Hivi Ndivyo Ali Kiba na Diamond Walivyojaza Nyomi la Watu Kwenye Show za Kenya na Rwanda (picha na video)

Wasanii wakali wa Bongo fleva wanaozidi kufanya vizuri Diamond Platnumz na Ali Kiba, wamedhihirisha ukubwa wa muziki wao kila mmoja kwa wakati wake.

Mwishoni mwa wiki hii iliyopita wasanii wote wawili walikuwa na shoo nje ya nchi ambapo Diamond alikuwa na shoo ya kufunga mwak nchini Kenya, Naivasha na Ali Kiba alikuwa na shoo nchini Rwanda.

Ali Kiba

Alikiba alidhihirisha ukubwa wa muziki wake baada ya kupiga shoo ya peke yake nchini Rwanda iliyovuta watu wengi ambapo ilisemekana kuwa Kiba alipiga bonge la shoo kwenye uwanja huo wa mpira ambao alijaza mashabiki walioenda kumuona akitumbuiza.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazomuonyesha Kiba akitumbuiza sherehe yake ya kufunga mwaka na Kiba:

 

 

 

  1. Diamond Platnumz

Diamond alizidi kudhihirisha ukubwa wa muziki wake nje ya nchi baada ya kupiga bonge la shoo la kimataifa nchini Kenya katika mji wa Naivasha ambapo katika ukumbi huo aliopiga shoo naweza thubutu na kusema kuwa Alijaza maana kulikuwa bonge la nyomi la watu.

Hizi ni baadhi ya picha na video zinazoonyesha nyomi la Watu walioenda kwenye show ya Diamond;

 

Mwanamke Mkenya Aganda Nyumbani Kwa Diamond Akidai Amezaa Naye

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnunz amerudi tena kwenye headlines baada ya mwanamke mwingine kumtuhumu kuzaa naye kisha kutekelezwa.

Mwanamke mmoja raia wa Kenya ameripotiwa kuweka kambi nje ya nyumba ya Diamond akidai kuwa hapewi pesa ya matunzo ya mtoto aliyezaa na msanii huyo. Mwanamke huyo aliyejitambulisha kama Mama Pensheni Salama anayedai kuwa raia wa Kenya aliripotiwa kukesha yeye na mtoto wake nje ya nyumba ya Diamond ikiwa ni jitihada ya kumpata msanii huyo.

Mama Pensheni alipohojiwa alieleza kuwa ni kwa muda mrefu sasa amekuwa akimtafuta Diamond bila mafanikio na amekuja Nyumbani kwake baada ya kusikia mzazi mwenza na Diamond, Zari atakuwepo nchini Tanzania hivyo ataweza kumsaidia kwani na yeye ni mwanamke kama yeye.

Walinzi wa mtaa anaoishi Diamond baada ya kumkuta Mama Pensheni  amelala nje ya nyumba ya msanii huyo walimpeleka kwa mjumbe wa mtaa kwa ajili ya kumhoji. Mjumbe wa mtaa huo, Christina Chilumba alipotafutwa na kuhojiwa alikiri kuwa ana taarifa za ujio wa mwanamke huyo na kueleza kuwa mwenyekiti ndio ana taarifa zaidi kumhusu. “Ni kweli huyo mwanamke alikuja na kulala na mtoto wake pale getini kwa msanii huyo baadae alipelekwa ustawi wa jamii lakini kwa maelezo zaidi mtafuteni mwenyekiti ambaye kwa sasa yupo kikaoni yeye atawaeleza zaidi”. Aliongea Christina.

Walipomtafuta Mwenyekiti wa mtaa huo Deo akamugisha alikiri kupata taarifa za mwanamke huyo ambaye alikiri kutokea nchini Kenya na kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kumtafuta Diamond aliyedai ni baba wa mtoto wake.

 

 

Baba Diamond: Sijawahi Kuongea na Zari Ila Hamisa na Wema Nimeshaongea Nao

Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Mzee Abdul  Juma amefunguka kuhusiana na uhusiano wake na mkwe wake Zari na kukiti kuwa hajawahi kuonana naye wala kuongea naye ila ameshaongea na Wema pamoja na Hamisa.

Sio siri kuwa Diamond na Baba yake Mzee Abdul hawana uhusiano mzuri sana miaka michache iliyopita Baba wa Diamond alienda kwenye vyombo vya habari na kutangaza kuwa mwanaye Diamond hamjali kwa chochote kile na amemtupa, Diamond aliweka wazi kuwa baba yake alimkataa tangu akiwa mdogo na ni mama yake pekee ndiye aliyemlea.

Tangu hapo Diamond na  baba take wamekuwa wakiongea vitu viwili tofauti na vyombo vya habari. Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu Baba Diamond alirudi kwenye vichwa vya habari miezi michache iliyopita baada ya kushiriki kwenye Arobaini ya mtoto wa Hamisa ambayo mwanaye Diamond na familia yake hawakuudhuria.

Baba Diamond alipofanya mahojiano na Millard Ayo alifunguka mengi kuhusu wajukuu zake na mkwe wake Zari:

Nikitaka kuwasiliana na wajukuu zangu walio nchi za nje naonana na Mama Nasibu nampa salami tu basi lakini nikitaka kuonana na mjukuu wangu mtoto wa Hamisa kwa kuwa yupo hapa Dar karibu na ninapoishi hivyo wanakuja tu kunichukua basi lakini kusema kweli Zari sijawahi kuzungumza naye ila katika wakwe zangu mtu wa kwanza kuzungumza naye alikuwa Wema Sepetu na Hamisa Mobetto ambaye kusema kweli namshukuru kwa kunipa heshima zote Kama babu kwa kumpa mjukuu wangu jina langu kwa kweli namshukuru Sana”.

 

Mwana FA- Sina Bifu na Diamond Wala Simchukii

Mwanamiziki mkongwe wa Bongo fleva Hamis Mwinjuni ‘Mwana FA ‘Mwanafalsafa’ amefunguka na kudai kuwa hana tatizo na msanii mwenzie Diamond Platnumz wala hajawahi kumchukia.

Kumekuwa na tetesi nyingi Sana kuwa Mwana FA na Diamond hawapatani hata kidogo hii ikihusishwa na Mwana FA kuwa na urafiki na mahasimu wakubwa wa Diamond ambao ni Ali Kiba na ukaribu alionao na Ommy Dimpoz.

MwanaFA ameshatoa nyimbo na AliKiba kitendo kilichotafsiriwa na mashabiki wa Diamond (Team Diamond) kuwa amechukua upande wa mahasimu wa Diamond hivyo atakuwa mpinzani na atakuwa namdiss Diamond.

Kwenye Mahojiano aliyofanya na Sky, Dizzim Online Mwana FA aliweka wazi hisia zake kuwa haelewi maneno hayo yanatokea wapi kwani hasa ikiwa wazi kuwa hajawahi kugombana na Diamond hata siku moja na kusistiza hana bifu naye na wala hamchukii:

Unajua mashabiki ni mashabiki hiki kitu kingekuwa kikubwa kama Diamond mwenyewe angekuja akasema mimi nahisi Mwana FA hanipendi hapo tunhweza kuwa na mjadala lakini mimi siwezi kujadiliana na watu ambao wanafikiria nina imani Diamond hawezi kusema vitu wanavyosema wao inawa huwezi kusemea kichwa cha mtu lakini nina imani hawezi kuwa na mindset ambayo wale jamaa wanayo, lakini humu kwenye muziki watu wanajuana lakini mtu ana marafiki zake kwa mfano kitu ambacho nilikiona naulizwa ni mbona Diamond akitoa wimbo humposti? Lakini hawajiulizi kwanini mimi nikitoa nyimbo Diamond haniposti na sijawahi kulalamika mahali popote hapa ndio nipapokwambia kila mtu ana marafiki zake, mbona hakuna ambaye amewahi kunilalamikia kwa nini Shilole ametoa nyimbo sijaposti panini Ommy Dimpoz asipoposti nyimbo yangu tutakuwa na matatizo kwasababu ni rafiki yangu and am supporting him. Lakini Mimi sina tatizo na Diamond hata kidogo wala hatujawahi kugombana”.

 

Waka Ya Diamond Yazidi Kuvunja Rekodi Katika Nchi Zaidi Ya Saba

Mwanamuziki wa Bongo fleva na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz ameweka rekodi mpya kupitia wimbo wake wa Wqka aliomshirikisha rapa maarufu kutoka Marekani, Rick Ross.

Diamond aliachia ngoma hiyo wiki iliyopita na moja kwa moja ilishika namba moja kwenye mtandao wa YouTube na kuipiku nyimbo iliyoshika namba moja kwa wakati huo ya Abdu na Ali Kiba inayoitwa single.

Ingawa hii haikuwa mara ya kwanza kwa Diamond kutoa ngoma na kisha ngoma hiyo kukubalika kimataifa zaidi alishafanya hivyo na ngoma kama My no. 1 remix aliyomshirikisha Davido lakini pia alisumbua na ngoma yake ya Hallelujah aliyomshirikisha Morgan Heritage kwa mwaka huu.

Siku mbili baada ya kuachia goma hilo la Waka ilishika nafasi ya kwanza kwa kutrend kwenye mtandao wa YouTube kwenye nchi tatu za Africa Mashariki yaani ilikuwa namba moja Tanzania, Kenya na Uganda.

 

Diamond hakuishia hapo akiwa amezidi kushika namba moja nchini Tanzania pia aliweza kukamata nafasi za juu kabisa kwenye nchi kama Zimbabwe, Nigeria, Ghana , South Africa na Kenya na Uganda.

 

Mpaka sasa video hiyo ya Diamond iliyoachiwa siku kumi zilizopita Ina jumla ya watazamaji milioni 2.8 huku ikizidi kushika namba moja.

Mume Wa Mama Diamond Akumbwa na Skendo Mpya Za Utapeli

Mume wa Mama Diamond anayejulikana kwa jina la Maisara Abdul Shamte ameingia kwenye vichwa vya habari za udaku baada ya habari kuenea kuwa ni tapeli tu.

Mama mzazi wa msanii Diamond Platnumz anayejulikana kwa jina la Bi. Sandrah alikamata headlines wiki iliyopita baada ya kumtambulisha mume wake mpya ambaye kwa watu wengi alionekana kijana Sana kuliko yeye lakini alizua mzozo zaidi pale aliposema kuwa anataka kumzalia mume wake mtoto ambaye atakuwa mdogo wa Diamond.

Sasa mume huyo mpya wa mama Diamond amerufi tena kuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya habari kusambaa kuwa ni tapeli we kutupwa anayewinda wamama watu wazima ili awatapeli mali zao.

Mange Kimambi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika tuhuma hizo nzito dhidi ya mume wa Mama Diamond.

Huyo Maisara Abdul Shamte ni tapeli wa kutupwa, yaani Benki ya CRDB anadaiwa milioni mia na thelathini alimdanganya meneja wa crdb kuwa atamuoa akachukua mkopo akaingia mitini…amesababisha nyumba ya mama mmoja mjane imeuzwa na benki na shauri hhuyo Bi. liko mahakamani, na huyo mjane alimlaghai kwa  mapenzi akachukulia mkopo nyumba yake na huo mkopo akanunulia gari na matanuzi mengine”.

Lakini chanzo hiko hakikuishia hapo kumrushia tuhuma hizo za utapeli pia kimedai kiwa sababu pekee Shamte amekubali kumuoa Mama Diamond ni ili amtapeli kwa sababu ameona kuna mwanya wa kula pesa za Diamond:

Yaani huyo Shamte a.k.a Uncle ni tapeli sijui nikuelezeje ameshamaliza wanawake watu wazima wengi sana kuna mama wa kichaga alimuoa akamfilisi kila kitu alivyomaliza ndo amehamia kwa Mama Diamond, majuzi alijifanya ameagiza unga Irani akachukua pesa kwa Huyo Bi. Sanura ndiyo Kisa cha kumdanganya na kufunga naye ndoa na huyo Bi Sandrah alimpa Shamte milioni nane nzimaa akaenda kuzirukia bata anamdanganya eti mzungu wa unga anajifanya  anaongea lugha ya Kiirani ili awaingize mkenge”.

Mpaka hivi sasa Shamte na  familia ya Diamond haijakubali wala kukataa tuhuma hizi lakini zinazidi kusambaa mitandaoni.

Mrembo Irene Amekiri Kuwa Alibeba Ujauzito Wa Diamond (video)

Mrembo na Video queen maarufu Irene au maarufu mitandaoni kama Officiallynn amefunguka na kukiri kuwa miezi michache iliyopita alibeba ujauzito wa Diamond lakini kwa bahati mbaya ujauzito uliharibika.

Irene  alijipatia umaarufu zaidi baada ya kutokea kwenye video ya msanii wa Wasafi Classic Co. (WCB) anayejulikana kama Rayvanny kwenye wimbo wake wa kwetu na natafuta kiki.

Lakini Irene alizidi kujipatia umaarufu pale habari zilipoanza kusambaa kuwa anatembea na msanii maarufu wa Bongo fleva, Diamond Platnumz lakini taarifa hizi zilipata umaarufu zaidi kwa sababu katika kipindi hiki chote Diamond bado alikuwa jwenye uhusiano na mama watoto wake Zari.

Habari za Irene kuwa na mimba ya Diamond zilianza kusikika miezi michache iliyopita lakini kulikuwa hamna uhakika wowote kuwa kama taarifa hizi zina ukweli wowote kwani kuna watu waliodai kuwa mimba ile ilikuwa ya msanii Rayvanny, lakini tetesi hizo zilisimama baada ya mimba hiyo kuacha kuonekana na watu kudhani kuwa ameitoa au alikuwa hana mimba kabisa.

Siku ya Jana Irene alifanya mahojiano na Dizzim Online na katika mahojiano hayo Irene alikiri kuwa ni kweli alikuwa mjamzito na Mimba hiyo iliharibika na baba alikuwa Diamond:

Nilikuwa nina Mimba kweli ila ikaharibika, na ilikuwa ya Diamond”.

Tetesi za Diamond kutoka na mrembo Irene zilizidi kushika hatamu hata pale ishu ya Hamisa ilipobumburuka kwani kuna taarifa mbali mbali zilizoenea mtandaoni kuwa walionekana nchini South Africa pamoja.

Mashabiki Wamjia Juu Mama Diamond Baada ya Kutomtaja Mtoto Wa Hamisa Kama Mjukuu Wake

Mama mzazi wa msanii Diamond Platnumz Bi. Sandrah, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mashabiki kumsema baada ya kugoma kumtambua mtoto wa Hamisa.

Miezi michache iliyopita Diamond alikiri mbele ya uma wa Watanzania kuwa alimsaliti mpenzi wake na mama wa watoto wake Zarinah Hassan na kuzaa na mchepuko wake Hamisa Mobetto. Lakini kilichowavutia watu wengi ni kuwa Diamond hakumkataa mtoto wake bali alimkubali kwa moyo mmoja.

Lakini tangu kipindi hicho kipite hali imekuwa tofauti na watu wengi walivyofikiria kwani Diamond hana uhusiano wowote na mtoto wake na ni miezi michache tu iliyopita Hamisa ametoka kumburuza Diamond mahakamani na kudai kuwa tangu mtoto amezaliwa hajatoa matunzo yoyote.

Pia kwa upande wa familia ya Diamond haijaonyesha ukaribu wowote na mtoto wa hamisa Kama ilivyokuwa na watoto wa Diamond na Zari. Mama Diamond amekuwa akilaumiwa na mashabiki wengi kwa kumtenga mtoto wa Hamisa kwani anaonyesha mapenzi kwa watoto wa Zari lakini sio mjukuu wake kwa Hamisa.

Siku ya leo Mama Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwajia juu watu wote wanaomkosoa kwa kupenda kuwaposti wajukuu zake wawili tu na hata mkwe wake Zari na hili ndio lilikuwa povu lake:

Mapenzi niliyonayo kwa wanangu hawa hayana mfano. Ninapomposti mkwe wangu Zari na mwanangu Diamond sifanyi kwa ajili ya kuwaridhisha wasiotupenda…Nawaposti kwa ajili ya mapenzi makubwa kwao na wajukuu zangu Tiffah na Nillan . Imani yangu sio kumkwaza mtu  au kumkebehi bali ninawapendaga sana. Akaunti hii ni Mali yangu kwaiyo asitokee mtu wa kunipangia cha kuposti au kujifanya mama/baba ushauri maisha kuchagua sio kuchaguliwa”.

Mashabiki walimjia juu Mama Diamond na kumtuhumu kuwa anamtumua Zari ili kumrusha roho na kumuumiza Hamisa lakini pia watu wamemsema Mama Diamond kwa kuwapenda watoto wa Zari Latino kumtenga mtoto wa Hamisa.

Familia Ya Diamond Yadhihirisha Utajiri Wao Baada Ya Kumwaga Mamilioni Kwa Romy

Familia ya Supastaa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz ilidhihirisha utajiri waliokuwa nao baada ya kumwaga mamilioni ya pesa kama zawadi kwenye harusi ya Rommy Jones.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Kaka na Dj wa Diamond, Rommy Jones alimuoa mpenzi wake wa siku nyingi anayejulikana kama Kay. Katika harusi hiyo ya kifahari iliyo hudhuriwa na mastaa kibao Familia ya Diamond ilihakikisha kuwa wanamwaga pesa za kutosha kama zawadi kwa Rommy na mkewe mpya Kay.

Diamond kama kaka wa Rommy na mtu wakw wa karibu kabisa alitoa zawadi ya nyumba iliyo na thamani ya milioni 100 ambapo Diamond aliongea maneno haya ili kuonyesha jeuri ya pesa:

Kwanza kabisa naomba nimshukuru kaka yangu kwani nimekuwa naye toka chekechea tumesoma wote mpaka sekondari kwaiyo ina maan akama asingekuwa ananiongoza pia nisingekuwa hapa nilipo, lakini pia sijamwambia Rommy mimi ntampa zawadi gani lakini mimi namwambi azunguke atafute nyumba inayofika milioni 100 mimi namlipia”.

 Lakini pia zawadi hazikuishia hapo kwani mama yake na Diamond anayejulikana kama Bibi. Sandra ambaye ni Mama mdogo wa Rommy Jones alitoa zawadi ya kiwanja ambacho kina thamani ya shilingi milioni 80 ambapo aliambiwa hati ikakamilika basi atakabidhiwa na wakili wa Mama Dangote.

Pia familia hiyo ilionyesha kufuru ya pesa baada ya maharusi hao kutunzwa pesa nyingi sana walizokuwa wanarushiwa kwa kutunzwa ukumbini hapo.

Christian Bella: Mimi na Alikiba ni Wahenga Ila Diamond ni Digitali

Msanii wa bongo fleva anayefanya mziki wa dansi nchini, Christian Bella amefunguka na kudai kuwa yeye na msanii mwenzake Alikiba ni wahenga lakini Diamond ni msanii wadigitali.

Hivi karibuni kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa Christian alidai kuwa yeye na Alikiba ni wasanii wazuri lakini hawawezi kupambanishwa katika kitengo kimoja kwani wanafanya mziki Mkubwa.

Christian Bella amepiga stori na Bongo 5 na amefunguka na  kuzungumzia ukongwe wake kwenye muziki bila kutetereka na kumsifia msanii mwenzake Alikiba na kudai kuwa Diamond  ni msanii wa digitali sio msanii wa zamani kama yeye na Alikiba.

Kwenye mahojiano hayo alifunguka yafuatayo:

Unajua wasanii kama Diamond, Belle 9 na wengineo walioingia kwenye gemu kuanzia mwaka 2010 ni wasanii wa digitali, lakini  mimi nampa sana saluti msanii mwenzangu Alikiba ambaye naweza sema ni mhenga kama mimi au msanii wa analogi mwenzangu maanaalianza kuhit kitambo sana yaani amevuka kutoka kwenye analogies mpaka sasa bado yupo anapambana na vijana wa kwenye digitali alafu mimi nakuja Tanzania  2005 namkuta Alikiba tayari ana-hit yaani supastaa ana ngoma nyingi zinapendwa kwaiyo ni artist mkongwe kwenye gemu kama mimi “.

Lakini Christian Bella amekiri kuwa Diamond ni moja kati ya wasanii waliokuza mziki wa bongo fleva tangu aingie kwenye gemu miaka ya 2010 kwani katika kipindi hicho mziki wa dansi ulikuwa umeitoa Bongo fleva kwenye ramani na hivyo Diamond aliurudisha mziki wa Bongo fleva kwenye chati na kuua mziki wa dansi.

Diamond na Zari Wang’ara Kwenye Harusi Ya Rommy Jones na Kay (picha)

Mwishoni mwa wiki hii DJ maarufu Bongo ambaye pia anajulikana kama official DJ wa Diamond Platnumz, Rommy Jones alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi mwanadada anayejulikana kama Kay.

Harusi hiyo ilifanyika siku ya Ijumaa na Reception ya harusi ilifanyika Siku ya jumapili kwenye ukumbi wa Cardinal Rugambwa Oyster bay. Pamoja na maharusi kupendeza kupita kiasi lakini watu walioiba shoo ukumbini hapo ni Diamond ambaye ni kaka wa bwana harusi na mpenzi wake Zari. Diamond alitumbuiza mwanzo mwisho lakini pia wawili hao walikuwa wasimamizi wa harusi lakini naomba niseme tu kuwa macho yote ya wageni waalikwa yalikuwa kwa Diamond na Zari ambao walipendeza kupita kiasi.

Harusi hiyo ilitawaliwa na wageni waalikwa wasanii maarufu na hizi ni baadhi tu ya picha za harusi hiyo;

Rommy na Kay
Diamond na Zari
Rommy na Kay Wakiserebuka
Maharusi pamoja na Wasimamizi wao
Maharusi pamoja na Familia
Diamond na Zari
Esma na Petit Man
Zari na Mpoki
Rayvanny na Fahima
Aunty Ezekiel na Moses Iyobo

 

 

 

 

Vj Penny Afungukia Tuhuma Za Kutoa Mimba Ya Diamond Wakati Wapenzi

Mtangazaji na Vj maarufu bongo Vj Penny amefunguka kuhusiana na tuhuma zinazomkabili za kutoa mimba ya aliyekuwa mpenzi wake Mwanamuziki Diamond Platnumz.

Siku chache zilizopita  Diamond aliachia ngoma zake mbili mpya ‘Sikomi’ na ‘Niache’ ambazo zilizua gumzo kwani kwenye nyimbo hiyo amezungumzia kuhusu wapenzi wake wa zamani ambao ni Wema, Penny, Zari, Hamisa.

Penny na Diamond walikuwa na uhusiano wa kimapenzi miaka minne iliyopita lakini waliishia kuachana baada ya picha za Diamond na Wema kusambaa mtandaoni wakiwa pamoja.

Wakati Diamond na Penny wakiwa kwenye uhusiano habari zilisambaa kuwa Penny alibeba ujauzito wa Diamond lakini baadae ghafla mimba ile haikuonekana tena na baadae Penny mwenyewe alikana taarifa hizo na kudai kuwa hakubeba mimba ya Diamond.

Kupitia wimbo wake wa ‘Sikomi’ Diamond ameongelea penzi lake na mrembo Penny na kudai kuwa Penny alibeba mimba yake taarifa alizozifurahia akamgharamia mahitaji yake yote ikiwemo kumnunulia gari lakini akaitoa mimba yake.

Penny aliulizwa kuhusu tuhuma hizi za kutoa mimba ya Diamond na Dizzim online na akafunguka yafuatayo:

Kwanza naomba nimpongeze kwa nzuri aliyoifanya halafu suala la kutoa mimba yake ni la siku nyingi yaani la muda mrefu ambalo limekuwa likizungumzwa yaani tangu zamani linaongelewa tu lakini Kama yeye mwenyewe aliona ni sawa kulikumbushia basi hakuna ubaya”.

Baada ya kutoa nyimbo hizi ambazo zinafanya vizuri kwa hivi sasa mashabiki wengi walimjia juu Diamond na kudai kuwa wanachoshwa na vitendo vya Diamond kuimba ma-ex zake kwenye kila nyimbo zake.

 

Diamond: Wema ni Mshkaji Wangu Nawajua Mabwana Zake Wote

Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz anaweza akawa ni mmoja kati ya msanii ambaye anaongelewa sana iwe kwa mziki wake au hata maisha yake binafsi lakini watu wengi wanavutiwa na Diamond kutokana na maisha yake binafsi hasa mahusiano yake.

Pamoja na kuwa ni kipindi kirefu kimepita tangu Diamond ameachana na aliyekuwa mpenzi wake muigizaji Wema Sepetu na sasa yupo na Zarinah Hassan lakini cha ajabu ni kuwa bado Diamond anahusishwa sana Wema tofauti na wasanii wa kike wengine waliowahi kuwa na uhusiano na Diamond kama vile Penny, Jokate, Wolper na wengineo.

Ingawa watu wengi wamezidi kueneza habari mbali mbali kuwa Diamond na Wema bado wanaonana hadi kufikia hatua ya kuonekana wote nyumbani kwa Diamond.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Dizzim Online siku za nyuma Diamond amefunguka na kueleza kwa nini bado anahusishwa sana na Wema na uhusiano wao ulivyo kwa sasa;

Wema alikuwa mpenzi wangu tukagombana tukawa maadui wakubwa sana japokuwa tulikuwa tunaficha lakini tulikuwa tuna uadui mkubwa ndani yake yaani ilikuwa mtu alikikaribiana na Wema tu simzimii maisha kama ni WCB nakufukuza kazi nikiona unajihusisha na Wema baadae bifu likaisha sahivi tumekuwa washkaji tunashirikiana katika mambo mbali mbali kama kuna kitu kinahitajika namsaidia na yeye hufanya hivyo hivyo lakini Wema nimoja kati ya wanawake ambao nilipata wakati mgumu sana kuachana naye coz niivyoachana ilikuwa hata kukutana naye sitaki Simu yake akipiga nakata yani ilikuwa ni vita mtindo mmoja”.

Lakini pia Diamond ameendelea kufunguka kuhusiana na uhusiano wake na Wema kwa sasa;

Nashukuru Mwenyezi Mungu ameweka mkono wake na sasa tumekuwa washkaji nimeshakutana naye sehemu tofauti tofauti akiwa na bwana ake na unajua sahivi mabwana zake wote anaokuwa nao nawajua yaani nikikaa sahivi najua Wema analiwa na huyu lakini pia yuko na mwanaume huyu kwa sababu naweza nikaongea naye anaweza akawa na stress za mwanaume wake basi ananiambia anaweza akawa analia basi mi nampa ushauri namwambia Fanya hivi na hivi kwaiyo ni mtu ambaye naheshimiana naye kwaiyo watu wasije wakahisi kuna michezo inayofanyika chini kuwa tunalalana hapana kwa kweli tumekuwa washkaji tu”.

Diamond Amewazuia Wasanii Wake Wa WCB Kutoa Albamu

Mkali wa Bongo fleva, Diamond Platnumz anayetamba na nyimbo yake ya ‘Halelujah’ ambaye pia ni miliki wa label ya Wasafi Classic Baby (WCB) amedaiwa kuwazuiwa wasanii wake kutoa Albamu.

Diamond ambaye yuko mbioni kuachia albamu yake ‘A boy from Tandale’ mda wowote kuanzia sasa amedaiwa kuwakataza wasanii wake kama Queen Darlene, Richi Mavoko, Rayvanny, Harmonize, Lava Lava kutoa albamu wenyewe na badala yake kutakiwa kumpisha Diamond atoe albamu ya kwake kwanza.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni  na kituo cha redio cha Magic Fm kwenye kipindi cha Daladala beats, Rich Mavoko amesema yeye pamoja na wasanii wengine ndani ya WCB walikuwa na mpango wa kutoa Albamu ila Diamond alipotoa taarifa kuwa ana mpango wa kutoa Albamu mwaka huu ilibidi wampishe.

Kusema ukweli mtu ambaye anatuchelewesha foleni yetu ni Chibu tu kwa sababu ni mtu wa kwanza kupata idea ya kuanza kuanza Albamu mwaka huu tulikuwa tunaliheshimu wazo lake sisi tukawa wa pili, kwa hiyo tangu zamani nilikuwa Nina wazo la kutoa kwa mwaka huu baadae tukakubaliana yeye aanze kutoa na mimi nifuate then wenzangu wote waje kutoa baadae kwa sababu watu tuna mingoma kibao ndani inasubiria foleni ya kutoka”.

Rich Mavoko amedai kuwa WCB wote walivutiwa na wazo la kutoa Albamu pale Diamond alipowaeelezea jinsi atakavyo kuja kuuza albamu hiyo ya ‘A boy from Tandale’.

Mange: Diamond Amezoea Kuchukua Kazi za Wasanii Wengine Bila Kuwalipa, Lazima Awalipe Msondo Ngoma

Mwanasiasa na mwanaharakati maarufu mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kudai kuwa msanii Diamond Platnumz amezoea kuiba nyimbo za wasanii mbali mbali hivyo ni lazima awalipe Msondo ngoma fidia ya shilingi milioni 300.

Mange amedai kuwa Diamond amekuwa na kawaida ya kuchukua na kutumia nyimbo za wasanii wengine bila kuwalipa fidia na msanii pekee aliyemlipa kwa kutumia nyimbo yake ni Saida Karoli.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange amefunguka yafuatayo;

Wanamuziki wengi hata Chris Brown wanachukuaga hata vipisi vidogo vya nyimbo za watu au hata kurudia nyimbo nzima lakini huwa wanawalipa wenye nyimbo tatizo la Diataka kuchukua kazi za watu bila bila kuwalipa chochote, Kwanza nashangaa ile nyimbo ya Hallelujah mpaka leo hajashtakiwa tu ile ndio nimbi ambayo amechukua kazi za watu kupita kiasi kutoka kwa wanamuziki wa Tanzania na Marekani. Kwa level aliyofikia Diamond anatakiwa awe anawalipa watu anapotumia kazi zao au kama hataki kulipa awe anapiga akili anatoa vitu original bila kuunganisha na kazi za watu wengine. Ila hii ya kuchukua kazi za watu alafu anajikausha as if katoa kichwani kwake sio haki especially sababu anaowachukulia kazi zao wanahitaji pesa kushinda yeye, awalipe bwana”.

Pia Mange aliendelea kuongelea msanii aliyewahi kulipwa na Diamond baada ya kutumia kazi yake ;

I hope atajifunzia hapa na kuanza kuwalipa watu kama alivyomlipa Saida karoli na wimbo wake wa Salome. Hao Msondo Ngoma hata angewalipa milioni 5 nina uhakika wangekubali ila alitakiwa kuingia nao mkataba kabla ya nyimbo yao ya ‘Zilipendwa’ haijatoka #TukutaneMahakamani”.

 

Diamond: Sijawahi Kulipa Kufanya Kolabo Na Msanii Yoyote Wa Marekani Wenyewe Wananikubali

Mwanamuziki wa Bongo fleva, Diamond Platnumz anayezidi kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘hallelujah’ amezidi kutengeneza headlines baada ya kushirikisha wasanii wakubwa kwenye nyimbo zake.

Diamond ambaye ni juzi tu ametoka kufanya video ya wimbo wake atakao mshirikisha mwanamuziki kutoka Marekani Omarion, pia wiki chache zilizopita ametoka nchini Marekani kwaajili ya kolabo yake na msanii na rapa maarufu kutoka Marekani Rick Ross. Pia mbali na hao wote ni juzi tu Diamond katoka kupokea tuzo yake baada ya mauzo ya nyimbo yake aliomshirikisha mwanamuziki mwingine kutoka Marekani ambaye ni Neyo, kufikisha platnum mara sita.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na dizzim tv Diamond alifunguka na kudai kuwa hajawahi kuwalipa hats senti wasanii hao wote wala hawafati bali wao wanaona kazi zake na wanavutiwa na kumtafuta:

Mimi sijawahi kulipia kufanya kolabo na msanii yoyoye wa Marekani, na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani sio kitu ambacho nimejishobokesha ni watu ambao wanatakiwa kunikubali na kuupenda mziki ninaofanya ili waweze kufanya kazi na mimi ndio maana sometimes unaona kuwa siposti nikiwa nao kwasababu wao wenyewe wanafurahi na wanapenda kuposti na pia naogopa kuposti nisije kuonekana najishaua wakati hiyo sio pointi yangu mimi nachotaka ni kuuchukua mziki wa Bongo fleva kuupeleka mbele”.

Pia Diamond aliongelea album yake mpya inayokuja hivi karibuni inayoitwa ‘A boy from Tandale’ aliowashirikisha wasanii mbali mbali ndani ya Afrika na nje ya Afrika na itahusu mambo mengi kama maisha yake binafsi na nchi ya Tanzania kwa ujumla.