“Usikubali Kuwa Mtumwa Wa Mapenzi”- Uwoya

Msanii wa Bongo movie Mrembo Irene Uwoya amefunguka kwa kutoa ujumbe mzito wa Kimapenzi na kuwasaidia watu wasikubali kugeuzwa watumwa wa mapenzi.

Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja wamekuwa wakitrend sana Kwenye mitandao ya kijamii na tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao na siku ya jana Uwoya kufichua kwamba mume wake huyo amewahi kuchepuka Kwenye ndoa yao.

Siku ya jana Uwoya ameibua maswali mengi mara baada ya kuweka ujumbe Kwenye ukurasa wake wa Instagram ulioibua maswali na kuonekana kama ni dongo kwa ndoa yake mwenyewe.

 

 

Irene Uwoya Amtuhumu Dogo Janja Kwa Kuchepuka Kwenye Ndoa Yao

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali anaye trend kwa kiasi kikubwa hivi sasa Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja amewahi kuchepuka.

Aiku za hivi karibuni Irene Uwoya na Dogo Janja wamekuwa Kwenye headlines za Media mbali mbali huku tetesi zinazopamba moto ni kwamba ndoa yao inapumulia mashine.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha The Playlist cha Times Fm, Uwoya amefunguka baada ya kuulizwa maswali kadhaa kuhusiana na ndoa yake:

 

Swali la kwanza – Ni kweli mmeachana na Dogo Janja ?….. Irene alikataa kulijibu na kusema uliza swali lingine,

Swali la pili – Ni kweli hamkai pamoja na Dogo Janja ?…….Irene alikataa pia kulijibu na kusema uliza lingine

Swali la tatu – Ni kweli Umemu-Uniffolow Dogo Janja Instagram …? Irene alijibu “Hapana”

Swali la tatu – Ni kweli mnategemea mtoto na Dogo Janja….. Irene alikataa kulijibu na kusema Swali lingine

Swali la nne – Ni kweli Dogo Janja alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yenu ?….Irene alijibu “Ndio”

Swali la tano – Ni kweli Irene Uwoya alishawahi kuchepuka kwenye ndoa yake ?…… Irene alijibu “Hapana”

Lakini mahojiano hayo Uwoya alifungukia skendo ya kupelekwa Nchi za nje Kula bata na mwanamume mwingine na kisha kumuacha Mumewe nchini.

Yeye kuonekana yuko nje ya nchi akionekana anakula bata bila Dogo Janja,Kila mtu anazungumza kile anachohisi kuzungumza na mimi siwezagi kuongelea mambo yangu kwenye media, Mimi kuonekana nje niko kwenye biashara zangu mbona Dogo Janja akiendaga kufanya video za nyimbo zake mfano Afrika ya Kusini hanibebagi ? kwahiyo mimi naendaga kibiashara kama yeye anavyoendaga kikazi”.

 

 

Uwoya Amwaga Povu Juu Ya Mahusiano Yake na Dogo Janja

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amejikuta akimwaga povu zito baada ya kuhojiwa kuhusu Mahusiano Yake na mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Siku za hivi karibuni Kumekuwa na tetesi nyingi zinazoizunguka ndoa ya Uwoya na Dogo Janja ikiwemo kuwa wawili hao wameachana baada ya Wolper kupata mwanaume mwingine mwenye pesa zaidi anayemuweka Mjini kwa sasa.

Kwenye mahojiano aliyofanya Global Publishers hivi karibuni Uwoya alihojiwa juu ya taarifa za kumtesa Kimapenzi Dogo mpaka kuishia kulazwa hospitalini halafu inadaiwa hakuenda kabisa kumuona badala yake alidaiwa kuonekana batani.

Wolper alimwaga povu zito baada ya swali hilo:

Wanasema anaumwa kwa ajili yangu? Basi hayo makubwa! Sijawahi kusikia kuna ugonjwa wa mapenzi. Kwa hiyo ina maana mimi huwa ninawatesa watu? Mimi huwa siteswi? Maana kila mtu Uwoya… Uwoya…ina maana kila ishu ya mapenzi mimi ndiye huwa natesa watu? Kwa hiyo mimi ni tesatesa au chinjachinja wa mapenzi? Ni kweli mimi ni mkali, lakini huyo mwanaume atakuwa na ugonjwa mwingine siyo mimi”.

Lakini pia Uwoya alipoulizwa endapo tetesi za kuachana Dogo Janja mpaka kuishi nyumba tofauti ni za kweli alijibu:

No Coment! Kwani wakati tunaanza tuliwatangazia? Hilo waambie sina majibu, nimesema no coment!”.

 

 

Irene Uwoya Adai Bata Zake Zinasimamiwa na Management Yake

Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Irene Pancras Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa uongozi wake mpya ndio unahakikisha anaishi maisha mazuri.

Global Publishers wanaripoti kuwa Uwoya amekuwa akila bata kwenye viwanja vya gharama kubwa ikiwemo mahoteli makubwa huko Dubai, Zanzibar na mikoani hivyo kuibua maswali kwa mashabiki wake kuwa ni mapato ya filamu tu au?

Mbali na matanuzi na shopping za nguvu, Uwoya amekuwa akibadili magari makali huku akiendelea na ujenzi wa klabu yake ya gharama kubwa ya Last Minute iliyopo Sinza- Mori jijini Dar.

Kwenye mahojiano man gazeti la Ijumaa Uwoya aliulizwa kuhusu matanuzi hayo na endapo kuna mtu mwingine zaidi ya Mumewe Dogo Janja anasimamia ambapo  alifunguka:

Hakuna mtu, unajua sipendi kuweka mambo yangu hadharani. Haya ndiyo maisha yangu, ni kawaida.

Kuhusu nguo mpya kila siku Ni mimi tu nimeamua kupendeza. Kama ni kubadili nguo mimi nguo ninazo nyingi sana, sema zamani nilikuwa navaa, lakini sipigi picha. Nadhani hii ishu ya kuvaa na kuposti mtandaoni ndiyo inafanya watu waone ni nguo mpya”.

Lakini pia Uwoya alitoa siri ya kuwa na Management kwa sasa ambayo inahakikisha anajijengea image ambayo anayo kwa sasa kama Msanii:

Kuna siri watu wengi hawaijui. Kwa sasa mambo yote yanasimamiwa na menejimenti yangu. Menejimenti ndiyo inanifanyia kila kitu ambacho watu wanaona ni jeuri ya fedha”.

Kutokana na maisha anayoishi hivi sasa Uwoya kuna tetesi zilikuwa zinadai kuna Kigogo mmoja mwenye pesa ndefu ndio anasimamia lifestyle ya Uwoya kutokana na ukweli Mumewe Dogo Janja hawezi kumfanyia mambo makubwa.

Dogo Janja Asipoachana na Irene Uwoya Ataishia Kufa- Mo Music

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Mo Music ameibuka na kumpa ushauri Dogo Janja na kumtaka kuachana na Mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Sio Siri ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja imetengenwza sana headlines siku za hivi Karibuni ambapo imekuwa ikisemekana Dogo Janja kapokonywa Mke na vigogo wenye pesa zao wanaoweza kumlea mtoto mzuri kama Irene.

Tetesi hizi zimepelekea Dogo Janja kuonekana kama mtu mwenye msongo wa mawazo kiasi ya kwamba kuonekana kwa Mwanasaiokolojia siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Mo Music ameibuka na kumshauri msanii mwenzake kuachana na Uwoya kwani asipofabya hivyo anamtabiria kukutana na Kifo mbeleni.

Unajua vitu vingine watu wanajitakia wenyewe ningekuwa mimi ndio Dogo Janja nisingejiingiza kule kwa sababu ingawa wanaweza mapenzi sio umri lakini Hizi nyingine zinakuja kama laana angeatakiwa kuwa na mtu wa umri wake lakini sahivi ni kama vile pressure inamuendesha kuwa na mtu kama yule.

Nimesikia tetesi kama hawaishi wote nyumba moja sasa ndio ndoa gani hiyo lakini mimi kama kaka yake namshauri ajitulize na atulize akili ajue jinsi ya kucheza na familia yake lakini akiendelea huvyo hivyo ataendelea kuugua kupata presha mwisho wa siku Kifo kabisa”.

 

“Sithubutu Kabisa Kugusa Simu Ya Mke Wangu”-Dogo Janja

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi maisha anayoishi na Mke wake movie star Irene Uwoya.

Dogo Janja amefunguka na kuongelea ndoa yake na kuweka wazi kuwa ingawa hakuna mipaka katika ndoa yao lakini hakuna mtu kati yao ambaye anashika simu ya mpenzi wake.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na Gazeti la Dimba, Dogo Janja ameweka wazi kuwa amekuwa akishirikiana kila kitu na mkewe huyo, lakini mambo ya kwenye simu hataki kuyasikia.

Yule ni mke wangu na ninaheshimu hilo…tunashirikiana vingi kwa kuwa ni zaidi ya wapenzi, lakini sitaki wala sijawahi kukagua simu yake na hata yeye ni hivyo hivyo”.

Dogo Janja amesisitiza kuwa yeye na Mke wake wamekuwa wakiheshimiana na kila mmoja amekuwa na uhuru na mwenzake, jambo ambalo anaamini litadumisha ndoa yao.

Dogo Janja na Uwoya Wabambwa Chumbani Baada Ya Tetesi Za Kuachana (video)

Staa wa Muziki wa Bongo fleva Dogo Janja na Mke wake Movie Star Irene Uwoya wamebambwa na kamera za Clouds Fm wakiwa wamekaa chumbani wakifanya yao.

Baada ya Tetesi kusambaa sana Kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanandoa hao wamepeana kibuti hatimaye wameonekana hadharani kwa mara ya kwanza Kupitia Clouds Tv.

Katika moja ya matangazo ya Fiesta Inayorushwa na Clouds Media , kamera ziliwanasa wawili hao pamoja wakiwa pamoja Kwenye moja ya vyumba hotelini.

Baada ya mtangazaji huyo kuingia, Dogo Janja amedai hakuwa na taarifa kama kuna mtu yoyote anakuja hivyo ameshtukizwa huku akidai yeye na mke wake huyo walikuwa wanafanya mazungumzo.

https://www.instagram.com/p/Bn7xlZxhUeg/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1tu3mwusko6nu

Madee: Dogo Janja na Irene Uwoya Hawajaachana

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Madee Ali amefungukia Mahusiano ya Msanii mwenzake Dogo Janja na Mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya.

Madee ambaye ni Baba Mlezi wa Dogo Janja ameibuka na kupiga chini tetesi hizo ambazo zimekua zikipamba moto Kwenye mitandao ya kijamii.

 

Madee amedai na  yeye mwenyewe anachangazwa na taarifa hizo kuzagaa mitandaoni, kwa watu kuongea masuala mengi juu ya ndoa hiyo bila ya kuwa na uhakika wa jambo husika.

Dogo Janja na Irene Uwoya hawajaachana nani amesema wameachana?, sidhani kama kuna kitu chochote kimewakuta ila ninachojua mimi wapo sawa, hadi dakika hii tunayozungumza na wapo pamoja kabisa”.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa wanandoa Irene na Dogo Janja wanaelekea kupeana talaka baada ya kusemekana Uwoya kupata danga lenye pesa ndefu.

Kalala Junior Adaiwa Kuvuruga Ndoa Ya Uwoya na Dogo Janja

Msanii wa muziki wa dansi nchini Hamza Kalala ‘Kalala Junior’ anadaiwa kuwa chanzo cha mvurugano ulioikumba ndoa ya staa wa Bongo movie Irene Uwoya na Dogo Janja.

Global Publishers wanaripoti kuwa taarifa zinazosambaa Kwenye mitandao ya kijamii ni kuwa ndoa ya Dogo Janja na Uwoya imeingiwa doa na inasemekana chanzo ni Kalala kwani Uwoya amemzimikia vibaya mno Msanii huyo kiasi cha kumuhonga mizawadi kibao.

Baada ya kunasa tetesi hizo kutoka kwa chanzo cha kuaminika, gazeti la Risasi Vibes ilimtafuta Kalala ili aweke wazi juu ya madai hayo ya kuhongwa na kuivuruga ndoa ya Uwoya huyo na Dogo Janja.

Ni kweli nimeyasikia hayo maneno. Hata kwenye mitandao nimeona, lakini si kweli kabisa na nikwambie tu, tangu yaanze kusemwa yananivurugia hata kwenye uhusiano wangu.

Nina mtu wangu ninampenda na sipo na Uwoya ingawa ni rafiki yangu na mtu ambaye tunafahamiana”.

Baada ya kupata ukweli kutoka kwa Kalala Junior GPL lilimsaka Uwoya ili kusikia ukweli kutoka upande wake lakini hakuweza kupatikana kwani alikuwa nje ya nchi (Dubai) na Dogo Janja alipotafutwa alikataa kuongelea lolote kuhusu ndoa yake.

Irene Uwoya Ageuka Mbogo Baada Ya Kuulizwa Kuhusu Dogo Janja

Msanii wa filamu za Bongo Movie Mrembo Irene Uwoya amemwaga povu zito baada ya kuulizwa sababu za kutomposti mume wake Staa wa Bongo fleva Dogo Janja Kwenye kitandani zake za mitandao ya kijamii.

Kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya na mume wake Dogo Janja hawana maelewano na tetesi hizo zimezidi baada ya wawili hao kutopostiana Kwenye social media kama siku za nyuma.

Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Uwoya amemwaga povu na kudai  kuwa siyo lazima kila mara atamposti kwani ana mambo mengi ya kuandika na atafanya hivyo endapo tu imebidi.

Siyo kila mara nitakuwa natumia kurasa zangu kumposti Dogo, nina mambo mengine ya kufanya pia, itakapobidi kufanya hivyo nitafanya”.

Lakini pia Uwoya alihojiwa hayo baada ya kila mara kuonekana akiposti picha za kuwa ndani ya ndege ambapo wapo waliosema kuwa kwa sasa amekuwa akisafiri na kumuacha mumewe huyo peke yake.

Siyo kweli, mimi sisafiri mara kwa mara, zile ni picha tu nimewahi kusafiri mara moja nilipokua nikienda Mwanza kwenye Miss Lake Zone”.

 

 

Mchepuko Adaiwa Kuwa Tishio Kwenye Ndoa Ya Dogo Janja na Uwoya

Ndoa ya staa wa Bongo fleva Dogo Janja anayefanya vyema na wimbo wake wa ‘Banana’ na Bongo Movie Star Irene Uwoya yadaiwa kupumulia mashine huku mchepuko akiwa chanzo.

Global Publishers wanaripoti kuwa ndoa Changa ya mastaa hao imedaiwa kuingia jini mkata kamba baada ya Mrembo anayeitwa Dayana kudaiwa kuwa na mawasiliano ya karibu na Dogo Janja.

Chanzo cha karibu cha couple hiyo kiliitonya GPL kuhusiana na tatizo katika Ndoa hiyo ya Dogo Janja na Uwoya:

Fuatilieni, Uwoya na Dogo Janja hawako sawa kabisa chanzo ni Dayana, nasikia wanawasiliana sana na mara kadhaa Dogo Janja ameshindwa kuvumilia hadi kumposti kimafumbo kwenye ukurasa wake wa Instagram”.

Baada ya Tetesi hizo Dayana alidaiwa ili kujibu tuhuma hizo lakini hakutaka kukubali wala kukataa lakini alimpa ujumbe mzito Uwoya:

Ningepanda sana kumshauri dada yangu Uwoya kuwa kwanza amsihi mumewe asiwe ananisumbua kwa simu kwa sababu mimi niko na mtu mwingine lakini najua atapata naye tabu sana kwa sababu Dogo Janja bado mdogo hivyo bado hajafika kwenye safari ya mapenzi.

Nafikiri ingekuwa vizuri kabisa Uwoya angemtafuta mtu ambaye analingana naye lakini hivi sio sawa atapata tabu sana ni bora kuwa na mtu mzima mwenzake”.

Baada ya GPL kuzungumza na Dayana, lilimtafuta Uwoya ili kusikia anamzungumziaje ‘mwizi’ wake ambaye pia amempa ushauri ambapo alipopatikana hakutaka kufunguka kwa kirefu zaidi ya kusema amepokea ushauri wake.

Sidhani kama kuna kitu kikubwa cha kusema ila tu nashukuru ushauri wake nimeupokea nitaufanyia kazi“.

 

Dogo Janja Amkingia Kifua Uwoya Baada Ya Sakata La Picha

Dogo Janja ameibuka na kumkingia kifua mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya baada ya picha ya utupu kusambaa mtandaoni.

Wiki iliyopita Irene alizua gumzo Mtandaoni na kusababisha watu kadhaa kutokwa na povu baada ya picha yake iliyomuonyesha maungo  yake ya ndani kusambaa mtandaoni.

Dogo Janja aliingizwa Kwenye sakata hilo na kusema kuwa haoewi heshima yoyote na mkewe kwani kitendo hiko cha mkewe kukaa uchi kimemdhalilisha.

Dogo Janja ameibuka na kudai si kweli mke wake alikuwa uchi kama inavyoelezwa bali ni vazi la kawaida kwa maeneo ya ufukweni, pia mke wake ni staa hivyo mambo kama hayo ni kawaida kutokana na kufuatiliwa na mapaparazi.

Irene kuvaa vile kwanza alikuwa ufukweni, Irene ni staa popote anapokuwa lazima kuwe na kamera, paparazi hawakosi, kwa hiyo popote wanapoenda paparazi kwao ni content, so alikuwa pale beach kabiga picha kavaa nguo hakuwa uchi”.

 

Hakuna Mwanamke Wa Kunipindua Kwa Dogo Janja- Uwoya

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Irene Uwoya amefunguka na kuweka wazi kuwa bado hajaona mwanamke ambaye anaweza kimpindua kwa mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Uwoya ameweka wazi kuwa yeye ni mwanamke anayejiamini sana na anaamini kuwa mume wake anampenda na anajua kuwa hakuna mwanamke anayeweza kuingilia penzi lao.

Irene Uwoya amefunguka hayo Kwenye mahojiano na Global Publishers ambapo amesema alipoamua kuingia kwenye ndoa na mwanamuz­iki huyo alijua wazi ‘nyakun­yaku’ wapo, la­kini kikubwa anajiamini.

Mimi sio mwan­amke wa kufuatana na mume nyuma kwa sababu najiamiani kuliko na ninajua wazi hakuna ambaye anaweza kunin­yakulia mume wan­gu. Najiamini kila idara mimi sina wasiwasi wowote”.

Uwoya amesisitiza kuwa hata mume wake aende wapi na aone mwanamke gani hawezi kumuacha yeye maaana anajiamini na anaamini kuwa amekamilika idara zote.

Uwoya na Dogo Janja walioana mwaka jana ambapo wiki iliyopita walifikisha miezi Tisa katika ndoa pamoja.

Wanaonisema Kuolewa na Dogo Janja Wanatamani Nafasi Yangu- Uwoya

Staa wa filamu za kibongo Irene Uwoya amefunguka na kumkingia kifua mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Uwoya amedai kuwa wanawake wengi ambao wamekuwa wakimbeza kwa kitendo chake cha Kuolewa na Dogo Janja hawana lolote zaidi ya wivu kwani wanatamani wangeolewa wao.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Ijumaa Wikienda, Irene Uwoya amesema kuwa kuna wengine wanashangaa kwa nini ameolewa na mwanamuziki huyo lakini yeye haimshitui kwani alishaziba masikio yake siku nyingi tangu alipoamua kumpenda Dogo Janja.

Unajua kuolewa ni heshima ambayo wanawake wengi wanaihitaji, kuna ambao wananisema vibaya kwa wivu, walitamani wao ndiyo waolewe lakini imeshindikana ndiyo wananisema vibaya, wala sijali, nafurahia maisha yangu ya ndoa na wala sina habari yoyote“.

Dogo Janja na Uwoya walifunga ndoa Miezi kama Tisa iliyopita lakini mpaka leo hii imekuwa ngumu kwa baadhi ya watu kuzoea Ndoa hiyo na hata bado wapo watu wanaoiponda Ndoa hiyo.

Dogo Janja na Uwoya Wahama Nyumba Kisa Mzimu wa Masogange

Msanii wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja na mkewe staa wa Bongo movie Irene Uwoya wamehama nyumba waliyokuwa wanaishi ili kukimbia mzimu wa Agnes Masogange.

Agnes Gerald au maarufu kama Masogange aliaga dunia Miezi miwili iliyopita kutokana na maradhi ya pumu.

Rafiki mkubwa wa Masogange alikuwa Uwoya ambaye pia walikuwa wanaishi pamoja maeneo ya Makongo Juu.

Lakini sasa Wanandoa hao wanafunguka kuwa sababu iliyowapelekea mpaka kuhama nyumba yao ya zamani ni kukimbia mzimu wa Masogange ambao walikuwa wanahisi kuuona.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv, Dogo Janja  amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi“.

Dogo Janja na Uwoya walianika nyumba yao kifahari kwa wageni wao walioalikwa kufuturu wikiend iliyopita.

Irene Uwoya na Dogo Janja Kuhama Nyumba Kisa Masogange

Staa wa Bongo movie Irene Uwoya na mume wake staa wa Bongo fleva Abdul Chende maarufu kama Dogo Janja wamefungukia mipango yao ya kuhama nyumba waliokuwa wanaishi na marehemu Masogange.

Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa wapo katika mipango ya kuhama nyumba hiyo ambayo walikuwa wanaishi na marehemu Agnes Gerald siku za nyuma.

Wapendanao hao walikuwa wanaishi maeneno ya Makongo Juu pamoja na marehemu Agnes ambazo yalikuwa makazi yake mpaka alipoaga dunia siku chache zilizopita.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Jumamosi kwa niaba ya mkewe, Dogo Janja alisema kuwa hawawezi kuendelea kuishi hapo tena kwa sababu kwao itakuwa ni majonzi kila siku na hiyo ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao kwa Masogange.

Kwa kweli mimi na mke wangu hatuwezi tena kuendelea kuishi Makongo Juu kwenye ile nyumba maana kwetu itakuwa ni simanzi tuu, Masogange alikuwa ni mtu wetu wa karibu sana na tulikuwa tukifanya vitu vingi pamoja, pia mke wangu atakuwa na huzuni sana akiendelea kuishi pale,”

Marehemu Masogange alikuwa na ukaribu sana Irene Uwoya ambao walikuwa marafiki wakubwa kwa miaka mingi.