Angalia Alichofanya Diamond na Kuwapita Wasanii Wote Wa Afrika

Mwanamuziki Diamond Platnumz amezidi kudhihirishia watu ustaa wake baada kuzidi kuupeleka muziki wa Bongo fleva mbele zaidi na kupata mafanikio kiasi cha kuvunja rekodi ya Afrika.

Siku ya Ijumaa nchini South Africa Diamond alipewa tuzo na label ya Universal music kwa wimbo wake wa Marry you aliomshirikisha mwanamuziki Neyo kutoka Marekani kuuza vizuri kwa kiwango cha platnum Mara 6 kuwahi kutokea kwa msanii wa Afrika kwa label hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond alifunguka yafuatayo kuhusu tuzo hiyo:

Leo nimekuwa msanii wa kwanza wa kiafrika alosainiwa Universal music group co kufikisha mauzo ya nyimbo yake platinum mara sita mfululizo kupitia nyimbo ya marry you  niliomshirikisha Neyo, kwa  niaba ya timu yangu na Neyo tungependa kuwashukuru mashabiki na media zote ulimwenguni”.

Mwishoni mwa wiki hii pia Diamond alionekana akifanya video ya wimbo na mwanamuziki mwingine kutoka Marekani Omarion, ambapo baadae Diamond alithibitisha kuwa amemshirikisha kwenye nyimbo yake mpya.

          Diamond na Omarion              

Kwenye mahojiano aliyoyafanya Mara baada ya kutua Tanzania siku ya Jana, Diamond alifunguka nyimbo hizo alizofanya na wanamuziki kama Rick Ross na Omarion zote zitapatikana keen he album yake mpya itakayoitwa A boy from Tandale ambayo hajataja tarehe rasmi ya kutoka.

 

 

Diamond Kaingizwa Matatani na Wimbo Wake Mwenyewe (video)

Mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Halelujah’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya vingozi wa dini kumjia juu kutokana na nyimbo yake hiyo ya ‘Halelujah’.

Suala la dini ni moja kati ya vitu nyeti sana kwa binadamu hasa kwasababu linahusisha suala zima la imani, Mwanamuziki Diamond anajulikana kuwa ni muumini wa dini ya kiislamu, mara baada ya kutoa wimbo ambao una jina lake linasindikizwa na imani ya kikikristo (haleluya) liliibua hisia za waislamu wenzake.

Mwanzoni mwa wiki hii kumekuwa na video imbayo imesambaa ambayo inamuonesha Shekhe yupo msikitini akielezea kuwa hajafurahishwa na kitendo cha Diamond kuimba haleluya huku akijua ni kinyume na maadili ya dini yao lakini pia alifunguka kuwa hajafurahishwa na kitendo cha kumuona Diamond akiwa amevaa msalaba katika video ya wimbo huo na wakati ni kinyume na maadili ya dini ya kiislamu.

Tazama Video hizi Ustadhi akifunguka;

Diamond Aelezea Kiundani Kuhusu Kolabo Yake na Rick Ross

Mwanamuziki anayezidi kufanya vizuri na kung’aa zaidi kwenye mziki wa bongo fleva, Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amefunguka zaidi kuhusiana na kolabo yake na Rick Ross.

Hivi karibuni Diamond alionekana kwenye video mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii akifanya video na rapa maarufu kutoka Marekani Rick Ross. Diamond aliyesafiri kwenda Marekani wiki mbili zilizopita alionekana akirekodi video na Rick Ross lakini hakutoa maelezo yoyote.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Dizzim Online Diamond alifunguka yafuatayo;

Joseph Kusaga ndiye aliyenitafuta na kuniambia kuwa Rick Ross anataka kufanya kolabo na mimi lakini kwa kipindi kile nilikuwa kwenye process ya kutengeneza ngoma yangu hii mpya ya Hallelujah ambapo nilikuwa nimeshatengeneza verse moja na chorus basi nikaelekea nchini Rwanda kwaajili ya Fiesta, pamoja na kwamba ngoma yangu ya hallelujah nashukuru ilipokelewa vizuri niwashukuru mashabiki zangu lakini bado nilikuwa na njaa zaidi so nikapanda ndege mpaka Marekani ambapo nilikutana na Rick Ross na nimemshirikisha kwenue nyimbo yangu mpya itakayotoka hivi karibuni lakini sitaki kusema vitu vingi sana kwa sasa nataka iwe surprise kwa mashabiki zangu lakini wategemee mambo mazuri”.

Diamond pia ameongelea shoo zake anazotegemea kufanya mwaka huu kwenye  nchi mbalimbali kama Dubai, Marekani.

Aslay Anatarajia Kumpa Kolabo Diamond

Mwanamuziki anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘natamba’ Aslay amesema anatarajia kumpa kolabo msanii mkubwa wa bongo fleva, Diamond Platnumz.

Aslay anayesifika kwa kutoa nyimbo mara kwa mara na sio bora tu nyimbo bali nyimbo zinazopendwa na mashabiki zake amesema kuwa anategemea kuachia nyimbo yake mpya hivi karibuni.

Mtayarishaji wa muziki hapa nchini, Shirko ambaye pia ndiye aliyeandaa nyimbo mbili za Aslay ambazo ni ‘natamba’ pamoja na ‘natamba’ amesema kuna uwezekano Mkubwa ambao wanatazamia kufanya ‘remix’ ya ngoma hiyo ambayo tayari inafanya vizuri ya ‘natamba’ na msanii pekee wanayemwangalia ili ashirikiane na Aslay kwenye wimbo huo si mwingine bali ni Diamond.

Diamond ambaye tayari na yeye anahit na wimbo wake wa ‘halelujah’ uliovunja rekodi na Kuwait msanii wa kwanza Tanzania kufikisha waangaliaji milioni moja kwenye mtandao wa Youtube ndani ya masaa kumi na tano. Pia na Diamond alishawahi kusema Kuwait angependezwa zaidi kama angepata nafasi ya kufanya kazi na Aslay kwaiyo bila Shaka utakuwa wakati mzuri kabisa kuwapa mashabiki zao kile kitu wanataka.

Aslay amezidi kufanya vizuri zaidi kwenye mtandao wa youtube kwani kwenye wiki ya kwanza video ya wimbo huo kutoka alimtoa Diamond kutoka kwenye namba moja na kuishikilia kwa wiki kadhaa mpaka alipokuja kutolewa juzi na msanii kutoka wasafi Harmonize na wimbo wake wa ‘shululu’.

 

Izzo Bizness- Kolabo Ya Diamond na Rick Ross Itainua Muziki Wetu

Mwanamuziki na rapa kutoka Mbeya City Izzo Bizness amefunguka na kuongelea kolabo iliyofanyika baina ya msanii wa bongo fleva Diamond Platnumz na rapa kutoka Marekani Rick Ross kuwa itasaidia kuinua muziki wetu wa Tanzania.

Izzo Bizness aliongea hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha East Africa;

Kwanza Big up kwa Diamond na timu nzima ya Wasafi classic kwani matokeo ya kolabo iliyofanyika Kati ya Diamond na Rick Ross yatakuwa makubwa na pia uongozi mzima wa Diamond wanajitahidi kupush katika kutangaza mziki wa bongo fleva na ukiangalia Rick Ross ni msanii mkubwa sana na hiyo ni bahati kubwa sana si kwa mziki wa hip hop tu hadi bongo fleva na sanaa yote ya kuimba kwa ujumla Rick Ross ni msanii mkubwa duniani amafanya kazi na wasanii wakubwa sana duniani kwaiyo hii kolabo italeta attention kwa wale wanamziki wa nje kuangalia huyu msanii anatokea wapi na kuanza kujaribu kuangalia sasa soko la Tanzania linakuje wasanii na kadhalika, kwaiyo mi nahisi hii itasaidia sana na kwa kiasi chake kusaidia katika kuinua muziki wetu wa Bongo fleva”.

Ikiwa taarifa zaidi kuhusu kolabo hiyo haijawekwa wazi bado kama jina la wimbo, msanii gani kamshirikisha msanii gani na kadhalika lakini ni hatua kubwa kwa msanii wa Bongo fleva kama Diamond kuweza kushiriki sanaa yake na mwanamuziki mkubwa duniani kama Rick Ross kwani hatua hii ni kubwa na itafungua milango mingi kwa wasanii wengi.

Diamond Sio Mpenzi Wangu- Husna Maulid

Miss Sinza mwaka 2011, Husna Maulidi amefunguka na kudai kuwa hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Diamond.

Wiki iliyopita picha zilienea zikimuonyesha Husna, ambaye pia ana urafiki na Hamisa Mobetto akiwa amekaa karibu sana na Diamond (zero distance) club. Pia kulikuwa na taarifa kuwa Husna alilala nyumbani kwa Diamond, Madale.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Millard Ayo Husna amekana taarifa hizo na kudai hawezi kuwa na uhusiano na Diamond kwani tayari ana mpenzi wake.

“Ni kweli nimeziona hizo skendo eti kuwa mimi natembea na Diamond na hiyo yote imekuja baada ya mimi kuenda kwenye birthday ya Naseeb, mimi Naseeb siwezi kutembea naye kabisa yaani mi namchukulia kama msanii yoyote yule napenda kusapoti kazi zake. Kingine watu walichozusha ni kwasababu Mimi nilijiita Mama Dee, kujiita mama Dee au Mrs Dee haimaanishi kama ni Naseeb, hapana wakina Dee wako wengi”.

Husna aliendelea kuelezea ni kwa jinsi gani skendo hizi zinavyoathiri mahusiano yake:

“Kusema ukweli mimi nina boyfriend wangu ila tu watanzania wanapenda kuzusha lakini hii pia inasababishwa na Hamisa kwasababu Hamisa ameshawahi kutembea na my ex boyfriend Mwami, na baada ya yeye kuona mimi nimeenda kwenye birthday ya Diamond akaanza kutuma watu waje kunitukana na pia watu walizidi kizusha baada ya kuniona nimemposti Diamond kumtakia birthday njema”.

Husna amewasihi watu wasisikilize habari ambazo hawana uhakika nazo kwani habari hizo za kizushi zimemsababishia matatizo sio tu kwa mpenzi wake bali hata kwa familia yake.

Diamond Platnumz Atangaza Kutoa Album Mpya

Mwanamuziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ametangaza rasmi kuachia albamu mpya itakayoenda kwa jina la ‘ A boy from Tandale’.

Diamond ametangaza habari hiyo njema kwa mashabiki zake jioni hii kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo aliweka cover ya album yake (Album cover) akaambatanisha na maneno machache yaliyosomeka:

 

“Album Soon Come… #AboyfromTandale”

Diamond yupo nchini Marekani tangu wikiend iliyopita ambapo alihudhuria Tuzo za Afrimma na aliweka wazi pia Ana shoo nchini humo. Siku ya leo video mbalimbali zilisambaa zikimuonyesha Diamond na Rayvanny wakiwa name rapper maarufu Marekani Rick Ross wakirekodi video kwa Pamoja kwa ajili ya wimbo wao mpya.

Diamond na Rayvanny wakiwa pamoja na Rick Ross.

Mapema mwezi uliopita Diamond alitangazwa kujiunga kwenye listi ya mastaa kama Rick Ross na Dj Khaled katika kuwa mabalozi wa kutangaza kinywaji cha ‘Belaire’. Mbali na hayo Diamond ameendelea kusisitiza kuwa yupo katika harakati za kuipeleka Bongo fleva mbele zaidi

Diamond Afunguka Kuhusu Skendo Zinazomkabili

Mwanamuziki Diamond Platnumz anayetamba na wimbo wake wa Halelujah amefunguka kuhusu skendo zinazomkabili mtandaoni. Mbali na wimbo wake kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni Diamond amekuwa katika vichwa vya habari kwa ajili ya maisha yake binafsi.

Baada ya tetesi kuenea kuwa Diamond ameachana na Zari tangu juzi wasichana mbalimbali wamekuwa wakidhaniwa kutembea na Diamond.

Kwa kupitia ukurasa wake Instagram Diamond amefunguka kuhusiana na tuhuma hizo;

“Mara Diamond kamla huyu mara nasikia anatembea na yule, mara inasemekana juzi alikuwa na yule, yaani kila ukiamka limezuka jipya utadhani yangu ina sukari au nakojoa dhahabu… Hebu niacheni kidogo  Niko busy nahangaika kupeleka bongo fleva yetu duniani..Sijamkaza yoyote na wala sina mahusiano na yoyote anayetajwa na siku nikimaliza mahusiano na aliye South Africa na  nikawa na mwingine na ikafikia kuliweka wazi ntaliweka wazi mwenyewe….Maana hakuna kitakachonizuia….Ndo kwanza Nina miaka 28, sijaoa na hata nikioa naruhusiwa kuwa na wake wanne Period!”.

Baada ya kuweka maneno hayo katika ukurasa wake Zari Alimjia juu na kumuomba asimuingize katika mambo yao kwani hayupo nae tena.

 

Mwanamuziki Quick Rocka Ampigia Saluti Diamond Platnumz

Mwanamuziki wa Bongo fleva Quick Rocka ameibuka na kumpigia saluti Diamond na kudai kuwa rekodi yake aliyoiweka ni nguma kuivunja.

Diamond alivunja rekodi hiyo baada ya wimbo wake wa Hallelujah aliyomshirikisha Morgan Heritage kufikisha jumla ya views milioni moja ndani ya masaa kumi na tano na kufikisha milioni mbili ndani ya siku moja.

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanamuziki Quick Racka alituma video akimpa hongera Mwanamuziki mwenzake Diamond Platnumz na kumpongeza pia kwa video kali aliyofanya na pia kumsifia mwanamuziki Morgan Heritage aliyemshirikisha.

“Hatari mzee big shout out to Diamond Hallelujah is a dope song meen Morgan Heritage ameua we mwenyewe umeua you know what am saying so i appreciate good work brother and the video its a movie so big shout out to you one million views in fifteen hours man thats a record man ujue labda atokee mwingine avunje rekodi in twelve hours lakini rekodi hiyo ngumu sana kuvunjwa salute brother dope tune”.

Diamond alivunja rekodi iliyowekwa na Ali Kiba kupitia wimbo wake wa seduce me wiki chache zilizopita na pia  na pia Quick Rocka alimpongeza Ali Kiba kwa mafanikio yake.

Wewe umeupokeaje wimbo huo mpya wa Diamond  Je unahisi atatokea mwanamuziki wa kuvunja rekodi ya Diamond?

Tafadhali toa maoni yako.

 

Mange Kimambi: Diamond Kaweka Rekodi Feki

Mange Kimambi ameibuka upya na kudai kuwa rekodi ambayo Diamond Platnumz ameweka ni feki Hili limekuja baada ya Diamond kuachia wimbo wake mpya siku mbili zilizopita uitwao Hallelujah aliomshirikisha  mwanamuziki Morgan Heritage, wimbo huo ulifanikiwa kufikisha jumla ya views million mbili kwenye mtandao wa Youtube ndani ya siku moja.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alifunguka yafuatayo juu ya suala hilo;

“#IssaFakeRecord Amenunua viewers huo ndo ukweli!!! Samahani kwa ntakaowakwaza…. Baba Dully ajifunze kukubali na kushindwa sometimes, hakuwa na haja ya kununua viewers ili tu avunje rekodi ya Ali Kiba”.

Mange aliendelea kusimamia msimamo wake juu ya suala hilo japokuwa alipokea ushindani mkubwa shidi ya mashabiki wa Diamond ambao walimlaani vikali;

“Mtanitukana sana Team Diamond ila wote mnajua kuwa sisemagi uwongo na maneno yangu kwa njia moja au nyingine huwa lazima mwisho wa siku yawe ya kweli! Naamini soon mtakuja kujua kuwa Mange aliwaambia ukweli kuwa Diamond alinunua viewers! Leo mtanichamba ila siku moja ukweli utajulikana. Haiwezekani nyimbo imetrend namba moja Tanzania peke yake ikapata waangaliaji milioni moja ndani ya masaa kum na tano wakati Seduce me iliyotrens Afrika Mashariki nzima ilipata waangaliaji milioni moj ndani ya masaa thelathini na nane, it doesnt make sense ata all #fact”.

Diamond alivunja rekodi hiyo iliyowekwa na hasimu wake Ali Kiba ambaye kwa kupitia wimbo wake wa seduce me alifikisha waangaliaji milioni 1 ndani ya masaa 38 na Diamond juzi alifikisha waangaliaji wa Video yake hiyo milioni 2 ndani ya siku moja.

 

Faiza Ally: Alikiba Anafanya Muziki Mzuri Kuliko Diamond

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Faiza Ally ameibuka tena na kudai kuwa anauelewa zaidi muziki anaofanya Ali Kiba kuliko muziki anaofanya Diamond Platnumz.

Katika mahojiano aliyoyafanya na TBC Faiza alidai kuwa wasanii wote wawili wanajitahidi katika kufanya muziki kwani wana vipaji tofauti kwani mmoja ni muimbaji na mwingine ni mburudishaji.

Faiza aliendelea kusema:

“Kwanza kati ya muziki wa Diamond na Ali Kiba , naupenda zaidi muziki wa Ali Kiba, muziki wake ni mzuri kuliko Diamond, kwani Diamond ni ile full entertainment ukimwangalia tu unatabasamu lakini Ali Kiba ana muziki mzuri. Nikizungumzia mtu aliyeutoa mziki akaupa heshima mpaka akampa changamoto Kiba na yeye akasimama mpaka tukaanza kumuona kwenye hali ya tofauti ni Diamond”.

Faiza ni moja ya watu ambao msimamo wake umekuwa ukibadilika kuhusu nani ni bora kati ya Diamond na Ali Kiba kwani mara kwa mara amekuwa akibadilika kwani leo anaweza akasema Diamond na kesho atasema kuwa ni Ali Kiba.

Lakini yote kwa yote ushindani huu ndo unafanya muziki wetu kuwa bora zaidi kwani Ali Kiba asingekuwa na changamoto kutoka kwa Diamond asinge kuwa bora alivyo sasa na hivyo hivyo kwa Diamond asingepata changamoto kutoka kwa Ali Kiba basi asingejitahidi kutupa muziki mzuri zaidi tunaopata leo hii.

Diamond Adaiwa Kuonekana Akiwa na Video Queen Irene

Mwanamuziki Diamond Platnumz ameingia tena kwenye vichwa vya habari leo baada ya stori za chini ya kapeti kudai kuwa ameonekana na model na video vixen mrembo Irene. Ikiwa ni wiki kadhaa tangu Diamond akiri kuzaa na Hamisa Mobetto na hatimaye kusamehewa na mzazi mwenzie Zari Diamond yupo tena kwenye maji ya moto.

Habari zinazoenea kwa kasi ya ajabu zinadai kuwa Diamond aliyekuwa nchini Afrika ya Kusini tangu wiki iliyopita kwaajili ya sherehe ya kuzaliwa ya mpenzi wake Zari, alionekana tena sehemu nyingine na Mrembo Irene ambaye na yeye alikuwa nchini humo kwa ajili ya kazi na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Pamoja na kuwa Diamond alikataa kuwa na uhusiano na mrembo toka Namibia Dillish, lakini stori za udaku zinadai kuwa walikuwa wote na pia dada huyo ni mjamzito ingawa yeye mwenyewe hajathibitisha kuwa mjamzito.

Diamond na Irene wamewahi kuongelewa kama wako pamoja kipindi cha nyuma yaani kulikuwa na tetesi kuwa diamond alikuwa anachepuka na binti huyo mrembo na hata ilisemekana kuwa binti huyo alishika ujauzito wa Diamond ingawa alipohojiwa alikataa na kusema yeye anampenda Zari na yuko na Zari hivyo habari hizo ni za uongo na zinaenezwa na wabaya wake.

Baba Diamond Amshauri Zari Amvumilie Diamond Kwa Mapungufu yake

Baba mzazi wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Mzee Abdul ameibuka na kumshauri Zari aendelee tu kumvumilia Diamond kwa makosa aliyoyafanya.

Katika mahojiano aliyoyafanya na Mllard Ayo Baba Diamond alipoulizwa akikutana na Zari atamshauri nini kuhusu mtoto wake ndipo aliposema kuwa atamshauri awe mvumilivu.

Baba Diamond amesema;

“Kwanza awe mvumilivu kwani mtoto wa kiume anakua mtu wa kudanganywa, mpotofu na ilimradi kashaambiwa kuna mke mwenzie basi awe mvumilivu ila kikubwa tu kuwe na heshima na adabu Zari kama Zari na Hamisa kama Hamisa waheshimiane wawe pamoja waangalie maisha tu yanaenda kama kawaida”.

Pia Mzee Abdul aliendelea kusema:

“Zari mi namwambia asipende kuwasikiliza waswahili ilimradi aangalie yake yanamwendea vizuri na Hamisa naye asipende kusikiliza ya Waswahili akae aangalie yake aendelee vizuri maana sisi waswahili kila neno linakuwa baya kwetu hamna neno zuri na mara nyingi tunakuwa hatupendani kupendeana mema mtu anapenda mwengine haaribikiwe asemwe tu, ila wakae pamoja tu waangalie haya maisha leo tupo kesho hatupo”.

Baba Diamond pia alimuomba Zari kama kuna uwezekano basi apewe nafasi awaone wajukuu zake akimaanisha Latiffah na Nilllan ambao amekiri hajawahi kuwaona kutokana na kutokuwa na  uhusiano mbovu na mtoto wake Diamond.

Baba Diamond aliongeza;

“Mi napenda kumwambia Zari nikiwa mimi kama mimi Baba Diamond aniletee wajukuu zangu kwanza niwaone au sio lazima nianiletee anaweza hata akaniambia sehemu gani naweza niweze kuenda kuwaona wajukuu zangu”.

Hawa ndo Warembo Saba Waliowahi Kuwa na Uhusiano na Diamond (picha ndani)

Diamond Platnumz ni msanii anayefanya vizuri sio tu Tanzania bali hata nchi za Afrika na Kimataifa zaidi. Watu wanavutiwa na uimbaji wake na hasa staili yake ya kipekee ya kucheza. Lakini zaidi ya hayo mashabiki wengi wa Diamond wanapenda zaidi kujua kuhusu maisha yake binafsi yaani kuhusu mahusiano yake.

Diamond ni moja kati ya supastaa Bongo anayejulikana kutokana na kuwa na mahusiano na wasichana warembo sana ambao wanaweza kuwa wanamuziki au waigizaji wa Bongo movie. Leo tutaangalia baadhi ya warembo hao aliowahi kuwa nao kimapenzi na kuweka wazi au kukubali kuwa nao.

  1. Zari The Bosslady
Zari ndo mpenzi wa sasa wa Diamond ambaye wako wote tangu mwaka 2014 na wamezaa watoto wawili pamoja.

2. Wema Sepetu

Wema ni moja kati ya mpenzi wa zamani wa Diamond aliyekiri kumpenda sana na kuwa naye kwenye mahusiano kwa muda mrefu kutoka mwaka 2010 mpaka mwaka 2014.

3. Penny ‘vj penny’

Penny alitoka na Diamond baada ya kuachana na Wema ambaye alikuwa rafiki yake, lakini waliachana baada ya picha kuvuja za wema na Diamond kurudiana.

4. Jaqueline Wolper

Diamond alikiri kutoka na Wolper baada ya kutoa wimbo wa Je utanipenda ambapo almuita mpenzi wake wa zamani.

5. Jokate

Jokate na Diamond walikuwa pamoja kwa kipindi kifupi lakini Diamond aliweka wazi kuwa alimpenda sana Jokate mahusiano yao yaliisha baada ya Diamond kuwa na uhusiano mwingine.

6. Naj

Diamond na Naj walikuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini hawakudumu pia kwa sasa Naj anatoka na Barakah the Prince.

7. Hamisa Mobetto

Diamond alikiri kuwa na uhusiano na Hamisa kwa miaka tisa akiimanisha kila mpenzi aliyekuwa naye alimsaliti na Hamisa mpaka sasa wana mtoto mmoja lakini hawana uhusiano tena.

Hiyo ndo listi nzima ya Ma-ex  wa Diamond je yupi unahisi alipendeza na Diamond? Tafadhali weka maoni yako.

Dkt. Mwakyembe- Sioni Sababu ya Kuwasuluhisha Diamond na Alikiba

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo mheshimiwa Harison Mwakyembe amefunguka kuhusu ugomvi unaoendelea kati ya wasanii wawili wakubwa Tanzania Ali kiba na Diamond Platnumz ambapo amesema kuwa hatarajii kuwapatanisha tena kama alivyohaidi mwanzoni.

Wadau mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva walimuomba waziri Mwakyembe aingilie kati beef hilo la wasanii hao wawili ambao kwa muda mrefu wamekuwa hawapatani huku sababu kamili ya ugomvi huo ikiwa haijajulikana huku watu wengi wakihisi bifu hilo limetokana na ushindani wa kimuziki baina yao. Bifu lao lilionekana dhahiri pale ambapo Ali kiba alitoa wimbo wa ‘Saduce me’ na kupokelewa vizuri na mashabiki wake ndipo Diamond naye alipoamua kutoa nyimbo yake mpya ya Zilipendwa masaa machache baadae ambazo ziliingia kwenye ushindani mkali kwenye mtandao wa youtube.

Mh. Mwakyembe amesema;

“Kama kuna ushindani kati ya Ali Kiba na Diamond ambao ni kiweledi, kitaaluma basi mimi nafikiri tungeuendeleza zaidi, hamna sababu ya kuwasuluhisha waendelee kushindana vizuri ili tupate miziki mizito.kwa hiyo mimi nawaomba watanzania wachukulie mvutano huo ni mzuri katika tasnia, mradi mimi sijasikia watu wameshikiana mapanga”.

Pia Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa ahadi yake aliyoitoa mwanzoni ya kutaka kuwaita Diamond na Alikiba ili kufanya wimbo kwa pamoja iko pale pale kwani anaamini wote ni vijana wenye vipaji na watafanya kazi nzuri kwa pamoja ila tu kwa sasa wakati haujafika.

Mashabiki wengi wa Diamond wamekuwa wakimtuhumu Alikiba kwa kung’aa kupitia Diamond yaani kuwa asingekuwa na bifu na Diamond Alikiba asingesikika yaani anafaidika zaidi na bifu hilo.

Je wewe unaonaje je ni kweli tuhuma hizo za Alikiba kung’aa kupitia Diamond? Na je wasanii hawa wanahitaji kuendelea kuwa na bifu au wapatane tu? Tafadhali toa maoni yako hapo chini.

Zari Amsamehe Diamond,Wamerudiana (picha ndani)

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu sakata la Diamond na Zari lichukue nafasi, baada Diamond kuwa na mahusiano ya siri na Hamisa kufikia hatua ya kumzalisha mtoto na kumkubali mtoto na Zari kutumia mitandao ya kijamii kudai kuwa hajamsamehe hatimaye Zari amemsamehe mpenzi wake.

Tarehe 23 jumamosi ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Zari  ambapo Diamond kwa kupitia ukurasa wake wa instagram aliweka ujumbe huu:

“Uzuri na urembo pengine ningetembea baadhi wanao pia. Lakini akili hekima pamoja na roho yako ya kwenye shida na raha kwangu ndio kitu pekee kinachonifanay nikupende na kukuthamini zaidi kadri siku zinavyozidi kuenda…wanaposema kwenye kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara hawamaanishsi anapika na kuosha vyombo hapaana ni mwanamke mwenyekuwa bega kwa bega na mpenziwe kwenye shida na raha…Happy birthday General”.

Siku hiyo kimya kimya Diamond alisafiri mpaka Afrika ya kusini ambako Zari yupo na kuweka picha mtandaoni akicheza na watoto wao Latifah na Nillan. Baada ya muda waliweka video na picha mbalimbali wakiwaonyesha wapendanao hao wakikumbatiana na kuweka wazi kuwa wamerudiana.

Hizi ni baadhi ya picha kutoka kwa Diamond na Zari:

1. Diamond na Zari wakienda kwenye sherehe ya Zari (Birthday dinner)
2. Diamond akiwa amelala na binti yake Latifah
3. Diamond akiwa anacheza na mtoto wake Nillan (Daddy son moments)

Pamoja na hayo yote yaliyotokea Zari amekiri kuwa ameamua kumsamehe Diamond ili waendelee kulea familia yao ikiwemo watoto wa Ivan, kwani Diamond ameshakuwa baba kwao na pia Diamond alikiri kutorudia kosa tena.