Faiza Ally Amwita Mtoto wa Mobeto Fake.

Mwanadada hasiye isha drama katika mitandao ya kijamii Faiza Ally amefunguka na kumjibu shabiki alitoa maoni ya kumshauri Faiza Ally hakumremba mtoto wake kama wanavyofanya wasanii wengine, lakini kitu cha ajabu wakati wa kumjibu shabiki Faiza Ally aliongea wazi kuwa hawezi kufanya hivyo kama anavyofanya Hamisa kwa watoto wake.

Katika maoni aliyoamua kujibu shabiki, faiza alisema kuwa hawezi kum-edit mtoto wake kama anavyofanya hamisa kwa mtoto wake na kumvalisha mawigi kwa sababu mtoto wake hivyo ndivyo alivyo.

siwezi kum-edit mtoto wangu mpaka apoteze uhalisia kama huyo wa mobeto , we are comfortable for who we are , na hizo nywele ndio asili yake ya uafrika , siwezi kumuweka dawa wala kumpachika viwigi …she born to be a star , she doesnt have to fake it , tunaishi maisha yetu kabisa.

Haijulikani kama kuna chochoko yoyote kati ya Hamisa na Faiza Ally mpaka afikie hatua ya kumuandikia hivi kuhusu mtoto wake.

 

 

Faiza Adai Gabo ni King’asti Kwani Alimtafutia Jimama La Kumlea

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally amefunguka mazito na kudai kuwa msanii mwenzake Gabo ni king’asti na hata kudai alimtafutia mwanamke mwenye hela ili amlee.

Bifu la Faiza na Gabo lilianza siku za nyuma baada ya kuigiza movie moja ambayo haijatoka mpaka leo ambapo Faiza ameonyesha kumlaumu Gabo na kudai amemtapeli.

Kwenye mahojiano na Kiss Fm Radio Faiza amefunguka na kukataa tetesi za yeye kuwahi kuwa Kwenye Mahusiano na Gabo na kuweka wazi kuwa Gabo alikuwa King’asti wa rafiki yake:

Ukweli ni kwamba Gabo alikuwa king’asti nilimpa  rafiki yangu anaitwa Karima yaani mtu ambaye nilimpa kazi na nikampa na demu ambaye ana hela”.

Faiza amedai mwanamke huyo ambaye alimpa Gabo ni mwanamama wa kizungu ambaye alivutiwa naye baada ya kumuona Gabo na mara moja wakaanzisha mahusiano na kudai kuwa Gabo amehongwa sana.

Ninaweza Kuzaa na Sugu Ana Mbegu Nzuri:-Faiza Ally

Mwanadada mjasiriamali amabe pia ni bongo movies faiza ally amefunguka na kusema kuwa hana mpango wa kuolewa na mwanaume aliyewahi kuzaa nae mtoto wake wa kwanza ambae ni mbunge wa Mbeya  mjini Mr Sugu lakini anaweza kuzaanae mtoto mwingine kwa sababu baba huyo ana mbegu nzuri.

Sugu ninaweza kuzaa nae mtoto mwingine kwa sababu ana mbegu nzuri sana kanipatia mtoto wa kike mzuri sana, ila sio kuolewa nae kwa sababu tulishashindwana hapo awali  sidhani hata kama tutawezana tena.

Faiza na Sugu walikuwa na watu wa kugombana katika mitandao kila siku kuhusu malezi ya mtoto huku mama huyo akisema kuwa baba hayupo makini katika kumhudumia mtoto wake, hata hivyo faiza amekuwa mtu wa kufunguka mambo mengi sana kuhusu sugu lakini sugu siku zote amekuwa kimya na hataki kuongea chochote kuhusu anayoyasema mzazi mwenzie.

 

Simuonyeshi Mwanaume Wangu Katika Media kwa Sababu Hatuna Malengo;-Faiza

Mwanadada Faiza Ally amefunguka ya moyoni na kuelezea kiundani sababu gani iliyomfanya hashindwe kuwa  namuweka wazi mpenzi wake ambae ni baba wa mtoto wake wa pili , Faiza ambae amekuwa akiweka picha isiyo taka kumuweka suara mwana ume huyo amesema kuwa sababu kubwa ni kutokana na kuwa hawana malengo yankusihi pamoja na mwanaume huyo lakini sio kwa sababu ni mume wa mtu kama watu wengi wanavyosema.

sipendi kumuonyesha kwa sababu hatuna malengo , hatutegemei kuishi pamoja wala kuoana kwaio i take my time ,when times come kuonyesha kwenye media  nitafanya hivyo.

Faiza anasema kuwa lengo kubwa ilikuwa nikuzaaa watoto wawili kabla hajafikisha miaka 35 na ndio maana amefanikiwa kwa hilo lakini swala la ndoa bado analifanyia kazi.

Faiza- Nampenda Sugu Ila Sio Kimapenzi

Muigizaji wa Bongo movie na Mfanyabiashara Maarufu Faiza Ally ambaye pia ni mzazi mwenza wa msanii na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amefunguka kuhusu uhusiano wao kwa sasa.

Siku chache zilizopita Sugu alitoka jela kwa msamaha wa Raisi alipokuwepo kwa miezi kadhaa baada yakukutwa na hatia ya kutoa kauli za uchi Hizi na kumchafua Raisi.

Faiza na Sugu wamekuwa na ugomvi au bifu la siku nyingi huku kwa upande wa Faiza Ikiwa ni kinyongo cha muda mrefu kwani alishawahi kuweka wazi kuwa bado anampenda mzazi mwenzake Lakini pia amekuwa haoni hatari kumwagia mvua ya matusi na hata kumdhalilisha mitandaoni.

Lakini hivi sasa tangu Sugu atoke jela Faiza ameonekana kuwa sawa na Sugu kwani amekiri kuwa anampenda Sugu ingawa hana hisia naye za kimapenzi.

Kwenye Interview aliyofanya na Bongo 5, siku ya Jumapili Kwenye uzinduzi wa filamu ya Mama ya Aunty Ezekiel, amefunguka haya:

Hisia na mapenzi ni tofauti, kwa sababu nampenda mapenzi ya kweli hayajawahi kufutika, i will always love him na kumpenda haina maana kuwa nina hisia naye. Nampenda ni ndugu yangu, baba watoto wangu”.

 

Faiza Amwaga Machozi Baada ya Kubeba Mimba Nyingine.

Mwanadada Faiza Ally amejikuta akiingia katika wakati mgumu baada ya kunasa mimba nyingine ya tatu huku mtoto wake wa kiume wa pili akiwa bado na umri wa miezi nane tu huku yeye mwnyewe akiwa anajipa moyo kuwa hawezi kupata mimba kwa sababu alikuwa akitumia vidonge vya kuzuia mimba.

Alikuwa akitoa taarifa juu ya swala hilo anasema kuwa Faiza  hakujua kama angeweza kubeba mimba kwa sababu alikuwa anatumia njia ya kuzuia mimba lakini kwa bahati mbaya laipata mimba huku akiendelea kunywwa dawa hizo ambazo zilikwedna na kuharibu mimba hivyo kuanza kuumwa bila kujua anaumwa nini.

Msemaji huyo anasema kuwa baada ya hapo alikwenda hospitali ambapo alikwenda na kugundua tatizo kuwa alikuwa na mimba iliyoharibka  kutokana na kutumia vidonge hivyo,alipofika hospitali waligundua tatizo hilo huku wakiona kuwa mimba ilikuwa imeharibika hivyo kuamua kumsafisha ili kumuweka sawa.

Baada ya kuongea na msemaji huyo  gazeti Moja   waliamua kumtafuta faiza ally mwenywe ilikuthibitisha habari hizo na ndipo aliposema haya”ni kweli nilikuwa mjamzito, unajua mimi na baba yake mtoto tunakaa mbalimbali kwahiyo inabidi tutumie dawa za kuzuia mimba, kumbe dawa tulizokuwa tukitumia hazikuwa za kuzia zilikuwa ni za kuharibu kabia kwaio hata ilipoingia kwa bahatimbaya iliharibiwa na dawa hizo, lakini haukutoka vizuri ndio nikawa najisikia vibaya  na kuumwa mpaka nilipokwenda hospitali.

Hata hivyo Faiza Ally alipoulizwa kama angekuwa tayari kuzaa kama mimba hiyo isingeharibika huku wakikariri amneno yake ya mwanzo kuwa watoto wawili wanatosha alijibu kuwa kwa sababu mimba iliingia kwa bahati mbaya hasingeweza kuitoa hata kidogo kwa sababu hawezi kufanya hivyo.

 

Faiza Ally Amchekelea Wema Sepetu

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally ameshindwa kuzuia hisia zake na kuchekelea baada ya Wema kupata ubalozi wa Star Times siku ya jana.

Siku ambayo Zari alikuja Tanzania baada ya kupata ubalozi wa bidhaa mbili tofauti Faiza alitoa povu zito na kulalamika makampuni hayo kwa nini yametoa nafasi hiyo kwa mtu ambaye sio Mtanzania.

Faiza Ally alilalamika kwa nini wanatoa ubalozi kwa mtu ambaye ni Mganda halafu wanaacha mastaa kibao ambao ni Watanzania ambao wanaweza kabisa kufanya jukumu hilo.

Siku ya jana Wema Sepetu na wasanii wenzake kadhaa wamelamba dili nono kutoka Kwenye kampuni ya Star Times na kwa kuwa mabalozi wao wote waliowachagua ni Watanzania Faiza amechekelea uchaguzi wa Wema Sepetu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza amemuandikia ujumbe huu Wema wa kumpongeza:

 

Faiza Ally Akiri Kumlilia Sugu Gerezani, Asema Penzi la Kweli Halifi

Mwanadada Faiza Ally amefunguka na kuonyesha hisia zake baada ya mtoto wake wa kike aliyezaa nae kipind akiwa katika mahusiano ya kimapenzi na mbunge na msanii wa hip-hop Mr Sugu  kutuma ujumbe na zawadi ya chocolate kwa baba yake huku yeye mwenyewe akiwa hajui kama mtoto wake alikuwa anadhamilia kutuma zawadi hiyo kwa baba yake.

Akielezea kwa uchungu, faiza ali anasema kuwa mtoto wae huyo amemliza sana na ameamini kuwa penzi la kweli kwa Sugu kutoka kwake na familia yake halkiwezi kuisha hata kama walishgaachana kitambo.

Nimeumia na kujikuta nikilia baada ya baba sasha kupokea zawadi ya chocolate kutoka kwa mwanae  akiwa gerezani, nimeumia sana na nimeimagine hali hiyo aliyokuwa nayo  na kama ningekuwa mimi maana nimeona ni kama movie.hata sikujua kama chocolate alizokuwa akizifungasha zilikuwa zikienda kwa baba yake, nalia na wala sikuwahi kujua kwamba kuna siku nitakuja kulia kwa sababu ya baba sashatena kwa uchungu.uwiii jamani kweli mapenzi ya kweli hayajawahi kuisha  dah!dunia ina uchungu wa kila rangi,@sashadesderia pole mamy labda unakuwa humaanishi kile ninachomaanisha mimi, au haujui uzito lakini kama mzazi imenigusa sana kutoka moyoni.

Faiza Ally Alilia Umoja na Ushirikiano Kwenye Bongo Movie

Muigizaji wa Bongo movie Faiza Ally amefunguka na kuendelea kulia na Bongo movie huku akiwa sihi wasanii wenzake wazidishe umoja na ushirikiano baina yao.

Faiza Ally ameongea hayo huku akilihusisha tukio la kusikitisha lililotokea siku chache zilizopita baada ya kifo cha Agnes Masogange na ushirikiano wasanii wote walionyeshana.

Faiza amewataka wasanii wa bongo movie kuwa na umoja na ushirikiano kwenye sanaa na kufanya filamu kama walivyokuwa kwenye msiba ambapo amesisitiza kama Ikiwa hivyo basi ni wazi kuwa sanaa hiyo itafika mbali.

Faiza alifunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo aliandika ujumbe huu:

Tunaishi kwa kujifunza na mara nyingi mitazamo ya nje sio halisi, naomba nimpongeze IreneUwoya kwa kuwa rafiki mwema a special kipindi hiki, nimemuona akishiriki na kwenye utulivu sana yaani kasimama kama rafiki na hivi ndio inavyo takiwa, yaani jambo linapo kufika la mtu wa karibu sio kulia sana au kupoteza fahamu lazima usimame ujue hatma ya mwenzio kwanza.

Nahisi Bongo Movie tuna vitu vikubwa sana wote kwa pamoja lakini sijui tunakosea wapi, maana kwa ushirikiano huo huo wa msibani, urudi kwenye kwenye kazi naamini kuna hatua kubwa sana tutapiga, nisema tu mpo vizuri sana, nyinyi ni wa maana sana“.

Agnes Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao Mbeya ambako alizikwa jana Aprili 24, 2018 kijijini kwao Utengule, Mbalizi

Wastara Ametaja Sababu Zilizomfanya Kuolewa na Kuachika Ndoa Tatu

Muigizaji wa Bongo movie Wastara Juma au maarufu kama Wastara Sajuki amefunguka na kuweka wazi sababu zilizomfanya mpaka hivi sasa awe ameolewa na kuachika katika ndoa tatu tofauti.

Wastara alifunguka hayo alipokuwa mgeni maaalumu katika Tamasha la Single mothers ambalo ni tamasha lililowakutanisha wamama wote wanaolea watoto wao wenyewe bila msaada wa Baba wa watoto kwa lugha nyingine ni Single mothers.

Wastara  alisema kuwa, siri kubwa ya ndoa zake kuvunjika ni kutokana na kukosekana kwa maelewano ndani ya nyumba na siyo kwamba huwa anapenda kuachika.

Unajua kuna vitu ambavyo ningevikubali kuvifanya nilipokuwa ndani ya ndoa, ungekuta sasa hivi nimeshakufa hivyo kuolewa na kuachika siyo kupenda, bali nilishindwa kukubaliana na mambo ambayo nilikuwa ninalazimishwa kuyafanya”.

Tamasha hilo la Single mothers lilifanyika katika hoteli ya De Mag Mwananyamala na liliandaliwa na msanii wa Bongo movie Faiza Ally kwa ajili ya kuwakutanisha wamama wote ambao ni Single mothers ili kuzungumzia mambo mbali mbali na kupeana ushauri.

Faiza Aja na Kampeni ya Single Mothers ,Ni Kwa Wamama Wenye Majukumu ya Kulea Watoto Peke Yao

                                                         

Mwanadada Faiza Ally ambae pia ni mfanya baishara maarufu bongo amekuja na kampeni ya single mothers itakayowakutanisha wanamama wanaolea watoto wakiwa peke yao bila kuwa na baba zao.faiz ameamua kufnaya hivyo ili kukutana na wanawake wanaobeba majukumu ya familia wakiwa kama mama na pia wakishika nafasi ya baba ambao wanapatikana wengi sana katika jamii zetu.

Akiwa kama mmoja wa wanawake hao kutokana na kulea mtoto wake wa kike peke yake kwa muda mrefu huku ikisemekana kuwa baba wa mtoto wake muda mwingi alikuwa akikataa kutoa matunzo kwa mtoto wake anaalika wanawake wengine kuja katika siku hiyo ya kukutana kwao ambapo itafanyika april 7 mwaka huu na kuongea matatizo yanayowakabili.

 

 

Faiza Ally Amtolea Povu Zito Gabo Adai Amechelewesha Mafanikio Yake

Msanii wa Bongo movie Faiza Ally amemtolea povu zito staa wa Bongo movie Gabo na kudai amemfelisha na kumkosesha kupata mafanikio aliyoyategemea.

Siku ya Jumapili kwenye Tuzo za Sinema Zetu International Film Festival (SZIFF) Gabo aliibuka kidedea na tuzo tatu ikiwemo msanii bora wa kiume  na kupelekea watu kadhaa kumpongeza huku wengi wakisema amestahili ushindi Ule.

Lakini Faiza amejitokeza na kumpongeza Gabo Lakini pia amemtolea povu zito huku akimtuhumu kwa kumfanyia dhuluma ambayo imemfanya apoteze hela na jitihada zake kurudi nyuma na kushindwa kupata mafanikio.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Faiza amemtolea povu zito sana Gabo:

 

 

 

Faiza: Ina Maana Watanzania Wote Hamkuwaona Mpaka Mkampe Dili Zari

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Faiza Ally amerudi tena Kwenye headlines baada ya kutoa povu zito Baada ya Zari kutangaza kama balozi mkuu wa bidhaa za Softcare.

Siku ya jana Zari pamoja na kampuni ya Softcare walifanya mkutano na waandishi wa Habari ambapo walimtangaza Zari kama Balozi wa kuuza Bidhaa hizo ambazo ni pampas za watoto.

Lakini dili hilo lilizua minong’ono kutoka kwa watu hasa kwa sababu kampuni ni ya Tanzania lakini Zari ni Mganda anayeishi nchini South Africa kwaiyo inakuwaje waache mastaa wote wa hapa Tanzania waende Uganda.

Faiza alitoa povu zito juu ya hilo na kuihoji kampuni hiyo kwa nini imewaacha wanawake wengine wengi ambao ni mastaa hapa Tanzania ambao nao wengeweza kufanya kazi hiyo na kumchukua mtu ambaye hata sio Mtanzania.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Faiza alitoa povu hili:

Hii sio mara ya kwanza kwa Watanzania kulalamika baada ya Zari kupewa Dili la kutangaza bidhaa za Tanzania alishawahi kuwa balozi wa Danube na Vodacom.

Sikuwahi Kuwaza Kuwa Single Mother:-Faiza Ally

Msanii wa Maigizo nchini faiza ally amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya ukuaji hakuwahi kuwaza kuwa single mother hata siku moja .Faiza anasema kuwa hata baada ya kupata mtoto alikuwa akijiuliza sana ni kwa sababu ya mwanaume ndio maana anaishi maisha ya kuteseka.

Katika Ukurasa wake wa Instagram Faiza Ally aliandika kuwa amekuwa katika wakati mgumu sana kuwa single mom lakini bado anajifariji kuwa ni bora kuliko mke.

Wakati nakua sikuwahi kuwaza kuwa single mom, lkn kutokana na misimimo yangu wanaume wajinga hawakunielewa nikajikita ktk kujitegemea, baada kuwa mama nikawa najiuliza ni kwa sababu tu ya mwanaume au baba mtoto ndio niishi maisha nisiyo yataka , nikaondoka nikiwa nauchungu mwingi mno lkn nikasema maisha yangu ni bora kuliko kuwa mke! Nikapitia mengi sana haikua rahisi lkn Leo nimesimama imara kwa sababu niliamua kuchagua maisha ninayo ishi kwa hiari ! Nilipita wapi na nikavuka vikwazo vyote ????? Njoo nita share stori yangu na wewe kuwa single mom sio mwisho wako ! Kuna maisha zaidi ya kukaa usipo stahili ! JUA THAMANI YA UANAMKE WAKO BILA KUJALI WANAO BWEKA NJIANI“.

 

“Natamani Ningekuwa na Mabwana Sita Ili Mmoja Aninunulie Simu Maisha Yangu Yaendelee”- Faiza Ally

Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amefunguka kuhusu kipindi kigumu anachopitia baada ya simu ya yenye thamani ya milioni tatu kushikiliwa na polisi kwa zaidi ya miezi mitatu.

Miezi michache iliyopita Faiza aliacha umma wa Watanzania midomo wazi baada ya kuamua kuanika picha yake mtandaoni akiwa uchi wa mnyama Leba wakati anajifungua mtoto wake wa kiume.

Baada ya kusambaa kwa picha hiyo Faiza alitakiwa kuwasili kituo cha polisi mara moja kwani iliangaliwa kama ni picha ya uchi na ni kinyume na maadili ya Kitanzania na alipofika kituoni hapo simu yake ilichukuliwa kama ushahidi.

Faiza leo kaamkia Instagram kulalamika juu ya suala hilo na ameandika maneno yafuatayo:

Kama kuna siku nimeamka na maumivu makali ni leo, leo nimetamani ningekuwa mzungu niishi kwenye nchi zenye haki za binadamu maana kuna wakati unaonewa kwenye nchi yako! Huu ni mwezi wa tatu tangu polisi wachukue simu yangu iphone 7+ yenye thamani ya shilingi milioni 3 inaniuma sana naenda kuripoti polisi sahivi nimepewa wiki mbili mbili kisa picha yangu ya leba wanahesabu kama pornography, Nimewaeleza polisi changamoto ninazopitia kwa kukosa simu mimi ni mfanyabiashara shughuli zangu zote zinategemea ile simu kuna emails contacts hata picha za biashara maisha yangu bila hiyo simu ni magumu mimi ni kama wa watoto wawili  mimi ndio nilipe ada ya mwanangu, kodi ya nyumba na maduka, ugali wa watoto ninunue”.

Lakini pia Faiza ametamani angekuwa na mabwana hata sita wamsaidie kununua simu mpya:

Nimewaza mpaka nimetamani ningekuwa na mabwana kama Sita hivi ili mmoja aninunulie simu niendelee na maisha yangu najitahidi nisimame bila mabwana lakini wakati mwingine wanawake tukizidiwa hakuna namna sasa hivi sio sawa mnakuwa kama mnarudisha juhudi zangu nyuma naomba mtoe huku ili maisha yaendelee”.

 

“Nimekuja Mpaka Marekani Kufanya Mapenzi na Baba Watoto Wangu” Faiza Amtolea Povu Mwanaume Aliyemtongoza

Faiza Ally ambaye ni muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameibuka na jipya leo hii baada ya kumwaga povu la aina yake kwenye mtandao wa kijamii.

Faiza amemtolea maneno mazito mwanaume mmoja ambaye ni shabiki anayemfuatilia kwenye mtandao wa Instagram ambapo Faiza amedai mwanaume huyo amekuwa akimtaka kimapenzi na kutaka kumzalisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faiza aliweka picha ya mwanaume huyo na kuandika maneno haya:

Nikiwaonyesha meseji za Whatsapp na Dm za huyu fal* mnaweza mkatambua kuwa muonekano na utu ni vitu tofauti sana. Sasa Malaya wa kiume ni hivi hizo nasty meseji zako ni za kunivunjia heshima yangu pumbavu wewe! Nataka kukwambia wewe hivii na mafala wengine wote kwamba sizalishwi na mtu yoyote hasa mwenye sura ngumu kama yako halafu ninapo posti picha zangu haina maana ninaposti ili nitongozwe kwa taarifa tu hapa nipo na bonge moja Handsome all the way kutoka Marekani kuja kufanya Mapenzi na mimi tu na ni baba watoto wangu sasa sitafuti bwana of course nina bwana na nikitaka mwingine nitapata lakini sio mbaya kama wewe. So kuanzia sasa stop sending your stupid messages on my DM na WhatsApp no yangu ni kwa ajili ya biashara sio kwa ajili ya wapumbavu kama wewe! IDIOT”.