Amber Lulu Akana Tetesi Za Kurudiana na Aslay

Video vixen maarufu ambaye pia ni msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayetamba na kibao chake cha ‘Jini kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kukamatwa kurudiana na msanii mwenzake Aslay.

Miezi michache nyuma Amber Lulu aliyoa siri ambayo haikujulikana kwa watu wengi kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa wapenzi siku za nyuma kabla hajawa maarufu.

Siku za hivi karibuni baada ya Amber kutangaza kuachana na aliyekuwa mpenzi wake Prezzo na kudai yupo single amesemekana kurudiana na Aslay ambaye pia ameachana na mama watoto wake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Amber amekana kurudiana na Aslay lakini alionekana kugoma kabisa kuiongelea ishu hiyo:

Mimi sina mahusiano yoyote na Aslay”.

Mapema mwaka huu Kwenye Interview moja aliyofanya Amber alidai katika wanaume Wote aliowahi kuwa nao Aslay ndio amewahi kumridhisha zaidi.

Amber Lulu Aomba Msaada WCB na Kumtupia Dongo Diamond

Video Vixen na Msanii maarufu wa muziki wa Bongo fleva Amber Lulu amezua gumzo kwenye mtandao wa Instagram baada ya kumtupia Dongo staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Siku chache zilizopita Diamond alizua gumzo baada ya kuposti picha akiwa amevaa cheni ya mguuni ‘kikuku’ ambacho kimezoeleka kuonekana kimevaliwa na wanawake.

Amber Lulu aliposti picha ya Diamond akiwa amevaa kikuku na kuomba nafasi ya kusainiwa ndani ya WCB lakini alisindikiza na maneno ya kejeli kuhusu kuvaa kikuku.

Amber alitumia picha hiyo kumuomba Diamond kumpa nafasi ya kuwa Bosi wake na kumuomba ampe mkataba wa kuwa mmoja kati ya wasanii walio chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB)

https://www.instagram.com/p/BlQ6eHthODV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1isnpb8nfnavt

Diamond ni CEO wa WCB na katika label hiyo kuna wasanii kadhaa wa kiume lakini kuna msanii mmoja tu wa kike ambaye nidada yake na Diamond, Queen Darleen kwaiyo itakuwa ni vema kupata msanii mwingine wa kike ingawa Diamond

Young Dee sio Type Yangu Akitoa Prezzo Sasa Labda Anaweza Kuwa Wizkid au davido :-amber lulu.

Baada ya mwana dada Amber Lulu kuthibitisha kuwa alipigwa na young dee studio  na kusema kuw aswala kubwa liliomfanya mwanaume huyo kumpiga ilikuwa ni wivu aliuonao kwa kuwa amekuwa akimuona yuko na wanaume wengine tofauti na yeye,

hata hivyo Amber Lulu anasema kuwa  Young Dee sio type yake tena kwa sasa kwa sababu kama ametoka kuachana na prezoo kutoka kenya wala hafikirii kuwa na Young Dee tena labda aende mbele zaidi kwa watu kama Davido au Wizkid.

Akihojiwa na mwandishi amber lulu anasema” Alinikuta nikiwa na meneja wang studio akataka kuanza ku-make drama naona akaona wivu lakini anashindwa kujua kuwa sio type yangu young dee kwa sasa hivi  kashatoka prezzo anatakiwa aje mtu  mwingine kama wizkid, au davido,

Amber lulu ambae aliwahi kuwa na mahusiano ya yong dee na baada waliachana na yeye akawa na mahusiano ya mapezni na msanii kutoka kenya ambae walikuja kuachana vbaya na Amber Lulu kutangaza kuwa yuko single na hataki tena kujihusisha na maswala ya mapenzi kwa sasa.

 

Amber Lulu Apewa Kichapo Cha Mbwa Koko na Young Dee

Video Vixen na msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na Single yake ya ‘Jini kisirani’ Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu amekiri kupokea kipigo cha mbwa koko kutoka kwa msanii mwenzake Young Dee.

Wiki iliyopita kipindi cha XXL cha Clouds Fm waliripoti kuwa Kwenye studio fulani hapa Mjini Amber Lulu alionekana akiwa anapigwa vibao, ngumi na hadi mateke na Young Dee.

Baada ya kipigo hiko Amber aliweka wazi kuwa sababu iliyomfanya mpaka Young Dee ampige ni baada ya kukataa kuwa naye Kimapenzi na kisha kutinga ndani ya studio hizo na mwanaume mwingine.

Kwenye mahojiano na Sam Misago Amber alikiri kupigwa na Young Dee lakini amesisitiza kuwa ulikuwa ni wivu wa kimapenzi:

Kweli Young Dee amenipiga kwa ajili ya wivu mimi ni mzuri lazima unitamani we mwenyewe umeona hili tak* usilitake Tena ? Mimi ni mzuri alafu ananitaka halafu mimi simtaki siwezi kuwa na bwana mariooo alivyoniona akaanza kuniletea Sholo nyingi alafu mimi sitaki shobo”.

Amber Lulu ameshawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee katika siku za nyuma lakini wawili hao walishaachana ingawa Amber amekiri mara kwa mara kuwa anampenda sana.

Amber Lulu Aweka Mapenzi Pembeni Baada Ya Kuumizwa

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jini kisirani’ Lulu Euggen maarufu kama Amber Lulu amedai ameamua kuweka masuala ya mapenzi pembeni.

Kwenye mahojiano na Global Publishers Amber Lulu ameweka wazi kuwa, amekuwa kwenye mahusiano mengi, lakini anaona ni kama anapoteza tu muda wake tu.

Mapenzi yameninyoosha bora niyapige chini maana wanaume wengi wananipenda kwa sababu ya umaarufu wangu, lakini unakuta hawana mapenzi ya kweli kwangu. Ninaona tu huko ninapoteza muda na kuambulia maumivu, kwa hiyo bora nijiweke wazi tu, hakuna namna“.

Amber Lulu amemaliza Mahusiano Yake ya kimapenzi siku chache zilizopita na Msanii kutoka +254 Nairobi, Kenya Kwa tuhuma za kuzidisha michepuko.

Amber Lulu Atangaza Kuwa Single, Asema Mapenzi Yamemshinda

Mwanadada Amber Lulu amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana muda wa mapenzi tena na ymeshamchosha kwaio anaona bora achane nayo na kubaki kuwa single kuliko kuenedelea kukaa katika mapenzi kwa sababu sio mapya na hayamuingizii kitu chochote katika maisha yake.

Amber lulu ambae akikuwa katika penzi nzito na mwanamuziki kutoka nchi Kenya, amefunguka  lakini hapo katikati penzi hilo lilionekena kuyumba kutokana na kuwepo kwa mahusiano mapya kati ya msanii huyo na mwanamke mwingine.

Katika ukurasa wake wa instagram, amber lulu aliamua kuandika ‘SINGLE GIRL’ akimaanisha kwa sasa hana mahusiano yoyote  na katika caption yake aliandika kuwa “nimechoka , maisha mengine yaendelee.ya mbwana yamenishinda ngoja nikitulize tu nitafute ela maana sio mapya.”

 

Penzi la Prezo na Ambaer Lulu Laingia Mdudu

Mwanadada Amber Lulu hapo siku za nyuma alikuwa akijitapa baada ya kuonekana akiwa katika mahusiano ya kimapezni na msanii kutoka Kenya Prezzo na kusema kuwa wawili hao hawawezi kuachana  kwa sababu wana mpnago wa kufunga ndoa lakini mambo yamekuwa sio baada ya kusambaa picha za mwanaume huyo akiwa na mwanamke mwingine.

Picha hizo zilizonyakwa huko mitandaoni zinamuonyesha prezzo akiwa na mwanamke mwingine huku katika ukurasa wa mwanamke huyo akiwa ameweka caption inayoashiria kuwa waili hao ni wapenzi .

Hata hivyo hapo awali kuna picha pia zilikuwa zikisambaaa katika mtandao zikimuonyesha aslay akiwa na amber lulu nahata ambaer lulu alipoulizwa alisema kuwa yeye na Prezo mambo yao hayajakaa vizuri lakini aliwahakikishai waandishi kuwa kila kitu kitakuwa solved.

Lakini siku za hizvi karibuni inaonekana kabisa kuwa pezni la wawili hao linaendelea kupumulia mashine kwanza kutokana na ukaribu wa kimapenzi kati ya prezzo na mwanamke mwingine lakini pia kutokana na picha Amber Lulu anazoweka katika ukurasa wake akimuomba mpenzi wake hyo msamaha.Hata hivyo amber lulu hajaongea chochote kuhusu mahusiano hayo mpaka sasa.

Amber Lulu Amuonea Huruma Hamisa.

Mwana dada Amber Lulu amefunguka na kusema amekuwa akimuonea huruma sana  Hamisa Mobeto kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiandamwa na watu hasa familia ya ndugu wa Diamond mwanaume ambae amezaa nae mtoto mmoja wa kiume na kuonekana kuwa hapendwi na familia hiyo.

Anachokisema Amber Lulu ni kwamba anaamini kuwa Mungu yupo na Hamisa na ipo siku atamuona na kumpigania sana na kumtoa katika kifungo icho cha mateso anachopitia kwa muda wote sasa.

Mimi ninamuamini sana mobeto na nina jua ni mwanamke anaejiamini sana,kwaio hilo linalomtokea sasa ni changamoto tu za maisha , niseme tu yeye aendelee tu na biashara zake  na kazi zake kwa nguvu zake zote na kulea familia yake,achukulie hiyo kama chngamoto tu na kufanya kazi zake kwa bidii na kama mwanaume anampenda basi atarudi tu.

 

 

Amber Lulu- Aslay Ameshawahi Kufaidi Penzi La Wema Sepetu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha ‘Jini Kisirani’ Amber Lulu amefunguka na kupasua kuwa Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameshawahi kufaidi penzi la staa wa Bongo fleva Aslay.

Amber Lulu, ametoboa siri ya Wema Sepetu na Aslay kuwa wapenzi miaka ya nyuma lakini pia amedai waliwahi kuishi pamoja kinyumba kama mke na mume.

Wiki iliyopita Amber Lulu alianika hadharani kuwa yeye na Aslay walishawahi kuwa Kwenye Mahusiano pale alipoanika orodha ya wanaume ambao ameshawahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers, Amber Lulu ameweka wazi kuwa kipindi alipokuwa na Aslay alisikia pia alikuwa na Wema Sepetu aliyekuwa anaishi naye nyumba moja kitendo kilichofanya Mahusiano yao yasiwe serious:

Kipindi hiko nilikuwa undergrad nikawa nasikia Aslay alishakuwa na watu wengi nasikia alishakuwa na Wema Sepetu na wakakaa nyumba moja na wakapika na  kupakua halafu mimi kipindi hiko bado kabisa nilikuwa nanyapia nyapia”.

Amber Lulu amedai kuwa Aslay alikuwa ni fundi mzuri sana kunako mausuala ya sita kwa sita huku pia akitumia sifa hiyo kumtofautisha na Mbongo Fleva mwingini, Young D ambaye nae pia alikuwa mpenzi wake lakini hakuwa fundi sana kama ilivyo kwa Aslay.

Amber Lulu- Ma-video Queen Wa Kibongo Hawana Hela Wanajua Kudanga Tu

Msanii wa Bongo fleva anayefanya vizuri na kibao chake cha Jini Kisirani Amber Lulu amefunguka na kuweka wazi kuwa mavideo Queen wa kibongo hawalipwi vizuri wanategemea kudanga tu.

Amber Lulu alijizolea umaarufu kutokana na kuwa video queen ambazo ameshaonekana Kwenye video za Wasanii kibao.

Baadaye Amber Lulu aligeukia muziki wa Bongo fleva ambao umekuja kumpa mafanikio Kupitia kibao chake cha jini kisirani.

Kwenye mahojiano na Wasafi Tv,  Amber Lulu anafunguka na kuweka wazi kuwa wasichana ambao wanatumika kama mavideo Queen Kwenye video za wasanii hawana pesa na hawalipwi vizuri hivyo wanaishia kudanga.

Kusema kweli kibongo Bongo bado uvideo vixen haulipi wengi wanakuwa wanadanga tu na labda uwe unafanya biashara nyingine extra lakini u-video vixen haulipi we mtu unakaa gheto kali lakini unavaa Brazilian hair, unashika simu kali alafu unasema unalipa nani anakulipa? Utaishia kupanda vibajaji hata uber hupandi”.

Lakini pia Amber Lulu amefunguka kuwa muziki unalipa sana mtu unaweza ukaendesha maisha yako kupitia muziki.

muziki unalipa unaweza ukafanya kila na kuendesha maisha yako kila kitu na hata kulipa bili mbali mbali “.

Amber Lulu Aanika Orodha Ya Mastaa Aliowahi Kubanjuka Naye

Video vixen maarufu nchini Amber Lulu ambaye hivi karibuni amepenya Kwenye tasnia ya Bongo fleva na anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jini kisirani’ ameweka hadharani majina ya wanaume wote aliowahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv, Amber Lulu aliulizwa listi ya wanaume mastaa ambao amesha wahi kubanjuka nao na akawataja hawa:

Barnaba, Aslay, Rammy Galis naYoung Dee lakini Young Dee sio sana, hao wanatosha, hao wengine hapana”.

Aslay nilishatoka naye ila alikuwa ni mtu fulani muelewa, yuko poa, ana heshimu mwanamke. Yuko noma, yuko vizuri, Aslay kiboko kabisa”.

Amber Lulu alipoulizwa kuhusu Prezzo aliweka wazi  kuwa ni mume wake na anampenda lakini pia Amber Lulu  aliweka wazi kuwa kutokana na video iliyovuja kati yake na Nuh Mziwanda imesababisha yeye Kutoswa na Prezzo.

Mrembo Kim Nana Adai Amber Lulu na Gigy Maney Sio Level Zake

Video Queen anayekuja kwa kiasi ya ajabu Kwenye tasnia Lilian Paul Kessy maarufu kama Kima Nana amewaponda vibaya mno wasanii Amber Lulu na Gigi Money huku akidai hawafai kuwa mavideo vixen.

Kim Nana alijizolea umaarufu baada ya kuonekana kwenye video za wanamuziki kama Beka Flavor ameibuka na kudai mavideo Queen hao ambao wameongia Kwenye Bongo fleva hawakuwa level zake.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, amefunguka na kudai ni bora wadada hao walivyoingia Kwenye muziki kwani hawakuwa na mvuto wa kuwa wauza sura wa Kwenye video:

Amber Lulu na Gigy Money hawanivutii kabisa na hawana mvuto wa kuwa ma-video queen. Bora ‘wa-stick’ hukohuko kwenye muziki walikokimbilia”.

Lakini pia mrembo huyo alijitamba ni bora kuliko mavideo Queen wote kwa Bongo kwa sababu ana muonekano wa kuwa hivyo tofauti na ilivyokuwa kwa Gigy Money na Amber Lulu.

Amber Lulu

Kim Nana alipoulizwa kuhusu tuhuma za mavideo Queen wengi Bongo kutembea na wasanii mbali mbali ili wapate umaarufu alikataa na kudai yeye yupo kikazi zaidi hana time hiyo:

Mimi ninajiheshimu, nikiitwa na mwanamuziki kuhusu kazi, tunafanya halafu basi. Tutaendelea kuwasiliana kwenye mambo mengine, lakini siyo mapenzi. Sijawahi kutoka kimapenzi na staa yeyote Bongo na sitarajii hilo kwa sababu kuwa na uhusiano na mastaa kuna-umiza kichwa. Wengi hawa-jatulia“.

 

Amber Lulu Apata Dili la Kutangaza Kondomu

Video vixen na msanii wa Bongo movie nchini Amber Lulu anekwaa dili refu la kutangaza Mipira ya kiume/ kondomu.

Amber Lulu amefunguka kuhusu Dili hilo nono aliloplipata huku akiweka wazi kuwa limeweza kumpatia mpunga mrefu:

Nimepata mpunga mrefu nimshukuru Mungu, ni hatua moja ambayo nimepiga, so inabidi tushukuru Mungu wote”.

Baada ya kupata dili hilo Amber Lulu aliweka Habari hiyo njema na kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Hii ni habari njema kwa Amber Lulu ambaye tayari anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jini Kisirani’.

Ommy Dimpoz Amfungukia Amber Lulu Baada Ya Kumwambia Hana Mvuto

Mwanamuziki wa Bongo fleva Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amemjibu msanii mwenzake Amber Lulu ambaye wiki iliyopita alisema Ommy hana muonekano wa kiume.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Jonijoo wiki iliyopita Amber aliulizwa kati ya Jux na Ommy Dimpoz ni mwanaume yupi ambaye anaweza akawa naye kimapenzi na moja kwa moja Amber Lulu alisema Jux kwa sababu Ommy hana muonekano wa kiume

Jux sawa, Dimpoz hajakaa kama mwanaume, Ommy Dimpoz hawezi kukaa au kushindana na Jux ni zero, hana mvuto wowote , hamna chochote kinachonivutia kutoka kwake”.

Baada ya video clip hiyo kutrend sana ambayo ilikuwa inamuonyesha Amber akiongea hayo Ommy Dimpoz alijibu tuhuma hizo za Amber Lulu kuwa hana mvuto na hana muonekano wa kiume ambapo ameweka nyeusi kwa kusema hataki kumuongelea mtu huyo (Amber Lulu).

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Ommy Dimpoz alifunguka maneno haya:

Mimi sijui chochote na sijui hizo stori zimetoka wapi na zimeanzia wapi lakini kikubwa sisi kama wasanii unajua kila siku vitu ambavyo vinatuzunguka ni mambo ya mitandao, kwa hiyo in short no comment”.

 

Nisha Akana Skendo Ya Kumtongoza Young Dee

Muigizaji wa Bongo movie anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya Bachela amejibu tuhuma alizotupiwa kuwa ana Mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Bongo fleva Young Dee.

Siku ya jana msanii wa Bongo fleva Amber Lulu alitoboa Siri na kusema kuwa kipindi ana Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee, mwanadada Nisha alikuwa anamtongoza Young Dee.

Amber Lulu aliweka wazi kuwa jambo hilo lilikuwa la wazi hadi alikuwa ana ushahidi kwani alikamata meseji za wawili hao huku alikiri kuwa Nisha ni fundi wa mapenzi maana alikuwa anampa maneno matamu Young Dee.

Baada ya kutupiwa tuhuma hizo Enews ya EATV ili mtafuta Nisha kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na moja kwa moja alikataa na kusema kuwa hajawahi kuwa na Mahusiano na Young Dee zaidi ya urafiki:

Mimi sina Mahusiano na Young Dee ila kilichotokea ni kwamba nilikuwa nataka ni kuingia kwenye muziki hivyo  Young Dee kama msanii wa Bongo fleva alikuwa ananisaidia na lazima niwe karibu na wasanii we zangu.

Alafu mimi nimemjua Young Dee kabla hata hajawa na Mahusiano na Amber Lulu kwaiyo ni mtu wangu wa karibu na trust me angekuwa mpenzi wangu nisingeweza kuficha maana mimi nikipenda nataka watu wote wajue”.

 

Amber Lulu: Nisha Alikuwa Anatembea na Young Dee Wakati Niko Naye

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Amber Lulu amepasua jipu na kumuanika hadharani msanii mwenzake Nisha na kudai alikuwa anaingilia penzi lake na staa wa Bongo fleva Young Dee kwa kumtongoza.

Amber Lulu aliyewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Young Dee amekiri kuwa wakati akiwa na Mahusiano na Young Dee alikuwa mtu wa michepuko sana kiasi ya kwamba alishawahi kubamba meseji za  Young Dee na Nisha wakichat kama wapenzi.

Amber Lulu alitoa siri hiyo Kwenye mahojiano aliyofanya na Enews ya EATV ambapo amesema ushahidi kuwa wawili hao walikuwa wakichepuka anao:

Nikiona meseji zao walikuwa wanavhat vizuri tu sema kiroho safi sikumaindi sana kwa sababu hatukuwa official na mimi mwenyewe nilikuwa na mambo yangu pembeni lakini nina ushahidi kuwa Nisha Kapita kwa Young Dee.

Nakusema ukweli Nisha fundi maana ana maneno matamu nini nilisoma mpaka mwenyewe nikakubali”.

Nisha alipoulizwa habari hiyo alikana kusema meseji alizoziona Amber Lulu zilikuwa ni meseji za kikazi tu lakini hajawahi kuwa na Mahusiano ya kimapenzi na Young Dee.