisindikizwa na maneno haya:

Toto Dee raha ya mtoto afanane na na Baba yake kwa kweli maana unaambiwa wako hujafanana naye hata kidole nasubiri wa shoga yangu Gigy Money najua Baba Candy sio mtu wa mchezo mchezo ila hongera mzaa chema”.

Lakini baada ya kuweka posti hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram kuna mtu akamuuliza Yule mwingine kafanana akimaanisha Nillan, Amber Lulu alionekana kajibu Kafanana na Baba yake Ivan mi sipo.

 

Kwa muda mrefu watu wamekuwa wakimfananisha na kudai mtoto wa Zari Nillan hafanani na Diamond na kuunganisha picha huku wakidai Nillan ni mtoto wa Marehemu Ivan jambo ambalo Zari amekwisha kataa na kusema sio kweli na hata Diamond alisema ameshakubali yule ni mtoto wake.

Young Dee Aliniita Nikampelekee Chakula Nikamkuta Na Mwanamke- Amber lulu

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber lulu amefunguka na kueleza moja kati ya matukio yaliyomuumiza kwenye uhusiano wake na msanii mwenzake Young Dee ambapo amedai ameshawahi kumfumania na mwanamke mwingine ndani.

Amber lulu amekuwa muwazi sana kila inapokuja kwenye hisia zake na Young Dee kwani ni  mara kwa mara ameweka wazi kuwa ampenda sana hata Kama amemuumiza sana kwa kuchepuka na wanawake wengine.

Amber lulu amekiri kuwa pamoja na kwamba yupo na Prezzo lakini Young dee ni moja Kati ya mwanaume ambaye alimpenda sana lakini pia amekiri kuwa tukio ambalo hatokuja kulisahau kwenye maisha yake ni siku ambayo Kwani alimfumania live.

Kwenye interview aliyofanya na East Africa redio kupitia kipindi cha Planet Bongo, Amber lulu alifunguka mengi:

Yaani hata leo hii Young Dee akimposti demu mwingine Instagram mimi naumia ingawa siwezi kumkataza lakini pia ikitokea nimeachana na Prezzo naweza nikarudiana naye ingawa ameniumiza sana kipindi cha nyuma kama nakumbuka kuna Siku alinipigia Simu akaniambia yuko studio somewhere akaniambia hebu my baby nipikie kile chakula ninachokipendaga ambacho kilikuwa ni ugali na maini basi mwenyewe nikjipikilisha pale unyamwezi pembeni nimemaliza nimebeba kile chakula nimpelekee alikuwa kwenye hoteli Fulani hivii kufika pale namkuta na msichana mwingine kusema kweli niliumia sana”.

 

Gigy Money Yupo Tayari Kuwa Mama- Amber Lulu

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Gigy Money anayeendelea kutamba na ngoma yake ya ‘Nampa papa’ alitangaza ujauzito wake wiki chache zilizopita baada ya kuenda BASATA kuripoti kwa Naibu waziri.

Gigy Money aliingia matatizoni na BASATA kutokana na vituko vyake ambavyo vilijumuisha picha zake za utupu alizokuwa amezoea kupiga lakini pia maneno aliyokuwa anaongea na vyombo vya habari hasa interview aliyofanya na kutaja orodha ya wanaume aliotembea nao.

Gigy Money alificha ujauzito wake na kuufanya siri lakini ulipogundulika ndipo maneno yalipoanza watu wengi wamehoji uwezo wake wa kuwa mama kutokana na historia yake na matendo yake aliyofanya kipindi cha nyuma.

Lakini mbali na mawazo ya watu wengi kuwa Gigu hataweza kuwa mama mzuri kutokana vitabia tabia vyake rafiki yake wa karibu Amber Lulu amefunguka kuwa anadhani Gigy Money yuko tayari kuwa mama bora.

Amber Lulu alifunguka hayo yote kwenye interview aliyofanya na Enews ya East Africa TV:

Kwanza hayo mawazo ya watu sio mazuri kwa sababu binadamu tunabadilika tunakuwa watu wapya kila siku na tunafanya vitu vikubwa, Gigy ambaye wanamuongelea wa 2017 na Gigy tunaemuongelea 2018 naweza sema ni watu sita tofauti  mnavyomuona kwenye social media hiyo inakuwa ni sehemu ya kazi kwaiyo vile mnavyomuona mtandaoni sivyo alivyo kwenye maisha yake halisi Gigy ni mwanamke mmoja tu poa na sahivi typo tayari kuwa mama na ndio maana amefungua sehemu yake ambayo inaweza kumuingizia kipato Kwaiyo ivo yaani tayari ameshakaa tamarind kuwa mama na Mimi namuona kabisa”.

Lakini pia Amber Lulu amefunguka na kudai kuwa endapo na yeye siku moja atakuja kuwa mama hatogopa kwasababu ya vituko alivyofanya kwani anaamini kuwa anataka mtoto wake ajifunze kutokana na makosa yake.

Amber Lulu na Diva Hawana Kinyongo Ku-share Penzi La Prezzo.

Msanii wa Bongo Fleva ambae pia ni video vixen,  Amber  Lulu amesema kuwa hana kinyongo kabisa na mwanamke mwenzie Diva The bossy kwa  sababu ya kushare penzi la Prezzo , msanii kutoka Kenya .Mwanadada Diva alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Prezzo wa Kenya mwaka 2103 lakini walikuja kukorofishana na sasa hivi msanii huyo yupo katika uhusiano wa kimapenzi na msanii mwingine bongo  Amber Lulu.

Amber Lulu ameiambia Clouds Fm katika kipindi cha XXL, kuwa pamoja na kwamba yeyey na Diva wametembea na mwanaume mmoja lakini wako vizuri na hakuna aliye na bifu na mwenzie hata mmoja na hata wanapokutana wamekuwa wakizungumza bila shida yoyote.

hapana hajawahi kabisa na juzi nilikwa nae yupo fresh kabisa,nafikiri hivyo ni vitu vya zamani na yeye kwa sasa ana maisha yake mapya na heri muziki, kwaio maisha ni mapya na ni maisha mengine yamebadilika kwaio hakuna kumaindiana kabisa. -Aliongea Amber Lulu.

amber lulu na prezzo walianza mapenzi yao mapema october mwaka jana na kufikia hatua ya kupost baadhi ya picha wakiwa nusu uchi uku wakiitana mama watoto , na penzi hilo lilikiki kwa muda kidogo katika mitandao ingawa kwa sasa kidogo limepungua.Amber Lulu alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wasanii kadhaa bongo akiwemo Young Dee.

 

Amber lulu Anusurika Yaliyomkuta Gigy, Mashabiki Wamtaka Ajifunze.

Amber Lulu ni rafiki wa karibu na Gigy Money na hata sakata la kutafuta wasanii wa kike wanaotupia piga za uchi katika mitandao  ya kijamii lilipoanza wengi walidhani kuwa atakuwa kwneye list ya wasanii wa kwanza, gigy money amekutwa na mkumbo huu lakini amber lulu ameponea chupuchupu katika janga hilo.

Hata hivyo baadhi ya mashabiki wameonekana kumpo ngeza msanii huyo na kumuomba ajifunze kutoka kwa wenzie ama Gigy na Pretty kindy ambao pia wamekutwa katika mkumbo huo.wakimshambuliana na kuandika maoni ya mawazo yao katika ukurasa wake na kurasa nyingine tofauti tofauti baadhi ya mashabiki walionekana kushangazwa kwanini yeye ameacha wakati wote wanafanya kitu hich hicho, lakini wengine wamemuomaba kujifunza na kuangalia jinsi wenzake walivyoumizwa na adhau hizo hivyo arekebishe mavazi yake na mwenendo wake kwa ujumla.

Gigy money ambae jana aliitika wito katika ofisi za BASATA, alionekana kutoka kwa majonzi katika ofisi hizo na kusema kuwa kunapotea kwa uhuru katika sanaa, lakini pia Pretty Kindy alipokea adhabu yake siku chache zilizopita kwa kufungiwa kutokufanya kazi kwa miezi sita.

Amber lulu anapaswa kujifunza kitu kutoka kwa wenzake, tena hsa anapoona rafiki yake wa karibua ambae amekuwa akifanya nae kazi hizo ameshatajwa katika list.watu husema UKIONA MWENZIO ANANYOLEWA ZAKO TIA MAJI.

 

Amber Lulu Akataa Prezzo Kufananishwa Na Young Dee

Msanii wa kike na aliyekuwa video queen maarufu nchini Amber Lulu  ambae pia kwa sasa ni msanii na amekuwa akifanya vizuri katika swala la muziki amefunguka na kuwakanya watu ambao wamekuwa wakimfananisha mpenzi wake wa zamani na huyo alie nae sasa hivi.Amber Lulu ambae alikuwa na mahusiano ya mapenzi na msanii wa bongo fleva Young Dee amekataa kumfanisha Young Dee na mpenzi wake  wa sasa ambae ni msanii mkubwa kutoka Kenya anaejulikana kwa jina la Prezzo.

Amber lulu na prezzo walianza mahusian kama miezi miwili iliyopita na wamekuwa ni moja ya watu wanao-trend sana katika mitandao kutokana na picha zao za mahaba kusambaa kila kona.mwanadada huyo amesema kuwa hapendezwi na watu wanaokaa na kuweka mpambano wa Young Dee na Prezzo kwa sababu wawili hao hawafanani kwa kitu chochote kile.

Usimfananishe mume wangu na watu wengi kwa sababu unapofanya hicyo unakuwa ni kama unamkosea heshima tu,kwaiyo Young Dee na Prezzo hupaswi kuwaweka sehemu moja kabisa, kwa sababu hao ni watu wawili tofauti kabisa hawafanani hata kidogo.

Amber Lulu na Young Dee walikuwa wapenzi kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kuchora tatoo ya young dee alkini baada ya kuachana alitumia muda mrefu kuifuta tatoo hiyo kwa sababu walikuwa kama wana dalili za kurudiana ingawa ilishashindikana.

 

Amber Lulu- Napiga Picha za Uchi na Kufanya Vituko Kwaajili Ya Pesa Sio Uhuni

Video vixen maarufu kama Lulu Eugene ‘Amber Lulu’ amefunguka na kudai vituko anavyofanya kama kupiga picha za nusu uchi sio kwasababu ya uhuni bali ni katika harakati za kutafuta maisha mazuri.

Amber Lulu aliyegeukia fani ya muziki amekuwa akitawala vichwa vya habari kutokana na vituko vyake kuanzia na uvaaji wake wa nusu uchi na uongeaji wake na hata tabia yake inayojionyesha mbele za watu.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni Amber Lulu amedai kuwa Watanzania wana kasumba ya kuamini kila kitu wanachosoma juu ya mtu au wanachosikia ila saa nyingine watu wanatafuta njia ya kutokea hivyo njia pekee ya kufanikiwa hilo ni kufanya vituko kama hivyo ili kupata umaarufu.

Jamani kwa mfano mimi nikipiga picha nimevaa nguo ya ndani tu utakuta ni kwa ajili ya kutangaza nguo hiyo sio kwamba najinadi au najiuza kwenye mitandao kama watu wanavyochukulia”.

Ni hivi karibuni tu Amber Lulu ametoka kuwaacha watu midomo wazi baada ya kusema yupo tayari kulala na hats kichaa ilimradi tu anampa pesa na anampenda.

Amber Lulu Akiri Kulala Na Chizi Kama Atampa Ela

Wadada wengi wa mjini imkuwa ni kama desturi kwao kutembea na mtu yeyote ilimradi mtu huyo awe katika hali nzuri ya kimaisha na aweze kumppa el, hata hivyo wapo wasachana wazuri na wadogo lakini wanajikuta wakijiingiza katika mahusiano na watu wasiendana nao kwa  umri au kwa kila kitu.Hii imethiirika pia kwa baadhi ya wasanii wa kike Tanzania na mmoja wapo akiwa ni Amber Lulu anasema anaweza kutemba hata na chizi ilimradi ampe ela.

Mwanadada huyo anaefanya vizuri katika kazi zake za muziki na anaetokea vizuri katika video za wasanii mbalimbali amefunguka na kusema kuwa yeye habagui mtu yoyote ilimradi tu mtu huyo awe anampa ela.Akiongea katika moja ya mahojiano na waandisho wa habari Amber Lulu alisikika akisema”mimi ninaweza kutembea hata na kichaa, as long as ananipenda, ananitake care , msambwanda anautake care vizuri mimi wala sina shinda hata chizi mi natembea nae, as long as ananiridhisha vizuri  mimi wala sina shida’ alifunguka Amber Lulu

Amber lulu ambae kipindi cha awali kala hajaanza kutokea katika video mbalimbali alikuwa alipiga picha za uchi na alikuwa na tetesi za kufanya biashara ya ngono , hata hivyo mwanadada huyu anaonekana kuwa anaweza kufanya kitu chochote ilimradi yeye amepata ela itakayo weza kumudu maisha yake na sio kuwa na mapenzi ya kweli na mtu huyo .Amber Lulu ni rafiki wa karibu sana na msanii na video queen Gigy Money na wanaonekanakuwa kazi zao zinafanana.

Katika kazi zake za muziki moja ya nyimbo zake ni pamoja na watakoma aliomshirikisha Country Boy .Amber Lulu alishawahi kutoka kimapenzi na msanii Young Dee na kufikia hatua ya kumchora tatoo lakini walipokuja kuachana aliifuta. Hivi jujzijuzi Amber Lulu tena alikuwa na tetesi za kuvujisha picha zilizokuwa zikimuonyesha yeye na msanii kutoka Kenya Prezzo aliekuja Tanzania na kusemekana kuwa alikuja Tanzania kwa ajili ya mrembo huyo, ingwa yeye mwenyewe alikuwa akipinga tetesi hizo.

Picha Tata Za Prezzo na Amber Lulu Zaleta Gumzo

Mwanamuziki Prezzo kutoka Kenya na Video vixen maarufu Bongo Amber Lulu wameingia kwenye skendo nzito mara baada ya picha inayowaonyesha wakiwa katika ukaribu kuvuja mtandaoni.

Tukio hilo lilitokea juzi ambapo inasemekana Prezzo alikuja Tanzania kwaajili ya kufanya kazi na msanii Dogo Janja.

Hizi ni baadhi ya picha zinazowaonyesha Prezzo na Amber lulu pamoja;

1
2. Hii ni picha aliyopost Amber lulu akiwa na Prezzo

Katika kipindi cha XXL cha Clouds FM mtangazaji Soudy Brown aliwatafuta Prezzo na Amber lulu walifunguka yafuatayo;

“Nilivyojaribu kumchek kwa simu alipokea na sauti yake ilikuwa inasound kama katoka usingizini nikamuuliza uko wapi? akajibu yupo nyumbani kwa mbaalii nikasikia sauti ya Prezzo nikamuomba Amber lulu ampatie simu Prezzo na yeye alikuwa sound katoka kulala, Nikamuuliza vipi mzee baba umeingia lini Bongo? Akajibu yupo tangu jana, Nikamuuliza uko wapi akajibu yupo boardroom ya Seacliff hotel nikamwambia mbona nasikia mwangwi? Akajibu it’s true wako boardroom na Amber lulu ni rafiki yake na ndugu yake hawezi kumtamani”.

Prezzo alipoulizwa kama yupo tayari kumuita Jaquar Mheshimiwa Mbunge akajibu yeye ni president hawezi kumwita Mheshimiwa mbunge wake.

 

Amber Lulu aacha mambo ya kuuza sura kwa video za wasanii wa Bongo

Amber Lulu ni mmoja wa warembo ambao wanatajika sana kwa kuuza sura (video vixen) kwenye video za wanamuziki wa Bongo.

Lulu ametokea kwenye video nyingi kama ile ya ya Dully Sykes na Harmonize ‘Inde’ na zingine. Mrembo huyo sasa hataki mambo ya kuuza sura kwa video za wasanii wa Bongo.

Akiongea na E-Newz ya EATV, Amber Lulu alisema kuwa ameanza kuimba na hataki kufanya mambo ya video vixen kwani itakuwa kama kupiga hatua nyuma.

 

“Sasa hivi nafanya muziki sio video vixen tena kwa sababu nimeshaingia kwenye muziki kwa hiyo nikifanya video vixen nakua kama narudi nyuma na mimi sitaki kurudi nyuma tena nahitaji nifanye vitu vipya. Inatakiwa kama ni muziki wangu niufanye wa international au nizidishe sitaki kurudishana nyuma.

“Maoni niliyoyapokea kwa watu wengi ni mazuri sana, wengi wananishauri vitu vingi kuhusu muziki, kuna baadhi ya wasanii kama wakina Shilole na Chege nimeshakaa nao kuna vitu wameniambia unatakiwa ufanye,” amesisitiza Amber Lulu,” alisema Amber Lulu.